Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Orodha ya wanajeshi waliopandishwa cheo na Rais Magufuli

$
0
0
Rais John Magufuli leo amewapandisha vyeo maofisa wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (JWTZ) akiwamo Meja Jenerali Peter Massao aliyepandishwa kuwa Luteni Jenarali.

Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo leo Aprili 12, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Meja Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maaofisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli (TMA) na kwa uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na maluteni jenerali wawili.

Wengine waliopandishwa vyeo na Rais Magufuli ni Brigedia Jenerali Henry Kamunde aliyepandishwa na kuwa meja jenerali.

Pia amewapandisha vyeo maofisa 27 wa JWTZ kutoka cheo cha kanali na kuwa brigedia jenerali na ofisa mmoja kutoka luteni kanali na kuwa kanali.

Waliopandishwa vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga, Z.S Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.

Wengine ni C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S Ismail, M.N Mkeremy, G.S Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E Gaguti.

Rais Magufuli Apata Mpambe Mpya

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameridhia na kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12, 2018 huku akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy ambaye amempandisha cheo na atapangiwa kazi nyingine jeshini.

Aidha, Rais pia amekukubali kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murunga na kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mkeremy.

Akitoa taarifa ya uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi, Jenelari Venancy Mabeyo amesema maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao watavalishwa vyeo vyao Ijumaa hii katika makamo makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es salaam.

Katika uteuzi huo Rais Magufuli amewapandisha vyeo maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa Jeshini.

Nandy Aomba Msamaha Baada ya Video Yake ya Uchi Kuvuja

$
0
0
Video ya msanii Faustina Charles maarufu Nandy inayomuonyesha akiwa faragha na mwanaume leo imezua gumzo mitandaoni ambapo mwenyewe amefunguka.

Nandy amekiri kwamba video hiyo ni ya kweli japo ni ya mwaka 2016 na kuwaomba Watanzania na Serikali msamaha kwa walichokiona.

Akielezea zaidi, amesema video hiyo ilichukuliwa akiwa katika uhusiano na mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva (jina tunalihifadhi), ambapo walikubaliana yawe ya siri.

“Sielewi ana maana gani kuitoa video hiyo kwa sasa na kufika kwenye mitandao, kwani ni vitu kama hivi vinafanyika kwa mtu yeyote anayekuwa kwenye mahusiano,” amesema.

“Nimesikitishwa sana na kitendo hicho na ‘ilishutiwa’ kwa mtindo wa ‘Snapchat’ na sijui kwa nini ameamua kuirushia sasa hivi, yaani sielewi nifanye nini.”

“Naomba radhi kwa mashabiki wangu, familia yangu, kanisani kwangu, Serikali kiukweli video imenichafua sana ila adhabu ya maumivu haya ninayoyapata sasa hivi ni kutokana na kumuamini mtu.”

“Sina cha kusema kwani hiki siyo kitu cha kwanza, kwani ni’shakuwa na mahusiano na mtu huko nyuma na akatishia kutoa picha zangu mpaka pale nilipoenda kuripoti polisi.”

Hata hivyo, Nandy amewaasa vijana kuwa waangalifu wanapokuwa katika uhusiamo kwani tukio hilo wengi wamelichukulia kama ‘kick’.

Waziri Mpango Apangua Hoja za CAG kuhusu Deni la Taifa

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema Tanzania inao uwezo wa kukopa ndani na nje ya nchi kutokana na viashiria vilivyopo.

Waziri Mpango ameyasema hayo leo Aprili 12 katika mkutano na wanahabari alipokuwa akijibu baadhi ya hoja zilizopo kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2017 mjini Dodoma.

“Tunapofanya tathmini ya uhimilivu wa deni la taifa, uwiano tunaouangalia siyo deni la taifa kwa pato la taifa peke yake, tunaangalia vigezo vingi,” amesema.

Amesema taifa lina uwezo wa kuendelea kukopa na si kwa kuangalia uwiano wa deni na pato la taifa peke yake.

“Takwimu nilizonazo ni za sasa, ile ripoti ya CAG ilikuwa inaishia 2017. Nitawapa taarifa za sasa,” amesema Dk Mpango na kuongeza:

 “Tulifanya tathmini ya uhimilivu wa deni Novemba 2017. Thamani ya sasa ya jumla ya deni la taifa kwa pato la taifa ni asilimia 34.4, ukomo wake kimataifa ni asilimia 56 kwa hiyo hapo tupo vizuri.”

Waziri Mkuu: Serikali Itaendelea Kumuenzi Sokoine

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya tano itaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma ili kuenzi fikra za hayati Edward Moringe Sokoine.

