Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polepole: CCM Haijamkosoa CAG......CHADEMA Ndo Waliomkosoa

$
0
0
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya CCM, Humphrey PolePole amefunguka na kusema kuwa wao kama Chama Cha Mapinduzi na serikali hakuna mtu kati yao aliyemjibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad bali CHADEMA ndiyo wamemjibu.

Polepole amesema hayo leo April 22, 2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kudai kuwa wao waliipokea ripoti hiyo na kumpongeza CAG na kuitaka serikali iendelee kuchukua hatua katika yale ambayo CAG ameyabaini.

"Kimsingi kwa CCM au Serikali yake hakuna hata mtu mmoja ambaye amemjibu CAG, sisi tulipokea, tulipongeza na tukaelekeza Serikali iendelee kuchukua hatua. Ambaye amejitokeza kujibu hadharani ni CHADEMA ndio pekee wamemjibu na kumkosoa CAG. Ila naona watu wachache pamba masikioni" alisisitiza Polepole

Polepole anasema yeye alipowaita waandishi wa habari hakumjibu CAG bali amedai kuwa alifanya ufafanuzi wa hoja mbalimbali ikiwepo ile ya Trilioni 1.5 ambayo kwenye ruipoti ya CAG inaonekana haina maelezo.

"Kuna tofauti kati ya kumjibu CAG na kufafanua hoja ambazo amezitoa kwa CCM na kuulaani vikali upotoshaji wa Zitto Kabwe juu ya taarifa ya CAG" 


Msanii wa Bongo fleva Jebby, afariki dunia

$
0
0
Msanii wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Jebby ambaye amewahi kufanya vyema na wimbo kama Swahiba amefariki dunia leo April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Watu wa karibu na msanii Jebby wamesema kuwa msanii huyo alikuwa anaumwa na mpaka umauti umemkuta Dodoma alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya bandama na ndiyo yaliyosababisha kifo chake.

Msanii Afande Sele pia amethibitisha hilo na kusema kuwa Jebby alikuwa anasumbuliwa na matatizo hayo ya bandama na kuwa leo ndiyo amefariki dunia.

"Hayupo tena duniani swahiba...pumzika kwa amani mdogo wangu wa haki Jebby.Tukimaliza kazi tutavalishwa taji" alisema Afande Selle

==>>Sikiliza Wimbo wa Swahiba hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya April 23

Rais Magufuli Ateua Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi Benki ya Posta

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).

Uteuzi wa Dkt. Mndolwa umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2018.

Dkt. Mndolwa anachukua nafasi ya Prof. Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake.

Galis ajitetea kuzimia akiwa kashikilia kitambaa msibani kwa Masogange

$
0
0
Baada ya picha yake inayomuonyesha kazimia huku kashikilia kitambaa mkononi kuibua gumzo jana mitandaoni, msanii wa filamu, Rammy Galis ameeleza kuwa hakuwa amezimia ila alijisikia kuishiwa na nguvu.

Galis alikuwa mmojawapo wa watu waliobeba jeneza la marehemu Agnes Gerald 'Masogange’ katika shughuli za kuuga mwili zilizofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam jana Jumapili, Aprili 22.

Galis amesema kutokana na kusimama muda mrefu wakati wa shughuli za kuuaga mwili alijikuta akiishiwa nguvu na kuomba msaada kwa wenzie wamuondoe eneo ilipokuwa inafanyikia shughuli hiyo.

"Unajua nilisimama sana tangu tunapofikisha mwili pale viwanjani mpaka watu wanaanza kuaga, nadhani kutokana na hilo nikajikuta naishiwa nguvu, hivyo niliwafahamisha wenzangu kwamba sijisikii vizuri na kuomba waniondoe eneo lile,”

“Hivyo pamoja na wao kuamua kunibeba sio kwamba nilikuwa eti nimepoteza fahamu na ndiyo maana hata kitambaa bado niliweza kukishikilia naomba watu waelewe hivyo na kuacha kunisema kuwa nilikuwa naigiza siwezi kufanya hivyo katika msiba," amesema msanii huyo aliyewahi kutamba kwenye filamu ya Chausiku.

