Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu: Ujenzi Wa Ukuta Mererani Umeokoa Mamilioni ...Mapato Yamepanda Kutoka Sh. Milioni 147 Hadi Sh. Milioni 714

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Mererani kutasaidia kuongeza mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya wizi na utoroshaji wa madini ya Tanzanite.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo uliozinduliwa Aprili 6, mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutasaidia pia kudhibiti ulanguzi na biashara ya magendo pamoja na kuimarisha usalama kwenye mgodi, kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Tanzanite.

“Kukamilika kwa ujenzi huo pia kutasaidia kuongeza mapato ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, Serikali imekusanya takriban shilingi milioni 714 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi milioni 147.1 kwa mwaka mzima wa 2017,” alisema.

Waziri Mkuu alisema kabla ya ujenzi huo, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya madini ya Tanzanite yaliyokuwa yanazalishwa kila mwaka, yalitoroshwa kwa njia za panya na Serikali yetu haikuambulia chochote. “Hii ni kutokana na kukosekana udhibiti wa kutosha wa madini ya tanzanite kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwa wauzaji,” alisema.

Alisema mbali na kuwepo kwa eneo la wachimbaji ndani ya ukuta wa Mererani, pia kutajengwa maduka ya Tanzanite na viwanda vya kuongeza thamani, hususan vya ukataji, uchongaji na ung’arishaji. Vilevile, kutakuwa na maeneo ya burudani ambayo yatastawisha zaidi biashara ya Tanzanite na kuwavuta watalii wengi kwenda kutembelea eneo hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) itakayokuwa na urefu wa km. 1,219 utarahisisha usafiri wa mizigo na abiria na kuongeza itaongeza biashara hapa nchini pamoja na nchi za jirani.

Waziri Mkuu alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kusafirisha tani milioni 17 kwa mwaka, ikilinganishwa na tani milioni tano za sasa na kwamba utaongeza mapato kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kutunza barabara ambazo zimekuwa zikiharibika mapema kutokana na kusafirisha mizigo mizito.

“Reli hii ya kisasa itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa takriban tani 10,000 kwa mara moja, ambayo ni sawa na malori (semi trailers) 500 yenye uwezo wa kubeba tani 20 kila moja. Hii, itasaidia sio tu kutunza barabara zetu bali pia kupunguza gharama za kukarabati barabara hizo mara kwa mara,” alisisitiza.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Akemea Upotoshaji Kuhusu Muungano .....Awataka Waulinde, Aonya Sukari Isiwe Sababu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waulinde Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na akawaonya wasitumie Bunge hilo kuupotosha.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

Waziri Mkuu amesema mjadala ulioibuka jana kuhusu suala la Muungano haukuwa na afya na kwamba hatarajii kuona hali hiyo ikijirudia tena Bungeni kuhusiana na suala la Muungano.

“Mjadala wa jana sijaupenda kabisa na wala haukuwa na afya, ulikuwa ni malumbano baina waheshimiwa wabunge wawili. Hatuzuii Mhe. Mbunge kuuliza jambo ili apate ufafanuzi lakini pia haturuhusu mtu na mtu watumie Bunge kupotosha ukweli wa mambo,” alisisitiza.

Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba kuna maboresho ambayo yanafanywa hivi sasa na Serikali za pande zote mbili lakini akatumia fursa hiyo kulihakikishia Bunge kwamba majadiliano bado yanaendelea kwenye vikao halali vya SMT na SMZ ambavyo vinaongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha malumbano hayo, Waziri Mkuu alisema kiini cha malumbano hayo ni suala la uagizaji sukari kutoka nje ya nchi ili kufidia upungufu wa sukari uliopo nchini (gap sugar). Alisema katika kutimiza azma hiyo, Serikali haiangalii kama muagizaji ametoka Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika mwaka 2016, upungufu uliojitokeza ulikuwa tani 140,000 lakini waagizaji waliopewa vibali walikuwa wawili kutoka Zanzibar, watatu kutoka Bara na kiwanda cha sukari cha Mahonda kilipewa kibali cha kuagiza tani 390.

“Katika mwaka 2017, gap sugar ilikuwa tani 140,000 na waliopewa vibali walikuwa ni wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara, lakini kwa mwaka huu (2018) gap sugar ni tani 135,000. Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii tumewapa vibali wenye viwanda ndiyo waagize sukari kutoka nje. Kwa hiyo, jambo hili la sukari lisivuruge Muungano wetu,” alisisitiza.