“Tutaendelea kusimamia maadili ya utumishi wa umma kwa kuzingatia yale yote ambayo Mheshimiwa Sokoine aliyaanzisha,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Aprili 12, 2018) wakati akizungumza na mamia ya wananchi na viongozi waliohudhuria ibada ya kumbukumbu ya miaka 34 ya kifo cha Sokoine, iliyofanyika kijijini kwake Engwiki, kata ya Monduli Juu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Ibada hiyo iliyoongozwa na Askofu Mkuu  Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha,  Mhashamu Josephat Lebulu, ilihudhuriwa na viongozi wa dini wa wilaya, viongozi wa Serikali na wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi,  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Tate ole Nasha na baadhi ya wabunge.

Waziri Mkuu amesema Mhe. Sokoine alikuwa adui wa wahujumu uchumi na alihakikisha uchumi wa nchi unakua kwa maslahi ya Watanzania wote. “Mungu alitupa hazina iliyong’ara na kuangaza. Sote tuendelee kuangaza kwa kutenda mema na kuendeleza yale yote aliyoyaanzisha mpendwa wetu,” alisema.

“Katika maisha yake,  hakuwa na ubinafsi, uroho, wala tamaa ya kujilimbikizia mali. Hili ni jambo la kuigwa na sisi viongozi wa umma. Nasi tulioko kwenye nafasi hizi za uongozi,  tumuombe Mungu atuwezeshe tutende yale aliyoyaanzisha,” alisisitiza.

Alitumia fursa hiyo kuwafikishia wanafamilia na wananchi waliohudhuria ibada hiyo, salaam za pole kutoka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

Mapema, akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mst. Lebulu alimuelezea hayati Sokoine kuwa ni kiongozi aliyechapa kazi kwa bidii, mwenye uzalendo, aliyeongozwa na upendo na uwajibikaji kwa wananchi anaowaongoza.

“Ili tuweze kuwajibika na kuwa wazalendo kwelikweli, tunapaswa kuwa waaminifu na watu tunaomcha Mungu. Mtu awaye wa dini yoyote ile, kama hamchi Mungu, hawezi kuwa muwajibikaji.”

Alisema kila mtu anapaswa kumheshimu mwenzake kwa dini na imani yake. “Tuheshimiane kila mmoja kwa dini na imani yake, kwa sababu sote tumeumbwa kwa sura na mfano wake. Siyo kwamba tuvumiliane, tunatakiwa tusidharauliane bali tuheshimiane,” alisisitiza.

“Ni lazima tuwe waaminifu, tuache unafiki, tuache kuwa na maisha yenye hila na hiyana na badala yake, tuongozwe na dhamiri safi. Tuwe waaminifu kwa wenzetu, kwa dini na imani zetu na zaidi ya yote tuwe waaminifu kwa nchi yetu,” alisema.

“Ni aibu kukuta Mtanzania anaitukana nchi yake. Tupende vijiji vyetu, tarafa zetu, mikoa yetu na nchi yetu. Tuipende, tuitunze na tuilinde ili iwe nchi bora. Tuwe mfano kwa watoto wetu na wazazi wetu katika kuijali nchi yetu,” alisisitiza.

Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Kabudi alipopewa nafasi awasalimie wananchi, alisema kuna watu wanakufa lakini bado wanaendelea kuwa hai na kwa hilo, wanafamilia wanapaswa kuendelea kumshukuru Mungu.

“Tangu alipofariki mwaka 1984, hakuna mtu aliyejua kwamba hadi sasa, ambapo ni miaka 34 imepita, Edward Moringe Sokoine ataendelea kuwa hai. Ninasema yu hai kwa sababu maneno na matendo yake, bado yanaishi,” alisema.

“Edward Moringe Sokoine amegoma kufa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere amekataa kufa. Na sisi wasaidizi wa Rais Magufuli, tunapaswa kujitoa kwa wananchi na Taifa; kujiongeza zaidi katika utumishi wetu na hasa kuwajibika kwa kulitumikia zaidi Taifa kuliko kudai mapato ili tutakapoitwa kwenye promosheni iliyo kuu, wanaosalia waone faida ya kuwepo kwetu hapa duniani,” alisema huku akishangiliwa.

Akitoa shukrani kwa niaba ya familia, msemaji wa familia ya marehemu Sokoine, Bw, Lembris Kivuyo alisema wanaishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa karibu sana na familia hiyo tangu Mhe. Sokoine alipofariki.

“Tunaishukuru sana Serikali na tunazidi kuwasihi Watanzania waendelee kumuombea Mheshimiwa Rais Magufuli ili aendelee kuongoza Taifa hili bila ajizi na sisi kama familia tutaendelea kumuunga mkono Mhe. Rais katika jitihada zake za kutetea rasilmali za Taifa,” alisema.

