Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa, Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana  March 23 , 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kitivo cha Taaluma na Utafiti.

Rais Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 March, 2018.

Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine (SUA).

Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Anna Makinda ataka viongozi wanawake kupewa elimu

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania mstaafu, Mama Anna Makinda ametoa elimu wa uongozi wa Kijinsia kwa madiwani wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo madiwani hao.

Akizungumza katika warsha hiyo, Bi. Makinda alisema suala la kuwajengea uwezo wanawake linapaswa kuanza mapema mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili kupata muda zaidi wa viongozi hao kupata elimu stahiki, kwani mara nyingi elimu hiyo hucheleweshwa kutolewa.

“…Kimsingi muda huu tumechelewa mikakati ya kuanza kumuwezesha kiongozi mwanamke hupaswa kuanza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi hii itatusaidia hata kujipanga mapema uongozini…,” alisema Mama Makinda akizungumza na madiwani hao.

Aliwataka wanawake wote viongozi kuwa pamoja hasa wanapopigania masuala ya wanawake ili kwani umoja mara zote ni nguvu na utengano ni udhaifu. Changamoto za wanawake hazitofautiani kiitikadi za chama, rangi wala imani hivyo kuna kila sababu ya kuungana pale wanapogombea ajenda za wanawake.

Pamoja na hayo aliwataka madiwani wanawake kujipanga kimikakati na kutokubali kuondolewa katika nafasi za uongozi kizembe, kwani uwezo wa kuwatumikia wananchi wanao tena wa kiwango kikubwa kama watajipanga vizuri.

“…Hivi unakubalije mtu aliye nje kuja kukutoa katika nafasi yako kirahisi rahisi ilhali wewe upo karibu na wananchi, usikubali tuwaoneshe kwa vitendo tulioingia tusitoke kirahisi bila kupenda labda tupande ngazi lakini sio kushuka,” alisisitiza Mama Makinda.

Aidha aliwaomba kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano na viongozi wa kiume kwani idadi yao ni kubwa hivyo ushawishi pekee ndio unaweza kuongezea nguvu ajenda zao. 

Alibainisha idadi ya madiwani na wabunge wa kiume ni kubwa ukilinganisha na wao hivyo njia pekee ya wao kufanikiwa ni kujenga urafiki, ukaribu na ushawishi kwa agenda anuai zinazobebwa na wanawake.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Bi. Suzan Lyimo akizungumza na madiwani hao aliwaomba kuwa kitu kimoja haswa wanapopigania masuala ya msingi kumuwezesha mwanamke.

Alisema kama wanawake hawatakuwa kitu kimoja hawawezi kufanikiwa katika agenda zao. Hata hivyo aliongeza kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kwani ndipo mipango mingi ya chama upangwa kwa utekelezaji zaidi.

Kesi ya CUF inayohoji uhalali wa bodi ya wadhamini ya Lipumba kusikilizwa Machi 27

$
0
0
Na Regina Mkonde
 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imepanga kusikiliza mashauri mawili Namba 557 na 558/2017 yaliyofunguliwa mahakamani hapo na Wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF dhidi ya Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi-RITA.

Kesi hizo zinahoji uhalali wa wajumbe wa Bodi ya Udhamini CUF walioteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba, zitasikilizwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Zainab Goronya Muruke.

Taarifa hiyo imetolewa jana kwa vyombo vya habari na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na UmMa CUF, Mbarala Maharagande.

Pia, Maharagande alisema Mahakama Kuu imepanga kusikiliza mfululizo kesi za CUF ambazo jana ziliahirishwa kusikilizwa kutokana na Jaji anayesimamia kesi hizo, Wilfred Ndyansobera kupata na udhuru.

Maharagande amesema kesi hizo ambazo ni Na. 28, 68, na 80 za mwaka 2017 zinazohusu Wizi wa fedha za Ruzuku ya CUF, Na. 21/2017 inayohusu Wabunge 19 wa CUF dhidi ya Lipumba na wenzake pamoja na kesi Na. 13/2017 iliyofunguliwa na Ally Salehe dhidi ya RITA, zitaanza kusikilizwa kuanzia Aprili 16, 17 na 18 mwaka huu.

