Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kesi ya Abdul Nondo yaahirishwa Mahakama ya Iringa

$
0
0
Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imeahirishwa leo (Jumatano).

Kesi hiyo imeahirishwa kutokana na hakimu kuwa na kesi nyingi na hivyo kuomba kupumzika.

Wakati huo huo upande wa Jamhuri ulifika na mashahidi wanne kati ya watano wanaotakiwa kutoa ushahidi huku mmoja akishindwa kufika mahakamani hapo.

Nondo anashtakiwa kwa makosa mawili ikiwemo kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni March 7 ya mwaka huu kuwa maisha yake yapo hatarini akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.

Kosa la pili limetajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini humo kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

Waliovunja kanisa na kuiba viti, vyombo vya muziki wakamatwa

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Misako na Doria za mara kwa mara ili kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na kuzuia matukio mbalimbali yakiwemo ya uporaji na ukabaji. 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendesha Misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya baada ya kupata taarifa za uwepo wa vitendo vya uhalifu wa kuvunja Makanisa nyakati za usiku na kuiba mali mbalimbali zilizomo katika Makanisa. 

Misako hii ilianza mnamo tarehe 31.03.2018 na ilifanyika katika maeneo mbalimbali ndani ya Jiji la Mbeya na katika Wilaya ya Rungwe ilifanyika maeneo ya Kiwira na Wilaya ya Mbarali ilifanyika katika maeneo ya Igurusi.

Katika Misako hiyo, watuhumiwa watatu walikamatwa kutokana na kuhusika katika matukio ya uvunjaji na kuiba Makanisani nyakati mbalimbali. Watuhumiwa hao ni:-
  1.  WILLIAM SANKE [23] Mkazi wa Isanga
  2. ELIUDI MWANSULE [28] Mkazi wa Mwakibete Viwandani
  3. NOA MOLELA [26] Mkazi wa Mama John
Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuhusika katika matukio ya kuvunja na kuiba Makanisani nyakati mbalimbali na mara baada ya kuiba mali hizo huwapelekea wauzaji ambao pia wamekamatwa. 

Watuhumiwa hao ni:-
  1. HURUMA JOHN [52] Mkazi wa Igurusi Wilaya ya Mbarali
  2. HALID MWANGOKA [37] Mkazi wa Igurusi Wilaya ya Mbarali
  3. GODFREY MWALIMBA [28] Mkazi wa Mwakibete
  4.  GWAMAKA MWAIKAMBO [32] Mkazi wa Mwakibete
Baada ya kuhojiwa watuhumiwa wote walikiri kupokea mali hizo kutoka kwa mtuhumiwa WILLIAM SANKE na wenzake na baada ya kuzipokea huziuza kwa watu mbalimbali.

Misako hii imefanikisha kupatikana kwa mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
  1.     Spika kubwa 15 za aina mbalimbali
  2.     Mixer 08
  3.     Amplifier 01
  4.     Viti vya Plastic 108 vya rangi mbalimbali.
Watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kupambana na wahalifu wanaojihusisha na dawa za kulevya. 

Kutokana na taarifa za kiintelijensia mnamo tarehe 11.04.2018 majira ya saa 17:00 jioni tuliweza kubaini kuwa huko maeneo ya Mlima James, Kiwanja kilichopimwa Plot Na.2590 Kitalu X Mwakibete, Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, jiji na Mkoa wa Mbeya kuwa kuna wakulima ambao wanalima mazao mbalimbali kwa kuchanganya na miche ya Bhangi ipatayo 83.

Miche hiyo iling’olewa na wananchi wa eneo hilo kwa kushirikiana na viongozi wao wa Serikali za Mitaa chini ya usimamizi mkali wa Jeshi la Polisi. Jitihada za kumtafuta mhalifu wa tukio hili zinaendelea.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU anatoa wito kwa jamii kuachana na tamaa ya mali hasa kwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu ili wapate mali na badala yake wafanye kazi halali. 

Aidha Kamanda TAIBU anaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukulia dhidi ya wahalifu. 

Pia Kamanda TAIBU anawasihi wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake kuachana na tabia ya kilimo cha Bhangi kwani watakaokamatwa watahusika wenyewe katika kuteketeza mashamba hayo lakini pia sheria kali itachukuliwa dhidi yao.

Mbunge aitaka serikali ibatilishe ndoa za walio chini ya miaka 18

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu, Kiteto Koshuma ameitaka serikali kutamka wazi kuwa wanawake walioolewa chini ya miaka 18, ndoa zao ni batili.