Mbunge Mwingine CCM Ampinga Makonda

$
0
0
Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima (CCM) leo amehoji uhalali wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuagiza wanawake waliotelekezwa na waume zao wafike ofisini kwake na wapate msaada wa kisheria.

Pia ametaka baada ya akinamama kusaidiwa katika hilo, waitwe na akina baba waliotelekezwa na wake zao na kuachiwa watoto.

Sima alikuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais (Tamisemi) na ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mjini Dodoma leo Aprili 12.

“Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ametoa tamko na amefanikiwa akinamama zaidi ya 2000 wamefika pale, lakini nataka nifike mahali nishauri, Makonda amefanikiwa kwa sababu ameonyesha kuna mifumo ya serikali imeshindwa kufanya kazi yake, kwa mfano ustawi wa jamii, mifumo hii imeanguka,” amesema.

Hata hivyo, Sima amehoji Makonda anapata wapi mamlaka ya kisheria ya kuamua kuwaita akinamama hao?

Amesema kama ni jambo jema basi na wakuu wa mikoa wengine wanatakiwa wapate mamlaka ya kufanya kile anachokifanya Makonda.

“Ndugu zangu leo Makonda anatoa bima za afya, ni jambo jema sana, lakini kuna watoto yatima, hawana baba wala mama, nani atawapa bima za afya,” amesema.

Amesema anachotakiwa kufanya Makonda ni kuwasikiliza na kisha kuwarudisha katika mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali.

“Naiomba Serikali kwenye eneo hili iwe makini sana, hasa wasaidizi wa Rais watambue kuwa wanatakiwa warudi kwenye mifumo rasmi,” amesema.

Sima ameomba kuwa baada ya jambo hili alilolifanya Makonda kwa akina mama wanaume waliotelekezwa nao waitwe na wasikilizwe  ili kuwe na usawa.

Spika Ndugai Aitupilia Mbali Hoja ya Kubenea

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitupilia mbali hoja ya Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) kuhusiana na marekebisho ya masuala yanayohusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Akizungumza bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 12, Spika Ndugai amesema Kubenea alileta kusudio la kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka bunge lifanye marekebisho ya masuala yanayohusiana na NEC.

“Ili ikidhi matakwa ya mfumo wa vyama vingi hapa nchini sasa kwa kuwa Tume hiyo ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa na Katiba katika Ibara ya 74 marekebisho yote juu ya tume hiyo yanatakiwa kuletwa kwa kupitia muswada wa marekebisho ya Katiba na si hoja binafsi ya Mbunge.

“Nafikiri naeleweka katika ninachokisema unapoleta jambo ambalo linahusu Katiba basi upo utaratibu wa kufuata ili iendane na marekebisho ya katiba na siyo hoja tu ya Mbunge.

“Kwa hiyo kwa kuwa kanuni ya 58 kanuni ndogo ya kwanza ya Bunge imenipa madaraka ya kukataa hoja inayovunjwa Katiba.

“kwa hiyo taarifa yako Mheshimiwa Kubenea naikataa kwa hiyo kajipange tena, kama bado una nia, uje katika utaratibu unaotakiwa kama hatukukuelewa tutatafuta muda ili tueleweshane zaidi ila sisi tumeelewa hivyo,” amesema Spika Ndugai.

Serikali Kuajiri Watumishi 52, 436

$
0
0
SERIKALI imesema imeanza mchakato wa kuajiri watumishi 52,436 wanaohitajika katika kada mbalimbali nchini.

Hayo yalielezwa jana bungeni mjini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alipowasilisha hotuba yake kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha.

Alisema uhakiki wa mahitaji ya rasilimali watu katika utumishi umma ikiwamo mikoa yote, umefanyika kupitia Mfumo wa HCMIS na kubaini idadi hiyo ya mahitaji ya watumishi wa kada mbalimbali.

"Serikali imeanza mchakato wa kuajiri watumishi hao kwa kuzingatia maeneo ya kipaumbele na kuimarisha kada zenye upungufu mkubwa," alisema.

Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala, alibainisha kuwa kada ya afya ina upungufu wa watumishi 14,102, elimu 16,516, kilimo 1,487, mifugo 1,171 na uvuvi 320.

Aliongeza kuwa polisi kuna upungufu wa watumishi 2,566, magereza 750, uhamiaji 1,500, zimamoto 1,177, hospitali za mashirika ya kidini na hiari 174 na wengineo 12,673.

