Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Zari amlilia Masogange.......Aeleza mapenzi aliyokuwa nayo kwa watoto wake

$
0
0
WASANII  na watu mbali mbali wenye ukaribu na tasni ya burudani wameendelea kutoa  salamu za pole kufuatia kifo cha video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, Zari The Boss Lady naye hajakaa kimya.

Zari ameeleza kuwa Masogange alikuwa akimtafuta kupitia simu kila mwezi akimuulizia maendeleo ya watoto wake ingawa hawakuwa marafiki sana. Kupitia mtandao wa Snapchat Zari ameandika;

"We were not friends as such but ever since you got my number you’ve been dropping me a text every month and i mean no month passed without you asking how are the kids. in peace sis."  

Kwa kiswahili;
“Hatukuwa marafiki sana lakini tangu upate namba yangu umekua ukinitumia meseji kila mwezi na hakuna mwezi uliopita haujauliza kuhusiana na watoto wanaendeleaje pumzika kwa amani dada”
Masogange enzi za uhai wake aliweza kutokea kwenye video za wasanii kama AY na Mwana FA, Belle 9, Tunda Man, Izzo Bizness na wengineo. 

Amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Mwili wa Masogange kuagwa Leaders, kuzikwa Mbeya

$
0
0
Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Wilayani Mbozi, mkoani  Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.

Dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni siku ya kesho Jumapili kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Ambapo misa itafanyika viwanjani hapo kisha kuanza safari rasmi kuelekea Mbalizi mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa marehemu Agnes Gerald mahali pema peponi.

“Tutaaga kesho asubuhi saa 3 pale Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.

Aidha imeelezwa kuwa kutakuwa na mabasi mawili yatakayobeba wasindikizaji wa mwili huo mpaka mkoani Mbeya.

Agnes Masogange amefariki jana Aprili 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pumu.

Waziri Mkuu: Uzalishaji Wa Chakula Nchini Umeimarika

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa mwaka 2016/2017 na 2017/2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.

Pia Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa kuiwezesha Wizara ya Kilimo kuongeza uwezo wa hifadhi ya Taifa ya chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 700,000 ifikapo mwaka 2025.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Aprili 21, 2018) wakati akiweka jiwe la msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula, Kizota  mjini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mkakati huo utahusisha ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuuzwa nje ya nchi na hivyo kutoa fursa za ajira na kuwaongezea kipato wananchi.

Amesema Serikali imefungua mipaka na inaendelea na jitihada za kutafuta masoko ya nje pamoja na kuboresha miundombinu ya kuhifadhi chakula kwa kujenga maghala na vihenge vya kisasa katika maeneo mengine yenye uzalishaji mkubwa wa chakula.

Pia Waziri Mkuu amewasihi wananchi watumia fursa za kiuchumi kwenye maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa kwa lengo la kuboresha na kuinua hali zao za maisha, hivyo watakuwa na uwezo wa kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye mradi huo mkubwa na baada ya kukamilika utakuwa na faida kubwa kwa Taifa, hivyo amewataka viongozi wa NFRA wahakikishe kwamba hakuna mahindi yatayoharibika katika maghala yao.

”Mikakati ya Serikali ni kuhakikisha NFRA inakuwa na uwezo wa kuhifadhi akiba ya kutosha ya chakula kwa ajili ya dharula lakini pia kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wakulima na wafanyabiashara kuuza mazao yao nje ya nchi bila vikwazo”.

Hata hivyp, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Fedha na Mipango na Wakuu wa Mikoa ambayo mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wahakikishe wanatimiza wajibu wao ili mradi ukamilike kwa wakati.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Bibi Vumilia Zikankuba alisema mradi huo unatekelezwa katika maeneo manane ya Kanda za Wakala huo ambayo ni Dodoma (Dodoma), Mpanda (Katavi), Songea (Ruvuma), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe), Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga (Shinyanga), Babati (Manyara).