Waziri Mkuu alisema nia ya Serikali ni kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini ili nchi ijitegemee na kawataka Mawaziri wa Biashara wa Zanzibar na Tanzania wawe makini ili sukari inayoagizwa nje isije kufurika soko la ndani kwa sababu gharama za uzalishaji sukari ya ndani ni kubwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri azungumzia maandamano ya Mange Kimambi bungeni

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amefunguka na kutoa ushauri kuhusu suala la maandamano na kusema kuwa mtu yoyote ambaye ana ratibu maandamano lazima afuate sheria hata kama maandamano yanatambulika kikatiba.

Jenista Mhagama amesema hayo bungeni na kudai kama kila mtu ataamua kuandamana kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu hilo litakuwa jambo ambalo si sawa hivyo amevitaka vyama vya siasa kufuata sheria za nchi na si kuvunja sheria za nchi.

"Suala la maandamano katika nchi yetu ya Tanzania linaratibiwa na sheria za usalama ndani ya nchi chini ya vyombo vya usalama hasa polisi na Katiba haiwezi kuchukuliwa kwamba ni kigezo cha kuviruhusu vyama kufanya maandamano bila kuzingatia taratibu na sheria zilizowekwa.

"Ninaomba sana Watanzania wote na niviombe vyama vyote vya siasa katika nchi yetu ya Tanzania wahakikishe wanazingatia sheria. 

"Katiba yetu imeruhusu maandamano lakini maandamano yameratibiwa kisheria na kama yameratibiwa kisheria lazima tuhakikishe kwamba tunazingatia sheria katika kuratibu maandamano nchini kwetu Tanzania"

Jenista Mhagama aliendelea kutoa maelezo kuhusu masuala ya maandamano

"Labda niulize swali moja tukiamka hapa siku moja asubuhi na kila mtu ameamua kuandamana wakulima, wafanyakazi yaani kila mtu aamue tu kuandamana kwa sababu tu Katiba imesema nadhani itakuwa siyo sawa na nichukue nafasi hii kuviomba vyama vya siasa kuheshimu Katiba na sheria katika kutekeleza wajibu wao na siyo kuvunja sheria za nchi yetu Tanzania"

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya April 11

Dansa Wa Diamond Naye Kakumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto

$
0
0
Dansa kutoka WCB ambaye ni mchezo shoo wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zungu amekumbwa na skendo ya kuwa mmoja kati ya wanaume waliotelekeza watoto wao Dar.

Siku ya jumatatu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda aliwakusanya wanawake wote ambao wametelekezwa na wanaume ambao wamezaa nao ambapo hawawahudumii watoto wao.

Mmoja kati ya Wanawake waliojitokeza ni mwanamke ambaye alijitambilisha kama mzazi mwenza wa Dansa wa  Diamond anayejulikana kama Zungu ambapo alidai alimtelekeza yeye pamoja na mtoto wake baada ta kuachana ambapo amekuwa hataki kumtunza mtoto wake.

Baada ya tuhuma hizo Zungu alitafutwa na Timamu Tv ambapo amefunguka na kusema yule mwanamke ana matatizo ya akili pia ni mkorofi na amedai kuwa hajawahi kumkataa mtoto wake na amesema yupo tayari hata leo kwenda kwa Makonda na kujielezea na kama ikitokea anatakiwa amchukue mtoto wake amesema yupo tayari kumlea mwanaye mwenyewe.

Aliyezaa na Mchina awa gumzo mitandaoni

$
0
0
Kambi  ya siku tano inayoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwatafuta wanaume waliotelekeza watoto wao imempa umaarufu mitandaoni msichana aliyejitambulisha kwa jina moja la Safina.

Picha za msichana huyo ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu alipoonekana nje ya ofisi za Mkuu wa Mkoa juzi asubuhi akiwa na mtoto wake anayefanana na Mchina.

Mwanamke huyo alipigwa picha akiwa amekaa kwenye ofisi hizo na mtoto wake huyo akisubiri foleni ya kupata msaada kutoka kwa wanasheria, maofisa ustawi wa jamii na polisi kutoka Dawati la Jinsia.

Baada ya picha hiyo kusambaa iliibuka mijadala kwenye mitandao hiyo wengi wakihoji kama kweli baba wa mtoto huyo atakuwa Mtanzania.