Mkuchika alisema kuwa katika mwaka huu wa fedha, usimamizi wa ajira za watumishi wa umma umefanyika kwa waajiri wote ambapo watumishi wapya 15,000 wameajiriwa, wakiwamo jumla ya walimu 4,348 wa masomo ya sayansi na watumishi 3,152 wa kada ya afya ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye Orodha ya Malipo ya Mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti.

"Maofisa utumishi 1,595 wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufungiwa dhamana ya kuingia katika mfumo wa HCMIS, kufikishwa mahakamani na wengine kesi zao zipo Takukuru," alisema Mkuchika.


Mbunge CHADEMA 'Ajilipua' Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul amesema wakuu wa mikoa ambao wametolewa kwenye vyama vya siasa wanafanya mambo ya ajabu katika maeneo yao ya kazi.

“Mimi nataka nibomoke, sitaki kuumia kifua....Hawa wakuu wa mikoa wanaoteuliwa bila kuangalia wamehudumia katika utumishi wa umma kwa muda gani, wanafanya mambo ya ajabu,”amesema.

Gekul ameyasema hayo leo Aprili 12, bungeni na kumuomba Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ‘abomoke’ bungeni akimaanisha kuongea yaliyo moyoni mwake wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Gekul amesema kuwa viongozi wa wilaya na halmashauri kuanzia Hanang, Tunduma na kwingineko wanafanya kazi ya kisiasa na si maendeleo.

“Ni maeneo yote kuanzia Hanang ambako hata mzoefu Mama Nagu anawekwa ndani, wanafanya kazi ya siasa na sio kazi ya maendeleo,” amesema.

Zitto ataka Tamisemi imtafute mwenyekiti aliyetoweka

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe amemtaka waziri wa Tamisemi kulitafutia ufumbuzi suala la kutoweka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko, Simon Kangue.

Amesema hayo bungeni leo Aprili 12, 2018 alipochangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, yenye wizara za Tamisemi; na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Habari zinazosambaa Kibondo tayari ameuawa. Tunataka maelezo ya mtu huyo, sisi watu wa Kigoma ni Kigoma kwanza kabla ya kuwa Watanzania naomba hilo mlielewe,” amesema.

Zitto amesema mara ya mwisho kuonekana mwenyekiti huyo aliitwa kwa mkurugenzi na kukutana na ofisa usalama wa wilaya.

Amesema tangu siku hiyo hajulikani alipo mwenyekiti huyo licha ya jitihada za kumtafuta kufanyika.

“Familia imechukua hatua mbalimbali, imelalamika na sisi wajumbe wenzake tumehoji kwenye vikao, hakuna maelezo yoyote kutoka serikalini,” alisema Zitto.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 13

Mahakama Yaelezwa Hali ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ni Mbaya

$
0
0

Mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hali ya Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva ni mbaya (very Serious), na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kufuatia hali hiyo, mahakama jana ilishindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH)  rais huyo Simba ambaye anashtakiwa pamoja na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu.

Kesi imeahirishwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Aveva ni  mgonjwa (very Serious)  amelazwa katika hospitali ya Taifa  ya Muhimbili.

Swai aliomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.

Hakimu Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya awali, ili tarehe inayokuja waweze kusomewa PH na siku ikianza kusikilizwa, isikilizwe mfululizo. Kesi imeahirishwa hadi Aprili  25/ 2018.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.

Waziri Jafo: Hati Safi zimeongezeka katika Mamalaka za Serikali za Mitaa.....Watumishi 434 Tumewabana

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo amesema katika Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Halmashauri zilizopata Hati Safi zimeongezeka  kutoka Halmashauri 81 kwa mwaka 2015/16 mpaka kufikia Halmashauri 166 (90%) kwa mwaka  2016/17.

Jafo ameyasema hayo wakati kwa Kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ukumbi Bunge kuhusu utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo ya CAG kwa hesabu za Mamlaka za Serikali  za Mitaa kwa  mwaka Ulioishia  Juni 30, 2017.

Alisema “napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa maelekezo yao mazuri yaliyosaidia sana utendaji kazi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mikoa na MSM; Michango yao, ushauri na maelekezo yamewezesha kuongeza Idadi ya Hati Safi.

Akizungumzia kuhusu hoja zilizobainishwa katika ropoti ya CAG Mhe. Jafo alisema tumefanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa katika ripoti zilizopita ambapo watumishi 434 wamechukuliwa hatua baada ya kubainika kusababishia halmashauri zao hasara/hoja zisizo za lazima kutokana na kutotekeleza ipasavyo wajibu wao ama kujihusisha na vitendo vya ubadhirifu.

