Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Wawekezaji Wazawa Wapewa Rai Kujenga Viwanda vya Dawa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa rai kwa wawekezaji wazawa na wafanyabiashara nchini kujenga viwanda vya dawa na vifaa vya tiba hapa nchini ili kuongeza kasi ya ujenzi wa uchumi wa viwanda na kukuza ajira.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo jana Jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya uzinduzi wa magari 181 yenye thamani ya shilingi bilioni 20.7 ya kusambaza dawa na vifaa vya tiba yaliyotolewa msaada na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD).

“Asilimia 94 ya dawa zinanunuliwa nje ya nchi, hivyo wawekezaji wazawa watumie changamoto hii kama fursa ya kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa hapa nchini kwetu,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alibainisha kuwa ujenzi wa viwanda hapa nchini utasaidia kuongeza ajira kwa Watanzania hasa vijana pamoja na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa nje ya nchi zikiwemo dawa na vifaa vya tiba.

Aidha Rais Magufuli alitoa wito kwa wataalamu na wasomi wazawa wa masuala ya afya na tiba kujiunga pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa ili kuchochea uchumi wa viwanda na kuongeza mapato.

“Tunapoteza shilingi bilioni 500 kila mwaka kwa ajili ya kununua dawa nje ya nchi lakini tungekuwa na viwanda vyetu fedha hizo tungetumia kwenye mambo mengine ya maendeleo,” alisisitiza Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli alisisitiza kuwa madereva watakaoajiriwa kuendesha magari hayo mapya wachaguliwe kwa umakini ili kupata watu waaminifu watakaoweza kuyatunza kwa manufaa ya Watanzania.

Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) ilianzishwa mwaka 1994 kwa ajili ya kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa vya tiba nchini kote.

Wolper: Sitoi Kiki Kuhusiana na Ishu ya Brown na Nisha

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper ameibuka na kuweka wazi hana mpango wa kuwapa kiki Nisha na Brown walioanika penzi lao hivi karibuni.

Wiki iliyopita msanii Salma Jabu ‘Nisha’ alianika Hadharani Penzi lake na Ex boyfriend wa Wolper anayejulikana kama Brown jambo lililowashangaza watu wengi hasa kwa sababu ya urafiki wa Wolper na Nisha.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Nisha na Brown walianza kunyemeleana tangu Brown akiwa na Wolper Lakini pia inasemekana wawili hao walikuwa wanawasiliana kwa siri siri Jambo lililosababisha migogoro na Wolper.

Baada ya stori hizi kutrend sana Wolper alitafutwa ili kutaka kujua kama alikuwa ana taarifa kuwa alinyakuliwa na Nisha:

"Jamani mimi sijui lolote, niko bize na cherehani yangu na mambo mengine hayanihusu kabisa lakini Sasa hivi sitoi kiki kwa mtu yoyote, niko bize na mambo yangu, mimi mambo ya watu hayanihusu kabisa”.

Nisha na Brown wamekuwa waki posti video na picha Kwenye mitandao ya kijamii kuonyeshana mahaba na hata Brown kafuta tatoo ya Wolper Kifuani kwake na kumuweka Nisha.

ACT-Wazalendo wamvaa Waziri Ndalichako.....Wapinga Kigezo cha Umri Kujiunga Kidato cha 5

$
0
0
Chama cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako aondoe kigezo cha umri walichokiweka katika udahili wa wanafunzi kwa madai kitendo hicho kitapelekea kuwanyima elimu watoto wa kimasikini.

Hayo yameelezwa na viongozi wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT jana (Machi 26, 2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama chao yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT Jijini Dar es Salaam.

"Walichokifanya wizara ya elimu kwa kuweka kikomo cha umri wa udahili kwenye shule za serikali na binafsi kitapelekea kupungua wanafunzi wa elimu ya juu, kwa kuwa kikomo hicho kitawakwamisha hasa wananchi masikini wanaoishi vijijini na mijini katika kupata elimu. Kwenye hili tunamtaka Waziri wa Elimu aondoe kigezo cha ukomo wa umri kwasababu kigezo hicho kina kiuka Katiba", walisema viongozi hao.  na kuongeza;

"Wametoa kikomo hicho bila ya kuwa na tafiti yeyote ambayo wamefanya wao kama Wizara au taasisi nyingine iliyopo nje ya serikali. Kuna athari kubwa katika kikwazo hicho kwa maana kuna watu walichelewa kupata elimu kutoka na maradhi, kusimamisha masomo kutokana na ada hivyo tunataka kigezo hicho kiondolewe ili watu wa aina wasikose kupata elimu".

Kwa upande mwingine, Viongozi hao wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT imeunga mkono waraka uliotolewa na Maaskofu wa Kanisa la KKKT nchini Tanzania na kuwataka viongozi wa dini nyingine wasikae kimya wafanye kama walivyofanya maaskofu.
 
 “Ngome ya vijana inawapongeza sana kwa kutekeleza wajibu wao, ushauri wa maaskofu na maoni yao inabidi kuchukuliwa uzito wa hali ya juu, wamezungumzia kuhusu uhuru wa kutoa maoni, mauaji ya watu, katiba mpya, uchumi na ajira kwa vijana, ni mambo muhimu kwa watanzania wote bila kujali tofauti zetu kuyaunga mkono,.

