Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mimi Mars Kurejea Kwenye Utangazaji Tena

$
0
0
Msanii wa Bongo Flava kwa sasa, Mimi Mars amefunguka kuhusu kurejea katika utangazaji wa TV.

Muimbaji huyo aliyekuwa akitangaza kipindi cha Weekend Gossip kupitia TV 1 amesema mipango ya kurejea katika utangazaji ipo ila bado ni vigumu kuweka wazi ni kipindi gani hasa.

“Mipango inafanyika kikubwa ni ku-keep up na mimi na watajua na watapata kusikia ni lini, wapi na sehemu gani,”

Katika hatua nyingine amezungumzia maisha ya muziki na yale ya utangazaji, utofauti upo wapi.

“Hamna utofauti kwa sababu kile kipindi watu walikuwa wanakifurahia, kusema kweli kile kipindi ndio kilinianzisha watu waweze kujua Mimi Mars ni nani na mashabiki wangu wengi nimewapata kupitia kipindi kile hadi nilipoingia kwenye muziki,” amesema Mim Mars katika mahojiano na Bongo5

Mimi Mars ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ‘Papara’ ana historia yenye kushabiana na ile ya dada yake, Vanessa Mdee ambaye awali alikuwa mtangazaji wa MTV Base na Choice FM kabla ya kuingia katika muziki.

Serikali Kuajiri Walimu 6,000 June

$
0
0
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), imesema hadi kufikia Juni 30 mwaka huu inatarajia kuajiri walimu 6,000 wa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali, ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuondoa changamoto katika shule za kata ikiwamo upunguzu wa walimu wa Hisabati na Sayansi.

Pia, Bobali alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu wananchi kuchangia kwenye chakula ambacho wameona ndio chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi katika Mkoa wa Lindi. Alisema hadi Desemba mwaka 2017, Serikali ilikuwa imeajiri walimu 200 wa Hisabati na Sayansi kwa ajili ya shule za sekondari.

Kadhalika, alisema serikali haijazuia wananchi kuchangia maendeleo ya shule walichokataza ni kumzuia kumpa adha ya kukosa masomo mwanafunzi ambaye ameshindwa kuchangia michango hiyo.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alitaka kujua kama serikali imefanya tathmini juu ya ubora na changamoto zilizopo katika shule za sekondari za kata nchini.

Akijibu Kakunda alisema hadi Oktoba 2017, Shule za kata 3,103 zilikuwa na wanafunzi 197,663 ambao kama zisinge kuwepo wangeikosa elimu ya sekondari.

Kakunda alisema maamuzi ya kuanzishwa kwa shule ya sekondari kila kata ili kuhakikisha watoto wengi zaidi waliokuwa wanakosa nafasi za masomo ya sekondari licha ya kufaulu mitihani ya darasa la saba kwa sababu tu ya uchache wa shule wanapata nafasi hizo.

Alisema tathmini mbili za serikali zilizochambua kwa kina sekta ya Elimu kupitia Tume ya Prof. Mchome ya mwaka 2013, iliyochambua sababu za ufaulu hafifu wa wanafunzi kwenye mitihani ya mwaka 2012 na kamati ya kuhuisha na kuoanisha sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995, Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996.

Pia alisema sera ya Taifa ya Elimu ya juu ya mwaka 1999 na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa elimu ya msingi ya mwaka 2007, iliyoongozwa na Mwalimu Abubakar Rajab mwaka 2013, ndizo zilizobaini na kuishauri serikali kuanzisha sera mpya moja ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.

“Sera mpya imetoa maelekezo mahususi kuhusu namna ya kuboresha elimu ya awali, msingi, sekondari, elimu ya ufundi na elimu ya juu na mitaala imesharekebishwa, ikama, vifaa, samani na miundombinu vyote vinaendelea kuboreshwa,” alisema.

Irene Uwoya Ammwagia Maneno Matamu Dogo Janja....Awashangaa Wanaosema ni Mdogo

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka mazito kwa mumewe staa wa Bongo fleva Dogo Janja ambapo amedai kuwa ni moyo wake na kukiri kuwashangaa watu wanaosema yeye ni mdogo.

Ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya ilishangaza watu wengi ilipofungwa mwaka jana mpaka hivi sasa kuna watu ambao hawaamini kuwa wawili hao wameoana.

Na imekuwa ngumu kwa watu wengi kuzoea Mahusiano hayo hasa kwa sababu tofauti kubwa iliyopo baina yao kuanzia umri mpaka vitu vingine ambavyo vinaonekana baina yao.

Lakini kadri siku zinavyozidi kuenda wapendanao hao wameendelea kuuthibitishia uma wa Watanzania kuwa wanapendana na watazidi kuwa pamoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya kamfungukia mazito mumewe Dogo Janja ambapo amekiri kuwa anampenda mumewe na kusema anawashangaa watu ambao wanekazana kumsema ni mdogo kwani yeye anamuona mtu mwenye akili sana:

"Nakupenda sana sijawahi kukutana na mwanaume mwenye akili kama wewe na muelewa kama wewe….mdogo lakini mmmnh mimi ndio ninajua ndio maana wakiongea nawaangalia tu nasema iiiiii Dogo Janja wewe ndiye moyo wangu”.

Dogo Janja naye anaonekana amekolea na penzi la Irene kwani mara kwa mara anamposti mkewe na kumwagia sifa lukuki kama mke mwema na mwaminifu na kadhalika.

Mvua zaendelea kuleta madhara nchini

$
0
0
Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbali mbali nchini zimeendelea kuleta madhara mkoani Rukwa, ambapo zimesababisha uharibifu wa mashamba ya vyakula na kuharibu mazao.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa, George Kyando ambapo amesema kuwa mvua hizo zimezoa mazao kwenye mashamba mkoani humo na mengine kuyafunika kwa udongo, hali ambayo imeleta hasara kwa wakulima.

Kamanda Kyando amesema kuwa barabara mbalimbali zimekatika na kukosa mawasiliano, huku baadhi ya madaraja yakizolewa na maji lakini hakuna taarifa ya vifo waliyoipata mpaka sasa.

“Huku Rukwa kuna barabara inayopita bonde kwa bonde kutoka mkoa wa Rukwa kwenda Katavi, kutokana na hizi mvua zinazonyesha madaraja yamechukuliwa na maji, barabara zimekatika, mashamba ya mipunga na mahindi yamefunikwa na udongo, kwa hiyo tumepata hayo majanga lakini tunashukuru Mungu hakuna mtu yeyote ambaye amedhurika na hiyo mvua, ni miundombinu na mashamba tu,”amesema Kyando

Hata hivyo, kutokana na mvua hizo Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imewataka wananchi kuwa makini wanaposafiri na kutembea, kwani mvua kubwa zaidi inatarajiwa kunyesha siku za hivi karibuni.

Mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani George H W Bush Afariki Dunia

$
0
0
Mke wa rais wa 41 wa Marekani, George H W Bush, mama Barbara Bush ambaye pia alikuwa mwanaharakati amefariki dunia.

Mama Bush ambaye pia ni mama wa rais wa zamani wa Marekani, George W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 92.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na ofisi ya rais, George H W Bush na ilieleza kuwa kifo chake kimetokana na matatizo ya kiafya.

Aidha, mara kadhaa mama Bush alilazwa hospitalini mara kwa mara ambapo siku ya Jumapili aliamua abakie nyumbani akiwa na familia yake.

Januari mwaka 2017, yeye na mumewe rais mstaafu Bush walilazwa kwa wakati mmoja. Yeye alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya koo, huku mumewe akitibiwa kwa ugonjwa wa nimonia.

Mama Bush ni mmoja kati wanawake wawili tu nchini Marekani, kuwahi kuwa mke wa rais na mama wa rais. Abigail Adams alikuwa mke wa John Adams, na mama wa rais John Quincy Adams, rais wa sita wa Marekani.

Okoa Ndoa Yako Sasa : Je Umepungukiwa Na Nguvu Za Kiume Au maumbile Au Mpenzi Wako Hakutimizii Utakacho?