“Kati ya hao 9 wamefukuzwa kazi, Watumishi 210 wamepewa barua za onyo huku Watumishi 15 wakifikishwa kwenye vyombo vya dola. Watumishi 28 wamesimamishwa kazi, 13 wametakiwa kufidia hasara kutoka kwenye mishahara yao wengine 4 wameshushwa vyeo na wengine 10 wamebadilishiwa majukumu” alisema Jafo.

Aliongeza kuhusu MSM kupokea Fedha pungufu ya Bajeti Iliyoidhinishwa ni kwa sababu Serikali hutegemea makusanyo ya mapato kutoka vyanzo mbalimbali. Hivyo, kiasi kinachotumwa kwenye MSM hutegemea mwenendo wa mapato yaliyopatikana lakini pia fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa na Serikali kwa mwaka wa fedha uliotaguliwa 2016/17 zimeongezeka ikilinganishwa na mwaka  wa 2015/16.

Kwa  mwaka 2016/17 fedha za miradi ya maendeleo zilizopokelewa na MSM ni Tsh. 705,927,921,596.20 sawa na 57% ya bajeti iliyoidhinishwa ya Tsh. 1,242,616,839,000 akati mwaka 2015/16, fedha zilizopokelewa  zilikuwa ni Tsh. 390,525,992,297 sawa  39%  ya bajeti ya Tsh. 1,010,650,744,099.

Kuhusu changamoto katika Usimamizi wa Mapato katika Mhe. Jafo alieleza Wizara imeendelea kuziba mianya ya uvujaji wa mapato kwa kuhakikisha kuwa Halmashauri zinahamia katika matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato ujulikanao kama Local Government Revenue Collection and Information System (LGRCIS) ambapo takwimu zote za mapato zinatunzwa katika mfumo huo ambao pia umeunganishwa na mashine za kukusanyia mapato (Point of Sales) zinazotumiwa na Mawakala/Wakusanya mapato, na hivyo kuiwezesha Halmashauri kufahamu mapato  yaliyokusanywa na Wakala/Wakusanya mapato hao.

Vile vile, mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya benki, na hivyo kuwezesha Halmashauri kufahamu kiasi ambacho Wakala/Mkusanya mapato amekiingiza kwenye akaunti ya benki ya Halmashauri ikilinganishwa na kiasi alichokusanya. Mpaka sasa, Halmashauri zote 185 tayari zimewekewa mfumo huu wa LGRCIS.

Wakati huo huo alieleza Kuhusu Vitabu 379 vya Kukusanyia Mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi amesema  Licha ya kuwa  idadi ya Halmashauri na idadi ya vitabu vya kukusanyia mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa Wakaguzi imepungua kutoka  871 katika Halmashauri 57 kwa mwaka 2015/16 mpaka vitabu 379 katika Halmashauri 21 kwa Mwaka 2016/17, OR – TAMISEMI imeendelea kusimamia maelekezo ya Serikali ya Halmashauri zote ziachane na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi/vitabu vya kuandikwa kwa mkono, na badala yake mapato yakusanywe kwa kutumia mashine za kielektroniki.

Waziri Jafo alimalizia kwa kutolea ufafanuzi wa Soko la Mwanjelwa –Mbeya na kusema kuwa OR-TAMISEMI imeanza kuchukua hatua kuhusiana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa na kwa kuanza tulimuomba CAG kufanya ukaguzi maalum na taarifa iliashiria makosa ya kijinai na tayari Serikali imelifikisha suala hili kwenye vyombo vya Dola, ambapo pia Wahusika Wakuu wa mikataba husika na usimamizi wa utekelezaji wake, nao pia wameshafikishwa kwenye vyombo vya Dola kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi. Serikali itaendelea kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na CAG ili kuokoa hasara itokanayo na ujenzi wa soko hilo.

Deni La Taifa, Mishahara Inavyokomba Makusanyo Ya Serikali

$
0
0
Baada ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuonyesha kuwa makusanyo ya serikali yanafikia lengo kwa takribani asilimia 94, lakini fedha za maendeleo zinazotolewa ni takribani asilimia 50 pekee Serikali imesema kwa mwezi inakusanya wastani wa Sh trilioni 1.3, Sh bilioni 550 hulipa mishahara na Sh bilioni 600 hulipa deni la taifa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema hayo jana Alhamisi Aprili 12, wakati akizungumza na waandishi wa habari kujibu sehemu ya hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali (CAG), katika ripoti yake inayoishia Juni 2017 aliyoiwasilisha bungeni jana.