Mbali ya kucheza filamu ya Hukumu na Masogange enzi ya uhai wake,Galis pia alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu  uliodumu kwa mwaka mmoja (2016-2017).

Masogange aliyefariki Machi 20 mwaka huu akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya mama Ngoma, anatarajiwa kuzikwa leo Jumatatu, Aprili 23  jijini Mbeya.

Serikali kupima watu UKIMWI na TB hadi kwenye bar

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema katika mikakati yake ya kuwatambua wagonjwa wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na TB wameazimia kutembea maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo baa, migodini na mahali penngine ili waweze kuwatambua kiurahisi.

Hayo yameelezwa na serikali ya awamu ya tano kupitia Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile leo Aprili 23, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 15 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza kutoka kwa Mbunge Masoud Abdallah aliyetaka kufahamu serikali ina mikakati gani katika kutoa elimu maalum ambayo itaweza kuenea kwa kasi zaidi katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi zaidi.

"Serikali baada ya kuona kumekuwa na changamoto kubwa sana katika utambuzi wa makundi maalum ambayo wengi wamekuwa wakiathirika na ugonjwa wa TB na UKIMWI. 

"Hivyo tumeamua kujielekeza kutoa elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari lakini vilevile tuna mkakati mahususi wa kuwatafuta wagonjwa wa TB katika migodi sambamba na hilo tumetengeneza tumetengeneza mikakati jumuishi kati ya ugonjwa wa TB na UKIMWI", amesema Dkt. Ndugulile.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa hivi tumeanza kujielekeza mahali kwenye watu wengi ili tuweze kuwapata kwa pamoja hususani wanaume ambapo mara nyingi wanakuwa katika bar. Msishangae kutuona na sisi tunapita huko kuwaomba kufanya upimaji wa suala la ugonjwa wa UKIMWI pamoja na TB".

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kumgundua mgonjwa wa TB mapema na kumuweka katika matibabu ndio njia kuu ya kupambana na kulishinda tatizo la kifua kikuu jambo ambalo lipo kwenye mikakati ya serikali katika kufufua uwezo wa kufikia watu wote wanaohitaji huduma za TB ili kuwagundua mapema na kuwatibu kikamilifu.

Wabunge watakiwa kuwa msaada kwa walemavu

$
0
0
Wabunge wa wametakiwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya wanawake na watoto wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Ushauri huo umetolewa mara baada ya kufanyika kwa utafiti uliofanywa na shirika la ‘Action On Disability and Development’ kwa kushirikiana na shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania kubaini kuwepo kwa vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto wenye ulemavu.

Akizungumza na Wabunge katika semina iliyoandaliwa na Shirika la ADD, Mjini Dodoma, Mkurugenzi wa Shirika hilo Rose Tesha amesema kuwa baadhi ya ndugu na jamaa wamekuwa wakishiriki vitendo hivyo hususani kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na akili.

Aidha, Wakitoa maoni yao katika Semina hiyo baadhi ya wabunge wametaka sheria iweze kurekebishwa ili mfuko wa jimbo pia uweze kuwahudumia watu wenye ulemavu huku wengine wakitaka uboreshaji wa miundombinu kwa watu wenye ulemavu.

TCRA yashauri jinsi ya kusuluhisha changamoto kesi za mitandaoni

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja changamtoto tano za uendeshaji kesi zinazotokana na makosa ya mtandao.

Changamoto hizo zimetajwa kuwa ni uelewa mdogo wa majaji, mahakimu na wanasheria, ushahidi wa kuwasilisha, kufutika kirahisi, uchunguzi, na wapi pa kupeleka malalamiko hayo.

Mwanasheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Philikunjombe amewataka majaji na mahakimu na wanasheria kupata elimu juu ya uendeshaji wa kesi hizo kwani kumekuwa na makosa makubwa yanayotendeka.

Mbali na hiyo amesema bado kuna ugumu wa kujua ni namna gani ushahidi unatakiwa kuwasilishwa mahakamani pindi mtu atakapokwenda kulalamika kuwa katendewa makosa.

”Umetukanwa kwenye simu je upeleke simu ya aliyekuwa kwenye simu, je upeleke simu ya aliyekutukana mahakamani, Tutajuaje kama baada ya kumnyang’anya simu yake hukubadilisha ujumbe. Kama umechapisha katika karatasi, tutajuaje kama hukuongeza maneno au kupunguza? Hivyo, bado ni vigumu kupata ushaidi wa kesi hizi” amesema Philikunjombe.

Lakini pia changamoto nyingine ni ushahidi wa kesi hizo kuharibika kirahisi kwa sababu mtuhumiwa anaweza kufuta ujumbe hivyo haitakuwa rahisi kuthibitisha makosa hata kama ujumbe huo utakuwa nao mlalamikaji.

Kufuatia changamoto hizo wadau mbalimbali wanaotumia mitandao wameshauri wasimamizi wa kesi hizo kupewa elimu ya sheria zinazohusu makosa ya mtandao ili haki iweze kutendeka.

Serikali Kumwaga Ajira 25,000 kwa watumishi wa kada ya afya

$
0
0
Serikali imepanga kuajiri watumishi wa kada ya afya wapatao 25,000 katika mwaka wa fedha 2018/19.

Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini Dodoma leo Jumatatu Aprili 23, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kandege wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Issay (CCM).

Katika swali la msingi Issay alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuongeza watumishi katika Hosptali ya Wilaya ya Mbulu ambapo Kandege amesema tayari Tamisemi imeomba kibali cha kuajiri watumishi wa kada ya afya 25,000 ili kuhakikisha kunakuwapo na watumishi wenye sifa stahiki kwenye hospitali, vituo vyote vya afya na zahanati.

“Serikali inaendelea na ujenzi wa vituo vya afya 208 nchi nzima ili kuboresha huduna ya dharura kwa mama wajawazito, ujenzi wa vituo hivyo utagharimu Sh bilioni 132.9 hadi kukamilika.

“Sambamba na ujenzi huo, vituo hivyo vimetengewa Sh bilioni 35.7 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba ili kuviwezesha kutoa huduma kwa wagonjwa,” amesema.

Mwili wa Agnes ‘Masogange’ ulivyowasili nyumbani kwao

$
0
0
Mwili wa Agnes Gerald ‘Masogange” tayari umewasili nyumbani kwao eneo la Utengule-Mbalizi mkoani Mbeya.

Wema Sepetu Kakutwa na Kesi ya Kujibu.....Ataanza Kujitetea May 14

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya wana kesi ya kujibu, hivyo wataanza kujitetea.

Uamuzi huo, umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Constantine Kakula kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama lah.

Katika uamuzi wake Hakimu Simba amesema kwa mujibu wa sheria kama washtakiwa wakipatikana na kesi ya kujibu watatakiwa kujitetea, pia kama hawana kesi ya kujibu wataachiwa huru.

“Baada ya kupitia hoja zote, mahakama imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki kisheria kuanza kujitetea,” amesema Hakimu Simba.

Baada ya kusema hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 14 na 15,2018 ambapo washtakiwa watajitetea mfululizo.

March 23,2018 upande wa utetezi kupitia wakili Alberto Msando, uliwasilisha hoja katika mahakama hiyo kwamba washtakiwa hawana kesi ya kujibu.

Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa February 4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Aipongeza Tanzania Kwa Maendeleo

$
0
0
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dkt. Martin Ngoga ameishukuru na kuipongeza Serikari ya Tanzania kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa reli kwa sababu inaleta manufaa hata kwa nchi jirani.