$
0
0
Acha kujiona mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kwa sabubu ya kutokuwa na nguvu za kiume au uume wako mdogo dawa YA MAPRO POWERA ndio dawa sahihi na tiba tosha kwa sasa kutibu tatizo na kuponesha kabisa tatizo LA;
 1 KUWAI KUFIKA KILELENI KABLA YA MWENZI WAKO
2 KUSHINDWA KURUDIA TENDO LA NDOA NA MWILI KUCHOKA 
3 UUME KUSINYAA NA KUWA LEGELEGE 
4 KUUMWA NA TUMBO WAKATI UNAPOMALIZA KUFANYA TENDO

MAKAKANUA; HII NI dawa ya maumbili madogo...hufusha na kunenepesha saizi upendayo saiz 5-6-7-8 na unene sm 3-4-5

Tunarudisha mke au mpenzi ndani ya masaa matatu tu zipo dawa za presha kisukali vidonda vya tumbo korodani iliyovimba, dawa za uzaz,Mi tunapunguza matiti makubwa kitambi na mwili mkubwa dawa zipo 

FIKA OFISINI KWANGU MBAGALA ZAKHEMU. KWA WATEJA AMBAO AMTAKUWA NA NAFASI YA KUJA OFISINI AU MLIO MKOANI MTALETEWA. piga simu 0743362017. 0789234653 DR AGU

Polepole Amshambulia Zitto Kabwe Kwa Madai Kuwa Anapotosha Kuhusu Ripoti ya CAG....Ataka Achukuliwe Hatua

$
0
0
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey PolePole amefunguka na kuwavaa viongozi ambao wanazungumza juu ya ripoti ya CAG na kusema baadhi ya viongozi hao wanapotosha Umma kwa kusema mambo ya uongo.

Ameagiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watu wanaopotosha umma kufuatia ripoti hiyo ya CAG.

Polepole amesema hayo leo April 18, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema wapo viongozi wa vyama vya siasa hawazungumzi juu ya mambo mazuri yaliyofanywa na serikali kama ujenzi wa miundombinu na mambo wanayopiga hatua ila wamekuwa wakidakia mambo na kutoa taarifa za uongo.

 ”Kuna mtu mmoja anaongoza kwa upotoshaji juu ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Chama chake kina mbunge mmoja tu wa ACT Wazalendo. Sijui kasoma shule gani huyu. Kaja anasoma juu juu tu eti trilioni 1.5. Ana bahati ndugu Magufuli ni mpole ila tushawambia mwaka 2020 akatafute kazi ya kufanya. Pia arudi shule akasome kwani hakuna shilingi moja iliyopotea.

"Tunaweza tukakwambia tusaidie kuthibitisha sasa ukishindwa umesema uongo umeuhadaa Umma, umetoa takwimu za uongo ukichukuliwa hatua sio ndiyo utaanza kusema uongozi huu hatuna huruma, huruma kwa watu waovu? Waongo wanaopotosha kwa makusudi hilo halikubaliki".

Polepole katika mkutano huu ameeendelea kumtuhumu Zitto Kabwe  kushindwa kuwa na uhakiki wa maneno yake

"Kuna kipindi mtu huyu alizungumza kuhusu njaa, wewe unaijua njaa inatangazwa vipi sasa tumevumilia sana leo tumeshindwa tumeona tumsaidie kumuelewesha halafu tuseme wale ambao wana dhamana ya kuhakiki maneno tunayatoa kwa kweli wachukue hatua kwani hatupo tayari kuacha watu wachache waendelee kuudanganya umma wa watanzania hili halikubaliki" alisisitiza

Mwisho wa wiki iliyopita, Mbunge wa Kigoma Mjini kwa triketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliizungumzia kwa mapana zaidi taarifa ya CAG na kuonyesha mambo ambayo serikali imetuhumiwa kufanya ikiwa pamoja na upotevu wa fedha zaidi ya Trilioni 1.5 ambayo haina maelezo imetumikaje.

Aliyedai kuwa ni mtoto wa Lowassa atiwa mbaroni

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linamshikilia Fatma Chikawe 31 kwa kosa la udhalilishaji na kusababisha taharuki kwa jamii.

Kamanda  wa Polisi wa Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa amesema msichana huyo wananamshikilia na kumhoji kwa kosa la kumdhalilisha kiongozi mstaafu Edward Lowassa na kusababisha taharuki kwa jamii.