Dk. Mpango alisema; “kwa hiyo maana yake kwenye Sh trilioni 1.3, umebakiwa na bilioni 200 ambazo ndiyo hizo unatumia kuendesha Serikali, lakini humo namo kuna shughuli nyingine ambazo hazikwepeki, kwa mfano askari wetu shupavu wanalala nje lazima Serikali tuwape posho ya chakula, ndiyo sisi tunaweza tukaendelea na vurugu huku bungeni tukabishana, tukala nyumbani kwa amani.

“Kuna mishahara ya Majaji lazima ilipwe na marupurupu yao mengine, kuna viongozi wetu nao hawalali, niwahakikishie ni kawaida kabisa kumpigia Rais simu saa nane, saa tisa yuko macho, hawa viongozi wamebeba dhamana kubwa lazima Serikali iwahudumie.

“Kwa hiyo unaponiuliza hizi nyingine zinaenda wapi, naweza nikaendelea na kuendelea,” alisema Dk. Mpango.

Awali, Dk. Mpango alisema Serikali ya awamu ya nne, ilikuwa inakusanya Sh bilioni 850 kwa mwezi, lakini tangu Serikali  ya awamu ya tano kuingia, imekuwa ikikusanya wastani wa Sh trilioni 1.

“Kwa hiyo ni ni rahisi sana kuhesabu hicho kinachoingia mfukoni, lakini ni muhimu kuangalia sana hicho kinachotoka, zinatoka zinakwenda kwenye nini.

“Ulipaji wa deni la taifa inategemea, kwa mwezi inaweza ikatoka kati ya Sh bilioni 600, tumewahi kwenda mpaka Sh bilioni 900, kutegemea na hayo madeni yanaiva wakati gani, mwezi huu unaweza ukalipa Sh bilioni 600 na kidogo, mwezi ujao ukalipa Sh bilioni 700, ni kwasababu ya tofauti ile mikopo inaiva wakati gani.

“Ukichukua wastani wa Sh bilioni 550 mishahara, ukaongeza Sh bilioni 600 kwaajili ya kulipa deni, tayari Sh trilioni 1.1 umeitumia kwa hivyo vitu viwili ambavyo huwezi kukwepa,” amesema Dk. Mpango.

Mbunge Shabiby: Nondo Ana Umaarufu Gani, Mnachafua Serikali tu!

$
0
0
Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, amesema hakuna umuhimu mamlaka za serikali kutumia vyombo vya habari kuwaita baadhi ya watu kwa ajili ya kuwahoji kutokana na tuhuma wanazokabiliwa nazo.

Shabiby amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma jana Aprili 12, 2018  huku akitolea mfano tukio la Mwenyekiti wa TSNP ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (UDSM), Abdul Nondo, ambaye aliitwa na Mamlaka ya Uhamiaji kwa ajili ya kuhojiwa uraia wake, na kusema kwamba vitendo hivyo vinaichafua serikali kwa kiasi kikubwa.

“Sasa hivi kuna watu kwenye Utumishi ambao wanafanya mambo ya kuichafua Serikali ya CCM, kulikuwa na haja gani ya kumita yule kijana Abdul Nondo kumhoji sijui alete cheti cha kuzaliwa cha bibi cheti cha mjomba, cheti cha babu? Mamlaka inashindwaje kufanya investigations zake (uchunguzi) ili kubaini ukweli mapaka iite wanahabari?

“Tunawapa watu umaarufu wakati kesi ipo polisi, ipo mahakamani, kuna watu wengine watatumia hiyo kitu kusema Serikali ya CCM ikimtaka mtu inamuomba uraia wake, sidhani kama Serikali ina haja na mtu mdogo kama yule ambaye hata hana madhara yoyote,” alisema Shabiby.

Wanaume 18 Kupima DNA Kwa Makonda

$
0
0
Wanaume 18 kati ya waliofika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhojiwa kuhusu kutelekeza watoto wamekubali kupimwa vinasaba (DNA) na Mkemia Mkuu wa Serikali, taarifa iliyotolewa jana na Paul Makonda ilisema.

Makonda alisema hatua hiyo imefikiwa na wanasheria na maofisa ustawi wa jamii baada ya kuhoji wanaume waliodaiwa kuwatelekeza watoto, katika malalamiko yanayoendelea kutolewa na wanawake kuanzia Jumatatu katika ofisi hizo, Ilala.

Mkuu wa Mkoa Makonda alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maendeleo ya zoezi linalomalizika leo.

"Jumla ya wanaume 18 ambao walibisha kuwa watoto sio wao wamekubali kwenda kupimwa DNA kwa Mkemia Mkuu ili kupata uthibitisho wa uhalali wa mzazi na hao ni kati ya wanaume 198 walioitikia wito na kuja ofisini kwangu," alisema Makonda.