Baada ya muda kupita, ujumbe wa video iliyomrekodi msichana huyo ulisambaa akielezea alivyokutana na Mchina huyo na kuanzisha uhusiano ambao hatimaye ulisababisha kupatikana kwa mtoto huyo.

Kwenye ujumbe huo, msichana huyo alisema alikutana kwa mara ya kwanza na mchina huyo mwaka 2013 alipokuwa akifanyakazi kwenye kampuni ya ujenzi ya Hainan kutoka China.

Alisema wakati huo kampuni hiyo ilikuwa ikijenga majengo maeneo ya Gongolamboto jijini Dar es salaam na baadaye walihamia mkoani Dodoma na kuendelea na maisha.

"Nilikaa na baba yake huyu mtoto miaka mitatu mkoani Dodoma hadi alipopata matatizo na kuamua kurudi kwao China.... aliniambia atarudi na atanitafuta kwa njia ya simu lakini hadi leo sina mawasiliano naye," alisema.

Safina alisema anamlea mtoto huyo katika mazingira magumu bila msaada kwa kuwa mtoto huyo hana ndugu yeyote wa upande wa baba hapa nchini.

Safina alikuwa akizungumza huku akionyesha picha mbalimbali zinazoonyesha hatua za mahusiano yao, ikiwemo inayomwonyesha mzazi mwenzake akiwa amembeba mtoto huyo alipokuwa mchanga huko mkoani Dodoma.

Pia alikuwa akiwaonyesha waandishi wa habari vibali vya muda vya ukaazi alivyokuwa akitumia raia huyo wa China alipokuwa akifanyakazi nchini ambavyo vimeisha muda wake.

Msichana mwingine ambaye ujumbe wake wa video umesambaa ni Mwajuma Mohamed ambaye alisema kuwa ametelekezwa na mzazi mwenzake hivyo utaratibu ulioanzishwa na Mkuu wa Mkoa ni ukombozi kwao.

Alisema kwa sasa maisha ni magumu na kwamba ingawa yuko hai lakini anashindwa kuyamudu na kuhoji kuwa itakuwaje kama ikitokea akafariki na kumwacha mtoto wake bila baba.

Anahofu anaweza kuwa mtoto wa mitaani, alisema zaidi.

"Nawaambia wanaume huko waliko waache kutubebesha mimba na kututelekeza, huyu mtoto sijazaa na mzazi wangu nimezaa na wewe mwanaume uliyenikimbia, yaani nina dukuduku natamani nimkamate huyo mwanaume nimkamue ili aone uchungu wa maisha," alisema Mwajuma.

Awali, kambi hiyo ilipangwa kufanyika kwa siku tatu lakini kutokana na wingi wa wanawake waliojitokeza Makonda alitangaza iendelee kwa siku tano mfululizo ili kuhudumia wengi zaidi.

Wanawake hao wanapewa msaada wa kisheria na wanasheria mbalimbali, polisi na maofisa wa ustawi wa ajamii.

Thea Atoa Pongezi Zake kwa Makonda ....... Ni Baada ya Kampeni ya Kusaidia Wanawake

$
0
0
Msanii wa bongo movies Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea ameandika ujumbe mrefu kwa ajili ya kumpongeza Mh Paul Makonda baada ya kuanzisha kampeni ya kusaidia wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao na kuwaachia watoto kulea peke yao.

Thea aliandika hivi kuhusu kampeni hiyo ya Mh Paul:
"Kwanza nimpogeze mheshimiwa paul makonda kwa kujitolea na kulikumbuka kundi hili la wanawake waliojitokezwa, kwakweli tatizo hili ni kubwa sana  na kumuachia Mh Makonda peke yake haitwezekana kwa sababu tatizo sio kwa dar peke yake bali ni Tanzania nzima.

"Niombe wadau wa maendeleo ya wanawake tanznia kutafuta suluhu ambayo ni endelevu kwa tatizo hili.upo ukatili unaotokea kama ajali lakini ukatili huu mwingi kwa wanawak na wasichana utokana na umaskini.

"Wanawake hawa waliojitokeza leo inamaanisha kuwa hawajaweza kumudu mahitaji ya msingi, nitoe wito kwa wanawake na wadau wengine kumuunga mkono Mh Paul Makonda ili kuweza pia kuwakwamua wanawake hawa kiuchumi.

"Tuwasaidie wanawake hawa kuwa na uchumi imara kwa sababu sio wanaume wote wanakataa kutoa matunzo kwa makusudi, wengine wamekuwa wakiyumba.