“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema vuongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao.”

RC Paul Makonda Atoa Ujumbe Mzito Akiponda Wanaotoa Waraka wa Kuikosoa Serikali

$
0
0
Ni vigumu sana Kusimama Katika HAKI Kwenye Dunia iliyojaa Uovu , Kwamaana Unapigwa Katika Kila Upande  na Hata Waliotakiwa Kuzama Katika Maombi nao Wamekengeuka .
 
Ninapoitazama Kazi ya Msalaba Naelewa Kwanini Yesu Kristo alibaki Peke Yake .
 
Umepigana VITA ya Madini sikuona Waraka , Umejenga Ukuta Mkubwa Mererani Kulinda Rasilimali Yetu ya Tanzanite , Sikuona Waraka ,Umepigana Vita ya Rushwa,Umeanzisha Mahakama za Mafisadi sikuona Waraka Umepambana na Wazembe Maofisini sikuona Waraka, Umetoa Elimu BURE Sikuona Waraka , Umefufua Shirika la NDEGE, Unajenga  Treni ya Mwendo Kasi (SGR) Sikuona Waraka. Umeanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Vyanzo Vipya Vya Umeme (Stigglers Gorge), Hatujaona Waraka.
 
Lakini Kama Haitoshi Umekomesha Mauaji ya Kutisha Ya Rai wasiokuwa Na Hatia kule Kibiti , Hatujaona Waraka ,Umekomesha Tabia Ya Askari kuvamiwa Na kuuwawa Vituoni wakiwa wanatimiza  Majukumu yao Ya Kulinda Raia , Hatujaona Waraka.Nakumbuka Kulikuwa na Tabia Ya kutorosha Wanyama kwa Kuwapandisha Ndege, Leo Umekomesha , Hatujaona Waraka .
 
Lakini Niwakumbushe , Umeongeza Bajeti ya Ununuzi wa Madawa Na Vifaa Tiba Kutoka Bilioni 31 Mpaka kufika Bilioni 260 , sijawai Kuona Waraka .
 
Tangu Umeingia Madaraka Umeongeza Vivuko katika Maeneo Yote Yanayohitaji Vivuko vya Majini , pamoja Na Madaraja Ya Kupitia Juu kwa wananchi Kuvuka , Pamoja Na Ununuzi wa Meli Kubwa Za Mizigo Na kubeba Abiria, Sijaona Waraka.
 
Umeamisha Makao Makuu ya Nchi Kupeleka Dodoma ,Unaongeza Uzalishaji wa Umeme Huku Ukiwapelekea Wananchi Mpaka Vijijini , Umeongeza Nidhamu Serikalini Unaongeza AJIRA Kupitia Viwanda , Yote haya na Mengine Mengi  Sijaona Waraka .
 
Leo Hii wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wanaunganishiwa Maji Mpaka kwa Mkopo , Sijaona Waraka.
 
Leo Hii Mtulia Kuhama Chama Ambapo Ni Haki yake Kikatiba Ndio Nimeona Waraka .Ninakusihi na Kukuomba nikiwa  Mtumishi wa Mungu Ninae TAMKA  mambo na Kutokea.
 
Ninaye Yaona Mambo Yasiyo ONEKANA kwa  macho ya Mwili, Naiona Tanzania Mpya katika Uongozi wako.Shupavu.
Usifadhaike wala usihuzunike  kwa Sababu Unayoyasikia LEO na Kuyaona Hutayasikia tena kwa jina la Yesu Krsito Mwana wa Mungu aliye Hai.
 
Nakwasababu Wamebadili Kusudi la Kufa kwa Yesu Kristo , na kupoteza maana ya Pasaka.Bwana wa Majeshi anakwenda Kupindua Meza zao Kama ilivyotokea YERUSALEM.. Endelea.
 
Ujumbe huu Ukawatie Moyo Watu Wote Wanaoipenda Nchi na Kukuombea   kwa Roho na KWELI
 
 Ni mimi Mtumishi Wenu
 Paul Makonda
 Niliyepewa kipande cha Dar es salaam

Mrembo Aibuka na Kudai Alihaidiwa Ndoa na Diamond

$
0
0
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekuwa akitawala headlines za social media tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake Zari.

Wiki chache zilizopita Diamond alitangaza nia yake ya kutaka kuoa mwaka huu lakini hakuweka wazi atamuoa nani huku kila mwanamke wake wa zamani akitajwa katika nafasi hiyo.

Mrembo anayejulikana kwa jina la Rehema Fabian ambaye aliwahi kushiriki kinyang’anyiro cha Miss Kiswahili 2009, ameibuka na kudai alikuwa na historia ndefu na Diamond kuliko wanawake wengine wote.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda Rehema alisema kuwa, amesikia kuhusu Diamond kutangaza kuwa atafunga ndoa mwezi wa sita mwaka huu, lakini ni vyema Watanzania wakajua kwamba yeye na Diamond walikuwa ni wapenzi wakati msanii huyo anatoka kwa mara ya kwanza.

