Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mvua Dar es salaam : Nyumba 12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi zasombwa na maji

0
0
Nyumba 12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti jijini Dsm zimesombwa na Maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko hatarini kuanguka kutokana na Mmomonyoko wa Udongo unatokana na kupanuka kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika mtaa huo wamesema hali ni mbaya katika eneo hilo, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha huku mto huo ukiendelea kutanuka baada ya kuacha njia yake ya asili na kuingia katika makazi yao.

Diwani wa Eneo hilo Omar Kumbilamoto amesema walifanya juhudi za kupambana na mto huo kwa kuwashirikisha wananchi ambao kiasi cha Million 2 zilichangwa, lakini alidai baadhi ya watumishi katika manispaa hawakuonyesha ushirikiano na kuomba wizara ya mazingira chini ya ofisi ya makamu wa rais kuingilia kati.

Ommy Dimpoz Amfungukia Amber Lulu Baada Ya Kumwambia Hana Mvuto

0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amemjibu msanii mwenzake Amber Lulu ambaye wiki iliyopita alisema Ommy hana muonekano wa kiume.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jonijoo wiki iliyopita Amber aliulizwa kati ya Jux na Ommy Dimpoz ni mwanaume yupi ambaye anaweza akawa naye kimapenzi na moja kwa moja Amber Lulu alisema Jux kwa sababu Ommy hana muonekano wa kiume

"Jux sawa, Dimpoz hajakaa kama mwanaume, Ommy Dimpoz hawezi kukaa au kushindana na Jux ni zero, hana mvuto wowote , hamna chochote kinachonivutia kutoka kwake”.

Baada ya video clip hiyo kutrend sana ambayo ilikuwa inamuonyesha Amber akiongea hayo Ommy Dimpoz alijibu tuhuma hizo za Amber Lulu kuwa hana mvuto na hana muonekano wa kiume ambapo ameweka nyeusi kwa kusema hataki kumuongelea mtu huyo (Amber Lulu).

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka maneno haya:

"Mimi sijui chochote na sijui hizo stori zimetoka wapi na zimeanzia wapi lakini kikubwa sisi kama wasanii unajua kila siku vitu ambavyo vinatuzunguka ni mambo ya mitandao, kwa hiyo in short no comment”.

Mvua yauwa Watu wawili Jijini Mwanza

0
0
Wakati mvua zikiwa zinaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi na kusababisha mafuriko,  Jijini Mwanza watoto wawili wa familia moja wamefariki baada ya kudondokewa na ukuta kipindi mvua hizo zikinyesha zilizokuwa na upepo mkali.

Akizungumza kutoka kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema watoto hao wamefariki majira ya usiku wa April 9 wakati wakiwa wamelala katika nyumba waliyokuwa wanaishi katika mtaa wa Buguku kata ya Buhongwa wilayani Nyamagana Jijini Mwanza.

Kamanda Msangi amewataja watoto hao kuwa ni Mariam Saimon (4) pamoja na Musa Baraka (2) huku majeruhi wakiwa watatu katika tukio hilo.

Sakata la kufungiwa nyimbo za wasanii Laibuka Bungeni

0
0
Sakata la kufungiwa nyimbo za wasanii limeibuka bungeni na kusababisha kelele za wabunge pande zote.

Hata hivyo Serikali imeendeleza msimamo wake kuwa itaendelea kuzifungia nyimbo hizo ili  kulinda maadili ya nchi huku Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiwatuhumu wabunge kushabikia mambo ilihali wabunge wa mataifa mengine hawafanyi hivyo.

Mbunge wa Viti Maalumu Catherine Magige aliibua sakata hilo wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo ametaka kujua ni kwa nini Serikali imekuwa ikiwafungia wasanii na kama kamati ya maudhui imeshindwa kazi yake kwanini inasubiri hadi nyimbo zitoke.

Waziri Mwakyembe amesema Serikali haina vita na wasanii bali kinachofanyika ni kulinda utamaduni wa Mtanzania ili taifa lisiwe kokoro la kila mmoja.

Amesema baadhi ya mataifa yanafanya kazi kwa umakini katika kuangalia kazi za wasanii wao na baadhi wanafungiwa.

Dk Mwakyembe ametolea mfano wa wasanii kutoka Nigeria na Marekani pamoja na mkongwe Koffi Olomide ambao hivi karibuni baadhi ya nyimbo zao zilifungiwa.