Kadhalika, alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo baada ya kuandikiwa barua za wito, 179 walikubaliana na wanawake waliozaa nao mikakati ya kulea watoto husika.

"Familia 179 zimefikia muafaka," alisema Makonda na "haya ni mafanikio makubwa. Kama watu waliokuwa hawahudumii familia na leo hii wamekubali kuhudumia na kurudi nyumbani kwa amani, kazi hii imezaa matunda."

Makonda alisema kati ya wanaume 198 waliofika katika ofisi hizo kutafuta mwafaka, 19 kati yao mashauri yao yamepelekwa mahakamani ili kutafuta suluhu.

"Kazi inaendelea vizuri, tunaona mafanikio kwa sababu wanawake waliojitokeza ni wengi wanaokosa huduma kutoka kwa wanaume zao," alisema. "Wanaume waliopewa barua za wito nao wamekuja wakasilikizwa na mwafaka ukapatikana."

Pia alisema wanawake 1,498 wamejitokeza katika siku tatu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao na kupewa msaada wa kisheria.Makonda alisema kutokana na kuwapo kwa idadi hiyo kubwa ya wanawake, wameongeza wanasheria 200 na maofisa ustawi wa jamii 60 na kusababisha kuwapo kwa watoa huduma 378.

"Kwa sababu ya mwitikio mkubwa wa wanawake, tumelazimika kuongeza wanasheria na maofisa ustawi wa jamii ili kazi hii ifanyike kwa haraka," alisema Makonda.

Aidha, Makonda alisema baada ya kusikiliza wanawake waliotelekezwa, kanzia Jumatatu itakuwa zamu ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito.

"Ingawa wapo baadhi ya wanaume ambao wameandikiwa barua za wito na wameshakuja kusikiliza walichoitiwa, kuanzia Jumatatu itakuwa ni siku ya kuwasikiliza baada ya kuwasikiliza wanawake," alisema Makonda.

Alisema wanaume ambao wamepewa wito huo wanatakiwa wajitokeze kusikiliza na endapo watakaidi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Makonda pia aliwataka wanawake na wanaume wenye matatizo ya kutelekezewa watoto kweli wajitokeze katika ofisi hizo ili wapate msaada wa kisheria bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii.

"Kama kweli mtu ana matatizo ni wajibu wake kuja hapa ili asikilizwe na kupatiwa msaada bure badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii ambako hakuna majibu," alisema Makonda.

Leo ni siku ya mwisho ya kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake ambao walitelekezewa watoto na wanaume waliozaa nao.

Msanii Godlucky Haamini kukutana na Raisi na Kumpa Mkono.

$
0
0
Mwanamuziki anaefanya vizuri katika nyimbo za injili, Godlucky Gosbeth amefunguka na kusema kuwa hakuamini alipokuatana na raisi katika sherehe za uzinduzi wa taasisi ya Jakaya  Kikwete  iliyofanyika juzi   jijini Dar es salaam.

Godlucky anasea kuwa kwake ni bahati sana  na hakutegemea kama angeitwa pale mbele kwa ajili ya kusalimiana na viongozi wakubwa wa serikalai mpaka alipotoka ikulu ndipo alipoaanza kuamini kuwa ni kweli jambo lile limetendeka.

Godluck  anasema kuwa , kuonekana kwake na kusalimiana  na viongozi wakubwa imemfanya apokee simu nyingi sana zikimpongeza kwa kazi hiyo nzuri aliyoifanya na hata yeye pia anashukuru Mungu kwa kuwa anazidi kumbariki.Godlucky aliyaongea hayo alipokuwa akiongea na radio clouds fm.

Hata katika ukurasa wake wa instagram , Gudluck aliandika maneno ya kumshukuru Mungu kwa kuandika kuwa katika maisha yake hakuwahi kuwaza kama kuna mambo makubwa kama hayo yangeweza kutokea katika maisha yake lakini anachoamini ni kwamba Mungu amekuwa akitimiza ahadi alizokuwa ameweka kumtimizia maishani mwake.

Makalio Yampatia Aunty Lulu Wachumba Watatu

$
0
0
Mtangazaji na muigizaji wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama aunty Lulu amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya kudai kalio lake kubwa limemsaidia kupata wachumba watatu nchini China.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Aunty Lulu alifunguka na kudai kuwa kwenye Safari yake ya kibiashara nchini China hivi karibuni alihudhuria kwenye ukumbi mmoja ambao kulikuwa na msanii ambaye ni Mtanzania ambaye alikuwa anapiga shoo.

Aunty Lulu amedai baada ya muziki kuanza kupigwa alianza kucheza na kukata mauno kiasi ya kwamba wanaume walianza kumtolea macho na usiku huo alipata wachumba watatu ambao wapo tayari kumuoa.