Koshuma ametoa kauli hiyo leo Aprili 18 bungeni wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2018/19.

Amesema sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1972 inakwenda kinyume makubaliano ya kimataifa.

Mbunge huyo ametoa masikitiko kuwa serikali haiwatendei haki wanaharakati ambao walipeleka kesi ya kupinga sheria hiyo mahakamani na wakashinda lakini serikali imekata rufaa.

Serengeti: Wakatana mapanga hadi kufa, kisa wivu wa mapenzi

$
0
0
Mtu mmoja amefariki dunia na wawili kujeruhiwa baada ya kukatana kwa visu na mapanga katika ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi uliotokea katika Kitongoji cha Kirenero wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alisema tukio hilo limetokea jana Aprili 17, 2018 asubuhi katika kitongoji cha Kirenero kijiji cha Kichongo wilayani Serengeti mkoani Mara.

Amemtaja aliyefariki kuwa ni Kibure Samwel (39) ambaye alichomwa kisu tumboni na kifuani wakati Nyang’anyi Waitara (44) mkazi wa Itununu, katika tukio hilo alikatwa mkono.

Munge Samwel (44) kaka wa marehemu alikatwa pajani na mtuhumiwa.

Amesema chanzo ni wivu wa mapenzi kwa kuwa mwanamke ambaye awali alikuwa mke wa Waitara kwa sasa ameolewa na Munge.

Kamanda huyo amesema tangu mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina aolewe na Munge kumekuwa na mgogoro baina yao kuhusiana na hilo, na walipokutana inadaiwa walianza kushambuliana kwa maneno kisha kuanza kukatana.

“Aliyekufa ni mdogo wake na Munge Samwel ambaye katika ugomvi huo alifika kwenye tukio na kukuta kaka yake anashambuliana kwa silaha na Waitara, akaamua kuchukua panga kumsaidia ndipo mtuhumiwa akamchoma tumboni kisha kifuani na kufa papo hapo,”alisema.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Joseph Mwita alisema mgogoro huo ni wa muda mrefu ambapo Waitara alimshutumu Munge kuwa chanzo cha mgogoro wa ndoa yake mpaka mke akamfikisha mahakamani na kuomba talaka.

“Waitara (mtuhumiwa) aligoma kurudishiwa mahari na Munge ili amchukue mke wake kwa madai kuwa ameshazaa naye watoto watatu, hali iliyomlazimu Munge kumhamishia mwanamke huyo Tarime kwenye mji wake mwingine,” alibainisha.

Rais Magufuli Amteua aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu UDOM, Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

Mawaziri, Msukuma Wampinga Makonda

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria,  Palamagamba Kabudi ameikosoa kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake wenye watoto waliotelekezwa na waume zao  na kusema kwamba ilipaswa kufanyika kwa faragha.

Kabudi ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kuhoji uhalali wa kampeni hiyo.

Profesa Kabudi amesema shughuli hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika kwa faragha si kama inavyofanyika sasa.

Wakati Kabudi akisema hayo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha.

Ndoa ya Alikiba kufungwa kesho alfajiri

$
0
0
Ndoa ya mwanamuziki Alikiba na mchumba wake Amina inatarajiwa kufungwa kesho alfajiri katika msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo jijini Mombasa.

Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Bi Asma Said anasema ndoa hiyo itafungwa katika msikiti huo uliojengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.

Anasema baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.

Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Ommy Dimpoz.

Bi Asma anasema maandalizi yanaendelea vizuri na nyumbani kwa bibi harusi mwandishi alishuhudia wanawake wakiwa wanajipamba huku wengine wakijipaka henna.

Alibainisha kuwa tayari bwana harusi ameingia nchini Kenya huku wadokezi wakisema kuwa Alikiba alikuwa katika hoteli ya English Point Marina ambapo ni karibu na nyumba ya bibi harusi iliopo eneo la Kongowea.

“Kijana ametoka Tanzania na kuja kuoa Kenya mimi sikujua kama mtoto wangu ataolewa na Alikiba lakini Mungu ndio aliyepanga,” akasema Bi Asma.

Walichokibaini BASATA baada ya kumhoji Diamond

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limeeleza kuwa, baada ya kufanya mahojiano na msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, wamebaini kuwa vijana wengi hawana elimu juu ya sheria mpya ya mitandao iliyowekwa.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 18, Katibu wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa baadhi ya watu wanaona kama msanii Diamond amelewa umaarufu jambo ambalo sivyo kama wanavodhani.