Nyimbo ambazo zilifungiwa ni pamoja na Pale kati Patamu na Maku Makuz zilizoimbwa na Ney wa Mitego, kibamia wa Roma Mkatoliki,

Wimbo wa Amani Hamisi maarufu kama Manifango wa Hainaga Ushemeji pia umefungiwa, sawa na I am Sorry JK wake Nikki Mbishi.

Nyimbo nyingine ni Tema mate tumchape (Hamad Ali maarufu Madee), Uzuri Wako (Juma Mussa Mpolopoto maarufu Jux), Nampa Papa (Gift Stanford maarufu Gigy Money) na Nampaga (Barnaba Elias maarufu Barnaba).

Nyimbo za Diamond, ambaye jina lake halisi ni Nasib Abdul, zilizofungiwa ni Hallelujah (aliomshirikisha Morgan Heritage ) na Waka Waka (aliomshirikisha Rick Ross).

Hatua zitakazochukuliwa na serikali kwa vyombo vya habari vitakavyorusha matangazo ya kukera

0
0
Serikali imesema kuwa zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari kwa jamii hususani watoto.

Hatua mojawapo ambazo zitachukiwa na serikali ni pamoja na kutoa onyo, kufungiwa, kufungiwa kutoa huduma kwa kipindi kitakachotajwa au kufungiwa kutojihusisha kabisa na utangazaji.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mororogo Kusini, Prosper Joseph Mbena aliyehoji kuongezeka kwa matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari  na kwamba  baadhi ya matangazo hayo huwakera na kuleta hisia tofauti kwa baadhi ya watu hasa watoto kutokana na maudhui mabaya ya baadhi ya matangazo hayo

“Serikali tayari ina vyombo vya kusimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini yakiwepo maudhui katika matangazo vyombo hivyo ni mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ambayo iliundwa na Kamati ya Maudhui ya kifungu namba 26, Kamati hii inayosimamia maudhui na matangazo ya Kielekronic yaani redioni na Televisheni pamoja na mitandao ya kijamii,” amesema Shonza.

“Chombo cha pili ni bodi ya Filamu Tanzania ambayo inasimamia maudhui katika picha jengezi zinazoonyeshwa katika jumba la sinema, hadharani vilevile katika michezo ya kuigiza 

" Idara ya Habari Maelezo ni chombo cha tatu ambayo imewekwa chini ya kifungu cha sheria namba nne kifungu cha sheria ya habari namba 12 ya mwaka 2016 kinachosimamia maudhui katika machapishombalimbali yakiwemo magazeti, majarida pamoja na vipeperushi,” ameongeza.

“Zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika bila kutia shaka kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari kwa jamii

" Hatua hizo ni pamoja na kutoa onyo, kufungiwa, kufungiwa kutoa huduma kwa kipindi kitakachotajwa au kufungiwa kutojihusisha kabisa na utangazaji au uchapishaji wa habari pamoja na matangazo.

"Serikali inaendelea kuhimiza jamii nzima kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika kusambaza habari mbalimbali kwa jamii.”

Wanaume Nao Waanza Kumiminika kwa Makonda

0
0
Wanaume zaidi ya kumi wameibuka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulalamika kupokwa watoto, huku mamia ya wanawake wanaodai kutelekezewa watoto wakiendelea kumiminika kwenye ofisi za mkuu huyo wa mkoa.

Wanaume hao ambao wamefika leo Jumanne Machi 10, 2018 wamesema hawashindwi kulea watoto isipokuwa wake zao wamewapoka kwa madai ya umasikini.

Wamesema kama Makonda ameamua kuwasaidia wanawake basi ajue wapo wanaume wanaolia kunyanyaswa na wake zao.

"Mke wangu alinikimbia nilipougua miguu kiasi cha kushindwa kutembea, aliondoka na watoto wangu wote watatu, nimekuwa mtu wa mawazo kiasi cha kupata vidonda vya tumbo naomba awarudishe," amesema Tito Chemba, mkazi wa Kijichi jijini Dar es Salaam.

Tito (35), amesema ujio wake kwa Makonda ni kutaka kurejeshewa wanawe wanaoishi Bukoba kwa ndugu wa mkewe.

