Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbunge Bwege: Siwaelewi Mnaposema Nchi Iko Salama, Ina Amani

0
0
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Suleiman Bingara maarufu kwq Jina BWEGE amesema anashindwa kuelewa kauli ya Waziri Mkuu kuwa nchi ipo salama, kutokana na vitendo vinavyoendelea kujitokeza.

Akizungumza leo Bungeni Suleiman Bungara amesema matukio ya mauaji na unyanyasaji yanayofanywa na watu wanaoaminika ni polisi, yanafanya nchi kuwa sio sehemu salama hivyo hakubaliani na kauli hiyo, huku akitolea mfano wa tukio lililofanywa na polisi huko Chumo wilayani Kilwa.

“Askari walikwenda Chumo msikitini, wakapiga risasi wakachukua watu 10 tumefika damu zimetapakaa, walivyorudi mmoja kafa, mmoja hana jicho, mmoja wakamnyoa ndevu kwa kumchoma moto, mnapotuambia nchi hii ina amani na utulivu mimi siwaelewi, nchi imeharibika, tumetengenezewa waislamu wakisema jambo kuhusu waislamu wenzao tunaambiwa sisi magaidi, ndio maana mashehe hawasemi, akipigwa muislam akisema tunaambiwa magaidi”, amesema Bungara.

Bungara ameendelea kwa kusema kuwa ili nchi iwe yenye utulivu na kuishi kindugu, lazima misingi ya kidemkrasia ifuatwe, na ndipo tutakapoweza kutekeleza mengine.

“Nchi yetu kama haitakuwa na uhuru na haki, basi undugu na amani hautakuwepo, kwa mujibu wa katiba yetu”, amesema Mbunge huyo maarufu kwa jina la Bwege.

Nape Aikaba Koo Serikali Bungeni

0
0
Mbunge Nape Nnauye amefunguka na kuibana serikali ya awamu ya tano kupitia Waziri wake Mkuu kuwa kitendo cha hotuba yake Bungeni kutokuwa na hata neno moja linalohusu gesi ni usaliti mkubwa kwa wananchi wa Lindi na Mtwara kwa kudai gesi ndio yalikuwa makubaliano yao wakati wa kupiga kura.

Nape ametoa kauli hiyo leo (Aprili 09, 2018) Bungeni katika mkutano wa 11 kikao cha tano cha Bunge la 11 linaloendelea kufanyika Mjini Dodoma baada ya kuipitia hotuba ya Waziri Mkuu ambayo inatakiwa kusomwa mbele ya Wabunge huku ikiwa haina hata neno moja kuanzia mwanzo wa ukurasa hadi mwisho linaloshabiana na gesi na mafuta

"Tulipopiga kura mwaka 2015, tuliamini kwamba uchumi wa gesi kwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni ukombozi mkubwa na upo salama mikononi mwa Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano. Tulipopiga kura ndio ukawa mkataba wetu siyo kwa maneno, kwa hiyo kura alizozipata Rais Magufuli ni kwa sababu ya makubaliano yaliyopo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo ndani yake kuna masuala ya gesi kwamba atakwenda kuyaendeleza", amesema Nape.

Pamoja na hayo, Nape ameendelea kwa kusema "hivi ni bahati mbaya kwamba hotuba ya Waziri Mkuu imeshindwa kuliona jambo hili kuwa ni kubwa na ikaamua kuliacha au serikali imeamua kuachana nalo kwa sababu naona jitihada kubwa zinaenda kwenye umeme wa maji lakini umeme wa maji katika ilani haumo. Ilani tumezungumza nishati ya gesi tena kwa sehemu kubwa sana. Hii ndio ilikuwa imani ya wanalindi na mtwara kwa serikali ya awamu ya tano".

Aidha, Nape amesema wakati mchakato wa kupata madini hayo katika mkoa wa Lindi na Mtwara wananchi wengi walipoteza maisha yao huku wengine wakipata ulemavu na majeraha mbalimbali ili mradi kuiwezesha nchi yao iwe na nishati ya gesi na mafuta.

