Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kundi la kigaidi la ISIS latuma salamu za vitisho kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi

$
0
0
Kundi la kigaidi la ISIS limetoa vitisho vikali kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kumwambia kuwa atalipa damu za waislamu anaowaua nchini Syria.

Kundi hilo ambalo limeanza kusambaza vipeperushi mitandaoni vyenye maelezo yanayosomeka kuwa “Putin ni mtu usiyekuwa na imani na utalipa damu ya waislamu unaowaua Syria” vimeanza kusambaa mitandaoni kushinikiza Rais Putin kujiengua katika mapambano nchini Syria.

Vipeperushi hivyo ambavyo vinamuonesha mwanaume akiwa ameshika bunduki aina ya AK-47 vimeanza kusambaa kwa kasi katika miji mikubwa nchini Urusi kwenye maeneo yote muhimu ambayo yanamikusanyiko mikubwa ya watu.

Kwa mujibu wa mtandao unaofungamana na kundi hilo wa Wafa Media umeeleza kuwa lengo lao kubwa la ISIS ni kufanya mashambulizi ya kigaidi kwenye michuano ya kombe la dunia.

Vitisho hivyo vinakuja baada ya Rais Putin mwaka jana kutangaza kuisaidia serikali ya Syria inayoongozwa na Rais Bashar Al-Assad katika kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Katika hali ya kuimarisha usalama nchini Urusi, tayari serikali imetangaza kuchukua hatua mbalimbali za kiusalama ikiwemo kufungia mtandao wa Telegram ambao umekuwa ukitumika na kundi hilo na makundi mengine ya kihalifu duniani kutokana na usiri wa data zake.

Mwaka jana jeshi la anga la Urusi lilifanya mashambulizi dhidi ya ISIS katika sehemu za kuhifadhia silaha na kituo cha mawasiliano cha kundi hilo viliharibiwa vibaya nchini Syria.

Hii sio mara ya kwanza kwa kundi hilo kumtishia Rais Putin kwani mwaka jana ISIS walitangaza kufanya mashambulizi ya kigaidi kwenye michuano ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi June mwaka huu nchini Urusi.

==>>Soma Zaidi <<HAPA>>

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu Ataja Kasoro zoezi la Wanawake Waliotelekezwa

$
0
0
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kasoro pekee ya utaratibu ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwasikiliza wanawake na watoto ‘waliotelekezwa’ na waume zao ni kutokuwa na faragha kwa watoto.

Akizungumza leo Jumatano Aprili 11, 2018 wakati akihojiwa katika kipindi cha 360 kinachorushwa na televisheni ya Clouds, Ummy amesema kinachofanywa na Makonda kipo ndani ya sheria, hata watendaji wanaowasikiliza wanawake wametoka katika idara yake.

Amesema Wizara ya Afya inaunga mkono jitihada hizo, kwamba kasoro zilizojitokeza ni kwa baadhi ya wanawake waliotelekezwa kwenda na watoto na kutojali haki za kuwalinda katika hatua hizo za awali za mashtaka.

“Makonda amefanya kitu kizuri mwamko umekuwa mkubwa, ni sawa madawati yapo na ustawi wa jamii pia wapo lakini wengi wamekuwa wazito ila kwa sasa wameitikia wito kwakuwa yeye amewahimiza wanawake wenye matatizo hayo wafike kwake, kazi imekuwa nyepesi kwani hata wanaohudumia pale ni watu wetu wa Ustawi wa Jamii,” amesema Ummy.

Amesema kilichofanyika ni kama kuita kambi ambayo baadaye matokeo yatakayopatikana yatawanufaisha wanawake na ikiwa kutakuwa na ugumu kesi itakwenda mahakamani.

Hata hivyo, Ummy ametoa wito kwa wanawake wanaokwenda kutoa mashtaka yao kuhakikisha wanalinda haki za watoto wao kwa kutowaonyesha hadharani.