Mwanamume mwingine, Edmond Mbisho amesema mkewe aliondoka na mtoto wake tangu akiwa na miaka mitatu na sasa ana miaka sita.

“Ninachoomba ni kupata mwanangu si kingine, kwa sasa mwanamke anaishi na mtu mwingine," amesema.

Mwanamume mwingine, Vedasto Mdesa mkazi wa Iringa amesema watoto wake watatu waliozaliwa kwa pamoja walichukuliwa na ndugu wa mkewe na kupelekwa Urusi.

"Nilipokwa watoto kisa mimi ni masikini, hivi sasa naishi kwa tabu na sababu kubwa ni umasikini na wanasema sijasoma. Huyo mwanamke ana shahada na mimi ni mpiga picha nisiye na elimu," amesema.

OFA: Jipatie Riwaya Kali za Kusismua Toka kwa Mtunzi Makini

0
0
Nina kukaribisha kujiunga na group langu la hadithi lipatikanano whatsapp. Katika group kuna hadithi ya TANGA RAGA RAHA SEASON TWO na SIN. Kama ume soma TANGA RAHA season one hadi mwisho sasa ni wakati wako wa kuendelea na Tanga Raha(RETURN OF OLVIA HITLER). Ukijiung leo utapata ofa ya episode 80 bureee kabisa. Ada ya group kwa mwenzi ni sh 4000 tu.
 
Wasiliana nami whatsapp 0657072588 au 0768516188.

Pia pata kitabu cha President wife muendelezo wa Sorry Madam season two. Kitabu cha President wife kina patikana kwa sh 8000 tu.

Wahi sasa ofa hizi kwani ni kwa siku ya leo tu. Malipo ya huduma zote ni kupitia MPESA 0768516188 JOYCE MBWAMBO au TIGOPESA 0657072588 AZARIA MSULWA.

Karibuni sana
BY EDDAZARIA G.MSULWA

Serikali Yamjibu Nape Nnauye Mradi Wa Stiggler’s Gorge

0
0
Serikali imemjibu Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM), kuwa mradi wa uzalishaji umeme wa maji wa Stiggler’s George upo katika Ilani Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Majibu hayo yametolewa bungeni leo na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ikiwa ni siku moja baada ya Nape kuukosoa mradi huo akisema unatekelezwa wakati haupo kwenye ilani ya chama hicho na kuachwa ule wa gesi ulio kwenye ilani hiyo.

Akijibu hoja hiyo na baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge waliokuwa wakichangia Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu inayotarajiwa kupitishwa na Bunge leo, Dk. Kalemani amesema ilani ya CCM imetaja vyanzo vya umeme vitakavyoendelezwa kuwa ni vya maji, gesi, upepo na makaa ya mawe.

“Haijataja mradi mmoja mmoja, imeeleza vyanzo vya umeme vitakavyoendelezwa ili tupate umeme wa uhakika mpaka tuweze kukaa hapa na kusema mwingine tuuzie majirani zetu,” amesema Dk. Kalemani.

Amesema katika kile kinachodhihirisha kuwa miradi ya gesi haijatelekezwa, mpaka sasa megawati 787 za umeme unaotumika unatokana na nishati ya gesi.

“Na hii itaendelea kwa sababu mpaka 2020 pale Kinyerezi peke yake tutakuwa na megawati 1,560 zinazotokana na gesi pekee,” amesema Dk. Kalemani.

Akitoa hoja yake bungeni jana kuhusiana na mradi huo, Nape alisema anashangaa Serikali kuweka nguvu nyingi kwenye mradi wa umeme wa Stigler’s George ambao haupo kwenye ilani ya chama hicho na kuachana na umeme wa gesi ambao waliunadi wakati wa kampeni.

“Sasa ni bahati mbaya sana kwamba humu ndani hakuna kabisa kabisa (kwenye ilani), maana yake ni kwamba hili jambo pengine limenza kuachwa sasa tuende kwenye Stiglers lakini aje, hatusaliti ilani ya Uchaguzi ya CCM?

“Lakini je hatuwasaliti wana Lindi na Mtwara ambao walitupa kura na kutuamini kwamba gesi yao na uchumi wao uko salama,” alisema Nape.