"Kuna mali za watu zilipotea lakini tukaamini kuna neema kesho yake. Jambo hili bahati mbaya tulimkabidhi sisi Rais Magufuli tukaamini lipo salama, alipotupa Majaliwa tukaamini tupo salama zaidi kwa sababu Waziri Mkuu ametoka kwetu. Sasa ni bahati mbaya sana kwamba humu ndani hakuna kabisa neno gesi maana yake ni kwamba hili jambo limeanza kuachwa sasa ili tuende kwenye umeme wa maji. Lakini je hatusaliti Ilani ya uchaguzi CCM pamoja na wananchi wa Lindi na Mtwara waliotupa kura na kutuamini kwamba gesi na uchumi wao upo salama?", amehoji Nape.

Nape ameendelea kusisitizia
"Hili ni bomu kubwa, wakati wa mchakato hali ya kisiasa, kijamii Lindi kulikuwepo na tabu sasa imetulia tukiamini neema ipo lakini kiuchumi baada ya harakati za gesi na mafuta kusini watu walianza kuekeza na uchumi ulikuwa, ila hali ya sasa waekezaji wanaondoka na uchumi umeanza kudorola, hali yetu ngumu sana".

Kwa upande mwingine, Nape amemuomba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asikubali suala la gesi lisiwe mikono mwake yeye akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Kisa Kujadili Muungano, Wabunge CUF Wasusia Bunge

0
0
Wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, leo walitoka kwenye ukumbi wa Bunge baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan ‘Zungu’ kusitisha kujadili masuala yanayohusu muungano.

Hatua hiyo ya Zungu imetokana na mwongozo ulioombwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, ambaye alisema lugha zinazotumiwa katika mjadala wa suala hilo, unafanya Serikali ionekane kuwa haijali muungano.

Baada ya kauli hiyo Zungu alitangaza kusitisha mjadala wa Muungano, jambo lililofanya baadhi ya wabunge kusimama wakiomba mwongozo kutaka kujua ni kwa namna gani amesitisha hoja hiyo wakati iko kwenye Hotuba ya Waziri Mkuu inayotarajiwa.

Baada ya kutoka nje ya Bunge, Mbunge wa Mji Mkongwe, Ali Saleh amesema wameamua kutoka kwasababu ya kukatazwa kujadili mambo ya Zanzibar ambayo ndiyo wanayoyatetea ndani ya Bunge.

“Kama hawataki tujadili mambo ya Zanzibar tukae tufanye nini tena, leo tumetoka wenyewe lakini wakiendelea hivi watatufanya tutoke na watu wajue ni kwanini tumetoka na hapo watakuwa wamehatarisha Muungano,” amesema Saleh.

Mapema jana, suala hilo liliibuka likianzia kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mariam Msabaha (Chadema), akizungumzia kuwa serikali ya Muungano inaiminya Zanzibar na kushindwa kujitangaza kimataifa.

Hoja hiyo iliendelea kwa wabunge kuendelea kuchangia na kuomba miongozo lakini alipoanza kuchangia Mbunge wa Tunduru Frank Mwakajoka (Chadema) ambaye alitangaza kuwa wabuge wa chama tawala wanaiumiza Zanzibar na nia yao siyo njema kuhusu muungano.

Kauli ya mbunge huyo ilimuibua Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Kangi Lugola ambaye aliomba mwongozo na kuwataka wabunge kumtaja mbunge ambaye anapinga Muungano vinginevyo wasitoe kauli hizo.

Mbunge Alalamikwa Kupapaswa Sehemu Nyeti na Walinzi wa Bunge

0
0
Mbunge wa Kavuu, Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM), amedai kuwa walinzi wanaowakagua wakati wakiingia kwenye viwanja vya Bunge, wanawapapasa sehemu mbalimbali za miili yao.

Mbunge huyo amesema hayo leo wakati akiomba mwongozo wa kiti, jambo lililofanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, kupiga marufuku ukaguzi wa aina hiyo.

Amesema wanapopita kwenye mashine za ukaguzi hutakiwa kuvua mikanda, viatu, saa na vitu vingine na kwamba kibaya zaidi kwake ni suala la kupapaswa.