"Nimesikia kuwa Diamond anataka kuoa mwezi wa sita, natamani nijue anamuoa nani kwa sababu wengi tuliahidiwa kuolewa, lakini mwisho wa siku tulibwagwa, mimi ndiye msichana wa kwanza kabisa kuwa na staa huyo wakati anapata tuzo ya kwanza ya MAMA ambayo aliipatia nchini Nigeria na nilikuwa na mchango mkubwa katika kupata kwake mafanikio”.

Rehema aliendelea kufunguka kuwa, ameamua kusema haya kwa sababu Diamond hajawahi kumtaja popote kuwa alikuwa na uhusiano naye wakati yeye ndiye wa kwanza na katika mafanikio yake amechangia kwa kiasi kikubwa.

Rehema aliweka wazi kuwa sababu iliyopelekea wao kuachana ni Diamond kuchepuka na Wema na kuanzisha Mahusiano naye jambo alilodai lilimuumiza sana na aliweka wazi kuwa alikesha usiku na mchana anaomba waachane.

Lakini pia Rehema alimtaka Diamond kabla hajaoa akumbuke fadhila zake na aeleze umma ukweli wa penzi lao ili kufuta kile alichonacho moyoni kwani alitarajia baada ya kuwa na mafanikio, angemtafuta angalau kula naye bata, lakini hakuwahi kufanya hivyo ingawa alimuahidi mambo mengi mwanzo wa kusaka mafanikio.

RC Paul Makonda Katoa Ujumbe Mzito Kuwajibu Wanaotoa Waraka wa Kuikosoa Serikali

$
0
0
Ni vigumu sana Kusimama Katika HAKI Kwenye Dunia iliyojaa Uovu , Kwamaana Unapigwa Katika Kila Upande  na Hata Waliotakiwa Kuzama Katika Maombi nao Wamekengeuka .
 
Ninapoitazama Kazi ya Msalaba Naelewa Kwanini Yesu Kristo alibaki Peke Yake .
 
Umepigana VITA ya Madini sikuona Waraka , Umejenga Ukuta Mkubwa Mererani Kulinda Rasilimali Yetu ya Tanzanite , Sikuona Waraka ,Umepigana Vita ya Rushwa,Umeanzisha Mahakama za Mafisadi sikuona Waraka Umepambana na Wazembe Maofisini sikuona Waraka, Umetoa Elimu BURE Sikuona Waraka , Umefufua Shirika la NDEGE, Unajenga  Treni ya Mwendo Kasi (SGR) Sikuona Waraka. Umeanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Vyanzo Vipya Vya Umeme (Stigglers Gorge), Hatujaona Waraka.
 
Lakini Kama Haitoshi Umekomesha Mauaji ya Kutisha Ya Rai wasiokuwa Na Hatia kule Kibiti , Hatujaona Waraka ,Umekomesha Tabia Ya Askari kuvamiwa Na kuuwawa Vituoni wakiwa wanatimiza  Majukumu yao Ya Kulinda Raia , Hatujaona Waraka.Nakumbuka Kulikuwa na Tabia Ya kutorosha Wanyama kwa Kuwapandisha Ndege, Leo Umekomesha , Hatujaona Waraka .
 
Lakini Niwakumbushe , Umeongeza Bajeti ya Ununuzi wa Madawa Na Vifaa Tiba Kutoka Bilioni 31 Mpaka kufika Bilioni 260 , sijawai Kuona Waraka .
 
Tangu Umeingia Madaraka Umeongeza Vivuko katika Maeneo Yote Yanayohitaji Vivuko vya Majini , pamoja Na Madaraja Ya Kupitia Juu kwa wananchi Kuvuka , Pamoja Na Ununuzi wa Meli Kubwa Za Mizigo Na kubeba Abiria, Sijaona Waraka.
 
Umeamisha Makao Makuu ya Nchi Kupeleka Dodoma ,Unaongeza Uzalishaji wa Umeme Huku Ukiwapelekea Wananchi Mpaka Vijijini , Umeongeza Nidhamu Serikalini Unaongeza AJIRA Kupitia Viwanda , Yote haya na Mengine Mengi  Sijaona Waraka .
 
Leo Hii wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wanaunganishiwa Maji Mpaka kwa Mkopo , Sijaona Waraka.
 
Leo Hii Mtulia Kuhama Chama Ambapo Ni Haki yake Kikatiba Ndio Nimeona Waraka .Ninakusihi na Kukuomba nikiwa  Mtumishi wa Mungu Ninae TAMKA  mambo na Kutokea.
 
Ninaye Yaona Mambo Yasiyo ONEKANA kwa  macho ya Mwili, Naiona Tanzania Mpya katika Uongozi wako.Shupavu.
Usifadhaike wala usihuzunike  kwa Sababu Unayoyasikia LEO na Kuyaona Hutayasikia tena kwa jina la Yesu Krsito Mwana wa Mungu aliye Hai.
 
Nakwasababu Wamebadili Kusudi la Kufa kwa Yesu Kristo , na kupoteza maana ya Pasaka.Bwana wa Majeshi anakwenda Kupindua Meza zao Kama ilivyotokea YERUSALEM.. Endelea.
 