Msukuma Amwagiwa Sifa kwa Kuwatetea Watumishi Darasa la 7 Bungeni

0
0
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) kimefunguka na kumwagia sifa Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku maarufu kama Musukuma kwa kulivalia njuga suala la watumishi wa umma waliofukuzwa kazi wenye sifa ya darasa la saba, na mpaka serikali kuamua kuwarudisha kazini.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Mohamed Mtima  wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupita siku moja tokea serikali ilivyotoa kauli yake kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika ya kuagiza watumishi wa umma 1,370 walioajiriwa kabla ya Mei 20, 2004 ambao hawakufaulu mtihani wa kidato cha nne, (darasa la saba) na waliondolewa kazini kwa kigezo cha vyeti vya kidato cha nne, warudishwe kazini mara moja na wapewe stahiki zao zote ikiwemo mishahara yao tangu walipoachishwa kazi.

"Suala hili sisi tumeanza muda mrefu kulihangaikia lakini'last week' tuliwaona wabunge walivyokuwa wamechachamaa Bungeni wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku Msukuma kwa kuweza kulipigia kelele jambo hili.... tunawashukuru sana, kwa maana hata kama lingekuwa lipo kwenye mchakato la kufanyiwa kazi lakini wao waliliongezea kazi zaidi mpaka serikali ikatangaza kuwarudisha kazini", amesema Mtima.

Pamoja na hayo, Mtima ameendelea kwa kusema "kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU), napenda kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya tano kwa kuzingatia mapendekezo tuliyowasilisha serikalini Machi 22, 2018 na hatimaye jana yakafanyiwa kazi. 

"Kwa kweli jambo hili tunashukuru sana kwa maana serikali imekuwa sikivu. Pia tunapenda kutoa shukrani kwa Waziri Mkuu kwa namna alivyoweza kutusaidia kipindi tulivyokuwa tunahangaikia mchakato huu".

Kwa upande mwingine, Mtima amesema wanachama wake wamefurahishwa na uamuzi huo wa serikali kwa kuwa umeweza kurudisha matumaini mapya kwa watumishi hao waliofukuzwa kazi hapo awali.

Diamond Platnumz: Kwangu Huu Sio Msalaba Bali ni Alama ya Kujumlisha Yenye Siri Nzito

0
0
Msanii mkubwa  Tanzania wa Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’,   amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa anavaa msalaba ambao hauendani na imani yake lakini ukweli unabaki kuwa siri ya msalaba huo anaijua yeye na kwamba kwake yeye ule sio msalaba bali ni alama ya kumjumlisha ambayo kwake ina maana sana.

Diamond amesema  hayo kwa sababu kuna kipindi aliwahi kuongelewa hadi  na viongozi wa dini kuwa amekuwa haeleweki kwa sababu anavaa misalaba ambayo ni kunyume na imani ya dini yake ya kiislamu.

“Cheni ninayovaa na watu kunidisi kwamba ni msalaba kiukweli huwa ninashangaa sana kwa maana watu huzungumza kile ambacho hawakifahamu. Kwangu huo si msalaba, bali ni alama ya jumlisha ambayo ninaona haina tatizo lolote, kwani alama hiyo inamaana kubwa kwangu ambayo itabaki kuwa siri yangu!”Aliongea Dimaond akichonga na kipindi cha Mikito Nusu Nusu cha GPL

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Mke wa 8 wa Mfalme Mswati III, Senteni Masango amejiua kwa kunywa vidonge

0
0
Mke wa nane wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III), Senteni Masango amefariki dunia akiwa chumbani kwake wikiendi iliyopita.

Vyombo vya habari nchini Swaziland vimeeleza kuwa Bi. Masango alitumia dawa aina ya AMITRIPTYLINE kupita kiasi (Overdose) kitu ambacho kimepelekea mwanamke huyo kupoteza masiha, hii ni baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari nchini humo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Face 2 Face umeeleza kuwa Bi. Masango alichukua uamuzi huo wa kujiua Ijumaa ya Aprili 07 ya wiki iliyopita, Baada ya mumewe kumkataza kuhudhuria kwenye mazishi ya dada yake yaliyofanyika Jumapili ya Aprili 01, 2018.

Kufuatia tukio hilo, tayari serikali nchini Swaziland kupitia kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Dkt. Sibusiso Dlamini imetuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Mfalme Mswati (III).

Bi. Masango aliolewa na Mswati (III) mwaka 1999 na ameacha watoto wawili wa kike na leo Aprili 10, 2018 mwili wake unatarajiwa kuzikwa kwa heshima nchini humo.