“Miradi hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa kwa kasi si kwamba inachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania, bali hata wa nchi nyingi za jirani kwa kuwa nazo zitanufaika na miradi hiyo kwani si nchi zote zina bandari”.

Dkt. Ngoga ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 23, 2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Bungeni mjini Dodoma.

Amesema tayari wamejadili ripoti iliyotokana na ziara iliyofanywa na wabunge hao katika upande wa korido ya kuishi na korido ya kaskazini ambapo wametoa mapendekezo yatakayofanyiwa kazi na baraza la mawaziri.

“Tayari tumeshajadili miswada miwili inayohusu Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na  mswada wa Takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  ya mwaka 2017.”

Pia Spika huyo amesema wamefurahia uwepo wao nchini, ambapo mbali na shughuli zao za kibunge pia kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wameshiriki kampeni ya kukijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1,000 kwenye eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema amefarijika na uamuzi wa Bunge la EALA kufanya vikao vyake katika nchi wanachama kwa sababu unatoa fursa ya kujua mazingira ya nchi hizo pamoja na maendeleo yake.

Amesema nchi wanachama wanamatumaini makubwa na bunge hilo katika kuimarisha na kuboresha maendeleo ya mataifa yao,  hivyo amewatakia mjadala mwema.

Katika hata nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wabunge hao na marafiki zao kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya viwanja, utalii, kilimo na madini.

Kwa mara ya kwanza vikao vya Bunge la Afrika Mashariki, (EALA) vinafanyika Dodoma katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa ulipo ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vikao hivyo vilianza Aprili 17, 2018 na vinatarajiwa kumalizika Aprili 29, 2018.

Rais Uganda aonya wanaotumia ulimi kufanya mapenzi na Wanawake

$
0
0
Rais Yoweri Museveni amewaonya wananchi wa Uganda dhidi ya vitendo vya kutumia mdomo katika kufanya mapenzi, akisema "mdomo uliumbwa kwa ajili ya kula na si mapenzi".

Rais huyo wa muda mrefu nchini Uganda amesema utamaduni huo wa kutumia mdomo katika mapenzi uliletwa na wageni.

“Nichukue nafasi hii kuonya watu wetu hadharani dhidi ya vitendo visivyo sahihi vilivyoletwa na vinavyoendelezwa na wageni. Mojawapo ni mapenzi ya kutumia mdomo. Mdomo ni kwa ajili ya kula si mapenzi.” Museveni alisema hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni.

Vyombo vya habari vya Uganda vimeripoti onyo hilo na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, ambako baadhi ya watu wanapingana naye na wengine kumpongeza.

Kauli yake ilitoka siku chache baada ya kusambaa kwa picha zinazomuonyesha ofisa mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Makerere akimnyonya sehemu za siri  mwanafunzi wake ofisini kwake.

Ofisa huyo, anayehusika na utawala, ameshasimamishwa kazi na analipwa nusu mshahara, wakati tukio hilo likichunguzwa.

Tukio hilo lilijulikana baada ya mwanafunzi huyo kusambaza picha alizojipiga wakati ofisa huyo akimfanyia kitendo hicho.

Mwanafunzi huyo alisema ofisa huyo wa Makerere alimbusu sehemu zake za siri kwa nguvu na alipiga picha hizo ili apate ushahidi kwa kuwa ofisi hiyo haikuwa na kamera za usalama.

Usambazaji wa gesi Majumbani kuanza kesho jijini Dar

$
0
0

Usambazaji wa gesi majumbani katika jiji la Dar es Salaam unaanza kesho Jumanne, Aprili 24 huku bei ya gesi ikipungua kwa asilimia 40 ya bei ya sasa kwenye mitungi.

Waziri wa Nishati, Dk Medadi Kalemani ametoa kauli hiyo muda mfupi  wakati akijibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  katika utaratibu wa mawaziri waliojiwekea.