“Shauri la Msingi Namba 23/2017 kuhusu Uhalali wa Uenyekiti wa Lipumba ambalo lilikuwa Mahakama ya Rufaa Tayari lisharejeshwa Mahakama Kuu na limepangwa kutajwa Tarehe Aprili 19, 2018 mbele ya Jaji Ignus Paul Kitusi,” amesema.


Polisi Wamtia Mbaroni aliyejifanya JWTZ na Usalama wa Taifa

$
0
0
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara mmoja kiasi cha sh. Million 8.

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi kwa  utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi ya cheo cha Kaptein.

Wengine ni Emmanuel Michael (45) mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela (50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.

Serikali kuwatumia waganga wa kienyeji Kuwasaka Wagonjwa wa TB

$
0
0
Katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) nchini, serikali imesema kuwa itawatumia waganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao ili waweze kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata tiba sahihi.

Kauli hiyo imetolewa jana (Machi 23, 2018) mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yanayofanyika leo (Machi 24, 2018).

Waziri Mwalimu alisema kuwa waganga wa kienyeji ni wadau muhimu katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa wagonjwa wengi hukimbilia kwao kwa kudhani kuwa wamerogwa.

Aidha, Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO inakadiriwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua kifua kikuu kila mwaka duniani huku milioni moja kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15 na hapa nchini kila mwaka jumla ya watu 60,000 wanaambukizwa ugonjwa huo wakati mwaka 2016 watu 65,908 waliogundulika kuugua na kuanza matibabu.

Profesa J Naye Kawavaa BASATA

$
0
0

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia kwa sasa ni mbunge Profesa Jay, amefunguka juu ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufungia wasanii na baadhi ya kazi zao, na kusema kuwa suala hilo sio sahihi.

Prof Jay amesema BASATA wanapaswa kukaa na wasanii na kuzungumza nao, ikiwezekana kutoa semina elekezi, lakini sio kuwafungia kwani wasanii wanapitia mengi magumu kwenye kutengeneza kazi zao.

Prof. Jay amesema kwamba serikali inafahamu kubwa ya jamii ni vijana, na wengi wao wanajishughulisha na sanaa ili kujipatia kipato, wanapofanya hivyo wanawakwamisha vijana hao ambao wanapigana kujitoa kimaisha..

“Unajua asilimia kubwa ya taifa ni vijana, na wengi wao wanajishughulisha na sanaa mbali mbali, suala la kufunginwa huu mziki tumetoka nao mbali sana, mtoto akikosea usimchinje kichwa, tujaribu kufanya semina elekezi, kumfungia mtu kama roma ni kitu kikubwa, hii inarudisha nyuma na inakatisa tamaa”, amesema Prof. Jay.

Prof Jay ameendelea kwa kusema kwamba yeye kama muwakilishi wa wananchi na wasanii pia, atalisemea hili bila kuchoka.

Mbarawa : Serikali itaendelea kuiwezesha TMA.

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kuwezesha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati na usahihi kwa manufaa ya taifa.

Profesa Mbarawa amesema hayo jana mjini Dodoma  wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Hali ya hewa, na kusisitiza kuwa kwa sasa TMA imeongeza imani kwa wananchi kwani imekuwa ikitoa utabiri wa kuaminika kwa  sababu ya kuwa  vifaa vingi na vya kisasa vya utoaji taarifa.

“Nipende kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwezesha TMA na kuhakikisha kuwa inatoa utabiri ambao ni sahihi na wa uhakika kwani kuwepo kwa utabiri sahihi kutawezesha vyombo husika kuchukua hatua mapema kabla ya madhara makubwa kutokea” alisema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuepuka kuchafua maeneo ya bahari ili kuepusha athari zinazoepukika zikiwemo uharibifu wa miundombinu ya  uchukuzi.

 “Niwaombe wananchi wote watunze mazingira kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu katika maeneo mbalimbali yasiyotakiwa kulimwa au kujengwa, alisisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa kwa kutoa fedha kununua vifaa mbalimbali ambavyo vimewezesha mamlaka hiyo kutoa utabiri uliosahihi kwa zaidi ya asilimia 70.