Hata hivyo kutokana na kampeni hii kila mtu amekuwa na muonekano tofauti kwa sababu wapo wanaosapoti na pia wapo wanaosema zoezi haliwezi kumaliza tatizo.

Wafanyakazi wa TPA, mtoto wa Kova, watinga mahakamani kwa uhujumu Uchumi

$
0
0
Wafanyakazi  watatu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), akiwamo Masoud Kova (36) na wenzao, jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kughushi.

Mashtaka mengine ni kujipatia fedha na kuisababishia TPA hasara ya Dola za Marekani 15,618.76 (Sh. 26,041,782.73) baada ya kupitisha kontena 16 bila kulipa ushuru.

Mbali na Kova, washtakiwa wengine ni Lydia Kimaro (52), Ally Mkango (54), Aron Lusingu (35) na wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Grace Komba (41) na Juma Ng 'oka (41).

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Kombakono akisaidiana na Inspekta wa Polisi, Hamis Said.

Katika shtaka la kwanza na la pili, Kombakono alidai kuwa yanawakabili Kimaro na Kova kwamba kati ya Agosti na Septemba, 2014 walitoa taarifa ya uongo kuonyesha kwamba TPA imepitisha nyaraka za malipo ya Dola za Marekani 15,618.76 (Sh. 26,041,782.73) kwa kampuni ya Freight Forwarders (T) Ltd.

Katika shtaka la tatu, ilidaiwa kuwa kati ya Septemba na Oktoba, 2014, jijini Dar es Salaam washtakiwa wote sita walijipatia dola hizo baada ya kudanganya kuwa fedha hizo ni malipo ya ushuru wa bandari kupitia akaunti ya TPA iliyopo benki ya CRDB.

Shtaka la nne, ilidaiwa kuwa kati ya Septemba na Oktoba, 2014 mshtakiwa Mkango na Lusingu wakiwa waajiriwa wa TPA walishindwa kuzuia kufanyika kosa na kusababisha kampuni ya Freight Forwarders (T) Ltd kupitisha kontena 16 bila kulipa ushuru wa dola hizo.

Upande huo wa Jamhuri ulidai katika shtaka la tano, kati ya Septemba na Oktoba, 2014 jijini Dar es Salaam, kwa pamoja washtakiwa wote sita waliisababishia hasara hiyo TPA.

Washtakiwa walikana mashtaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka amewasilisha kibali cha kesi hiyo kusikilizwa na Mahakama ya Kisutu, haukuwa na pingamizi la dhamana.

Hakimu Simba aliwataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili na mmoja kati yao awasilishe Sh. milioni 2.2 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

Alisema kesi hiyo itatajwa Aprili 25, mwaka huu na washtakiwa walitimiza masharti ya dhamana.


Rais Magufuli Kuzindua Rasmi Taasisi Ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) Ikulu

$
0
0
RAIS Dk. John Magufuli  anatarajia kuzindua rasmi  Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete ulioko Ikulu, Dar Es Salaam.

Rais mstaafu Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya JMKF na uzinduzi huo rasmi utahusisha maofisa waandamizi wa Serikali, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania na hasa mabalozi wa Afrika ambako Taasisi hiyo inalenga kufanya kazi mbali ya Tanzania, wakuu wa taasisi mbali mbali za kimataifa, wadau wa Taasisi ya JMKF, wakuu wa asasi zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) na wakuu wa taasisi za kijamii wakiwemo viongozi wa dini.

Taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Pioneer Communications Limited kwa niaba ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)imesema uzinduzi huo  utafuatiwa na chakula cha jioni ambacho Rais Magufuli atawaandalia wageni watakaohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi, akiwemo Rais Kikwete mwenyewe na mkewa Mama Salma Kikwete.

"Taasisi ya JMKF iliyosajiliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka Februari, 2017, ilianza kazi Machi, mwaka jana wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Wadhamini ya Kimataifa ya Taasisi hiyo ilipofanya kikao chake kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt mjini Dar Es Salaam,"imesema taarifa hiyo.

Imeongeza taasisi hiyo inayolenga kufanya kazi na kuelekeza nguvu zake katika maeneo matano, itaanzia na maeneo matatu ambayo ni Afya ya Mama na Mtoto, Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji wa Wakulima Wadogo katika maeneo ya vijijini na mashambani katika jitihada zao za kujinasua katika umasikini ama kupunguza athari na madhara ya hali ya umasikini.