“Ni kweli tunamshikilia huyo msichana aliyejitokeza na kudai ni mtoto wa Lowassa hivyo tunamhoji baada ya kukiri amedanganya kwa makosa ya kumdhalilisha na kusababisha taharuki kwa jamii,”amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema wanaendelea na upelelezi na utakapokamilika watamfikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

Aprili 10 msichana huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa akitaka kupewa msaada wa kisheria baada ya kudai baba yake ni Edward Lowassa na toka azaliwe hajawahi kumuona baba yake.

Aprili 15 ilionekana video ya msichana huyo ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii akiomba radhi kwa kumdhalilisha Lowassa na kusema tukio hilo limechukuliwa kisiasa na sasa anakosa amani.

Mtalaam Na Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Nayaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume

$
0
0
Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni Sado 3 Mix Power,Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

Sado 4 Mix; Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI DR. ULIMWENGU BINGWA Anapatikana dar magomeni moroco hotel
SIMU NO; 0759 030343 / 0622790494

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Zitto Kabwe amjibu Humphrey Polepole. .....Asema yupo tayari kukamatwa na hata kuuawa

$
0
0
Baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey PolePole kusema Zitto Kabwe alidanganya kuhusu Ripoti ya CAG ya upotevu wa TRILIONI 1.5, Zitto amemjibu kwa kuandika  yafuatayo;

"Kuna mtu anasema nikamatwe kwa kupotosha Kuhusu TZS 1.5trn zinazohojiwa na CAG

"Mimi Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mwenyeji wa Kigoma, Muislam, NAAPA kwamba Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano imeshindwa kuonyesha kwa CAG matumizi ya shilingi trilioni MOJA na Bilioni MIA TANO

"Nipo tayari kukamatwa kwa kusema hivyo ( haitafuta ukweli wa ubadhirifu huo ). Nipo tayari kuuwawa kwa kusema hivyo ( mawazo yangu hayatakufa) , Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie"

Afisa utawala Chuo Kikuu cha Makerere afukuzwa baada ya kushitakiwa kwa kumdhalilisha Mwanachuo kimapenzi

$
0
0
UGANDA: Afisa Utawala Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Makerere, Bwana Kisuze Edward asimamishwa kazi baada ya picha yake akimnyonya mwanafunzi Racheal Njorogi sehemu za siri kusambaa mitandaoni

Racheal anadai aliwasili chuoni hapo kufuatilia taarifa zake za usajili ambapo alikutana na usumbufu mkubwa na baadaye alipopata nafasi ya kuingia ofisini kwa Msajili, alishangaa ghafla Afisa huyo akimvamia na kuanza kumnyonya matiti kisha sehemu zake za siri na alishindwa kumdhibiti kutokana na kumzidi nguvu

Kwa mujibu wa maelezo ya Racheal, anasema alilazimika kupiga picha (selfie) wakati tukio hilo likiendelea ili picha hiyo itumike kama ushahidi pindi atakapoenda kuripoti polisi

Tukio hilo limejiri ikiwa ni siku chache baada ya Rais Yoweri Kaguta Museveni kukemea vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo

Tiba ya Fangasi Sugu, Vidonda vya Tumbo, Kuondoa Chunusi na Nguvu za Kiume

$
0
0
MAKANGA 3 POWER: Hutibu nguvu za kiume dakika 10 na kupona  ndani ya siku 3. Huimarisha misuli ya uume iliyolegea, pia ipo dawa ya kurefusha uume mfupi nchi 4 handi nchi 7

Tuna tiba ya kudumu ya kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kuopata choo vizuri, busha( bila opareshen)

Pia tunatibu  kisukari, presha, muguu kuuma, fangasi sugu, vidonda vya tumbo, kupunguza unene, maziwa, kuondoa chunusi pete na cheni za bahati.

Onana na Dr. Shilindes shida zako zote zitakwisha.

Tupo Mbagala Rangi tatu:  0784460348  au 0659103360

Serikali yawasimamisha kazi mawakili sita

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mawakili sita wamesimamishwa kufanya kazi ya uwakili kwa miezi sita hadi miaka mitano kwa makosa ya nidhamu.