Ujumbe huu Ukawatie Moyo Watu Wote Wanaoipenda Nchi na Kukuombea   kwa Roho na KWELI
 
 Ni mimi Mtumishi Wenu
 Paul Makonda
 Niliyepewa kipande cha Dar es salaam

Urusi Yaendelea Kuitikisa Dunia.......Wanadiplomasia Wake Waendelea Kutimuliwa na Nchi Mbalimbali

$
0
0
Australia nayo imewafukuza wanadiplomasia wa Urusi kutoka nchini kwake kutokana na shambulio la jasusi wa zamani wa urusi nchini Uingereza Sergei Skripal na binti yake ambao wako katika hali mbaya kiafya.

Waziri mkuu Malcolm Turnbull amesema uamuzi huo unatokana na shambulio hatari la kutumia kemikali za neva zinazotengezwa na Urusi na zilitomiwa mara mwisho vita vya pili vya dunia.

Idadi ya wanadiplomasia wa Urusi wanaofukuzwa inazidi kuongezeka, na hii ndio idadi kubwa kuwahi kutokea katika historia.

Zaidi ya nchi 20 zimeungana na umoja wa Ulaya kuwafukuza zaidi ya wanadiplomasia 100.
 
Donald Trump amesema Urusi inapaswa kuachana na tabia zake hatarishi kwa mataifa mengine

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema hatua hiyo ya nchi nyingine kuungana na Uingereza ni matokeo ya tabia ya Urusi kuingilia nchi za watu.

''Ambacho kimesababisha nchi zote hizi kuungana na sisi, ni kutokana na vitu ambayo urusi imefanya, nchi nyingi ndani ya miaka kumi wameshuhudia kama sio jaribio la mauaji kufanyika nchini mwao basi wameingiliwa katika uchaguzi wao na mitandao yao, aina zote za tabia zisizo kubalika za Urusi,'' alisema Johnson.

Seneta wa Urusi Andrey Klimov anasema kuwa hakuna ukweli wowote wa shutuma dhidi ya Urusi bali ni propaganda dhidi yao.
Iceland imetangaza pia itasimamisha mazungumzo na mamlaka za Urusi na viongozi wake hawatahudhuria michuano ya kombe la dunia mwezi wa sita.

Mapema Uingereza ilisema kuwa hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya Malkia kushiriki kombe la dunia.

Itakumbukwa kuwa mwaka 1986 rais wa Marekani Ronald Reagan aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Urusi.

Na mwaka 2016 uongozi wa Barack Obama uliwafukuza wanadiplomasia 35 kutokana na kudukua chama cha Democratic.

Kauli ya Msemaji Mkuu wa Serikali Baada ya Kuulizwa Msimamo wa Serikali Kuhusu Matamko na Waraka wa Viongozi wa Dini

$
0
0
Waraka uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua mjadala mkubwa nchini.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi.

Mambo hayo kwa mujibu wa waraka huo ni Utekwaji wa watu ,utesaji, kupotea kwa watu, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, alipoulizwa msimamo wa serikali kuhusu waraka na matamko mbalimbali ya viongozi wa dini  alijibu kuwa   kwa sasa serikali haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.

Hata hivyo, Jana Rais Magufuli aliwashauri maaskofu nchini waanze kuhubiri ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi badala ya kuishia kukosoa na kulalamika .

Alitoa kauli hiyo akiwa katika halfa fupi jijini Dar es salaam ya uzinduzi wa  magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.

RC Paul Makonda Katoa Ujumbe Mzito Kuwajibu Wanaotoa Waraka wa Kuikosoa Serikali

$
0
0
Ni vigumu sana Kusimama Katika HAKI Kwenye Dunia iliyojaa Uovu , Kwamaana Unapigwa Katika Kila Upande  na Hata Waliotakiwa Kuzama Katika Maombi nao Wamekengeuka .
 
Ninapoitazama Kazi ya Msalaba Naelewa Kwanini Yesu Kristo alibaki Peke Yake .
 
Umepigana VITA ya Madini sikuona Waraka , Umejenga Ukuta Mkubwa Mererani Kulinda Rasilimali Yetu ya Tanzanite , Sikuona Waraka ,Umepigana Vita ya Rushwa,Umeanzisha Mahakama za Mafisadi sikuona Waraka Umepambana na Wazembe Maofisini sikuona Waraka, Umetoa Elimu BURE Sikuona Waraka , Umefufua Shirika la NDEGE, Unajenga  Treni ya Mwendo Kasi (SGR) Sikuona Waraka. Umeanzisha Mchakato wa Ujenzi wa Vyanzo Vipya Vya Umeme (Stigglers Gorge), Hatujaona Waraka.
 
Lakini Kama Haitoshi Umekomesha Mauaji ya Kutisha Ya Rai wasiokuwa Na Hatia kule Kibiti , Hatujaona Waraka ,Umekomesha Tabia Ya Askari kuvamiwa Na kuuwawa Vituoni wakiwa wanatimiza  Majukumu yao Ya Kulinda Raia , Hatujaona Waraka.Nakumbuka Kulikuwa na Tabia Ya kutorosha Wanyama kwa Kuwapandisha Ndege, Leo Umekomesha , Hatujaona Waraka .
 