"Mheshimiwa Kikwete anasaidiwa katika uendeshaji wa Taasisi hiyo na Bodi ya Wadhamini yenye sura ya Kimataifa ambayo wajumbe wake wanatoka nchi za Tanzania, Marekani, Afrika Kusini, Ureno na Malaysia.Wadhamini hao ni Balozi Ombeni Sefue aliyepata kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi wa Tanzania katika  Canada na Marekani.

"Pia Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa miaka mingi, Profesa William Mahalu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustine mjini Mwanza na Balozi Mwanaidi Sinare Majar ambaye amepata kuwa Balozi wa Tanzania katika Uingereza na Marekani,"imefafanua.

Wengine ni Mfanyabiashara maarufu Abubakar Saidi Bakhressa, Balozi Charles R. Stith aliyepata kuwa Balozi wa Marekani katika Tanzania, Msomi na Mtumishi wa Umoja wa Mataifa Bwana Carlos Lopez, Waziri mwandamizi katika Serikali ya Malaysia, Dato Sri Idris Jala na  Mtaalamu wa Masuala ya Fedha kimataifa Genevive Sangudi, Mtanzania mwenye makazi yake Afrika Kusini na Marekani.

Kutokana na kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Udhamini Machi mwaka jana, wataalamu mbali mbali pamoja na washauri wa kila aina, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa JMKF,  Omari Issa wamekuwa katika matayarisho makubwa ya kuandaa nyaraka mbali mbali za msingi za kuongoza dira na dhima ya Taasisi hiyo kwa ajili ya uzinduzi rasmi na kwamba shughuli hiyo ya Ikulu itatangazwa moja kwa moja kwenye Televisheni ya Taifa ya TBC na vyombo vingine.

Tundu Lissu Apasuliwa Tena Mguu ....Amshukuru Mungu kwa Kumpigania

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kwa amara nyingine tena, leo Aprili 11, 2018 ataingia kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kufanyiwa oparesheni ya mguu wake wa kulia ambao bado una matatizo kutokana na risasi alizopigwa Septemba 7 mwaka jana nyumbani kwake, Area D, Dodoma.

Lissu ambaye ameshafanyiwa upasuaji mara kadaa katika Hospitali ya Nairobi nchini kenya kisha Ubelgiji, amesema kwamba oparesheni hiyo ni sehemu ya tiba ya mguu huo huku akieleza kuwa kwenye mikono yuko salama kitabibu. 

==>>Hii ni Kauli yake 

Habari za leo popote mlipo wapendwa wangu. .
Napenda kuwajulisha kwamba ndani ya nusu saa ijayo ninaingia kwenye operesheni nyingine tena. .

Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na 'watu wasiojulikana.' Operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo. .

Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. .

Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu tarehe 7 September ya mwaka jana. Na hili pia litapita. .

Wasalaam.

Ogopa Mapenzi ya Kichawi

$
0
0
NIMEFANIKIWA  KUMRUDISHA  MWANAUME  NILIE MROGA MAPENZI  KATIKA  HALI  YA  KAWAIDA  KWA  NJIA  YA  MAOMBI.

Mwaka 2013 nilitoa  ushuhuda  wangu  katika  vyombo  mbalimbali  vya  habari  nikielezea jinsi nilivyo  kuwa  nikisubumbuliwa  na  ndugu  wa  mwanaume  niliye  mroga  kimapenzi na  kumfanya  kama  zezeta.

Ushuhuda  huo  ulisomeka  kama  ifuatavyo : OGOPA  MAPENZI   YA  KICHAWI.

Naitwa ,Mama Jessica, ni mwanamke mwenye umri wa miaka 35, mkaazi wa Tabata, Dar Es salaam.. Baada ya kuumizwa sana na wanaume katika mapenzi, niliamua kutafuta mganga wa kienyeji, shoga yangu alinipeleka kwa Mganga mmoja anayeitwa MUNGU WAKABILI, ambaye ni Mganga aliye bobea sana katika masuala ya UCHAWI NA UGANGA. 

Wakati naenda kumuona huyu mganga, tayari nilikuwa nimeanza uhusiano na mwanaume mmoja lakini na yeye akawa haeleweki heleweki. MUNGU WAKABILI, alinipa dawa ya mapenzi ambayo imenifanya nijutie kuitumia , kwani baada ya kumfanyia dawa mwanaume huyo, AMENIPENDA KUPITA KIASI! YANI AMEKUWA KAMA ZEZETA KABISA! 