“Ninasema hili ni kosa la mwanamke mwenyewe, kwa mfano yule mtoto Mchina nimesikitika sana kule ni kumnyanyapaa amesambazwa mitandaoni kila mahali anazungumziwa, niwaombe Watanzania tujitahidi kuwalinda watoto hawa, tusisambaze picha zao kwa maslahi mazuri ya mtoto,” amesema Ummy. 

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE; 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO 0754372325/ 0689013109/ 0620806813 

HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

OFA: Jipatie Riwaya Kali za Kusismua Toka kwa Mtunzi Makini

$
0
0
OFA YA KUJIUNGA NA GROUP LA TANGA RAHA SEASON TWO BADO INA ENDELEA
Baada ya Olvia Hitler kuwasumbua sana Eddy na Rahma katika Tanga raha Season two sasa. Mambo yanazidi kunoga katika group langu la Whatsapp. Nina kukaribisha msomaji wangu kuendelea na hadithi hiyo pamoja na hadithi nyingine mpya iitwayo Sin. Ukijiunga leo katika GROUP uta pata ofa ya episode 80 buree kabisa. Ada ya Group ni sh 4000 tu kwa mwenzi mzima.

Namba zangu za whatsapp ni 0657072588 au 0768516188 Pia una weza kunipigia kwa namba hizo.

Pia kwa wale wanao fwatilia kigongo cha AIIISSIII YOU KILL ME. Sasa Season two ya AIISSII YOU  KILL ME ambayo ina itwa AIIISSII YOU KILL ME LEGACY ipo tayari hadi mwisho. Leo 11/04/2018 Ukinunua vipande 20 ambavyo ni sawa n ash 5000/= uatapata ofa ya vipande 20 BUREEE KABISA.

Wahi ofa hizi kabla ya kuisha leo. Pia nina washukuru sana kwa kuendelea kunipa support ya kazi yangu hii ya uandishi kwani bila ya nyinyi siwezi kufanya mambo makubwa zaidi ya haya.

Kwa ushauri wau maoni, wasiliana nami kwa simu namba 0657072588 au 0768516188. Una weza kunitumia ujumbe kwa barua pepea eddazariaM@gmail.com

Mahakama Yaikemea Jamhuri Kushindwa Kumpeleka Sethi Muhimbili

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeukemea upande wa Jamhuri kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumpeleka  mshtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi kutibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi imeonyesha kutoridhishwa na kitendo hicho leo Jumatano Aprili 11, wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.

“Kila chombo kifanye kazi kwa kuheshimiana kwani haipendezi kila mara amri za mahakama haziheshimiwi.

“Mahakama lazima ifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria na haipendezi amri za mahakama kutoheshimiwa. Wala huhitaji kuwa daktari, ukimuangalia kwa macho tu mshtakiwa wa kwanza anaonekana anaumwa, suala la ugonjwa wake tumuachie daktari,” amesema Shaidi akijibu hoja za Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga kwamba lazima daktari wa mshtakiwa huyo awepo.

Katuga amedai kuwa Sethi aliomba wakati anapelekwa Muhimbili Daktari wake wa Afrika Kusini awepo ambapo wanasubiri taarifa kutoka kwa mshtakiwa na kwamba sababu nyingine ya kutotekeleza amri ya mahakama kwa wakati ni kwa mshtakiwa kuhamishwa gereza kutoka Segerea kwenda Ukonga.

Akijibu hoja hizo wakili wa Sethi, Hajra Mungula alidai kuwa mshtakiwa hajaongea chochote na wanashtushwa na maneno yaliyotolewa na upande wa mashtaka.