“Watu wanaweza kuchukulia hiyo kwamba Diamond amelewa umaarufu, amelewa mafanikio. Lakini mimi niseme kama baraza na masimamizi wa wasanii wote, tusimhukumu mtu kabla hatujamsikiliza wala kuongea nae. Sidhani kama ni umaarufu uliompelekea Diamond kufanya mambo kama hayo,” ameema Mngereza.

Mngereza amesema sababu kubwa ya wasanii na vijana wengi kufanya makosa ya kimtandao ni kutokana na sheria hiyo kuwa mpya kwao na hivyo kutaka elimu ya kutosha juu ya sheria hiyo kutolewa ili iweze kueleweka na kufuatwa.

“Kwa vijana wengi wa kitanzania ni sheria mpya. Tunahitaji kuwaelimisha zaidi kwamba kuweka picha au clip za aina hii hazikuongezei umaarufu,” amesema.

hatua hii imekuja ikiwa ni siku chache baada ya msanii Diamond kushikiliwa na Jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano, baada ya kuweka katika mtandao wa instagram video zinazomuonyesha akiwa katika faragha na mama watoto wake, Hamisa Mobeto.

Hatua hiyo iliibua maswali mengi kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wa muziki wake, kwani tukio hilo limetokea siku chahe baada ya kuvuja kwa video iliyowaonyesha msanii Nandy na Bilnass nao wakiwa katika faragha.

Jambo hili liliwafanya watu wengi kuibuka na mwaswali, huku wengine wakidhani ni ‘kiki’ ambayo ingefuatiwa na kuachiliwa kwa wimbo ama video mpya kutoka kwa wasanii hao.

Hata hivyo, wasanii hao wote, Diamond, Nandy, Bilnass pamoja na mwanamitindo Hamisa Mobetto walishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano yaliyochukua muda wa saa kadhaa, kisha kuachiliwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Diva Ammwagia Mvua Ya Matusi Ya Nguoni Michael Lukindo

$
0
0
Msanii na mtangazaji wa kipindi cha Ala za roho cha Clouds Fm Loveness Malinzi ‘Diva The bawse’ amemtolea povu zito msanii mwenzake wa Bongo fleva Michael Lukindo ‘ML’ baada ya kudai ni wapenzi.

Siku chache zilizopita Michael Lukindo alifanya mahojiano na XXL ya Clouds Fm na alikuwa anatambulisha ngoma yake mpya lakini Kwenye mahojiano hayo alifunguka kuwa yupo Kwenye Mahusiano na Diva.

Baada ya kusikia taarifa hizo Diva alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumwaga povu zito na kukataa kata kata kama yupo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Michael Lukindo.

Baada ya Tetesi hizo kusambaa Soudy Brown alimsaka Michael ambaye alikiri kuwa alikuwepo Kwenye Mahusiano na Diva lakini walifanya siri na mpaka sasa Diva hayupo tayari kuzungumzia hayo mahusiano.

Baada ya kusikia maneno hayo Diva ambaye kwa muda huo alikuwa studio alimtolea matusi mazito Michael Lukindo:

"Wewe mata** unikome shika adabu yako umeshawahi kuwa na Mahusiano na mimi lini na wapi?na nilikwambia kabisa kwamba nimekushtaki I have defamation letter for you utajifunza kufunga huo mdomo wako sitaki mambo ya kise*** k*** la mama ako umeenda umemzungumzia Jokate on the same same thing haukutosheka ukamuandika Miriam Odemba kuwa una Mahusiano naye sasahivi unataka kwangu mimi kunitafutia kiki sasa mimi ntakukomesha nimeshakushtaki”.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 19

Serikali Yataifisha Basi na Magari ya Kifahari

$
0
0
Serikali imetaifisha dhahabu ya mabilioni ya shilingi na magari ya kifahari kutokana na wahusika wake kukamatwa na kuhukumiwa kwa makosa ya rushwa katika mwaka huu wa fedha.

Pia imetaifisha, pikipiki, mafuta, mashine za kuhesabia fedha na basi la abiria lililokuwa linatumika kusafirisha meno ya tembo.

Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi, aliyasema hayo jana alipowasilisha bungeni mjini hapa hotuba ya makadirio ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha.

Alibainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha, mali zilizotaifishwa kwa ujumla wake zinakadiriwa kuwa na thamani ya Sh. bilioni 5.685.

Waziri huyo alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ilipokea majalada 683 ya tuhuma za rushwa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru).