Bibi Vumilia alisema katika Kanda ya Dodoma wanajenga vihenge vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na kufanya kanda hiyo kuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 59,000 kutoka uwezo wa sasa wa tani 39,000.

Alisema Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.

“Utekelezaji wa mikataba kati ya NFRA na wakandarasi ulianza Desemba 2017 ambapo muda wa utekelezaji ni miezi 18 tangu tarehe rasmi ya kuanza utekelezaji wa mikataba ya wakandarasi, hivyo kabla ya 2020 utakuwa umekamilika”.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira  na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama.

Wengine ni Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na  Ajira, Anthon Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na Balozi wa Poland nchini Tanzania, Balozi Krzysztof Buzalski.

Waziri Aipa Siku 30 TANESCO

$
0
0
Serikali ya awamu tano kupitia Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa mwezi mmoja kwa mameneja wote wa mikoa wa Shirika la Umeme nchini Tanesco kuwaunganishia umeme wananchi ambao tayari washalipia huduma hiyo na meneja atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo ajiuzulu kazi mara moja.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini (REA), awamu ya tatu katika maeneo mbalimbali wilayani kyela na kusema wananchi wamekuwa wanaolipia huduma ya kuunganishiwa umeme wamekuwa wakipatia kero nyingi bila ya kupewa huduma hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Hunter Mwakifuna ameishukuru Wizara ya Nishati kuwa kuwaelekeza wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kuwashirikisha viongozi wa maeneo husika, hatua ambayo imepunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.

Idris Sultan achaguliwa kuwa balozi wa Uber Tanzania

$
0
0
Mchekeshaji maarufu, muigizaji  na mshindi wa Shindano la Big Brother Afrika mwaka 2014, Idris Sultan amepata dili la kuwa balozi wa chapa ya kampuni ya usafiri ya Uber nchini.

Idris alitangazwa rasmi jana na kampuni hiyo ambapo Meneja Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Elizaberth Njeri amesema kampuni hiyo ilifanya utafiti kwa miezi kadhaa ili kujua nani anawafaa, na Idris ameonekana sahihi kwao kutokana na mtindo wake wa maisha.

“Idris Sultan ni mcheshi, msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji, tamthilia, na utangazaji wa vipindi vya redio. Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu yeye anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati,” amesema Njeri.

Kwa upande wake Idris ameshukuru kwa heshima aliyopewa na kusema amekubali kuwa balozi wa Uber si kwa kuwa amepata dili ambalo litamlipa, lakini yeye anaichukulia kama harakati ya kuwakomboa vijana wenzake katika changamoto ya ajira.

Amesema Uber isichukuliwe tu kama programu ya kutoa huduma ya usafiri bali ajira kwa vijana, hata wasomi hawatakiwi kuogopa kuwa washirika wa huduma hiyo kwa kuogopa kuitwa dereva.

“Kijana ambaye ana mawazo ya kutafuta, hapaswi kuwa na woga kwamba watu wengine watamchukuliaje bali kujali ni kiasi gani cha fedha kinaingia na maisha yako yanakwenda vipi,” amesema Sultan.

Meneja wa Uber nchini, Alfred Msemo amesema mchango wa Idris Sultan katika sanaa ya Tanzania unaendana na dhamira ya Uber ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo huo  nchini.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 22

Polisi Atiwa Mbaroni Kwa Rushwa ya 250,000

$
0
0
Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) inamshikilia ofisa wa jeshi la polisi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa ZAECA, Mwanaidi Suleiman Ally, alisema ofisa huyo Rajabu Juma Simba, mkazi wa Meli Nne-uzi, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000 kutoka kwa vijana wawili ambao majina yao yamehifadhiwa.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4.30 asubuhi nje ya kituo cha polisi cha Mwanakwerekwe, baada ya kuwakamata na chombo walichokuwa nacho aina ya Pasola, kwa kuwatuhumu wanaenda kununua dawa za kulevya aina ya bangi.