Kwa upande wake Wakili wa mfanyabiashara James Rugemarila, Cuthbert Tenga amedai amri za mahakama zinachukuliwa kirahisi na kwamba kila siku upelelezi haujakamilika ambapo ameomba Kamishna wa Magereza aitwe mahakamani ili aeleze kwanini amri za mahakama hazitekelezwi. Kesi hiyo omeahirishwa hadi Aprili 25, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 83 na 84 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
ILIPOISHIA  

Nikiwa katika kuwatazama tazama wanajeshi hawa wa kisomali, nikamuona kijana mmoja ambaye naye amenikazia macho. Kumbukumbu yangu ikarudi hadi siku ambayo tulikuwa Tanga na raisi, na njiani tukakutana na magari ya wasomali, na tukapambana nao na kuwaua wote. Mmoja wa vijana ambao nilipambana nao ni huyu anaye nitazama sana. Kijana huyu akasimama huku bunduki yake akiwa ameishika vizuri, akaanza kupiga hatua huku akinifwata akionekana kuwa na jazba kubwa usoni mwake. Nikatamani kufanya kitu ila uwezo sina, na kitu kingine ninaogopa sana hawa watu wakifahamu kwamba mimi nilikuwa mpelelezi nchini Tanzania na nimiongoni mwa watu nilio sababisha vifo vya ndugu zao wengi sana jambo ambalo nahisi hadi leo wameweka uhasama mkubwa na nchi ya Tanzania.
          
ENDELEA      
Cha kumshkuru Mungu hawa akawahi kumzuia kijana huyu, na wezake wawili wakakimbilia sehemu tulipo na kumkamata huku wakimpokonya bunduki yake. Hawa akaanza kuwafokea vijana hawa, walimo mkamata mwenzao kwa lugha ambayo siielewi. Wakaondoka nakijana huyu huku wakiendelea kumvuta na kumbeba juu juu.
“Samahani mwanye Dany”
“Bila samahani”
“Huyu kijana ana matatizo ya akili, kwa hiyo akiona watu wapya basi inakuwa ni shida, sana. Sasa sijui imekuwaje hadi wamemuachia akatoka nje”

“Ahaa kumbe”
“Yaa akili yake haipo sawa kabisa, yaani anashida sana.”
“Kwani hapo mwanzo alikuwa na hali kama hii?”
“Hapana, huyu kijana nimekuwa naye kabisa, akili zake zipo kama kawaida, ila tatizo linalojotokeza alipo okoka kufa, nchini Tanzania. Kuna kazi moja walikwenda kuifanya, basi kati ya watu wote walio kuwa wamekwenda kule yeye ndio wa pakee ambayo elinusurika kufa”
“Duuuuu”
“Yaa ndio hivyo bwana”
Hawa alizungumza huku tukiendelea kutembea taratibu akinionyesha baadhi ya maeneo katika ngome hii iliyo jekwa kwa uimara mkubwa sana. Hata ukuta wake ninaweza kuufananisha na kuta kubwa zilizo kuwepo kwenye ngome za kifalme huko nchini Italia

“Sasa baada ya hao wezake kuuwawa, mumeamuaje?”
“Daaa ni mpango mkubwa sana ulio andaliwa dhidi ya Tanzania, ila utaufahamu, hali yako ikiwa vizuri”
“Ahaa sawa sawa”
Nilizungumza kana kwamba sielewi kitu ambacho kinaendelea. Sikuhitaji kuuonyesha wasiwasi wangu mbele ya Hawa, kwa maana hili nalo linaweza kuwa kosa, na wala sikuhitaji kuuliza swali jengine juu ya huo mpango wao ambao wameupanga dhidi ya Tanzania. Kwa mwendo  huu wa taratibu tunao utembea tukafika sehemu ambayo kuna jishe la wasichana na wanapata mafunzo yao.
 