“Tunavua nguo, watu wanainua mashati kuvua mikanda na tunaona vitovu vya wanaume halafu miili inasisimka tukidhani wanataka kufanya maandalizi ya, mwili wa binadamu una vivutio vingi.

“Leo nimepita mashine moja vizuri na nilipofika ya pili ikalia. Nikaambiwa nikaguliwe sasa kibaya nakwenda kukaguliwa ananishikashika maeneo mbalimbali, hapa tuna mwezi mmoja huku si kutiana hanjamu,” amehoji.

Dk. Kikwembe amemtaka Spika kutoa agizo kukomesha jambo hilo, akisema halikubaliki na linawadhalilisha wabunge kila wakati.

Akijibu mwongozo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameagiza ukaguzi kwa kuwashika shika wabunge mwilini uachwe mara moja kwa kuwa unawadhalilisha na kuagiza utaratibu ufanyike kwa kuangalia namna bora ya kuwakagua wabunge kwani kinachofanyika ni ukaguzi wa kizamani uliopitwa na wakati.

Mtama, Ndizi, Mihogo Vyachangia Kushuka Kwa Mfumuko Wa Bei

0
0
Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Machi, umepungua hadi kufikia asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 4.1 ilivyokuwa Februari, mwaka huu.

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni mtama kwa asilimia 7.1, unga wa muhogo asilimia 6.7, maharagwe asilimia 3.9, mihogo mibichi asilimia 16.6 na ndizi asilimia 16.7.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema hali hiyo inamaanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Machi imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Februari.

“Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki, nchini Uganda umepungua hadi asilimia 2.0 Machi, kutoka asilimia 2.1 Februari, mwaka huu huku Kenya ukipungua hadi asilimia 4.18 Machi, kutoka asilimia 4.46, Februari, mwaka huu,” amesema.

Spika Ndugai Asimulia Alivyopigania Uhai Wake

0
0
Spika wa Bunge Job Ndugai amesimulia jinsi alivyopigania uhai wake wakati akiwa amelazwa nchini India ambapo amesema kuna kipindi alikuwa akihisi hawezi kuiona kesho.

Spika ameyasema hayo bungeni leo ambapo ameongoza kikao kwa mara ya kwanza mwaka huu tangu arejee, mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.

“Kuna wakati nilikuwa nikiona kabisa siwezi kuiona kesho, baadhi yenu labda hamjawahi kulazwa hospitali mkiwa mnaumwa sana na kama ukiwa peke yako, halafu ukaona jinsi ambavyo mawazo yanavyokuja na kuzunguka na wakati mwingine kunakuwa na dalili zinaonesha kama vile kesho hakuwezi kukucha.”

Spika Ndugai amesema kuna raha na tabu yake kidogo ambapo hawaombei wabunge hao wapitie katika mambo hayo huku akiwaombea wasipate machungu hayo aliyoyapata ambapo pia amewashukuru wale wote waliomuombea wakati akiwa mgonjwa.

“Niwashukuru wote walioniombea kwani binadamu siyo jiwe lazima kupita katika mapito na kila binadamu ana mapito ambayo anaweza kupitia kulingana na alivyopangiwa.

“Kwa hiyo ukipata msalaba unaubeba kwa amani ninaendelea kumuomba Mwenyezi Mungu msalaba wangu na mimi usiwe mzito sana uwe wa kadri tu.

“Vinginevyo nashukuru tumerudi tupo pamoja na niwashukuru sana wasaidizi wangu hapa mezani Naibu Dk. Tulia( Akson) Chenge (Andrew) Najma (Giga) Zungu (Musa) Katibu na timu yake pamoja na wabunge kwa kipekee kabisa Wapigakura wangu wa Kongwa, nawaomba tuendeleze gurudumu letu.

“Kipekee nimeshukuru Waziri Mkuu, (Kassim Majaliwa), tulikuwa tunawasiliana kipekee alikuwa akinitia moyo sana nilipokuwa kitandani kule,” amesema Spika Ndugai.