Alidai baada ya kuwapekua hakuwakuta nazo na kuwaamuru kwenda nao kituo cha polisi Mwanakwerekwe kwa mahojiano zaidi.

Alisema mara baada ya mahojiano, ofisa huyo aliwaamuru vijana hao wampatie Sh. laki mbili ili awaachie na chombo chao, vijana hao walimpatia shilingi laki moja na baadae kuwachiwa wao na kuendelea kukushikilia chombo chao.

Kwa mujibu wa sheria namba moja ya mwaka 2012 ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi afande huyo atakuwa amefanya kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu hicho cha sheria.

Alisema uchunguzi wa jalada hilo utakapokamilika litapelekwa kwa Mkurugenzi wa mashtaka kwa hatua za kisheria.

Kamanda wa Polisi Zanzibar, Muhammed Haji Hassan, alisema jeshi hilo halitamvumilia askari wake yeyote atakaebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Alisema jeshi la polisi linafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria zao hivyo wanapotokea wachache wenye dhamira ya kutaka kulichafua jeshi hilo ikiwamo kuomba rushwa hawatavumiliwa.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa jeshi hilo au mamlaka husika iwapo watagundua askari yeyote anajihusisha na rushwa kwa lengo la kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kukubali kutoa rushwa ni miongoni mwa vishawishi ambavo wakati mwingine huchangia kutendeka kitendo alichokiita adui wa haki.

Baada ya Alikiba kufunga ndoa Mbasha ajitupa kwa Jokate, ‘Usihofu yakwetu inakuja’

$
0
0
Baada ya msanii Alikiba kuoa, maneno mengi na maswali yamekuwa yakielekezwa kwa mrembo Jokate Mwegelo.

Sababu ni kwamba mara kadhaa mrembo huyo alidaiwa kuwa katika mahusiano na Alikiba, hivyo kitendo cha Alikiba kuoa mwanamke mwingine kilizidi kuibua mijadala ya hapa na pale kuhusu Jokate.

Sasa muimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amemuelezaJokate kuwa asijali kwa kuwa ndoa inakuja, hata hivyo haijafahamika iwapo ni yao wawili au laa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

“Usihofu Mungu hajakuacha Jokate Mwegelo yakwetu inakuja, tv zote zitakuwa live ukumbini hadi wasafi tv,” amesema Mbasha.

Katika kuhadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa March 20, 2018 Jokate aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa ingawa hakuweka wazi ni nani atahusika katika ndoa hiyo.

Utakumbuka pia muimbaji Mbasha kwa sasa hayupo katika ndoa na hii ni baada ya kuachana na aliyekuwa baby mama wake, Madam Flora ambaye aliolewa April 30, 2017 na Daudi Kusekwa.

Waziri Tizeba Aagiza Mkurugenzi Wa Bodi Ya Korosho Kusimamishwa Kazi

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
Waziri wa wizara ya kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kusitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndg Hassan Jarufo.

Waziri Tizeba ametoa agizo hilo kwa katibu mkuu wa wizara hiyo  Jumamosi 21 Aprili 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma ikiwa ni muda mchache mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Akielezea sababu za kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, Mhe. Dkt Tizeba alisema kuwa hayo yamejili baada ya kuangalia mwenendo wa Ndg Jarufo na kutafakari jinsi zao la korosho linavyoendeshwa, ikiwa ni pamoja na kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati.

Aidha, Mkataba huo umesitishwa kuanzia leo tarehe 21 Aprili 2018 hivyo Katibu Mkuu wa wizara hiyo atapaswa kufanya taratibu zote za kiutumishi ikiwa ni pamoja na kumpatia taarifa haraka muhusika na utekelezaji wake kuanza haraka.

Alisema ndani ya muda mfupi Wizara ya kilimo itamtangaza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo ili kuchukua nafasi hiyo kuendeleza kusimamia sekta hiyo.