“Hili ni jeshi langu, hawa wote unao waona hapa, wapo chini ya mamlaka yangu”
Kwa haraka haraka wasichana hawa nimewahesabu idadi yao wanafika kama hamsini hivi. Mafunzo wanayo fundishwa kwenye hivi viwanja unaweza kusema kwamba si watoto wa kike kwa maana wapo kikakamavu kama wanaume. Tukaendelea kuzunguka na kuelekea maeneo mengine ya kutengenezea silaha za kivita.
“Hapa kuna wataalamu  wengi sana wa kutengeneza, bunduki, mabumo, majambia. Yaani tumejipanga kisawa sawa”
“Kweli hata mimi naona. Ila kwa nini unaniambia mimi haya yote?”

Nilimuuliza Hawa swali hili kwa kumtega tu, kwa maana sijaielewa maana yake ya kunieleza mimi kila kitu isitoshe hawafahamu kwamba mimi ni nani na ninamaisha gani kabla sijafika hapa.
 
“Ninakuonyesha haya yote kwa kuwa, hadi sasa wewe ni moja ya wanachama wa kundi la baba yangu. Na yeye ndio ameagiza mimi kukuonyesha haya yote. Naamini hadi hapo utakuwa umenielewa?”
“Yaaa”
“Naamini ukipona utajifunza haya yote ambayo wezako wanafundishwa”
“Kweli nitaweza?”
“Utaweza, wapo ambao walikuja hapa hata ngumi kurusha hawawezi, ila kwa sasa nikikuonyesha huto weza kuamini”
“Wee”
“Njoo huku”
Tukaingia kwenye moja ya ukumbi, tukakuta watu wanajifunza maswala ya kareti. Hawa akaanza kunionyesha mtu mmoja baada ya mwengine ambao kipindi wanaingia kwenye huu ukumbi walikuwa hawajiwezi kabisa katika maswala ya mapambano. Kila anaye nionyesha yupo vizuri katika kupamban.

Mbunge CCM Amvaa Makonda Sakata la Wanawake Waliotelekezwa

$
0
0
Mbunge wa Ulanga (CCM), Gudluck Mlinga ameomba mwongozo wa Spika bungeni akitaka kujua namna chombo hicho cha Dola kinavyoweza kuzuia wanawake waliofika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai ya kutelekezwa na watoto wao.

Mlinga ameomba mwongozo huo leo Jumatano Aprili 11, 2018 akisema kitendo hicho kinawadhalilisha watoto ambao hufika katika eneo hilo wakiwa na mama zao, akidai kuwa kinavunja Katiba ya nchi.

Mwongozo huo uliibua kelele bungeni baada ya mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kutoa majibu kwamba suala hilo ni la kisheria, kupingwa na wabunge waliohoji sheria ipi.

Mlinga alitaka kujua namna ambavyo Makonda anavyovunja Katiba kwa kuanika mambo ya siri hadharani jambo ambalo linakwenda kinyume na Katiba, akitaka Bunge liingilie kati na kukemea kitendo hicho.

Ajali ya ndege Algeria yauwa 257

$
0
0
Ndege ya kijeshi ya Algeria iliyokuwa imebeba wanajeshi imeanguka Jumatano asubuhi na kuuwa watu 257.

Maafisa wamesema kuwa ndege hiyo imeanguka karibu na kituo cha ndege za kijeshi cha Boufarik muda mfupi baada ya kuruka.

Wizara ya ulinzi ya Algeria imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea kwenye eneo la Tindoufkusini mashariki mwa taifa hilo.

Mpaka wakati huu sababu za kuanguka ndege hiyo hazijaweza kufahamika.

Rais Magufuli amteua Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo tarehe 11 Aprili, 2018.

Prof. Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
11 Aprili, 2018

Serikali yakubaliana na Bulaya, yampa ahadi

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekubalina  na hoja iliyotolewa na Mbunge Ester Bulaya kuwepo kwa changamoto la upungufu wa walimu wa sayansi katika jimbo lake na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo kwa madai ni tatizo la nchi nzima sio kwake pekee.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Ole Nasha leo Aprili 11, 2018 kwenye kikao cha saba mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linafanyika Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la nyongeza la Bulaya aliyetaka kujua ni lini serikali itaamua kupeleka walimu wa sayansi katika jimbo lake kwa kuwa amechoshwa na wilaya yake kuwa miongoni inayofanya vibaya katika masomo hayo.