Kinana Aongoza Viongozi Wa CCM Maombolezo Ya Winnie Madikizela Mandela

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania kutokana na kifo cha Mke wa zamani na Rais wa Afrika Kusini, Hayati Mzee Nelson Mandela, Mama Winnie Mandela aliyefariki Aprili 2, mwaka huu.

Mama Winnie Mandela ambaye pia ni Mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, amefariki jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 81. Mwanaharakati huyo anatarajiwa kuzikwa Aprili 14, mwaka huu.

Pamoja na viongozi wengine wa CCM, Kinana ameongozana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Gaudensia Kabaka, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI, Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi, Seif Shaban Mohamed na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka.

Msigwa Adai Wafungwa Segerea Wanalala Kwa ‘Alarm’

0
0
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), amedai Tanzania kwa sasa kuna msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu magerezani hususani Gereza la Segerea.

Amesema kutokana na hali hiyo, wafungwa na mahabusu wa gereza hilo wanalazimika kulala upande mmoja mmoja kwa zamu baada ya muda inapigwa ‘alarm’ kisha wanageukia upande mwingine hatua aliyosema ni ukiukwaji wa haki za binadamu na watoto.

Akiuliza swali la nyongeza leo bungeni Msigwa amesema Gereza la Segerea limezidiwa na mahabausu ambapo lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700, lakini waliopo sasa ni mahabusu na wafungwa 2,400.

“Ukienda katika magereza zetu kuna msongamano mkubwa sana kwa mfano Gereza la Segerea ambalo nililipitia juzi lina uwezo wa kuchukua mahabusu 700 lakini sasa hivi lina mahabusu na wafungwa 2,400.

“Ni kwanini Serikali imekuwa ikipeleka wanasheria wao ambao wamekuwa wakilazimisha wale ambao wanaweza kupata dhamana waende kukaa mahabusu kama ambavyo kesi zetu zilikuwa zina dhamana lakini mawakili wa Serikali walikuwa wanalazimisha tuende kule tukaongeze msongamano,” amehoji Msigwa.

Akijibu kwa niaba ya Serikali, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema kuwekwa ndani kwa muda mrefu kwa mahabusu si kweli kwamba Serikali haitaki kesi hizo zimalizike haraka.

“Sababu za msingi ni sababu ya usalama wao, wakienda nje wanaweza wakapata matatizo ikiwamo Serikali kuwalinda pili kuna watuhumiwa wakitoka nje wataenda kuharibu ushahidi,” amesema.

Rais Magufuli kuhutubia Bunge la Bunge la Afrika Mashariki(Eala) Dodoma

0
0
Rais John Magufuli anatarajiwa kulihutubia Bunge la Afrika Mashariki(Eala) katika mkutano wake wa nne kikao cha kwanza ulioanza leo mjini Dodoma ikiwa ni mara ya kwanza vikao vya bunge hilo kufanyika huko.

Taarifa ya Eala kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisa Habari Mwandamizi, Bobi Odiko ilisema mkutano huo utafanyika kati April 9 hadi 28 mwaka huu na Rais Magufuli atalihutubia katika muda utakaopangwa na taarifa itatolewa wiki ijayo.

Spika wa Bunge hilo, Martin Ngoga ataongoza mkutano huo wa wiki tatu ambao utajadili miswada na maazimio mbalimbali wakati kamati za bunge zimeendelea kuandaa miswada kwa ajili ya mkutano huo.

“Kwasasa ipo miswada miwili itakayojadiliwa kwa kina inayohusu Itifaki ya Sarafu Moja ambayo ni mswada wa taasisi ya Fedha na  mswada wa Takwimu yote ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  ya mwaka 2017,”alisema Odiko.

Amesema miswada hiyo iliwasilishwa katika bunge hilo na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri  wa EAC, Dk Kirunda Kivenjija na ilishasomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa pili uliofanyika  Januari jijini Kampala.