“Hizi hatua tunazochukua ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi kwani pamoja na kuondolewa Mkurugenzi huyo lakini shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo” Alikaririwa Mhe. Dkt Tizeba

Kigwangalla: Sitaki Kuona Askari Mwenye Kitambi

$
0
0
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala ametuma salamu kwa majangilli wanaojihusisha na uwindaji haramu wa wanyama kwenye Hifadhi za Taifa ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Amesema Serikali na wadau wengine wamejipanga kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa kwa kudhibiti ujangili wa wanyama na viumbe hai vyote vinavyotokana na maliasili yetu ya asili kwenye hifadhi za Taifa.

Dkt. Kigwangala alituma salamu hizo kupitia Mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika  jana Aprili 21, 2018 kwa kuanzia Lango Kuu la kuingilia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu mkoani Arusha.

Pamoja na kuwa mgeni rasmi kwenye mbio hizo, Dkt. Kigwangala pia alikimbia kilomita 21 kuanzia saa 3.30 asubuhi na kumaliza saa 6.20 mchana, na kusema hiyo ni ishara tosha ya kujipanga na kukabiliana na majangili. 

Dkt. Kigwangala alisema kwa kumaliza mbio hizo, sio tu anawatishia majangili kuwa yupo vizuri kukabiliana nao, bali anataka askari wote wa wanyama pole wawe wakakamavu na asimuone askari yeyote mwenye kitambi.

“Moja ya malengo ya mbio za Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu ni kupambana na ujangili na majangili. Na sikumaliza mbio hizi za kilomita 21 kwa bahati mbaya, bali ni kuwadhihirishia majangili na watu wote wenye nia mbaya na rasilimali zetu kuwa nipo fiti.

“Lakini sio kwa majangili, hata kwa askari wetu, nataka kuwaeleza kuwa kuanzia sasa sitaki kuona askari anakuwa na kitambi. Hatuwezi kupambana na majangili kama askari wetu wana vitambi na wapo legelege… Na nataka kuwaeleza askari kama wanataka twende nao pamoja kwenye hili basi wajipange” alisema Kigwangala.

Dkt. Kigwangala alisema nia nyingine ya NCAA kudhamini mbio hizo ni kutangaza shughuli za utalii ndani na nje ya nchi, kwani anaamini kupitia waandishi wa habari na washiriki wa mashindano hayo kutokea ndani na nje ya nchi, itawezesha kuongeza watalii na hifadhi hiyo kujulikana zaidi.
 
Naye Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka, alisema moja ya mambo yanayotushinda nchini ni kujitangaza, lakini hapo hapo kushindwa kupenda vya kwetu, kwani pamoja na kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, lakini matangazo yake mengi yapo Kenya.

Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alisema amefurahishwa na uongozi wa NCAA kudhamini mashindano hayo, kwani yatawezesha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kufahamika duniani kote.

“Kwenye Serikali ukiwa na mtu kama Dkt. Fred Manongi (Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) mambo yatakwenda vizuri. Tumempa taarifa wiki mbili kabla ya mashindano kumuomba atudhamini, lakini akawa amekubali na mambo yamekwenda vizuri.

“Hiki cha kukubali kudhamini mashindano haya ni kikubwa sana. Sasa anatufanya Watanzania tuanze kujitangaza na kupenda vya kwetu. Hili tatizo la kushindwa kujitangaza ni kubwa ndiyo maana kila siku kuna malalamiko kuwa Kenya wanajitangaza Mlima Kilimanjaro ni wa kwao. Sisi sasa tujitoe na kuonesha rasilimali hizi za utalii ni za kwetu” alisema Mtaka.

TMA: Mvua Itaanza Kupungua Jumatatu April 23

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema hali ya mvua katika maeneo mengi ya nchi itapungua kuanzia usiku wa leo Aprili 21, 2018.
 