"Ni kweli upo uhaba wa walimu wa sayansi nchi nzima. Naomba nimuhakikishe Bulaya kuwa tunafahamu uwepo wa upungufu nasio katika Jimbo la Bunda pekee, kwa hiyo tutaendelea kuhakikisha kwamba upungufu huo tunaufanyia kazi ipasavyo", amesema Ole.

Kwa upande mwingine, Ester Bulaya amesema halmashauri yake imepata walimu ambao hawazidi hata 60 katika masomo yote na kuanza kufafanua kama ifuatavyo, walimu wa hisabati mahitaji ni 55 waliopo 20 pekee yake, fizikia mahitaji 27 waliopo 10, Biologia mahitaji 32 waliopo 15, huku akidai Chemistri kidogo ndio wamejitahidi kutoa walimu wengi kwa kuwa mahitaji 29 waliopo 21 bado 8.

Ni Dr. Chief Malunde Pekee Anaetibu Nguvu Za Kiume Na Kumtuliza Umpendae Kwa Kutumia Dawa Za Asili

$
0
0
"NI DR. CHIEF MALUNDE PEKEE ANAETIBU NGUVU ZA KIUME NA KUMTULIZA UMPENDAE KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI"
-baada ya kujichimbia katika nchi za kiarabu kwa zaidi ya miaka (10)sasa amewasili nchini na dawa za tiba asilia.
 
1/NGOLO 3 POWER-ni dawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, ina ubora wa hali ya juu wa kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wasiojiweza kufanya tendo la ndoa, inaimarisha misuli iliyolegea na kusinyaa, inarutubisha mbegu za kiume na kukufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15-25 kuwa na hamu na tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila kuchoka, inarefusha uume inchi 5-8 na kunenepesha hadi cm 4 kwa wenye maumbile madogo, dawa hii imeboreshwa na hutibu matatizo haya kwa muda mfupi tu.
 
2/MAGOYE MVUTO- dawa hii ina uwezo mkubwa sana kumvuta na kumtuliza aliekuacha awe mpenzi, mme/mke itamfanya akutafute mwenyewe ndani ya masaa 3tu na kukutimizia mahitaji yako kwa haraka na kumfunga asiwe na mtu mwingine.
 
3/SUPER LUBEJA- ni dawa ya kushepu umbo no.8 mguu wa bia, kuongeza hips, na makalio kwa muda wa siku 5tu unapata saizi uipendayo, kuondoa makovu, chunusi, harufu mbaya ya mwili michirizi, kupunguza tumbo na maziwa kwa siku 6tu.
 
4/NG'WESHI MIX- ni dawa ya biashara ya kupata wateja wengi, kusafisha nyota, kurudishwa kazini na kupandishwa cheo, kurudisha mali iliyoibiwa au kudhurumiwa.
 
PIA TUNATIBU MAGONJWA SUGU KAMA: vidonda vya tumbo, ngiri, chango na uzazi kwa kina mama: (dawa zote hazina madhara kwa mtumiaji) HUDUMA HIZI UTAZIPATA POPOTE ULIPO: TUNAPATIKANA DSM BUGURUNI SHELI AU PIGA SIM NO_ 0763-181099.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0766340868

Baada Ya Kuficha Mahusiano Yao Kwa Muda Mrefu, Hatimaye Nandy na Bilnass Wayaanika

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy anayetokea nyumba ya vipaji THT na mpenzi wake rapa Billnas hatimaye wameanika penzi lao hadharani baada ya kulificha kwa muda mrefu.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi kuwa Nandy na Billnas wana mahusiano ya kimapenzi na hata picha zao wakiwa maeneno sawa kwa wakati mmoja zilisambaa lakini kila mmoja alikana mahusiano hayo na kusisitiza kuwa ni marafiki.