Dk Kalemani amesema gharama za kuunganisha gesi kwa wateja watakaopitiwa na bomba hilo itakuwa Sh 200,000 hadi 1 milioni kutegemeana na umbali kutoka lilipo bomba kuu.

Ametaja baadhi ya maeneo yatakayoanza kunufaika kuanzia kesho ni Ubungo, Mwenge, Kijitonyama, Gongolamboto, Shekilango na Mikocheni na kazi hiyo itadumu kwa miezi miwili.

Serikali: Hakuna tiba ya kisukari Dunia Nzima

$
0
0
Wizara ya Afya imesema duniani kote hakuna dawa iliyogundulika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kisukari na kupona.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile amesema matibabu yanayotolewa kwa sasa ni kumpatia mgonjwa kiwango bora cha kuishi na kuhakikisha kiwango chake cha sukari mwilini kinakuwa ndani ya kiwango kinachotakiwa.

Dk Ndugulile ametaja dawa hizo ni sindano za  insulin ambayo mgonjwa hulazimika kuchomwa kila siku kwa maisha yake yote pamoja na vidonge ambavyo humeza kila siku.

Katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalumu(CCM), Christina Ishengoma  amehoji Serikali ina mpango gani wa kufanya tafiti kuhusu dawa za kisukari.

Waziri amesema ugonjwa huo huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 35 na kuendelea ingawa watoto na vijana wanaweza kupata ugonjwa huo kwa kutozingatia misingi ya lishe.

Amesema kuna tafiti zinazofanywa duniani kote ili kutafuta dawa itakayoweza kutibu kabisa ugonjwa huu ingawa tafiti hizo hazijazaa matunda.

Raman Ya Jiji la Dar es Salaam Yafumuliwa Upya

$
0
0
Serikali imeachana na ramani ya mipango miji ya Jiji la Dar es Salaam iliyokuwepo tangu mwaka 1979 na badala yake imechora mpya ili kuondokana na matatizo mengi ikiwemo mafuriko katika jiji hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu, Aprili 23 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akitoa ufafanuzi wa hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kwa muda sasa kumekuwapo na kelele nyingi kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo wadau na wasomi kuwa Jiji la Dar es Salaam ramani yake haifuatwi na ndiyo sababu kumekuwa na mafuriko ya mara kwa mara.

Hivi karibuni aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Profesa Anna Tibaijuka alisema ramani hiyo iliachwa na watu kuanza kujenga kiholela na hivyo kusababisha mpangilio mbovu wa kuzuia njia za maji na kusababisha mafuriko mara kwa mara.

“Ni kweli, master plan ya Jiji la Dar es Salaam hatujaipitia kwa muda mrefu, ni kama iliachwa, lakini tumeamua kuachana nayo na kutengeneza master plan mpya na imeshachorwa, lakini kwa sasa inafanyiwa mapitio pale wizarani kwangu,” amesema Lukuvi.

Waziri huyo amesema katika utaratibu wa kawaida, ramani za mipango miji hupitiwa kila baada ya miaka sita, lakini ramani ya Jiji la Dar es Salaam haijapitiwa tangu wakati huo na hivyo Serikali imeachana nayo na kuamua kuanza mpango upya.

Akizungumzia hoja za CAG, Lukuvi alikiri kuwa suala la upimaji na ugawaji wa viwanja haliendi vizuri kama alivyoeleza katika taarifa yake akitaja sababu za ukosefu wa watalamu uliokuwepo.

Makonda agharamia mazishi ya Agness Masogange

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegharamia gharama mbalimbali katika msiba wa Agnes Gerald alimaarufu kama Masogange ambaye amefariki April 20, 2018 na kuzikwa leo April 23, 2018 jijini Mbeya.

Akiongea mbele ya waombolezaji na Mkuu wa mkoa wa Mbeya mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Matebe Mathias 'MC Pilipili' ambaye ndiye 'MC' wa shughuli za mazishi ya Agnes Masogange amesema kuwa wameona mkono wa serikali katika hilo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye aliyefanikisha na kulipia magari ambayo yamewapeleka wasanii mbalimbali Mbeya.