Dkt Kijazi ameongeza kuwa kwa sasa taarifa za hali ya hewa hasa kwenye usafiri wa anga zimeimarika ambapo hutolewa kila baada ya nusu saa na kuwawezesha watumiaji wa usafiri huo kupata taarifa kabla ya kuanza safari zao.

“Kwa sasa utabiri wa usafiri wa anga ni wa  uhakika mpaka asilimia 90 na hutolewa kila baada ya nusu saa na marubani hupata taarifa hizo kwa wakati kabla ya kuanza safari zao, alisema Dkt. Kijazi.

Siku ya Hali ya Hewa duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi ambapo mwaka huu yanaongozwa na kauli mbinu isemayo“JIWEKE TAYARI NA ZINGATIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA”.

Majaji watatu kusikiliza kesi ya ACT Wazalendo dhidhi ya Jeshi la Polisi

$
0
0
Mahakama  kuu ya Dar es salaam Aprili 5, 2018 itaanza kusikiliza kesi ya madai ya chama cha ACT Wazalendo dhidi ya jeshi la polisi

Tarifa iiliyotolewa jana  na Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamisi  ilisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

"Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi. 

"Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

"Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba."- Ilisema taarifa hiyo

Diamond afanya mazungumzo ya siri na Basata

$
0
0
Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Ijumaa hii amefanya mazungumzo ya siri na Baraza la Sanaa Taifa ‘Basata’ ikiwa ni siku chache toka aingie kwenye majibizano na Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo “African Beauty” alitua viwanja vya basata  jana mchana akiwa na meneja wake, Sallam SK. Hata hivyo baada ya kufanya mazungumzo hakuweza kuzungumza chochote juu ya nini kilitokea.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Basata zinadai muimbaji huyo alifika katika taasisi hiyo ya malezi ya wasanii kwaajili ya kuzungumza na viongozi hao juu ya kauli zake ambazo amekuwa akizitoa juu ya Naibu waziri huyo.

Hata hivyo Basata hawajatoa taarifa yoyote juu ya kikao hicho cha siri ambacho kilichukua masaa kadhaa.

Wadau wa mambo ya sanaa wanadai huwenda muimbaji huyo alikwenda Basata kwaajili ya kuomba radhi juu ya mambo yanayoendelea.

Mapema wiki hii muimbaji huyo wakati anahojiwa na kituo cha redio cha Times FM aliitupia lawama Basata pamoja na Naibu waziri huyo baada ya kufungia nyimbo 15 za wasanii wa bongofleva zikiwemo zake mbili.

Kauli hizo zilimfanya Waziri wa Habari, Dk Mwakyembe kutoa kauli yake na kudai kwamba ameshtushwa na kauli za muimbaji huyo juu ya waziri.

Video Queen wa ngoma ‘Natamba’ Ya Aslay Akanusha Kutoka Nae Kimapenzi

$
0
0
Video Queen katika ngoma ya Aslay ‘Natamba’ amefunguka kuhusu taarifa za kutoka kimapenzi na muimbaji huyo.

Mrembo huyo ambaye pia aliwahi kutokea katika video ya Belle 9 na G Nako ‘Ma-Ole’ ameiambia The Base, ITV kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani kwa sasa wao ni marafiki wa kawaida tu.

“Hapana, sijawahi kutoka na Aslay, wala hatujawahi kuwa na mahusiano ni rafiki yangu tu basi na tutaendelea kuwa marafiki wa karibu mengine no, sio marafiki wa karibu kiivyo,” amesema.

Natamba pengine ndio wimbo wa Aslay wenye mafanikio zaidi, wimbo hao hadi sasa katika mtandao wa Youtube una views zaidi ya Milioni 5 na hakuna wimbo wa Aslay uliofikisha idadi hiyo.

Serikali Yakiri KUKOSEA Suala la Umri wa Kujiunga Kidato cha Tano

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na kuweka wazi utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.

Semakafu amesema kuwa yametokea makosa ya kiuandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika taarifa aliyotolewa jana

"Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi"  alisema Semakafu 

Kufuatia makosa hayo serikali imetoa waraka mpya kurekebisha ule wa mwanzo, na kipengele cha miaka 20 wameweka 25.

Mahakama imewaachia wangonjwa 55 wa akili.