TRA Yakusanya Trilioni 11.78 Ndani ya Miezi 9

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania imekusanya Tsh Tril 11.78 katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2017/18 kuanzia Julai 2017 hadi Machi 2018, ikilinganishwa na Tsh. Tril 10.86 ambazo zilikusanywa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, ambacho ni sawa na ukuaji wa 8.46%.

Jamhuri Kumleta Mpenzi wa Nondo Kutoa Ushahidi Mahakamani

0
0
Upande wa Jamhuri katika kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, Veronica Fredy anatarajiwa kuletwa makamani kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili mwanafunzi huyo.

Mbali na mpenzi huyo wa Nondo, Jamhuri pia inakusudia kuleta mashahidi wengine wanne ambao ni Koplo Salum, Alphonce Mwamule, Koplo Abdulkadir na mfanyakazi kutoka Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo.

Kesi hiyo ilikuja leo mbele ya hakimu Mkazi wa Wilaya ya Iringa, John Mpitanjia kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo Wakili wa Serikali, Abel Mwandalamo amesema Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kusambaza taarifa za uongo akiwa Ubungo jijini Dar Es Salaam na kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Wakili Mwandalamo amedai upande wa Jamhuri unakusudia kuambatanisha vielelezo vya ushahidi ambavyo ni taarifa za uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya simu, maelezo kutoka Mjini Mafinga yakidai Nondo katekwa na kuleta kielelezo cha simu za mkononi.

Hakimu Mpita Njia ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 18, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo, kutokana na maombi ya upande wa utetezi ya Wakili Charles Luoga.

Naibu Waziri wa Afya Akemea udhalilishaji watoto zoezi la Makonda

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amekemea udhalilishwaji wa watoto ‘waliotelekezwa’ na baba zao ambao tangu jana picha zao zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii baada ya kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa na mama zao.

Tangu jana wanawake waliotelekezwa na waume zao wamefika katika ofisi hizo zilizopo Ilala jijini hapa, kuanza kusikilizwa.

Katika ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter akijibu maoni ya wachangiaji, Dk Ndugulile alivionya vyombo vya habari kwa kushiriki kuonyesha picha za watoto katika mikusanyiko hiyo, huku akitaka utaratibu ufuatwe katika kusikiliza mashauri ya walalamikaji ikiwa ni pamoja na usiri.

“Ni kosa kisheria kwa chombo cha habari au mitandao ya jamii kuonyesha picha zenye kumdhalilisha mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto Namba 21 ya 2009. Navikumbusha vyombo vya habari kulinda haki za watoto na kutokuwa washirika katika kudhalilisha haki za watoto,” alisema Dk Ndugulile kupitia ujumbe wa Twitter.

“Ushauri wangu kama Wizara inayosimamia haki za watoto, suala kama hili linapaswa kufanyika kwa faragha, kwa sababu una deal na watu na litakuwa endelevu,” amesema Dk Ndugulile.

“Anachokifanya Makonda ni jambo zuri, lakini linahitaji uangalifu na tufuate mifumo sahihi. Nitoe rai kwa wananchi wote kufuata taasisi zinazohusika.”

Alipoulizwa sababu ya wananchi wengi kujitokeza kwa mkuu wa mkoa kama ishara ya kuzidiwa kwa idara ya Ustawi wa Jamii, Dk Ndugulile alikanusha ,

“Si kwamba Ustawi wa Jamii umezidiwa, inawezekana wananchi hawana taarifa za kutosha kwa hiyo kupitia mikutano kama hiyo watapata taarifa. Tufuate mifumo rasmi inayokubalika kisheria,” amesema.

Ni Dr. Chief Malunde Pekee Anaetibu Nguvu Za Kiume Na Kumtuliza Umpendae Kwa Kutumia Dawa Za Asili

0
0
"NI DR. CHIEF MALUNDE PEKEE ANAETIBU NGUVU ZA KIUME NA KUMTULIZA UMPENDAE KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI"
-baada ya kujichimbia katika nchi za kiarabu kwa zaidi ya miaka (10)sasa amewasili nchini na dawa za tiba asilia.
 