Lakini Niwakumbushe , Umeongeza Bajeti ya Ununuzi wa Madawa Na Vifaa Tiba Kutoka Bilioni 31 Mpaka kufika Bilioni 260 , sijawai Kuona Waraka .
 
Tangu Umeingia Madaraka Umeongeza Vivuko katika Maeneo Yote Yanayohitaji Vivuko vya Majini , pamoja Na Madaraja Ya Kupitia Juu kwa wananchi Kuvuka , Pamoja Na Ununuzi wa Meli Kubwa Za Mizigo Na kubeba Abiria, Sijaona Waraka.
 
Umeamisha Makao Makuu ya Nchi Kupeleka Dodoma ,Unaongeza Uzalishaji wa Umeme Huku Ukiwapelekea Wananchi Mpaka Vijijini , Umeongeza Nidhamu Serikalini Unaongeza AJIRA Kupitia Viwanda , Yote haya na Mengine Mengi  Sijaona Waraka .
 
Leo Hii wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Wanaunganishiwa Maji Mpaka kwa Mkopo , Sijaona Waraka.
 
Leo Hii Mtulia Kuhama Chama Ambapo Ni Haki yake Kikatiba Ndio Nimeona Waraka .Ninakusihi na Kukuomba nikiwa  Mtumishi wa Mungu Ninae TAMKA  mambo na Kutokea.
 
Ninaye Yaona Mambo Yasiyo ONEKANA kwa  macho ya Mwili, Naiona Tanzania Mpya katika Uongozi wako.Shupavu.
Usifadhaike wala usihuzunike  kwa Sababu Unayoyasikia LEO na Kuyaona Hutayasikia tena kwa jina la Yesu Krsito Mwana wa Mungu aliye Hai.
 
Nakwasababu Wamebadili Kusudi la Kufa kwa Yesu Kristo , na kupoteza maana ya Pasaka.Bwana wa Majeshi anakwenda Kupindua Meza zao Kama ilivyotokea YERUSALEM.. Endelea.
 
Ujumbe huu Ukawatie Moyo Watu Wote Wanaoipenda Nchi na Kukuombea   kwa Roho na KWELI
 
 Ni mimi Mtumishi Wenu
 Paul Makonda
 Niliyepewa kipande cha Dar es salaam

Breaking News: Kesi Imemponza Nondo....UDSM Wamemsimamisha Kuendelea na Masomo Hadi Kesi Yake iishe

$
0
0
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemsimamisha kuendelea na masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu, Abdul Nondo baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), amesimamishwa kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye.

Profesa Anangisye amesema mwanafunzi anapokuwa amepandishwa kizimbani na akawa na kesi ya kujibu husimamishwa na akishamaliza kesi yake anarejea kuendelea na masomo.

LHRC Wampinga Waziri Nchemba Matumizi ya Viboko Shuleni

$
0
0
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetofautiana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba ya kutaka walimu kutumia adhabu ya fimbo kuweka nidhamu kwa wanafunzi shuleni

Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dk. Nchemba alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi, ili kutengeneza hatima ya nchi.

Alisema wakati walimu wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kunyoosha nidhamu kwa wanafunzi kwa kutumia fimbo, wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiwalalamikia na kuwataka wawaache watekeleze majukumu yao.

“Wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi, wapo watu wengine huwalalamikia tu, na hawajui kwamba kinachofanyika ni kwa manufaa yetu. 

"Niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo, ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk. Mwigulu.

Akizungumzia kauli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo Bisimba, amesema kutumia fimbo kwa mwanafunzi hakuwezi kusaidia kumjengea nidhamu.

Pia, amesema kutumia adhabu hiyo kunaweza kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao kielimu.

“Ni kweli kwamba walimu wanapaswa kuachwa watekeleze majukumu yao bila kuingiliwa, lakini linapokuja jambo la adhabu au kujenga nidhamu kwa wanafunzi lazima uangaliwe mfumo unaotumika,” alisema Dk. Kijo Bisimba na kuongeza:

“Zipo adhabu ambazo mwanafunzi anaweza kupewa akikosa, lakini si kwa kuchapwa fimbo. Unaweza ukafikiri ukimchapa ndio unamjenga, lakini kumbe ndio unambomoa zaidi. 

"Nasema hivyo kwa sababu unapoanza kumchapa mwanafunzi hawezi kufanya vizuri tena darasani. Mimi namuomba waziri a-deal (ashughulike) na mambo ya wizara yake, ya elimu ayaache.”

Vigogo CHADEMA Waripoti Polisii Wakiongozwa na Mbowe

$
0
0
Viongozi waandamizi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jumanne Machi 27, 2018.

Viongozi wengine waliofika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji, manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na mweka hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee bado hawajafika kituoni hapo.

Viongozi hao waliripoti polisi Machi 22, 2018 na kutakiwa kuripoti leo. Siku hiyo Mdee na Matiko hawakuwepo huku Mnyika na Heche wakihojiwa kwa zaidi ya saa mbili kutokana na kutoripoti siku za nyuma.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Aeleza Alivyokataa Rushwa ya Milioni 800

$
0
0
MAMLAKA ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya imemtia mbaroni mfanyabishara wa kemikali bashirifu, mkazi wa Mwanza ambaye alitaka kuwahonga mamilioni ya fedha makamishna wa mamlaka hiyo ili wavuruge kesi inayomkabili.