$
0
0
Jumla  ya wagonjwa wa akili 55 waliokuwa wametenda makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai wakiwa na ugonjwa wa akili, wameachiwa huru baada ya mahakama kutowatia hatiani.

Hayo yameelezwa jana mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

Kamati hiyo ilikuwa nchini ya Uenyekiti wa Najma Murtaza Giga.

Profesa Kabudi ameieleza kamati hiyo kwamba, kifungu cha 219 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20, kinampatia Waziri mwenye dhamana ya masuala ya sheria mamlaka ya kuwaachia huru wagonjwa wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai yakiwamo ya mauaji.

“Kutokana na mamlaka hayo ya kisheria, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, nilisaini hati ya kuachiliwa huru wagonjwa 55 wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai wakiwa na ugonjwa wa akili na hivyo mahakama kutowatia hatiani,” amebainisha Profesa Kabudi.

Aliongeza kuwa kwa muda mrefu wagonjwa hao walikuwa wakihifadhiwa kwenye Taasisi ya Isanga kusubiri amri ya Waziri.

“Na kutokana na hali ya afya zao za akili kuimarika, iliamua waachiliwe huru, ili waungane na familia zao na kuendelea na matibabu wakiwa nje ya taasisi hiyo,” ameeleza.

Pamoja na kuelezea hilo, Profesa Kabudi pia alianisha mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na wizara pamoja na taasisi zake katika suala zima la utoaji na usimamiaji wa haki katika kipindi cha bajeti cha 2017/2018.

Baadhi ya mafanikio hayo ni kwa Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya daawa ilipata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na thamani ya Sh 1,064,581,955,743.

Kwa mujibu wake, ushindi huo umewezesha pamoja na mambo mengine maamuzi ya serikali pamoja na sheria za nchi kutobadilishwa kwa msingi wa kukiuka Katiba.

Mafanikio mengine aliyoyataja ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea na utoaji wa ushauri wa kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali yanayofanywa na Wizara Idara na Taasisi za Serikali.

Katika eneo hilo, hadi kufikia Februari mwaka huu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki na kutoa ushauri wa mikataba 691 yenye thamani ya Sh 1,720,026,713,823 na Dola za Marekani 1,0884,472,366, mikataba hiyo ilihusu ununuzi, ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii na ujenzi wa barabara.

Aidha, kwa upande wa mali zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya Sh 2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya Sh 908,019,979.

Mali nyingine zilizotaifishwa ni pamoja na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika bandari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba.

Mali nyingine zilizotaifishwa katika kipindi hicho ni pikipiki, mifugo, mafuta na basi la abiria lililokuwa likitumika kusafirishia meno ya tembo zinazokadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya Sh 3,242,787, 915.
 
Credit:Habarileo

Baba Ahukumia Jela Miaka Minne kwa Kosa la Kumpa Mimba Binti yake

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tabora imemhukumu mkazi wa Manispaa ya Tabora, Sadick Masunzu (47) kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 16 na kumpatia ujauzito.

Akitoa hukumu hiyo jana, hakimu wa mahakama hiyo, Joctan Rushela alisema ameridhika na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili Tito Mwakalinga kuthibitisha bila shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Hakimu huyo aliongeza kuwa kitendo kilichofanywa na mshtakiwa si cha kiungwana katika jamii ya Watanzania, hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo na inamhukumu kwenda jela miaka minne ili liwe funzo kwake na kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Awali wakili wa Serikali, Mwakalinga alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alimbaka mtoto wake wa kumzaa na kumsababishia ujauzito.

Mwakalinga alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo katika tarehe tofauti Januari 2017 na kumsababishia ujauzito binti huyo aliyekuwa mwanafunzi wa Sekondari ya Lwanzali iliyopo katika Manispaa ya Tabora ashindwe kuendelea na masomo.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa kwa kuwa kitendo cha kumbaka na kumtia mimba mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi kimemharibia maisha yake.