Prof. Kabudi alisema kati ya hayo, majalada 288 yaliandaliwa hati za mashtaka na 275 yalirudishwa Takukuru kwa uchunguzi zaidi.

Alisema majalada 115 yako katika hatua mbalimbali yakifanyiwa kazi na mengine matano yalifungwa.

"Washtakiwa waliotiwa hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa ambapo jumla ya Sh. bilioni 4.484 zilitozwa kama faini kutoka kwa washtakiwa," alisema na kuongeza:

"Mali zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu zenye thamani ya Sh. bilioni 2.012 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya Sh.milioni 908.092.

"Mali zingine zilizotaifishwa ni magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika Bandari ya Dar es Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba, pikipiki 34, mafuta, mashine za kuhesabia fedha na basi la abiria lililokuwa linasarifirisha meno ya tembo."

Prof. Kabudi alisema mwaka huu wa fedha pia mali za vyama vya ushirika vya Mwanza (Nyanza Cooperative Union) na Shinyanga (Shirecu) zikiwamo nyumba, viwanja na viwanda, zimerejeshwa serikalini kutoka mikononi mwa watu ambao walizichukua bila kufuata utaribu wa kisheria.

Waziri huyo pia alisema mwaka huu wa fedha kulikuwa na mashauri sita yanayohusu ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi yaliyoshughulikiwa.

Alisema kuwa kati yake, mashauri manne yalikamilika kwa watuhumiwa kutiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu za kifungo cha kati ya miaka minne hadi 20 na mashauri mawili yaliyobaki yanaendelea kusikilizwa.

Kikwete, Ridhiwan washindwa kuhudhuria harusi ya Ali Kiba

$
0
0
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wameshindwa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba anayefunga  ndoa na mchumba wake, Amina Rikesh kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Hayo yameleezwa na mtoto wa Rais Kikwete na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiwa mjini Dodoma anapohudhuria vikao vya Bunge.

Ridhiwan amesema kuwa, walipewa mwaliko wa kuhudhuria harusi ya mwanamuziki Ali kiba, lakini Rais mstaafu Kikwete kwa sasa anahudhuria shughuli nyingine Marekani, naye Ridhiwani anahudhuria vikao na shughuli mbalimbali bungeni mjini Dodoma hivyo hawataweza kuhudhuria harusi ya mwanamuziki huyo Kenya.

Ruby Akiri Kuvutiwa na Jux

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Ruby amefunguka na kuelezea mapenzi yake kwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Juma Jux Kwenye upande wa uimbaji wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Ruby amekiri kuwa anavutiwa sana na uimbaji wa Jux hasa kwa sababu nyimbo zake nyingi zinawagusa wanawake huku akitaja wimbo unaoikonga sana nyoyo yake ni utaniua:

"Kwa sababu nyimbo za Jux karibia zote zinawashika kwanza wanawake, halafu pia uimbaji wake ni RnB ambayo anaweza kuimba mwanaume au mwanamke, kwa hiyo nafikiri ule uliniingia zaidi”.

Jux ameonekana kama moja kati ya wasanii wa kiume ambao wanavutiwa sana na mabinti kwani kuna watu maarufu kadhaa waliokiri kuvutiwa na Jux akiwemo Socialite maarufu kutoka Kenya anayejulikana kama Huddah na hata Amber Lulu.

Ruby amerudi kwa kasi ya ajabu Kwenye muziki na hivi sasa anafanya vizuri kwa wimbo wake wa One and only alioshirikishwa na Nedy Music.

Rais Magufuli Awajulia Hali Wagonjwa Waliolazwa Katika Taasisi Ya Moyo Ya Jakaya Kikwete .......Awapongeza Madaktari Kwa Kazi Nzuri

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Jijini Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo.

Mhe. Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli ametoa pongezi hizo hizo tarehe 18 Aprili, 2018 alipotembelea taasisi hiyo na kuwajulia hali wagonjwa wanaopatiwa matibabu akiwemo Waziri Mstaafu Dkt. Juma Ngasongwa.

Mhe. Rais Magufuli amesema JKCI ambayo imepata mafanikio katika matibabu ya moyo kwa njia ya upasuaji wa tundu dogo na kufungua kifua imesaidia kuokoa vifo kwa Watanzania wengi waliokuwa wanakosa uwezo wa kifedha wa kwenda kutibiwa nje ya nchi, imepunguza gharama za kutibiwa nje ya nchi na imeijengea heshima Tanzania.