Mfanyabiashara huyo ambaye jina lake halikutajwa kutokana sababu za usalama, inasemekana baada ya kukamatwa, aliahidi kumhonga Sh milioni 800  Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers Siang’a   amsaidie kufuta shitaka lake.

Pia, mtuhumiwa huyo aliahidi kumpa rushwa ya Sh milioni 400  Kamishna wa Sheria wa Mamlaka hiyo, Edwin Kakolaki ili naye amsaidie kuvuruga kesi iliyokuwa ikimkabili.

Siang’a alikuwa akizungumza juzi mjini hapa wakati wa semina ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Ukimwi na Dawa za Kulevya.

Alisema viwango vikubwa vya kemikali bashirifu ambayo mara nyingine hutumika kutengenezea dawa za kulevya,  imekuwa  ikiingizwa nchini.

“Kuna zaidi ya kampuni 2000 zimekuwa zikiingiza kemikali bashirifu nchini  lakini kasi ya kuzikagua kemikali hizo imekuwa ndogo kutokana na wingi wa kampuni na uchache wa rasilimali watu na fedha.

“Lakini  Desemba mwaka jana, kuna mfanyabiashara mmoja wa kemikali bashirifu alitaka kumpa hongo Kamishna Kakolaki, ya Sh milioni 400  avuruge kesi, ila kwangu alisema akinifikia  atanipa Sh milioni 800,” alisema   Siang’a.

Kamishna wa Kinga na Tiba kwenye mamkala hiyo, Dk. Peter Mfisi, alisema hadi sasa   Watanzania 1050 wamekamatwa katika nchi mbalimbali wakituhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Alisema kitendo hicho kimekuwa kikichafua hadhi ya Tanzania katika sura ya  mataifa.

“Hata hivyo, udhibiti wetu umefanikiwa kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo nchini na kusababisha kuongezeka kwa watu wanaohitaji matibabu ya ‘methadone   na kupanda kwa bei ya dawa hizo mtaani.

“Kwa ujumla, hali bado ni mbaya kwa watumiaji wa dawa hizo hasa kutokana na kuambukizana magonjwa ya Ukimwi, TB na homa ya ini kwa sababu watumiaji hao  wana tabia ya kuchangia sindano.

“Lakini mtumiaji akimuona mwenzake anasinzia wakati akiwa amejichoma sindano, basi hunyonya damu ya mwenzake kwa kutumia sindano kisha kujidunga akiamini kuwa damu ya mtu huyo ina dawa za kulevya,” alisema.

Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema kutokana na udhibiti wa dawa hizo kuimarika, wafanyabiashara wameanza kuwatumia watoto wa viongozi na matajiri wakiamini wana uwezo wa kununua dawa kwa urahisi.

“Pamoja na hayo, Serikali itawasaka kila kona bila kujali mtu au nafasi aliyonayo   kuhakikisha mtandao huo unatokomea,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Oscar Mukasa, alisema lengo la semina hiyo ni kuwapa mwanga wajumbe wapya wa kamati hiyo  wafahamu utendaji kazi na muundo wa mamlaka hiyo.

Pamoja na hayo, alisema kamati yake itashirikiana na mamlaka husika na Serikali ili vita dhidi ya dawa za kulevya, ifanikiwe.

Breaking news: Rais Magufuli Kawasimamisha KAZI Wakurugenzi Wawilii

$
0
0
Rais John Magufuli amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa halmashauri za Kigoma Ujiji,  Boniface Nyambe na Daud Mlahagwa (Pangani).

Rais Magufuli ametoa uamuzi huo leo Jumanne Machi 27, 2018 wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad iliyobaini madudu katika ukaguzi wa serikali za mitaa na mashirika ya umma.

“Kuanzia leo mkurugenzi wa Pangani na Kigoma Ujiji wasimamishwe kupisha uchunguzi, uchunguzi ufanyike kuanzia leo lazima tuchukue hatua,” amesema.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Profesa Assad amesema serikali za mitaa 140 zilishindwa kukusanya mapato ya Sh116 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 22 ya mapato yake.

“Zaidi ya hayo pia tuliona mawakala kutowasilisha Sh3.5 bilioni ya makusanyo lakini hawakuwasilisha, ni usimamizi mbovu tu wa halmashauri kwani kama mawakala wamekusanya kwa nini usikusanye mapato yako,” amesema Profesa Assad.

Madudu mengine aliyobaini CAG ni kupotea kwa vitabu 379 vya mapato ya Serikali, ambavyo haikujulikana ni kiwango gani cha fedha kilichopotea kutokana na upotevu wa vitabu hivyo.

“Kitabu cha mapato kisipokuja kwetu hatuwezi kujua ni kiwango gani kimetumika katika vitabu hivyo, lakini tuliona katika halmashauri za Bihalamuro, Karagwe na Mpwapwa, kulikuwa na miradi mitatu ambayo thamani yake ilifikia Sh1.6 bilioni iliyocheleweshwa kukamilishwa,” amesema.