Watu 27 wakamatwa kwa madai ya kuchoma kituo cha polisi

$
0
0
Watu 27 wanashikiliwa mkoani hapa kwa tuhuma za kuchoma moto kituo kidogo cha Polisi cha Mwandoya katika Wilaya ya Meatu na kuteketeza samani na mali zote zilizokuwa zikitumiwa na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Boniventure Mshongi alisema tukio hilo lilitokea Machi 22 mwaka huu, saa 2:45 usiku.

Kamanda Mshongi alisema wahalifu hao walivamia kituo hicho wakiwa na matofali, mawe na silaha za jadi na kuharibu samani zote na kisha kuchoma moto nyaraka mbalimbali za kituo hicho.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mali nyingine zilizoharibiwa kwa kuchomwa moto na majambazi hayo ni milango sita, meza tatu, viti vitano vya mbao na vingine 16 vya plastiki na kabati la kutunzia mafaili ya kituo.

Vingine vilivyoharibiwa ni mashine ya kupimia kilevi na pikipiki yenye namba DFPA 1171 mali ya polisi.

“Baada ya kutekeleza uhalifu huo, kundi hilo lilikwenda kwenye makazi na vibanda vya biashara vya askari polisi wanaofanya kazi kituoni hapo pamoja na duka la kuuza dawa za binadamu la Magreth Isapi wakafanya uhalifu pia kwa kuchoma moto mali hizo,” alisema

Aliongeza, “Walikwenda pia nyumbani kwa askari ambaye anaishi uraiani kitongoji cha Muungano na walichoma moto nyumba aliyokuwa akiishi na kuunguza vitu vyake vyote pamoja na vyeti vya taaluma ikiwamo vyeti vya sekondari, udereva na walichoma pia cheti cha ndoa na kompyuta ya askari huyo.”

Alisema kuwa watuhumiwa hao walichoma maduka yanayomilikiwa na askari kisha kuiba kompyuta, kamera na vifaa vingine vinavyotumika kusafishia picha.

Kamanda Mshongi alisema kundi hilo pia lilikwenda kwenye duka la dawa la Magreth Isapi na kuvunja mlango na kuiba dawa mbalimbali za binadamu ambazo thamani yake haijajulikana na baadaye kulichoma moto.

‘’Wakati kundi hilo likiendelea na uharibifu kuelekea maeneo mengine, polisi Meatu wakiongozwa na OCD F. Bongole akisaidiwa na Kaimu OC/CID Nassib waliwahi eneo la tukio na kuwadhibiti wahalifu hao, na hadi sasa thamani ya vitu vilivyoharibiwa na kuibiwa bado haijafahamika’’ alisema Kamanda Mshongi.

Ujumbe wa Pasaka toka kwa Maaskofu wa KKKT......Wasikitishwa na matukio ya kupotezwa watu, kubanwa kwa Uhuru wa Mahakama, Bunge na Tume ya Uchaguzi‬

$
0
0
Bwana wetu Yesu Kristo mfufuka, alipowatokea wanafunzi wake wakiwa wamejifungia ndani kwa hofu ya Wayahudi, aliwasalimu na kujifunua kwao kwa salaamu ya kuwatakia amani. 


Wapendwa watu wa Mungu, katika umoja wetu, sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tunawasalimuni nyote kwa kuwatakia amani. Bwana wetu Yesu Kristo Amefufuka kweli kweli - Haleluya!. Yeye ni amani yetu, na pia ni amani kwa watu wote wenye mapenzi mema. Kwa kufufuka kwake, upendo umeishinda chuki; unyenyekevu umeushinda ubabe; nuru imelishinda giza; haki imeshinda udhalimu; msamaha umeshinda visasi; ujasiri umeshinda hofu; na kwa hiyo uzima umeshinda kifo.

Mwaka 2017, Kanisa letu limeadhimisha miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa. Tukiwa wana Matengenezo tumekumbushwa tena kuwa mwanadamu anaokolewa kwa Neema ya Mungu tu: Wokovu Hauuzwi; MwanadamuHauzwiwalakununuliwa;naUumbajihauuzwi. Kanisa zima na dunia kwa ujumla tunaitwa kusimama pamoja na kuueleza ukweli huu unaoziweka huru dhamiri zetu (Yohana 8:31-32).