Alikuwa na mke wa ndoa na watoto watatu, ila amewatelekeza wote na kuja kuishi na mimi. Nyumba aliyo jenga na mke wake ameiuza na kuninunulia mimi nyumba nyingine ili tuishi pamoja, kama hiyo haitoshi alikuwa na magari mawili moja amempa mdogo wangu wa kiume, jingine ameliuza na kunifungulia duka la nguo Kinondoni. 

Ni mambo mengi sana, yote siwezi kuelezea, ila kibaya zaidi ni kwamba, sasa ameshindwa kuendelea na biashara zake,anataka kuwa na mimi wakati wote kwa sababu amekuwa na wivu sana, anahisi akiniacha hata kwa dakika mbili tu nitaibiwa na mwanaume mwingine. 

Kibaya kuliko vyote sasa ndugu wa mume, mke wake na ndugu wa mke wake, wameanza kunitishia maisha yangu . Nilijaribu kwenda kumuomba huyu MUNGU WA KABILI anipe dawa ya kumrudisha huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida lakini amegoma kufanya hivyo, anasema yeye hawezi kuharibu dawa aliyo kwisha itengeneza tayari na kwamba alinionya mapema.. 

Hapa nipo njia panda na sijui hatma ya jambo hili, natamani nikimbie mji lakini nashindwa. Nimeamua kuandika waraka huu ili kwanza, kuwaonya wanawake wenzangu waachane na MAPENZI YA KICHAWI ili yasije kuwakuta kama yaliyo nikuta mimi, kwani naona wanawake wengi sana, wa Dar Es salaam, wanamkibilia mtu huyu kwa ajili ya kupata dawa za mapenzi.. 

Nakuonya usifanye hivyo mwanamke mwenzangu, kwani mtu huyu licha ya kuwa na umri mdogo tu tena wa miaka chini ya thelathini, lakini dawa zake ni za hatari sana na zina nguvu za ajabu sana! Usijaribu kabisa mwanamke mwenzangu, utaumbuka,kwani kila mtu atajua umetumia uchawi! Lakini, pili, ninawaomba wanawake wenzangu mnisaidie kumshawishi MUNGU WA KABILI ili amrejeshe huyu mwanaume katika hali yake ya kawaida.. 

Naweka namba za simu za MUNGU WA KABILI hapa na ninaomba sana, umalizapo kusoma waraka huu, umpigie simu au kumtumia meseji huyu Dokta. MUNGU WA KABILI kupitia simu yake ambayo ni 0744 000 473, mwambie, Mama Jesca anapata shida sana, na sasa ameanza kusambaza vipeperushi mtaani akielezea jinsi ulivyo mfanyia kitu kibaya. Naamini hili linaweza kumshawishi na hatimaye kumrudisha kaka wa watu kwenye hali yake ya kawaida.

MREJESHO : Nilikutana  na  watumishi  wa  Mungu ambao  kwanza  waliniombea  mimi  na  pia  wakasaidia  kumuombea  mwanaume  huyo na  kuvunja   vunja  vifungo  vyote  vya  kichawi nilivyo  kuwa nime mfunga  mwanaume  huyo   na  sasa mwanaume  huyo  amerudi  katika  hali  yake  ya  kawaida  kabisa na  anaendelea  na  maisha yake ya  kawaida.  Mwanaume huyo  pamoja  na  familia  yake, wote  wamenisamehe  na sasa  kila  upande  unaendelea  na  maisha  yake  kama  kawaida.

USHAURI  WANGU  KWA  WATU WOTE :  Ukiwa  na  shida  yoyote  mtegemee  Mungu. Usiende  kwa  waganga. Waganga  ni  mawakala  wa  shetani. Huwezi  kupata  chochote  kizuri  kutoka  kwa  shetani. Jiulize  swali  moja  fikirishi. 

Shetani  toka  alipo  asi  mbinguni  amekuwa  na  uadui  mkubwa  sana  na  wanadamu  na  lengo  lake  kuu  haswa  ni kuwaangusha  wanadamu  ili wasiweze  kuurithi  ufalme wa  Mbinguni.. 

Sasa  unadhani  kitu gani  cha  kumfurahisha  shetani  hadi  akupe  wewe  vitu  vizuri ? Chochote  kizuri  utakacho pewa  na  shetani  kitakuwa  cha  muda tu. Mrudie  Muumba  wako na  achana  kabisa  na  masuala  ya  imani  za  kishirikina  kwani  mwisho  wake  huwa  sio  mzuri  siku zote. 