"Kalio langu limenipatia wachumba wa Kichina watatu, sasa baada ya wote kuniambia wanataka kunioa, niliwatajia mahari yangu kuwa ni shilingi milioni 50 na walikubali, lakini niliwapa mtihani mwingine kwamba atakayekuwa wa kwanza kufika Bongo ndiye atakayenioa, hivyo ninasubiri na ndoa yangu itakuwa ya mkataba”.

Waziri Mhagama awageukia viongozi wa dini.....Awataka Waendelee Kuliombea Taifa

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Jenista Mhagama amewageukia viongozi wa dini mbalimbali na kuwasii waendelea kuliombea taifa ili iweze kudumishwa amana na utulivu huku akiwapongeza uongozi wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kufanya hivyo.

Waziri Mhagama anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu nchini ametoa pongezi hizo alipokutana na uongozi wa Kanisa hilo Bungeni Dodoma ili kujadili na kuipongeza serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo.

"Niwapongeza sana uongozi wote wa Kanisa la Baptist nchini kwa kuendelea kutuombea na kuikumbuka nchi yetu kwani bila uwepo wa amani na utulivu maendeleo hayawezi kuwepo", amesema Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha inaboresha na kuleta maendeleo ya nchi yake bado kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na ushirika mzuri na viongozi wa dini na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt.John Magufuli katika kufikia azma yake ya  "Tanzania ya Viwanda".

"Kipekee niwashukuru kwa kuona umuhimu wa kutuweka mikononi mwa Mungu uongozi wote wa nchi, kuanzia kwa Mhe. Rais wetu, Baraza la Mawaziri na viongozi wote kwa ujumla wao, ili kuhakikisha tunakuwa na hekima na weredi wa utekelezaji wa majukumu yetu kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo", amesisitiza Waziri Mhagama.

Askofu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase akifanya maombi kwa kifupi walipomtembelea Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama kuzungumza masuala yao na kuipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada za kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Pamoja na hilo aliuomba uongozi huo kuendelea kuchangia katika huduma za kijamii hususani kupitia mchango wanautoa kwa jamii wa kuwa na shule, vyuo na zahanati zinazohudumia wananchi wanaochangia katika uzalishaji na maendeleo ya nchi yao.

kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Baptist nchini Arnoid Manase ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa hatua kubwa iliyoifanya katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo tangu ilipoingia madarakani na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kuona nchi inaendelea na kuondokana na baadhi ya changamoto zilizopo.

Baba amnywesha sumu mwanae Aliyezaa na Mchepuko Ili kulinda ndoa

$
0
0
Mtoto wa miezi miwili (jina limehifadhiwa) mkazi wa Manispaa ya Shinyanga amedaiwa kunyeshwa sumu na baba yake mzazi kwa madai ya kutaka kuficha kizazi hicho ili mkewe asijue amezaa nje ya ndoa.

Akielezea makasa huo jana, mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Shija (22) alisema lilitokea Machi 24, mwaka huu majira ya saa tatu usiku.

Maria alisema siku hiyo baba wa mtoto huyo, Edson Damian (37) alikwenda nyumbani kwao anapoishi yeye na mama yake kwa ajili ya kumsalimia mtoto huyo, na ndipo akamywesha sumu ya panya kwa lengo la kumuua wakiwa wamekaa nje.

Mzazi huyo alisema kabla ya mzazi mwenzake kufanya kitendo hicho, alikuwa akimtuma maji ya kunywa ndani mara kwa mara kitu ambacho si kawaida yake.

Alisema aliporudisha kikombe ndani mara ya mwishho ndipo akasikia harufu ya sumu ya panya, na aliporudi haraka kwa mtoto akamkuta ameanza kutoa mapovu na mwanaume huyo kukimbia.

“Baada ya kuona mtoto kapewa sumu nikakimbia kwa jirani ambaye ana zizi la ng’ombe, ndipo nikachukua maziwa nikamnywesha na baadae nikachukua bodaboda hadi kituo cha Polisi kupewa RB na kisha kwenda hospitali ya Rufani ya mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu," alisema Maria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi Simon Haule alithibisha kutokea kwa kisa hicho na kwamba mtuhumiwa huyo yupo mbaroni.

Alisema upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.

Akielezea historia ya mapenzi yao, Maria alisema Damian wakati anamtaka kimapenzi alimwambia hana mke, lakini baada ya mtoto kuzaliwa akasema ana mke, hamtaki kwani atavunja ndoa yake.

Mtu wa karibu na familia ya Maria, Jumanne Kagusa alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images