Kabudi ameyasema hayo leo bungeni wakati akiwasilisha mipango wa makadirio ya bajeti ya wizara ya Katiba na Sheria.

Amesema uamuzi huo umetolewa na kamati ya nidhamu ya mawakili baada ya kupokea malalamiko hayo

Profesa Kabudi, amesema kamati hiyo ilipokea malalamiko 18 ya mawakili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na hivyo kufanya jumla  ya malalamiko yaliyokuwa mbele ya kamati kufikia 48.

“Katika kipindi hicho, malalamiko 22 yalisikilizwa na kutolewa uamuzi ambako mawakili sita wamesimamishwa kazi ya kufanya uwakili kwa muda wa miezi sita hadi miaka mitano,” amesema.

Ametoa wito kwa mawakili wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakitambua kuwa wao ni maofisa wenye dhamana kubwa ya kufanikisha utoaji wa haki kwa wakati.

Waziri Jaffo Awataka Watumishi Kujitathmini Katika Utendaji Wao

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Serikali imewataka watumishi wa umma kujitathmini katika utendaji wao wa kuwahudumia wananchi wanyonge kwa matendo yao kama yanalingana na mwenendo wa mh. raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkta John Pombe Magufuli katika kuwahudumia wananchi wanyonge.

Kauli hiyo imetolewa jana na waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo wakati akizindua mnara wa magufuli kwenye chuo cha serikali za Mitaa Hombolo ambapo amewataka kuhakikisha wanajitathmini katika matendo yao ya kila siku katika kuwahudumia wananchi.

Amesema kuwa wanafunzi wanaosoma hapo wanatakiwa kuanza kujitahmini kimatendo kama wana uwezo na moyo wa kuitumikia jamii kwani wajibu wao wa kwanza kujua wanaenda kushughulikia kero za jamii.

"Nawasihi vijana kuanza kujiangalia na kujitathini kiutendaji wao kama wanafanana matendo yao na mh.rais ili kuweza kuisaida jamii kwani wajibu wa msingi ni kufanyakazi kwa bidiii" alisisitiza Jaffo.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa chuo hicho Suleiman Ngware  wazo la kujenga mnara huo utakaoitwa (MAGUFULI SQUERE) Lilibuniwa na bodi ya chuo lieweka mbele maslahi mapana ya utendaji wa umma katika kutoa huduma bora bila kuangalia wala kubagua wananchi kwa hali zao.

Amesema kuwa sehemu hiyo ni sehemu ya kuanza kujitathmini kwa matendo yetu ya kila siku katika kuhudumia wananchi na wanafunzi watakao toka hapa wana wajibu wakuwa mabalozi wazuri katika utumishi wao ili taifa lifikie malengo kusudiwa.

Nae Mkuu wa Chuo hicho Dkta Mpamila Madale amesema kuwa kila tarehe kumi nane chuoni hapo watakaa eneo la mnara huo kuangalia suala zima la utendaji na kujitathmini kama wamefikia malengo katika utendaji wao wa kila siku.

Amesema kuwa mnara huo lengo lake ni kuwa chemu chemu ya utendaji unaofanana na mh.rais kufikia maengo ya kutoa watumishi wenye uzalendo na nchi yao ili kila mtanzania ajue wajibu wake kwa nchi yake.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0766340868

Waziri: Huduma za Maji Zimeimarika....Teknolojia Kuondoa Matumizi ya Mkaa

Wawili wameongezwa kesi ya aliyekuwa Rais wa TFF

$
0
0
Leo April 18, 2018 Meneja wa Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya wameunganishwa katika kesi ya jinai inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzanke wawili.

Mahakama hiyo inatarajia kuanza kusikiliza kesi hiyo mfululizo kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka kuanzia May 14,17 na 21, 2018.

Washtakiwa hao wameunganishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri mara baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai kuomba kufanya mabadiliko ya hati ya mashtaka.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao upya 30 badala ya 28 yaliyokuwa yakiwakabili awali.

Mbali na Rais TFF, Jamal Emil Malinzi(57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF,  Nsiande Isawayo Mwanga(27).