ASANTENI  SANA.

Dada Amtaja Edward Lowassa Kumtelekeza...... Mtoto Mkubwa wa Lowassa Apangua Hoja

$
0
0
Mtoto mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Lowassa, ameshangaa mwanamke aliyejitokeza na kudai kuwa ni binti wa mwanasiasa huyo.

Aidha, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutumia vizuri mamlaka yake.

Kauli hiyo ya Fred imekuja  baada ya mwanamke mmoja mkazi wa Kigamboni, Fatuma Lowassa (31), kujitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, jana Jumanne Aprili 10, akidai kutelekezwa na baba yake ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.

Akiwa Monduli mkoani Arusha, Fred ametoa tamko akisema; “Nimesikia mwanamama mmoja akiongea kuwa yeye ni ndugu yetu kule Dar es Salaam.

“Kwa taarifa tu sisi watu wa Monduli kwetu watoto ni baraka na neema, nimeshangaa ametukosa ukoo mzima kujitambulisha.

“Namwambia Paul Makonda, nimetoka naye mbali sana, nasikitika sana anavyotumia nafasi yake vibaya kwa manufaa anayoyajua. Makonda nimekulea.” Ameandika Fred.

Mwanamke huyo amejitokeza jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikiwa ni mwendelezo wa Makonda kuonana na wanawake waliotelekezwa na watoto na waume zao.

Mwanamke huyo amesema yuko tayari kupima kipimo cha DNA na Lowasa kuthibitisha kama kweli ni baba yake huku akijinasibu kumtafuta baba yake huyo kwa muda mrefu bila mafanikio.

“Nilipeleka barua Ikulu kuomba kuonana na baba kipindi akiwa Waziri Mkuu lakini niliitwa mimi na mama katika Klabu ya Mamba iliyopo Kinondoni, alikuja mwanamume akiwa kwenye gari lenye ‘tinted’ akatuhoji mimi na mama akaondoka hakutupa majibu yoyote hadi leo,” amesema Fatuma.

Aidha, amesema aliwahi kukutana na Fred na akamuahidi kumsaidia lakini hadi sasa amekuwa kimya.

==>Msikilize Hapo Chini

Asilimia 5.8 ya Watanzania ni walemavu

$
0
0
Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu 2,641,802 sawa na asilimia 5.8 ya wananchi wote.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa ameliambia Bunge leo Jumatano Aprili 11, 2018  kuwa idadi hiyo inabainishwa kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ambayo ilijumuisha vipengele vya kuwatambua wenye ulemavu.

Amesema ulemavu umegawanyika katika makundi mbalimbali ambapo wenye ulemavu wa ngozi wapo 16,477 (0.04), wasioona  848,530 (1.19).

Amebainisha kuwa wasiosikia wapo  425,322 (0.97), wasioweza kutembea  525,019 (1.19), wanaopoteza kumbukumbu ni 401,931 (0.91).

Amesema idadi ya watu ambao hawawezi kabisa  kujihudumia ni  324,725 (0.74), ulemavu mwingine ni 99,798 (0.23).

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Khadija Nassiri Ali ambaye alitaka kujua Serikali kama inajua idadi kamili ya watu wenye ulemavu waliokuwa nao.

Msigwa afunguka kuhusu kutelekeza mtoto....Atishia Kujiuzulu Ubunge Kama Itathibitika Katelekeza Mtoto

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amejibu tuhuma za kutelekeza mtoto, baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao ikimuonyesha mtoto ambaye amefanana naye akitajwa kumtelekeza.

Msigwa amesema kwamba alichokiandika kwenye mitandao ya kijamii anamaanisha hivyo na  anamtaka mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa miongoni mwa walioenda kwa mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kwa kutelekezwa, asiishie hapo tu bali aende hata Bungeni.

“Ilikoanzia imeanzia kwa Jerry Muro ndiye kasambaza hizi habari, kitu ambacho nakijibu hapa amekianzisha Jerry Muro, sasa mimi nasema kama huyo mtu yupo, nimetoa namba zangu na kama sipatikani aje hapa Bungeni”, amesema Peter Msigwa.

Hapo jana Peter Msigwa ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema kwamba iwapo kweli mwanamke huyo yupo na akithibitisha ni kweli amemtelekeza, basi yupo tayari kujiuzulu ubunge wake alionao.