Taarifa ya TMA iliyotolewa jana imesema maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
 
Pia, TMA imesema maeneo mengine ya mikoa yatakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
 
“Matazamio kwa siku ya Jumatatu Aprili 23, 2018, mvua inatarajiwa kupungua katika maeneo mengi ya nchi,”  imesema taarifa hiyo ya TMA

Mdogo wa Ali Kiba Naye Kafunga Ndoa

$
0
0
Alikiba ambaye siku ya alhamisi ya tarehe 19, April, 2018 alifunga ndoa na binti Aminah Rikesh kutoka nchini Kenya katika mji wa Mombasa ambapo inatarajiwa Alikiba kuirudisha sherehe hiyo nyumbani Tanzania tarehe 29. Siku hiyo Alikiba aliweka wazi mdogo wake Abdukiba kuwa ataoa karibuni.

Hatimaye ahadi hiyo ya Alikiba kuhusu mdogo wake imetimia kwani msanii huyo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ya 'Jeraha' amefunga ndoa pia na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika familia yao kama ambavyo mdogo wake wa kike Zabibu anavyosema kuwa mwanzo walikuwa wawili tu yeye na mama yake lakini ameongezeka mke wa Kiba na kudai anatarajia kuongezeka mwingine wa nne karibuni ambae ndiye mke wa Abdukiba.

Kupitia mtandao wa Instagram msanii H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina Alikiba ameweka wazi kuwa Abdukiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.

"Hongera sana Abdukiba kwakuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa nijambo la kheri" alisema H Baba

Alikiba na Abdukiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja April 29, 2018 jijini Dar es Salaaam ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa.

OFA: Jipatie Riwaya Kali za Kusisimua Toka kwa Mtunzi Makini

$
0
0
OFA OFA OFA OFA
Baada ya siku kadhaa za AIIISSII YOU KIILL kusimama, hadithi sasa ina endelea hewani. Kwa wasomaji wangu wa whatsapp leo hii 22/04/2018. Jipatie ofa ya hadithi ya Aiissii you kill me, ukinunua episode 20 ambazo ni sawa na sh 5000 una pata ofa ya episode 20 Bureeee kabisa. Pia season two ya AIISSII YOU KILL ME iitwayo AIISSII YOU KILL ME LEGACY kwa sasa ipo tayari.

Ukihitaji kuendelea na hadithi ya Tanga raha season two. Nina kukaribisha ujiunge kwenye group langu la hadithi whatsapp kupitia namba 0657072588 au 0768516188. Leo kuna ofa ina kusubiria, ukijiunga una pata ofa ya episode 80 buree kabisa. 

Katika group uta soma hadithi ya TANGA RAHA(return of Olvia Hitler) na hadithi ya SIN, kwenye group uta soma story kuanzia jumatatu hadi juma mosi. Ada ya group ni sh 4000 kwa mwenzi tu.
 
Karibubu sana wasomaji wangu.
By Eddy Msulwa.

PolePole: Kaanze kumtukana Babako

$
0
0
Leo April 22, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amewataka baadhi ya watu wanaokaa kutuhumu kuwa Rais amelisababishia Taifa hasara kuacha kwani wakiomba wathibitishe wengi husema ulikuwa ni mjadala Twitter.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Polepole ameandika “Ukimtuhumu Rais amelisababishia hasara Taifa ukaombwa uthibitishe utaweza au utasema yalikuwa tu majadiliano ya twita baada ya chakula cha mchana?”

“Huko barabarani defamation ni kosa kubwa, lakini mbona mnataka viongozi wetu wadhalilishwe kisha tukae kimya, kaanze kumtukana babako” -Polepole

Rais Magufuli aguswa na kifo cha Masogange

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia ya Agness Gerald Waya kufuatia kifo cha mtoto wao Agness alimaarufu kama Masogange kilichotokea Ijumaa.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia kwa Mwenyekiti Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Bw. Kheri James na kusema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha binti huyo kwani kifo chake kinapunguza idadi ya vijana ambao ndiyo jeshi na watu ambao wanaweza kufikisha mbali taifa.