“Pia,  kulikuwa na udhaifu katika usimamizi wa rasilimali watu na udhibiti wa mishahara, kwa mfano kuna madai ya watumishi ambayo yanafikia Sh10 bilioni katika mamlaka za serikali za mitaa 19, ambao hawakulipa hadi mwisho wa mwaka wa Juni 2017.”

Ripoti ya CAG: Deni la Taifa Linatia Mashaka, Serikali Ichukue Hatua Mapema

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG), Profesa Mussa Assad amesema deni la Taifa linatia wasiwasi hivyo Serikali inatakiwa kuchukua hatua kupunguza ukubwa wa deni hilo.

Profesa Assad ametoa kauli hiyo leo Jumanne Machi 27, 2018 na kubainisha kuwa  deni hilo ni Sh46 trilioni kutoka Sh41 trilioni la mwaka uliopita, kwamba ni ongezeko la asilimia 12.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa uwasilishaji wa ripoti yake ya ukaguzi mwaka 2016/17 iliyobaini madudu Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma.

“Tulichosema hapa kwa kweli ukuaji wa deni tunasema ni himilivu lakini jinsi linavyoongezeka tunakaribia maeneo ya wasiwasi. Asilimia 72 ya GDP (Pato la Taifa) siyo mbaya lakini ikifika asilimia 76 nchi nyingine zimepata shida, inabidi tuangalie sasa namna gani tunaweza  ku-control ukuaji wa deni hilo,” amesema.

Updates: Mbowe na Viongozi Wenzake Wafutiwa Dhamani na Kutupwa Mahabusu

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam leo asubuhi Machi 27, 2018, wamewekwa mahabusu.

Viongozi wengine waliofika kituoni hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.
 
Wakili wa viongozi hao wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema kuwa wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa kutokea.

Viongozi hao waliripoti polisi Machi 22, 2018 na kutakiwa kuripoti leo. Siku hiyo Mdee na Matiko hawakuwepo huku Mnyika na Heche wakihojiwa kwa zaidi ya saa mbili kutokana na kutoripoti siku za nyuma.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Mchungaji Msigwa aunganishwa katika Kesi ya Akina Mbowe na Viongozi Wengine

$
0
0
Wakili wa viongozi wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa naye ameungwanishwa na viongozi waliowekwa mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Kihwelo amesema Mchungaji Msigwa aliitwa na alipofika polisi naye aliunganishwa na wenzake.

Viongozi hao wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa kutokea.

Viongozi waliowekwa mahabusu ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Polisi Mkoani Mbeya Watoa TAMKO Baada ya Vurugu Kubwa za Wananchi Wakilituhumu Jeshi Hilo kwa Kifo cha Mtuhumiwa Mmoja

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. 

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Oparesheni na Doria za mara kwa mara ili kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na kuzuia matukio mbalimbali yakiwemo ya uporaji na ukabaji na kama mtakumbuka siku za karibuni kulijitokeza vikundi vya uhalifu vilivyojiita majina ya wakorea weusi, weupe. Hata hivyo kumekuwa na matukio mawili kama ifuatavyo:-

Watuhumiwa wa uhujumu miundombinu ya TANESCO
Mnamo 24.03.2018 majira ya saa 00.15 usiku askari Polisi waliokuwa katika doria na oparesheni ya kukamata wahalifu huko maeneo ya Mtaa wa Airport ya Zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya na katika Doria hiyo walikamatwa vijana kumi na wawili akiwemo kijana mmoja ambaye alifahamika kwa jina la ALAIN ACHILE [22] Mkazi wa Airport ya zamani.

Mtuhumiwa huyu pamoja na wenzake baada ya kukamatwa walifikishwa kituo kikuu cha Polisi Mbeya Mjini na kufunguliwa mashitaka ya UZEMBE NA UKOROFI ambapo walishikiliwa na kuhojiwa.

Mnamo 25.03.2018 majira ya saa 10.45 asubuhi mtuhumiwa ALAIN ACHILE alidhaminiwa na ndugu zake na kwenda nyumbani kwao. Ilipofika majira ya saa 18.00 jioni zilipatikana taarifa kuwa mtuhumiwa huyo amefariki dunia.

Mara baada ya taarifa hizo, wananchi wa eneo hilo la Airport ya zamani hasa vijana walianza kufanya fujo kwa kutuhumu kuwa Polisi wamehusika na kifo hicho hivyo kwenda nyumbani kwa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa BOAZ KAZIMOTO [74] Mkazi wa Iyela kwa kumtuhumu kuwa yeye ndiye aliyewaita Polisi kwenda kumkamata marehemu ALAIN ACHILE na wenzake hivyo walipofika nyumbani kwa Mwenyekiti huyo walianza kuvunja madirisha ya nyumba yake, Baadaye walikwenda kwenye barabara za mtaa huo na kupanga mawe barabarani na kuchoma moto meza za wafanyabiashara wa Soko la Maendeleo.

Halikadhalika walikwenda Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyela na kubomoa milango yote, kuharibu samani za ofisi na kuharibu baadhi ya nyaraka mbalimbali za ofisi ambazo hadi sasa thamani yake haijajulikana. Sanjari na hayo pia walikwenda nyumbani kwa askari aitwaye H.4325 PC YOHANA wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na kuvunja madirisha ya nyumba yake huku wakitoa kauli ya kuwa wataichoma moto nyumba hiyo.