“Prof. Janabi, madaktari wote na wauguzi wa taasisi hii nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, natambua kuwa wapo baadhi ya waliokuwa wananufaika na wagonjwa kupelekwa nje ya nchi hawatafurahia kazi mnayoifanya lakini nyinyi chapeni kazi na Serikali ipo na nyinyi” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuitembelea taasisi hiyo na kuwatia moyo na ameahidi kuwa wataendelea kuchapa kazi kwa juhudi ili kuimarisha zaidi huduma za matibabu ya moyo.

Amefafanua kuwa JKCI imefanikiwa kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wanakwenda kutibiwa nje ya nchi kwa asilimia 83 na kwamba tangu mwaka 2015 idadi ya wagonjwa waliotibiwa katika taasisi hiyo ni zaidi ya 2,420 ambao wangehitaji wastani wa Shilingi Milioni 30 kwa kila mmoja kutibiwa nje ya nchi.

Kabla ya kutembelea JKCI Mhe. Rais Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli wamekwenda Kariakoo Jijini hapa kutoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo ambaye amefiwa na Mama yake Bi Rehema Paulo Mombuli, ambaye mwili wake unasafirishwa kwenda Arusha na baadaye Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Fursa Za Mafunzo kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika

$
0
0
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za mafunzo ya muda mrefu kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).

Mafunzo hayo ambayo yapo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu yatatolewa katika kozi mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi, Sayansi ya Afya, Usimamizi wa Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo, Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi wa Maji na Nishati.

Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na  miaka isiyozidi  30 kwa waombaji  wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji wanawake. Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.

Maombi ya mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua pepe ya pau-au.net. 

Mwisho wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili, 2018. Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia pau.scholarships@africa-union.org au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam

18Aprili, 2018

Wema Sepetu Awatoa Machozi Mashabiki Wake

$
0
0
Staa wa bongo movies Wema Sepetu amewaacha watu katika mshangao na kuchanganyikiwa baaada ya kuweka posti ya kusikitisha inayohusu mwanamke ambae alipata tatizo la kuharibika kwa mimba.

Watu wamekuwa wakijiuliza je post hiyo inamkumbusha mimba iliyoharika kipindi cha nyuma au ni mimba nyingine imeharibika tena.

Watu wengi wameonekana kuguswa na jambo hilo na kusema kuwa Wema anapitia kipindi kigumu sana kwa sasa kutokana na hamu yake kubwa ya kutaka kuwa na mtoto lakini inashindikana.

Wema aliweka picha hiyo katika ukurasa wake wa instagram na kuandika “Story of my life”

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Kwa Nini Wanaume Wengi Wanaupungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo?

$
0
0
Asilimia 45 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kuwatimizia vyema wake au wapenzi Wao na kuwasababishia kutoka nje ya ndoa zao.

NINI CHANZO CHA HAYO?Kupiga punyeto,Ngiri,Vidonda vya tumbo,Magonjwa ya moyo,Presha,Kisukari,Korodani moja kuvimba,Msongo wa mwazo,Kufanyiwa tohara ukiwa mtu mzima n.k.DOKTA MANYANDA sasa kapata tiba sahihi ya tatizo la NGUVU ZA KIUME.

MUHAMA:Hii hutibu na kuponyesha kabisa tatizo la nguvu za kiume,utakuwa na uwezo wa kurudia tendo zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dakika 15-20.DAWA hii imechanganywa miti 12.Hata wazee wenye umri mkubwa wanapona kabisa.OKO NDOA YAKO SASA. 

MANGUNGU MIX: Ndio tiba tosha kwa sasa ambayo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo inch 1-8 na unene sentimita 1-5,dawa hii ipo ya kupaka na kunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji.

NITOFAUTI NA ULIZO WAHI KUZITUMIA.Pia tuna dawa za kupatanisha mke,mme,mpenzi au bosi wako kwa mda mfupi sana,Uzazi,Kusafisha nyota,

Je unamali yako unauza hupati wateja?Wasiliana nami 0716-263605 

DOKTA MANYANDA ANAPATIKANA KASULU KIGOMA,Kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote pale.

Trump atishia kususia mazungumzo na Kim Jong Un

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong un hayatazaa matunda basi ataachana na mazungumzo hayo.

Katika mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, Trump na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe wamesema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti liendelee kwa kukataa kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Vile vile, Trump amethibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong Un.

Hata hivyo, kwa upande wake waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amemtaka rais Trump kusaidia kuachiwa huru kwa raia wa Japan waliotekwa nyara na Korea Kaskazini miaka ya 1970 na 1980.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images