Matengenezo (Reforms) ni dhana ya kibiblia. Tangu zama za Agano la Kale, Mungu kwa nyakati mbalimbali aliteua wajumbe wake kuwasilisha ujumbe wake kwa jamii na kwa watawala wa dunia. Kwa Umungu wake, aliwainua wanawake na wanaume kwa makusudi ya kutoa unabii yaani, ujumbe wa Mungu kwa jamii au watawala. Wakati mwingine aliinua manabii kuwasemea wasiokuwa na sauti. Unabii na Matengenezo ni njia ya Mungu katika kusimika utawala wa haki na unaostawisha uhuru na amani.

Kwa namna ya pekee, manabii kama Daniel, walionya juu ya uongozi unaojenga uhalali wake katika wingi wa watu wanaokubaliana na uongozi huo hata kama ni katika makosa. Haikuwa rahisi kibinadamu kuukosoa mfumo kama huo lakini Mungu alitumia manabii kuzungumza na mfumo wa namna hiyo. Unabii wa Daniel 3:7 unasema, “KwahiyowatuWOTE,marawaliposikiasauti zabaragumu,filimbi,kinubi,zeze, santuri, zumari, na sauti za ala nyingine zamuziki,waliangukakifudifudinakuiabuduile sanamu ya dhahabu ambayoMfalmeNebkadneza aliisimamisha”. Hapa tunaona kosa la kiongozi kutengeneza sanamu, linasababisha kosa la watu wanaokubali kuiabudu hiyo sanamu. Tumetafakari na kusadiki kuwa, kosa la kiongozi au mfumo, haliwaondolei hatia wanaomfuata kiongozi au kuufuata mfumo, hata kama watu hao walikula kiapo cha kutii maongozi ya kiongozi huyo na mfumo wake. Mbele ya Mungu hakuna ile kanuni ya kuwajibika kwa pamoja. Kila mtu kwa dhamiri yake anawajibika mbele za Mungu. Kwa upande mwingine, pamoja na uwajibikaji wa mtu binafsi, Nabii Ezekieli anatukumbusha na kutuonya kuwa tusipoonya na kusimama katika zamu yetu, hatia na damu ya wasio na hatia, itadaiwa mikononi mwetu (Ezekiel 33: 8-9).

Adhimisho la kufufuka kwa Yesu Kristo (Pasaka) na maadhimisho ya miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa, yanatusukuma kutafakari utume wa Kanisa katika jamii kwa nyakati zetu. Tunaalikwa kupeleka ujumbe wa amani kwa watu wote na kusimama kwa ujasiri katika kuwasemea wasio na sauti katika jamii ili kuenzi roho ya Pasaka na Matengenezo katika nyakati zetu. Kama Kanisa na kwa nafsi zetu mmoja mmoja, tunaitwa kwa upande mmoja, kufundisha, kushauri na kutia moyo. Kwa upande mwingine, tunaitwa kuonya, kukaripia, kukemea na kuelekeza kwa uvumilivu wote na upendo (2Timotheo4: 1-5).

Wajibu huu kwetu sisi maaskofu ni wito na utume usiokwepeka; na kwa watu wote wa imani, wajibu huu hauna mbadala. Tunaagizwa kuchochea ujenzi wa madaraja ya maridhiano katika upendo na amani, na kuwa kinyume na mifumo yote inayoendeleza chuki na marafakano. Kwa kufanya hivyo, imetupasa kusema wazi wazi ujumbe wa amani, upendo, heshima, utu, ustahimilivu na maelewano. Mfumo wowote unaojengwa katika utii wa sheria bila upendo; heshima bila uhuru; na amani bila haki, unajengwa katika msingi usio imara. Kupuuza wito huu kuna madhara kwa jamii yetu. Ni sawa na kujenga nyumba juu ya mchanga (Mathayo 7: 26). Tunasihi kwa machozi mengi, tuwe wajenzi wenye akili wajengao nyumba zao juu ya mwamba (Mathayo 7:24). Mwamba tunaotakiwa kujenga taifa letu lenye dini mbalimbali, vyama mbalimbali, na makabila mbalimbali, umetajwa katika sala kuu ya taifa letu, yaani, "DUMISHAUHURUNA UMOJA". Bila Uhuru hakuna umoja uwezao kuleta maendeleo; na bila umoja wa kitaifa, uhuru wetu hauleti amani endelevu. Kwa sababu ya nguvu ya dhamiri safi iliyo dira ya taifa letu, tunalazimika kumtii Mungu kuliko mwanadamu (Matendo 5:29).