Serikali yaendelea kupigilia misumari suala la wanafunzi waliopata ujauzito kurudi shule

$
0
0
Serikali kupitia Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha imesema kuwa haitarajii kuwarudisha wanafunzi waliopata ujauzito shuleni kwa njia yoyote ile.

Akizungumza leo, Bungeni mjini Dodoma, Nasha amesema kuwa ukiruhusu hilo ni mwanzo wa kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule.

“Hata sisi serikali kwa kweli hatupendi kusikia vitendo vya uonevu dhidi ya watoto wa kike, kwasasa mfumo wetu wa elimu umepangwa katika namna ya kuhakikisha wanafunzi wanaopata ujauzito wanapata fursa ya kusoma lakini nje ya mfumo rasmi 

"Kwahiyo kuna fursa nyingine nyingi za kusoma kama nilivyosema katika swali langu la msingi kupitia elimu ya watu wazima lakini vilevile vyuo vya ufundi,“ amesema Nasha.

“Serikali haitarajii na naomba niweke wazi wanafunzi ambao wamepata ujauzito kwa njia yoyote ile hawataruhusiwa kuendelea na masomo  kwasababu ukifanya hivyo  una halalisha na kuhamasisha ngono mashuleni wakati mila zetu na sheria zetu haziruhusu ngono katika shule za msingi na sekondari.“

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO 0758840958 / 0785687900

Tiba ya Fangasi Sugu, Vidonda vya Tumbo, Kuondoa Chunusi na Nguvu za Kiume

$
0
0
MAKANGA 3 POWER: Hutibu nguvu za kiume dakika 10 na kupona  ndani ya siku 3. Huimarisha misuli ya uume iliyolegea, pia ipo dawa ya kurefusha uume mfupi nchi 4 handi nchi 7

Tuna tiba ya kudumu ya kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kuopata choo vizuri, busha( bila opareshen)

Pia tunatibu  kisukari, presha, muguu kuuma, fangasi sugu, vidonda vya tumbo, kupunguza unene, maziwa, kuondoa chunusi pete na cheni za bahati.

Onana na Dr. Shilindes shida zako zote zitakwisha.

Tupo Mbagala Rangi tatu:  0784460348  au 0659103360

Kauli ya Spika kwa wanawake waliotelekezwa

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai ametaka kina mama wenye malalamiko ya kutelekezewa watoto na wabunge wafike kwake au wamwandikie barua kuhusu suala hilo.

Hata hivyo, amesema watakapofanya hivyo wapeleke na cheti cha uthibitisho cha vipimo vya vinasaba (DNA) ili waone ni namna gani ya kushughulikia suala hilo.

Ndugai alisema hayo jana Jumanne Aprili 10, 2018 kabla ya kuahirisha kikao cha sita cha Bunge mjini Dodoma.

Katika kauli yake iliyoambatana na vicheko Spika alisema, “Kule Dar es Salaam kuna zoezi linaendelea, huko sasa kidogo kiti cha Spika kimetikiswa hivi. Tunatuhumiwa mahali, kidogo tumeguswa hivi kwa hiyo natarajia kupata ushauri wenu waheshimiwa tunafanyaje katika mazingira haya kwa maana kuna watoto wetu wako barabarani.”

“Haiwezekani hata kidogo, kwa hiyo kina mama wale inabidi tufanye utaratibu tujue nini tutafanya lakini pia kuna kina baba wamejitokeza huko nimesikia na baadhi ya walalamikiwa ni kina mama wabunge, kwa hiyo hili jambo halina upande,” alisema Ndugai.

“Hawa kina mama kama wapo, basi waje kwa spika au wamwandikie spika lakini waniletee na DNA test certificate (cheti cha uthibitisho cha vipimo vya vinasaba) ili tuone namna gani ya kuwezesha.

“Kuna mafungu hapa tumepitisha tunaweza kuangalia namna ya kuweka sawasawa ili waheshimiwa wabunge wawe na utulivu katika kufanya kazi za Bunge na si kuwa na mawazo mengine,” alisema.

Wanawake na wanaume wamekuwa wakijitokeza katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko kuhusu kutelekezewa watoto.

Akizungumzia suala hilo jana Aprili 10, 2018 mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema kati ya wanawake 480 waliosikilizwa 47 walidai wametelekezwa na wabunge.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images