Lakini waswahili wanasema mapenzi kikohozi kwani baada ya kuficha kwa muda mrefu hatimaye wawili hao wameonekana wakiwa pamoja kwenye picha ambazo wameposti Kwenye mtandao wa Instagram.

Leo ni siku ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Billnas kama ilivyo desturi Nandy kamtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy kamuandikia ujumbe wa heri na kusindikiza na picha yao:

DNA Yamponza Mchungaji Msigwa

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa leo ameharibu hali ya hewa bungeni wakati akichangia Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, Utawala Bora, baada ya kusema viongozi walio kwenye ofisi za umma hawana sifa ambapo kabla hajamalizia baadhi ya wabunge walianza kuzomea wakisema; ‘DNA, DNA’.

Hali hiyo iliendelea na kumfanya Mchungaji Msigwa kukatishwa mara kadhaa na wabunge waliokuwa wakiomba mwongozo na wengine kutoa taarifa, jambo lililofanya Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kutumia muda mwingi kuwatuliza wabunge waliokuwa wakizomea ama kuangua vicheko.

Hali ya hewa ilianza kuchafuka baada ya Mchungaji Msigwa kusema; “unamchukua mtu kama Kitila (Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji) unampeleka kwenye Wizara ya Maji, anakaa ofisini badala ya kuzungumza mambo ya kumtua mama ndoo ambalo ni wazo zuri, yeye anakazana anataka amjibu askofu kwa sababu ya mawazo aliyotoa kwamba hakuna demokrsia,”.

Mchungaji Msigwa alikatishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Injinia Stella Manyanya, aliyeomba mwongozo akisema mzungumzaji anaingiza jambo ambalo halipo kwenye mjadala.

“Mheshimiwa tunza heshima yako usiharibu hii ajenda, jikite kwenye ajenda iliyo mezani,” alisema Injinia Manyanya.

Baada ya Mwenyekiti kumruhusu Msigwa kuendelea kuzungumza, alianza kwa kusema “haya ndiyo mambo ninayozungumza, dada yangu namheshimu sana na ni mhandisi lakini anashindwa kuunganisha utawala bora ninaozungumzia na mifano ninayotoa, hizi ndiyo appointment (uteuzi) ninazozungumzia, yaani haelewi kabisa”.

Wakati akiendelea kuchangia, ziliendelea kusikika sauti za baadhi ya wabunge wakisema DNA, DNA.

Msigwa aliendelea kusema; “mtu kama Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, anatumia vibaya ofisi ya umma kwa kugawa kadi za CCM na kusema hatashirikiana na wapinzani huo si utawala bora”.

Baada ya kauli hiyo, Mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini, Vuma Augustino,  aliomba kumpa taarifa Msigwa ambapo alisema Mkuu wa Mkoa ni mjumbe wa kamati ya CCM ya mkoa hivyo ana haki ya kutimiza wajibu wake.

Msigwa alimjibu kwa kusema anarudia kuwa hayo ndiyo alikuwa akiyazungumzia, na kumuita mbunge huyo kuwa kijana mdogo msomi lakini anashindwa kutofautisha kazi ya Mkuu wa Mkoa na shughuli za CCM na kuongeza kuwa hiyo  ni huzuni hawezi kuelewa.

“Unamchukua mtu kama Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda), kila siku anaharibu, alianza madawa ya kulevya….,” sauti za DNA, DNA zilianza tena na wakati huu zikiwa nyingi zaidi na kumfanya ashindwe kuzungumza.

Mwenyekiti wa kikao hicho, alitumia takribani sekunde 10 kutuliza wabunge.

Msigwa aliendelea kuzungumza akisema kama suala ni DNA yuko tayari na anaweza kushughulika vizuri, huku kelele nyingi zikisikika kutoka upande wa CCM.