Kutokana na vurugu hizo askari walifika eneo hilo ili kutuliza vurugu hizo lakini wakati wanafika wananchi hao walianza kurusha mawe ili kuwadhuru askari  waliokwenda eneo hilo.

Kutokana na vurugu hizo, Gari yenye namba za usajili PT 1987 aina ya Toyota Land Cruiser Mali ya Polisi Wilaya ya Mbeya mjini ilivunjwa kioo cha mbele kwa mawe hivyo kulazimu askari kufyatua mabomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.

Aidha katika vurugu hizo watuhumiwa nane [08] wamekamatwa kuhusika na vurugu hizo ambao ni:-
  1.     ELIUD  DAUD [22] Mkazi wa Iyela
  2.     BARIKI MASUDI [30] Mkazi wa Iyela
  3.     FRANK  KILEMI [33] Mkazi wa Airport ya zamani
  4.     KRIST NELSON [33] Mkazi wa Airport ya zamani
  5.     ESTOM MBALO [24]  Mkazi wa Airport ya zamani
  6.     ROBERT MWANGUPILI [24] Mkazi wa Iyela
  7.     ISSA NELSON [26] Mkazi wa Iyela
  8.     FELIX MBILINYI [21] Mkazi wa Airport ya zamani.
Watuhumiwa hao wanahojiwa na Jeshi la Polisi na watafikishwa Mahakamani wakati wowote mara baada ya taratibu za kisheria zitakapokamilika. Aidha juhudi ya kuwasaka wengine waliohusika na kuanzisha vurugu hizo zinaendelea.

Nichukue nafasi hii kuwapa pole wazazi, ndugu na hata walioguswa na kifo cha kijana huyu, niwathibitishie wananchi kuwa Jeshi la Polisi halikuhusika na kifo cha kijana huyu kwa aina yoyote. Aidha nimefungua jalada la uchunguzi [PE] kupitia Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai [RCO] ofisini kwangu kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha ALLAIN ACHILE.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WALIOINGILIA MIUNDOMBINU YA TANESCO.
Mnamo tarehe 23/03/2018 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na maafisa wa Tanesco lilifanya Oparesheni katika maeneo ya vijiji vya Isebe na Isajilo vilivyopo Wilaya ya Rungwe kufuatia taarifa za siri toka kwa raia wema kuwa kuna watu wanaingilia miundombinu ya Tanesco katika vijiji hivyo pamoja na kufanya wizi wa nguzo za umeme na kuwaunganishia umeme wakazi wa maeneo hayo kinyume cha sheria.

Katika Oparesheni hiyo, watuhumiwa wanne [04] wamekamatwa kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Shirika la Umeme [Tanesco]. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  1.    IDD HAMIS MWAMBUSYE [31] Mkazi wa Bagamoyo.
  2.     BENARD KIBONDI [40] Mkazi wa Kikota
  3.     THOBIAS WILFRED [42] Mkazi wa Iponjola
  4.     Eng.GEOFREY MSUNGA [30] Mkazi wa Mbeya
Aidha miongoni mwa watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa majumbani kwao walikutwa na vifaa mbalimbali vya umeme ambavyo ni:-
  1.  Mita za umeme 27 aina ya Tropical
  2. Nyanya za umeme mkubwa na mdogo za aina mbalimbali
  3. Kitoboleo cha nguzo
  4.  Stay Insulator
  5.  Plaizi
  6.  Tester za umeme
  7.  Seal za mita za umeme
  8.  Vibao vya tahadhari vinavyobandikwa kwenye nguzo za umeme
  9.  Nguzo 57 za umeme ambazo walikuwa zikitumika kuwaunganishia umeme wananchi.
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Aidha msako mkali unaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaojihusisha na uhujumu wa miundombinu ya Shirika la Umeme – TANESCO katika maeneo mbalimbali.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kutii sheria bila shuruti. 

Aidha anatoa wito kwa jamii kuachana na tamaa ya mali hasa kwa kujihusisha na vitendo vya kihalifu ili wapate mali na badala yake wafanye kazi halali.

Breaking News:Mbowe na Viongozi wengine CHADEMA wamefikishwa Mahakamani

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na vigogo wengine wanne wa chama hicho wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo baada ya kuwekwa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine waliofikishwa mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vincent Mashinji; manaibu katibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar) na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko.

Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Habari Masaa 24......Pakua Upya Application Yetu Tukuhabarishe Usike na Mchana

$
0
0
==>Pakua Upya Application yetu tukuhabarishe masaa 24 usiku na mchana.

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya Mpekuzi Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Maboresho Mapya Yamefanyika ili kukufanya upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile kuliko ilivyo sasa.

App ya zamani ilikuwa na tatizo kubwa la kuchelewa kufunguka, kuchelewesha habari na muonekano wake haukuwa wa kiwango kinachostahili.

Chakufanya, Ingia PlayStore, Download Upya Application yetu  MPYA. Ukishaipakua hii Mpya, ya zamani ifute tu.

NB: App mpya ina Icon ya Njano

Tumekurahisishia;

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Latest Images