"Kupitia jukwaa hili naomba nitoa salamu za Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye leo amewasili mjini Dodoma lakini ameomba niwasilishe kwenu salamu za pole kwa kuondokewa na kijana mwenzetu, 

"Mwenyekiti anafahamu nchii hii sisi vijana ndiyo warithi wa taifa hili sisi ndiyo tumebebe dira ya kulifikisha taifa ambapo tunadhani linafaa kufika hivyo anasikitishwa sana kuona katika jeshi kubwa kama hili la vijana tunapungukiwa na vijana wenzetu wanaondoka na kupunguza idadi ya askari wetu , naomba mpokee salamu za Mwenyekiti wetu" alisema Kheri James

Mwili wa Agness Masogange utazikwa jijini Mbeya nyumbani kwa wazazi wake Mbalizi

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0766340868

Baba Mzazi wa Agness Masogange Asimulia Alivyoagana na Mwanaye Muda Mfupi Kabla ya Mauti kumkuta

$
0
0
Gerald Waya, ambaye ni baba mzazi wa Agnes (Masogange), amesema mwanaye alikuwa nguzo katika maisha yake, hivyo ni pigo kubwa kwake na familia nzima.

Akizungumza nyumbani kwake Mbalizi II wilayani Mbeya, leo Aprili 22, 2018 Mzee Waya amesema Masogange ni mtoto wanne katika familia yake ya watoto sita, wa kike wakiwa watano.

Amesema Masogange alisoma Shule ya Msingi Utengule-Mbalizi na sekondari ya Sangu alikoishia kidato cha pili.

Waya amesema Masogange alipata matatizo hivyo akalazimika kuacha shule. Hata hivyo amesema hataki kuzungumzia mambo mabaya wakati huu anapoomboleza kifo cha mwanaye.

 “Aliishia form two (kidato cha pili), akapata matatizo ikabidi aache shule. Tulikosana kidogo lakini tukayamaliza yeye akaenda Dar es Salaam,” amesema.

Waya amesema, “Mwanangu alikuwa nguvu kwangu, alikarabati nyumba hii ninayoishi kwa sasa na nilikuwa nafarijika sana, lakini leo kusikia msiba huu kwa kweli inaniuma sana.”

Amesema Masogange alimpigia simu, “Tukaongea naye akaniambia ‘mimi baba ninaumwa’. Nikamuuliza nini tatizo akasema, “aah!   baba niombee tu kwa Mungu’. Na Jumamosi iliyopita nilimpigia simu wakati yupo hospitali kujua maendeleo yake lakini akaniambia ‘baba byee’.  Nikaanza kulia, na hapo sikuwasiliana naye tena hadi nilipopata taarifa za kifo chake,” amesema.

Msiba wa Masogange Wawakutanisha Diamond, Ali Kiba

$
0
0
Wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Ali Kiba wamekutana katika msiba wa Agnes Masogange na kusalimiana.

Mara baada ya wasanii hao kusalimiana kwa kupeana mikono wakiwa katika meza kuu, waombolezaji waliojaa kwenye Viwanja vya Leaders walipiga kelele.

Diamond alimsalimia Kiba kwa kumpa mkono, kisha wawili hao walikumbatiana na baada ya tukio hilo, MC Pilipili alisikika akisema: “Unaona sasa, hawana ugomvi hawa.”

Kumekuwa na taarifa za wanamuziki hao kuwa na ugomvi kwa muda mrefu ambao hata hivyo, unatajwa kutengenezwa na mashabiki wao wa ‘Team Kiba na Team Diamond.’

Akizungumzia katika viwanja hivyo, Ali Kiba ambaye ametoka kuchukua jiko hivi karibuni, amesema harusi na kifo vyote ni ibada na ndiyo maana amefika kuungana na waombolezaji wengine ingawa bado yupo fungate.