 Taarifa imesema lengo la mswada wa taasisi ya Fedha ya EAC wa mwaka 2017 unakusudia kuanzisha taasisi ya jumuiya ambayo itakua na majukumu ya kuweka taratibu za kuanza Umoja wa Sarafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.                                     

“Kwa mujibu wa Ibara ya 23 ya Itifaki iliyoanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki inataja Umoja wa Sarafu ya EAC, hivyo muswada huo unatarajiwa kuweka majukumu, uongozi na namna ya kupata fedha za kuendesha taasisi hiyo,”alisema Odiko.

Pia muswada wa Takwimu wa EAC wa mwaka 2017 unalenga kuanzisha taasisi ya takwimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama inavyotajwa kwenye Mkataba wa EAC ibara ya 9 na 21  ya Itifaki iliyoanzisha Umoja wa Sarafu wa EAC.   

Amesema Baraza la Mawaziri wa EAC wanatarajiwa kukutana mapema na kamati mbalimbali za bunge hilo kupitia mambo muhimu ya miswada hiyo huku kamati ya Mawasiliano, Biashara na Uwekezaji ikitarajiwa kukutana na wadau juu ya muswada wa Takwimu wa EAC.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 10

Rais Magufuli atajwa kuwania tuzo Afrika

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, zijulikanazo kwa jina la The African Prestigious Awards zinazotarajia kufanyika nchini Ghana.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk. Harrison Mwakyembe wakati akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo ambapo ameweka wazi kwamba Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika.

Amesema kuwa Utendaji uliotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.

“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika"  Dkt.Mwakyembe.

Ameongeza "Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika".

Monalisa anatarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo ambapo amewaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo.

Mkopo Wa Dola Milioni 65 Wa Kagera Sugar Wawekezwa Nchini

0
0
Na Benny Mwaipaja
Serikali imeeleza kuwa kiasi chote cha dola za Marekani milioni 65  zilizokopwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutoka Benki ya CRDB kwa udhamini wa  Serikali mwaka 2004 kimewekezwa nchini na hakijapelekwa kuwekeza katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda hicho kukopa kiasi hicho cha fedha ambacho kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo  wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji uliofanywa katika Kiwanda cha Kagera ni wa takribani dola za Marekani milioni 250 hivyo haiwezekani mwekezaji kukopa dola milioni 65 na kuzipeleka Congo ili hali kiwango cha uwekezaji nchini ni kikubwa.

“Mwekezaji wa Kiwanda hicho ni wa ndani na amejitahidi kuajiri watanzania wengi hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kukiwezesha kiwe cha mfano  ili kiendelee kuleta matokeo chanya kwa watanzania”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali la msingi la Mbunge huyo, alitaka kujua kiwango cha hisa ambacho Serikali inamiliki katika kiwanda cha Sukari cha Kagera na kiasi cha fedha kilichokopwa na kulipwa na mwekezaji huyo kupitia udhamini huo wa Serikali.

Dkt.  Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa sasa haimiliki hisa zozote katika kiwanda hicho na kuongeza kuwa  hisa zake katika kiwanda hicho ziliuzwa mwaka 2001 baada ya kukibinafsisha kiwanda hicho  kwa Kampuni ya Kagera Saw Mills Limited.

Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mwekezaji wa Kiwanda hicho alikopa kiasi cha dola za Maerekani milioni 65 kwa kutumia udhamini wa Serikali mwaka 2004, ikiwa ni udhamini (guarantee) wa kipindi cha miaka 12.

Alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho mimerejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 56.88, sawa na asilimia 87.5 ya mkopo wote, na kwamba  marejesho ya  mkopo uliobaki wa Dola milioni 8.12 yatafikia ukomo wake mwezi Julai, 2019.

Mamia Ya Wanawake Waliotelekezwa Na Waume Zao Wafurika Kwa Makonda........Majina ya wanaume waliotelekeza watoto kuanikwa hadharani

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda jana April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.

Ambapo alieleza  maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda alisema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.

Alieleza hawapo kwa  ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.