Baada ya hapo, Mbunge wa Siha Dk. Godwin Mollel, aliomba kutoa taarifa ambapo kabla hajasimama kuanza kuzungumza, Msigwa alisikika akimuuliza “kwani Mollel na wewe unataka kupimwa mbegu,” jambo lililozua kelele zaidi.

Akitoa taarifa yake, Dk. Mollel alisema wabunge hao wa Chadema wanachangishwa Sh milioni 75 kwa mwezi lakini wameshindwa kuajiri watu wanne wa kuwaandalia hotuba zao.

Wakati akiendelea baadhi ya sauti zilisikika zikisema “Dk. Shika, Dk. Shika” hali iliyosababisha wabunge wengi zaidi kuangua vicheko.

Baada ya wabunge kutulia, Dk. Mollel alisema; “mimi siendi kwenye DNA kwa sababu ni mambo binafsi,” kauli hiyo ilifanya aendelee kuzomewa jambo lililomkatisha kwa muda na baadaye kuendelea kwa kusema “umesikia mazuzu na misukule wananizomea.”

Kauli hizo zilifanya wabunge waangue kicheko huku wengine wakisema; “njaa, njaa,”.

Msigwa alipopewa nafasi ya kuendelea kuzungumza alianza kwa kusema anaomba kumsaidia Dk. Mollel huku akimuita bidhaa anayenunuliwa kama karanga barabarani huyu, mwanaume mzima ananunuliwa kama karanga.

“Hotuba ya Serikali haijaandaliwa na waziri imeandaliwa na timu kubwa, leo mnataka sisi tuandae kwa dakika moja kwasababu mnaona tunafanya mchezo hapa, nakupuuza wewe sijui Dokta wa wapi wewe,” alisema Msigwa.

Baada ya kumaliza kumjibu Mollel, aliendelea na mjadala wake akizungumzia ushauri waliotoa kwa serikali juu ya sekta ya madini.

Hata hivyo, alikatishwa tena na Jackline Ngonyani, aliyeomba kutoa taarifa akasema “nilitaka kumwambia Msigwa utawala bora anaozungumzia ni suala la msingi, lakini unapoanza kunyoosha kidole kwa mwenzako vidole, vingine vinakurudia wewe, angeanza mwenyewe kwenye suala la DNA, Dar es Salaam ameshaenda  na yule inasemekana ni mke wa mtu.”

Msigwa alipopewa nafasi ya kumjibu alisema “nataka nimwambie Mbunge, mama niko vizuri sana, kama unataka suala la DNA niko vizuri labda kama unataka vitu vingine nako niko vizuri.

“Anayetaka kuja aje tu, kama mnadhani hiyo ni kiki mnapoteza muda, sasa na Mawaziri wote tutawapima DNA humu ndani si mnataka tupimane, hamna shida.

“Ninachozungumza ndiyo haya, tunaacha kuzungumza mambo ya msingi ya nchi, tunazungumza mambo ya msingi watu wanakufa mnahangaika na DNA yangu,” alisema Msigwa.

Makonda: Wanaume Watakaogoma Kuja Mimi Ntaenda Kuwakamata

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefunguka na kuweka wazi kuwa kuanzia kesho April 12 viongozi mbalimbali wataanza kusambaza barua pamoja na kuwapigia simu wababa ambao wameshtakiwa na wanawake kutelekeza watoto na kusema ambao watagoma kufika ofisini kwake yeye atawakamata.
 
Paul Makonda amesema hayo alipokuwa akiongea na umati mkubwa wa mama ambao wamefika ofisini kwake na kusema kwa siku mbili hizi tayari wameshaweza kusikiliza wanawake zaidi ya elfu moja mia nne na kuwataka wamama hao wamepofika ofisini kwake wawe huru na kuongea mambo yote wasiogope wala kupangiwa mambo ya kuzungumza.