"Mkuu wa mkoa wa Mbeya kuna upendo mkubwa ambao tumeuona kutoka kwenu kwani ulikuwa karibu na sisi muda mwingi, ulikuwa ukitupigia simu kujua tupo wapi hivyo naamini usiku wa leo hujalala kabisaa. 

"Pia tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwani yeye ndiye aliyelipia magari mawili, matatu ambayo yametuleta hapa Mbeya leo kutokea Dar es Salaam, hata kamati ambayo ilikuwa imeandaa kuanzia kutoa heshima ya mwisho pale Leaders Club ambayo ilikuwa chini ya Steve Nyerere ilipewa nguvu na watu wa serikali tumeona serikali mmetupa support vizuri" alisema MC Pilipili

Mbali na hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliweza kuwapokea na kutoa neno la shukrani kwa wasanii na watu mbalimbali ambao wameweka tofauti zao pembeni na kuungana kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanampumzisha salama mwenzao katika nyumba ya milele.

"Mueendelee kuwa pamoja hivi hivi bila kujali tofauti zenu, mabifu yenu mzidi kuwa wamoja kwani hili jambo mmejenga heshima kubwa sana, naomba nitoe pole sana kwa familia kwa msiba huu" alisema Makalla

Mmiliki wa Shule Ajitolea kumsomesha mtoto wa Agness Masogange hadi chuo kikuu

$
0
0
Mmiliki wa Shule ya Sekondary ya St. Patrick ya jijini Dar  es Salaam, Ndele Mwaselela amejitolea kumsomesha mtoto wa marehemu Agnes Masogange, Sania(11) kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na akifaulu hadi chuo kikuu.

Hii ni neema nyingine kwa mtoto huyo wa pekee wa Masogange aliyemuacha, baada ya jana kamati ya maandalizi ya mazishi kupitia mweka hazina wake, Zamaradi Mketema kueleza kuwa wamemwekea Sh2 milioni zilizobaki katika michango ya msiba huo kwenye akaunti yake.

Zamaradi amesema fedha hizo zimewekwa mahususi kwa ajili ya kumsaidia kianzio katika cha ada atakapoanza kidato cha kwanza mwakani kwa kuwa mwaka huu anatarajiwa kumaliza darasa la saba.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili, 23 katika shughuli za mazishi, zilizofanyika nyumbani kwa baba wa Masogange, Kijiji cha Utengule, Wilaya ya Mbalizi, Mwalesela amesema mbali ya kumsomesha pia mtoto huyo atakaa hosteli kwa gharama zake kwa muda wote wa masomo yake.

“Akifaulu kidato cha nne pia atasomeshwa na mimi hadi kidato cha tano na sita lakini pia akifaulu atakwenda hadi chuo kikuu,” |amesema.

Kutokana na maamuzi hayo, alimtaka msanii Irene Uwoya ambaye mtoto wake naye anasoma katika shule hiyo, kuhakikisha anapokwenda kumsalimia mwanaye awe anakwenda kumsalimia na Sania.

“Hivyo wewe msanii Uwoya una mtoto wako pale shuleni kwangu naomba ukija kumuona hakikisha unamuona na mtoto huyo,” amesema Mwaselela

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0766340868

Mzee Majuto azidiwa, arudishwa hospitali

$
0
0
Muigizaji na mchekeshaji wa siku nyingi, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto, amelazwa tena katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam, baada ya kuzidiwa.

Mke wa mwigizaji huyo, Aisha  Yusufu, ameiambia MCL Digital leo Aprili 23  kwamba mume wake walimpeleka hospitalini hapo leo saa 7:00 mchana.

Aisha amesema kidonda alichofanyiwa upasuaji kimeleta shida, hivyo kumpeleka kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Majuto alilazwa hospitalini hapo Januari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji wa tezi dume.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images