Katika mashtaka hayo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za kimarekani 173,335 na Tsh 43,100,000.

Mwesigwa anakabiliwa na mashtaka sita  ya kula njama ,kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi  na utakatishaji fedha.

Mshtakiwa Nsiande anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji fedha, huku Zayumba akikabiliwa na mashtaka tisa ya kughushi na Frola anakabiliwa na shtaka moja la kughushi.

Baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo walikana na upende wa mashtaka ukadai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wakaomba kuwasomea maelezo ya awali.

Katika maelezo hayo ya awali washtakiwa walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo majina, nafasi zao za kazi na kuyakana maelezo mengine yote.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi May 14,17 na 21 ,2018 kwa ajili ya kusikilizwa.

Washtakiwa Zayumba na Flora walifanikiwa kupata masharti ya dhamana kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhamana kwa mujibu wa sheria.

Flora aliachiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh.mil 20, huku Zayumba akishindwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambao watasaini bondi ya Sh.milion 100 kila mmoja.

PICHA: Rais Magufuli katika msiba wa Mama mzazi wa RC Gambo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo April 18, 2018 amewasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kwa ajili kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli.

Manara Ampa Ushauri Mzito Wema Sepetu

$
0
0
Msemaji wa timu ya soka ya Simba Haji Sunday manara, amefunguka kuhusu umaarufu wa msanii wa filamu bongo Wema Sepetu,na kusema kwamba msichana huyo ni mrembo haswa lakini hajaweza kutumia umaarufu wake kutengeneza pesa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Television, Manara amesema anaamini Wema ni miongoni mwa wanawake wachache sana Tanzania ambao ni maarufu na warembo ambao wanaweza kusimamisha nchi, lakini hajatumia kipawa alichopewa, hivyo kwake ni sawa na bure.

“Wema ni msichana mzuri, mrembo, ni katika wasichana wenye nguvu sana na ushawishi Tanzania, ni mwanamke maarufu katika 'top 3' ya wanawake maarufu zaidi

" Anaweza akatumika hata katika matukio makubwa ya nchi, ni bado tu labda hajaweza kutumia hivyo vipawa Mungu alivyompa, kufikia mafanikio ya juu kabisa

"Naamini mwanadamu ukiwa maarufu wa kiwango kama cha Wema lazima uwe na kisu cha kufa mtu, sitaki umaarufu takataka halafu unakuwa mzigo huna”, amesema Manara .

Manara ameendelea kwa kusema kwamba anamshauri msanii huyo kutumia fursa ya umaarufu alionao kutengeneza pesa, kwani kipawa alichopewa cha kukubalika na kupendwa ni kikubwa zaidi.

Haji Manara : Wote ni CCM ila mimi maarufu kuliko Humphrey Polepole

$
0
0
Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa yeye ni maarufu zaidi nchini Tanzania kuliko Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.

Haji Manara amesema kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na Polepole anafanya kazi kama yake lakini hana jina kubwa kumzidi yeye kutokana na historia ya maisha yake na chama hicho.

Manara amedai kuwa CCM ndio chama kilichomsomesha nje ya nchi kuhusu masuala ya propaganda na ameshawahi kuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es salaam miaka ya 2007/10.

“Kwa upande wa siasa mimi ni mwanachama wa CCM haswa, nilikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam uongozi wangu ulikuwa 2007/10 

" Ilitokea tatizo ambalo ilibidi ifunguliwe kesi ya jinai kwangu, ilivyotokea nikafikiri 2010 tunaelekea kwenye uchaguzi na mimi ni msemaji wa chama changu cha CCM ndani ya Mkoa ndipo nikaamua kuandika barua ya kujiuzulu,“ameeleza Haji Manara kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kumtaja Polepole.

“Wote ni Makada wa CCM ila mimi ni maarufu zaidi, sisemi kwa kudhihaki mimi na Humphrey Polepole mimi maarufu, mimi ni kada wa chama cha mapinduzi na nimesomeshwa na CCM kwa wachina,  kuhusu Propaganda na nikikuambia hiki kikombe ni Kamera lazima utakubali ,“amesema Haji Manara.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images