Masogange alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge ambako alilazwa kwa siku nne.

Picha: Mwili wa Agness Masogange ulivyoagwa Leaders Club

$
0
0
Wasanii mbalimbali leo wameungana na watu wengine katika kuuaga mwili wa marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam, ambapo baadaye leo atasafirishwa kupelekwa Mbeya nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi.

Mahakama Yamwachia Huru Nabii Tito

$
0
0
Mahakama  ya Wilaya ya Dodoma, imemfutia mashtaka ya kutaka kujiua na kuamuru akapatiwe matibabu ya afya ya akili katika Taasisi ya Mirembe Isanga, mkazi wa mtaa wa Ng’ong’ona Manispaa ya Dodoma, Onesmo Machibya (44), maarufu kama ‘Nabii Tito’.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo baada ya kupokea ripoti za vipimo vya afya ya akili ya Nabii Tito kutoka Mirembe Isanga, vinavyothibitisha kuwa ana ugonjwa wa akili.

Awali, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Kalayemaha, aliagiza kuwa Nabii Tito apelekwe katika taasisi hiyo ya magonjwa ya akili ili kupatiwa matibabu ya afya ya akili na mahakama imemwondelea mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.

Alisema katika ripoti ya kitabibu inaonyesha kuwa Nabii Tito kweli ana matatizo ya afya ya akili, hivyo anatakiwa kupelekwa katika taasisi hiyo ya Isanga Mirembe ili kupatiwa matibabu.

Mahakama hiyo, Februari 5, mwaka huu, iliamuru kuwasilishwa kwa vielelezo vinavyoonesha Nabii Tito ana matatizo ya akili na kufanyiwa vipimo katika Taasisi ya Afya ya Akili Mirembe Isanga kutokana na mshitakiwa kudai kuwa ana matatizo ya akili.

Akitoa maelezo ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha, Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana, aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na kuwasilishwa kwa taarifa kutoka Isanga.

Kutokana na maombi hayo, Hakimu Karayemaha alimuuliza mshtakiwa kama amekuja na vielelezo kama alivyoamriwa na mahakama hiyo.

Mshtakiwa huyo alimwambia Hakimu kuwa ametekeleza amri hiyo na kwamba tangu amri hiyo itolewe amekuwa mahabusu na hajapelekwa kwenye taasisi hiyo ya Isanga.

Hata hivyo, Hakimu Karayemaha alisema mshtakiwa huyo amewasilisha vielelezo vyake kutoka Hospitali ya Taifa ya Mhimbili na kwamba mahakama inahitaji taarifa kutoka Taasisi ya Mirembe Isanga kama ilivyoagiza.

“Mahakama ilitoa amri apelekwe Taasisi ya Mirembe Isanga kwa mujibu wa kifungu namba 219 (2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai,” alisema Hakimu hiyo.

Kifungu hicho kinasema kama mshtakiwa atabainika kuwa kweli ana matatizo ya afya ya akili, mahakama itaamua kuwa alivyofanya tukio hilo hakuwa na akili timamu hivyo hana hatia.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Karayemaha alimwamuru Mkuu wa Magereza ya Isanga kutekeleza amri ya Mahakama iliyotolewa ya kumpeleka kufanyiwa vipimo mshitakiwa huyo.

“Namwamuru Mkuu wa Magereza Isanga atekeleze amri ya mahakama ili taarifa za mshtakiwa ziletwe kwa tarehe itakayopangwa ambayo ni Machi 5, mwaka huu, tutataja kesi na kupokea taarifa ya vielelezo vya vipimo vyake kutoka Isanga,” alisema Hakimu.

Nabii Tito alikuwa anashtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kujikata na wembe na kujijeruhi kwenye maeneo ya tumbo Januari 25, mwaka huu katika mtaa huo wa Ng’ong’ona alipokwenda kukamatwa na polisi.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images