"Wale watakao itwa na wakakaidi kuja mimi nitakwenda kuwakamata kwa hiyo wababa niwaombe tu tusipimane ubavu, msipime nafasi yangu kama ina nguvu au haina nguvu na wale wanaotaka mambo ya siri tunza mwanao ndiyo siri pekee, wewe umetelekeza watoto wamejaa mtaani, wengine wamekuwa ombaomba, wengine wanapelekwa vituo vya vya watoto yatima wakati wazazi wake wapo halafu unajidai kwa akili zako timamu hili jambo la falagha una akili sawasawa kweli? alihoji Makonda

Aidha Makonda amesema kuwa kwa jana na juzi watu maarufu ambao hawataki kuguswa na watu wenye heshima zao tayari wamefika mia moja na saba, Makonda amedai kuwa wapo watu kati ya hao 107 wamekuwa wakihitaji kukutana naye chemba au waje ofisi kwa nafasi za pekee hivyo amesema kuwa hataki kukutana na mtu yoyote chemba wala kupigiwa simu bali wanapaswa kufika ofisini kwake.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 12

Wolper: Nisha Hana Vigezo Vya Kutembea na Brown

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa Salma Jabu  maarufu kama Nisha Bebe hana vigezo vya kutembea na Ex boyfriend wake Brown.

Wiki iliyopita picha za Nisha na Brown zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha wakiwa wanakumbatiana na hata kubusiana jambo lililozua maneno huku ikisemekana kuwa ni wapenzi.

Lakini mwishowe Nisha aliachia wimbo wake wa Bachela ambapo ilionekana kuwa Brown alikuwa ni video king Kwenye video hiyo na wawili hao baadae walikana tetesi zozote za Mahusiano ya kimapenzi wakidai ilikuwa ni kazi tu.

Hatimaye Wolper amefunguka kuhusiana na Mahusiano hayo na kuweka wazi kuwa haamini kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Wolper amedai kuwa Nisha ni mchekeshaji hivyo haamini kabisa kama anaweza kutoka na mwanamitindo huyo na pia anazijua taype za wanawake wanaoweza kutembea na Brown haifanani kabisa na Nisha.

Serikali Kuzifutia Usajili NGOs Zitakazofanya Kazi Kinyume Na Sheria.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.

Bw. Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.

Ameongeza kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.

“Nawataka wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema Bw.Katemba

Bw.Katemba amesema kuwa mpaka sasa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 4,868 ndio yamehakikiwa na kuyataka Mashirika ambayo hayajahakikiwa  yafanye utaratibu wa kuhakiki kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa Tovuti mpya ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Mashirika ambayo hayatakuwa yamehakikiwa hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.

Naye mdau kutoka Shirika la Baraka Orphanage Bi. Patricia Kamugisha asema kuwa kikao hicho imewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawajafahamu na kuendelea kupata uzoefu utakaowasaidiza kuimarisha utendaji wa shughuli katika mashirika yao.

“Sisi kama wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali tunatakiwa kuzingatia Sheria na Taratibu zilizopo ili tuweze kufanya kazi bila kukinzana na Sheria” alisisitiza Bi. Patricia.

Dongo Janja Amtaka Irene Uwoya Achore Tatoo ya Jina Lake Sehemu Nyeti

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ameonekana kuzidi kukolea kwa penzi la mume wake Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja kwani jana ameonyesha tattoo ya Jina lake aliyochora.

Siku za hivi karibuni Uwoya na Dogo Janja wameonekana kuweka mambo yao hadharani kidogo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tangu ndoa yao ifungwe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameanika tattoo hiyo iliyochorwa na Uwoya kwenye maeneno ya bega iliyoandikwa Jina halisi la Dogo Janja ambalo ni Abdul.

Dogo Janja amemshukuru mke wake kwa kuchora tattoo ile na kumtaka amchoree tattoo nyingine lakini safari hii iwe kwenye maeneo nyeti kabisa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>