"Kama tukikuita hutaki, unajificha unajidai kulinda ndoa yako wakati mama yangu huku anateseka na mtoto huku sisi tutakuanika hadharani mkeo ajue una mtoto wa nje ya ndoa

"Mimi najua sijaanza leo kupigana hii vita najua wakina baba wasiopenda matokeo yao watanichukia lakini ukinichukia, ukinitukana, kunifedhehesha ni kama unanipaka mafuta yanayoning'arisha zaidi chuma kinaimarishwa na moto na viongozi wanaimarishwa na kebehi" alisisitiza Paul Makonda  

Alisema Makonda  ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto  na kuwe na usawa.

Aliwataka akina  Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.

Makonda alieleza  Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka pia Wanaume walioachiwa watoto wafike ofisini kwake ili wapatiwe msaada wa kisheria. 

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Wolper na Sarah Warudi Vitani Kwa Ajili Ya Penzi la Harmonize

0
0
Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper na Sarah mzungu ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize wamerudi kwenye ya vita ya mtandaoni.

Wolper na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi kabisa ni mpenzi wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.

==>Baada ya kutolewa povu hilo, Wolper alimrudishia kombora hilo Sarah na kuandika maneno haya:

Hii  sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO 0758840958 / 0785687900

Bi. Sylvia Mulinge(Mkenya) Ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania

0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom, Ian Ferrao ametangaza kuachia mikoba ya kuiongoza kampuni hiyo baada ya mkataba wake kufika tamani.

Kutokana na hilo, Ferrao atakabidhi majukumu kwa mrithi wake, Sylvia Mulinge kuanzia Juni Mosi na kuhitimisha miaka mitatu ya kuiongoza kampuni hiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya wateja nchini.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa bodi ya Vodacom, Ali Mufuruki inaeleza makabidhiano ya ofisi kati ya Ferrao na Sylivia yatafantika kwa miezi mitatu na kukamilika Agosti 31.

Mufuruki alimpongeza Ferrao kwa mchango mkubwa alioutoa katika kipindi alichoiongoza kampuni hiyo pekee iliyofanikiwa kujiorodhesha Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) licha ya Serikali kuzitaka kampuni zote za mawasilinao kufanya hivyo.

Nafasi ya Ferrao itachukuliwa na anayetokea kampuni ya Safaricom ya Kenya ambako kwa sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa Huduma kwa wateja aliyojiunga nayo tangu mwaka 2006.

Akizungumzia kuondoka kwa Ferao jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom, Ali Mufuruki alimpongeza kwa kuiendesha kampuni hiyo kwa mafanikio tangu alipojiunga nayo mwaka 2015.

“Bodi inamshukuru Ian kwa uongozi wake makini.  Ameivusha kampuni katika hatua muhimu, akiiacha na jina kubwa Tanzania. Ian ni rasilimali muhimu kwa Vodacom. Miaka yake mitatu ilikuwa endelevu iliyojaa mikakati na maoni yaliyoibadilisha Vodacom kufanya biashara kisasa. Anaiacha timu madhubuti iliyojizatiti kuleta mafanikio,” alisema Mufuruki.

Kabla ya kujiunga na Vodacom Tanzania, Ferrao alikuwa mkurugenzi mtendaji wa Vodacom nchini Lesotho. 

“Ilikuwa ni nafasi adhimu kuiongoza Vodacom Tanzania katika kipindi cha mabadiliko na ukuaji. Najisikia fahari kufanya kazi Tanzania na kusaidia kuipeleka katika ulimwengu wa kidigiti na mabadiliko ya teknolojia,” alisema.

Sylvia, aliyekuwa mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini Kenya, Safaricom aliyojiunga nayo tangu mwaka 2006.

Kwa majukumu haya mapya, Sylvia atalazimika kuendeleza mafanikio aliyoyapata Ferrao kwenye ukurugenzi wake.

Licha ya kufanikiwa kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake DSE zenye thamani ya Sh476 bilioni na kuwavuta zaidi ya wawekezaji 40,000 wa ndani, tayari kampuni hiyo imelipa gawio la Sh28.5 bilioni.