1/NGOLO 3 POWER-ni dawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, ina ubora wa hali ya juu wa kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wasiojiweza kufanya tendo la ndoa, inaimarisha misuli iliyolegea na kusinyaa, inarutubisha mbegu za kiume na kukufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15-25 kuwa na hamu na tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila kuchoka, inarefusha uume inchi 5-8 na kunenepesha hadi cm 4 kwa wenye maumbile madogo, dawa hii imeboreshwa na hutibu matatizo haya kwa muda mfupi tu.
 
2/MAGOYE MVUTO- dawa hii ina uwezo mkubwa sana kumvuta na kumtuliza aliekuacha awe mpenzi, mme/mke itamfanya akutafute mwenyewe ndani ya masaa 3tu na kukutimizia mahitaji yako kwa haraka na kumfunga asiwe na mtu mwingine.
 
3/SUPER LUBEJA- ni dawa ya kushepu umbo no.8 mguu wa bia, kuongeza hips, na makalio kwa muda wa siku 5tu unapata saizi uipendayo, kuondoa makovu, chunusi, harufu mbaya ya mwili michirizi, kupunguza tumbo na maziwa kwa siku 6tu.
 
4/NG'WESHI MIX- ni dawa ya biashara ya kupata wateja wengi, kusafisha nyota, kurudishwa kazini na kupandishwa cheo, kurudisha mali iliyoibiwa au kudhurumiwa.
 
PIA TUNATIBU MAGONJWA SUGU KAMA: vidonda vya tumbo, ngiri, chango na uzazi kwa kina mama: (dawa zote hazina madhara kwa mtumiaji) HUDUMA HIZI UTAZIPATA POPOTE ULIPO: TUNAPATIKANA DSM BUGURUNI SHELI AU PIGA SIM NO_ 0763-181099.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0766340868

Taarifa Ya Jeshi La Zimamoto Kufuatia Tukio La Moto Kwenye Ukumbi Wa Bunge Dodoma

Chanjo Saratani Ya Kizazi Yazinduliwa Rasmi

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti na ya mlango wa kizazi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi mkoani Dar es Salaam ambapo hafla ya uzinduzi zilifanyika kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala, wilaya ya Temeke.

Makamu wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika

“ Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu. Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo.” Alisisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.

Makamu wa Rais aliendelea kusema kuwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ni walengwa wa kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi  kwa mwaka huu 2018 ambapo jumla ya wasichana 6,16,734.

Makamu wa Rais ambaye aliwaeleza wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi kuwa anaunga mkono uwepo wa chanjo hiyo huku akitoa sababu mbili moja ikiwa ni kulinda jeshi la wanawake nchini Tanzania kwani wengi wamekuwa wakipoteza maisha yao kwa sababu ya Saratani na sababu ya pili ni kwamba Mama yake Mzazi alifariki kwa kansa hiyo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Wakati huo huo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia  Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania imeandika historia nyingine katika sekta ya afya kwa kuzindua chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa Kizazi.

Mwigulu Nchemba amjibu Mbunge Bwege

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, ametolea ufafanuzi suala lililoibuliwa na Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara, kuhusu polisi kushambulia watu msikitini na wengine kuuawa.

Akizungumza Bungeni leo Waziri Nchemba amesema kwamba yeye kama waziri mwenye dhamana amelisikia suala hilo na ameagiza uchunguzi ufanyike, ili kuweza kubaini mbivu na mbichi na sheria kufuata mkondo wake.

Sambamba na hilo Waziri Nchemba ameitaka jamii kutohusisha makosa ya uhalifu na masuala ya dini au siasa, kwani mhalifu anapokamatwa hakamatwi kwa imani ya dini au chama chake, bali ni kwa makosa aliyofanya.

“Nimewaelekeza wafanye uchunguzi wa ndani ili tuweze kupata taarifa kamili na tutatoa taarifa, na nimuombe mheshimiwa mbunge tuepuke sana kulinganisha jambo hilo na dini, linapotokea suala la uhalifu mtu hakamatwi kwa dini yake, anakamatwa kwa kosa alilolifanya, watu wanakamatwa kutokana na makosa aliyofanya wala asiunganishwe kwa dini yake au chama chake”, amesema Mwigulu Nchemba.

Hapo jana Mbunge wa kIlwa Kusini Suleiman Bungara maarufu kwa jina la Bwege alimtaka Waziri atolee ufafanuzi suala la polisi kuingia msikitini na kupiga risasi, na kuchukua baadhi ya watu ambao wengine walirudi wakiwa marehemu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images