“Sera ya gawio inataka walau asilimia 50 ya faida iliyopatikana itolewe kwa wanahisa lakini Vodacom imelipa asilimia 60,” inasema taarifa hiyo.

Mwenyekiti wa bodi alimtakia kila la heri Ferrao na kumkaribisha mkurugenzi mpya atakayeiongoza Vodacom kuwahudumia Watanzania kwa kuanzia Juni Mosi.

“Tunamtakia heri Ferrao na familia yake maisha mema. Naomba kumkaribisha mtendaji mkuu mpya ambaye nina uhakika atafanya kazi na timu ya Vodacom na tutafurahia mafanikio siku zijazo,” alisema Mufuruki.

Wema Sepetu: Tuzo Zangu Zimewatoa Povu na Sasa Nina Hasira Ya Kufanya Kazi Nzuri

0
0
Msanii wa Bongo movie Wema sepetu amefunguka tena kuhusiana na wasanii wenzake kumtolea povu baada ya kujishindia tuzo mbili kama msanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Wasanii kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna wasanii  wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.

Baada ya povu hilo Wema amewajia juu wasanii hao na kuwataka waache wivu kwani yeye amestahili tuzo hiyo kwa movie yake ya heaven sent kwani imeleta changamoto kwa wasanii wenzake.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Wema alifunguka haya:

"Kwanza kikazi kidogo tu cha heaven sent kimeleta maneno haya...kwahiyo wamenitia hasira na pia wamenifanya nione kuwa mimi ni tishio kwao, alafu huyo mtu ambaye anaongea nimesha fanya naye kazi alafu tumeshawahi kuwa karibu 

"Mimi sina tatizo na yeye nashangaa kwa Nini imekuwa hivi halafu nimeshafanya naye movie na nimemnyoosha kwenye kazi ambayo tumefanya lakini sijawahi kusema kitu chochote kibaya juu yake”.

Wema ameongeza kuwa kinachosababisha mpaka mambo yanakuwa hivi ni wasanii wa Bongo movie kuoneana wivu ambao unasababisha kunakuwa hakuna umoja kati yao hali inayosababisha tasnia hiyo kurudi nyuma.

Marekani yaapa kuichukulia hatua Syria

0
0
 Rais Donald Trump amesema Marekani inapanga kutoa jibu la nguvu kuhusiana na shambulio la kemikali katika mji wa Douma nchini Syria.

Rais Trump ambaye amekutana na washauri wake wa kijeshi amesema uamuzi unaweza kuchukuliwa katika saa zijazo.

Kauli yake hiyo inafuatia kauli mbalimbali za kulaani shambulio hilo ziliotolewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakati wa kikao hicho, Urusi na Marekani zilijikuta zikitupiana vikali maneno.

Balozi wa Marekani katika baraza hio Nikki Haley amemtuhumu Rais wa Syria Bashar al Assad kwa jinsi alivyowajibika kwa shambulio hilo.

Ametaka kupigwa kura hii leo, juu ya azimio la awali kuweza kufanya uchunguzi mpya juu ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Tayari Urusi ambaye ndiye mshirika wa Syria imesema haita unga mkono pendekezo hilo.

Mwakilishi wa Urusi, Vassily Nebenzia amesema tukio lililotokea katika mji wa Douma ni la kupangwa, na kwamba hatua za kijeshi zinazotaka kuchukuliwa na Marekani zinaweza kuwa na athari mbaya.

Akitoa kauli ya nchi yake, Rais Trump amesema tukio hilo litakutana uamuzi aliouita wa nguvu na kuongeza kuwa nchi yake ina njia na maamuzi mengi ya kijeshi na kwamba hatua zitachukulkiwa katika kipindi kifupi.

Naye Mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar Jaafari amesema Marekani na washirika wake wamekuwa wakifadhili ugaidi nchini Syria, na ndio wao wanapaswa kuwajibika na shambulio hilo la kemikali.

Kufuatia kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kauli iliyotolewa na Rais Donald Trump, kumekuwa na dalili zinazoonesha kuwa mataifa ya magharibi yataungana na Marekani kupanga hatua za kuchukua.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images