B. TAIFALETUNA AMANI YETU
Tunapoadhimisha sikukuu ya kukumbuka kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, tunatambua kuwa utume wa Kanisa letu katika taifa letu, unafanyika katikati ya changamoto kadhaa. Kwa kuwa Kanisa ni sehemu ya jamii, linaguswa na changamoto hizo. Katika kukaa pamoja na kuliombea taifa letu, sisi maaskofu wa KKKT, tumetafakari na kubaini changamoto hizo. Kwa njia ya salaam za Pasaka, tunaleta kwenu changamoto tatu ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.

1. Jamii na Uchumi
Kiini cha Utume wetu katika jamii kinatuingiza kwa nia njema katika maisha ya uchumi na mshikamano wa kijamii. Neno la Mungu linatufundisha kuwa "Mwanadamuhawezi kuishi kwa mkate peke yake" (Luka 4:4). Pia neno la Mungu linatuhakikishia kuwa Bwana wetu Yesu Kristo alikuja ili tuwenauzimatele (Yohana 10:10). Tunawiwa katika umoja wetu wa ubaba, kuipongeza serikali yetu kwa jitihada inazofanya kuboresha maisha ya wananchi. Tumeshuhudia jitihada na nia njema kuhusu uvunaji na umilikaji wa raslimali za nchi kwa manufaa ya taifa zima. Aidha, tunapongeza jitihada za ukusanyaji wa kodi ili kuiwezesha serikali kugharamia huduma za jamii. Hata hivyo, bila kukatisha tamaa jitihada hizo, tunawiwa kushauri yafuatayo:

I. Sekta binafsi na mashirika ya dini ni wadau wa maendeleo, si washindani wa serikali katika kuchangia maendeleo ya taifa. Mazingira yasiyo rafiki kuhusu wadau hawa, ni kikwazo kisicholeta mshikamano kati ya serikali na sekta binafsi na mashirika ya dini katika kuleta maendeleo. Jitihada za makusudi na za mara kwa mara zifanyike kuondoa dhana ya ushindani kati ya serikali na wadau hawa ili kuimarisha mahusiano mema kati ya serikali na sekta binafsi.

II. Ili mfumo wa ukusanyaji wa kodi uwe endelevu; jitihada za kukusanya kodi ziendane na elimu kwa mlipa kodi. Msisitizo wa uzalendo wa kulipa kodi uende sambamba na ustawi wa walipa kodi katika shughuli zao za biashara. Mivutano isiyo na tija kati ya walipa kodi (wafanya biashara) na mamlaka ya ukusanyaji wa kodi, inastawisha uadui unaopunguza makusanyo ya kodi na kujenga ushawishi wa rushwa. Mfumo wa kodi unaowafilisi wafanya biashara, haulengi kujenga uchumi wa viwanda.

III. Kutokana na ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira; jitihada za wazi na za makusudi zifanyike ili msukumo wa uchumi wa viwanda ufikie matumaini yanayoshikika miongoni mwa vijana wasio na ajira. Sekta binafsi, wawekezaji na wadau wengine, wahakikishiwe usalama wa mitaji yao kisheria. Hili likifanyika ni kichocheo kizuri cha ujenzi wa viwanda.

IV. Uchumi wa viwanda (vidogo na vikubwa) uendane na uwekezaji katika sekta ya kilimo maeneo ya vijijini. Kilimo na ufugaji ndizo sekta zenye wigo mpana wa viwanda vinavyogusa maisha ya watanzania walio wengi. Utozaji holela wa kodi na ushuru wa mazao unakatisha tamaa wadau wa kilimo. Migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa upande mmoja, na wakulima/wafugaji na wawekezaji kwa upande wa pili, si kivutio cha uwekezaji katika sekta ya kilimo.

2. MaishayaSiasa
Kwa umoja wetu katika utume, tunatambua siasa safi na uongozi bora kuwa ni misingi iliyoongoza maisha ya siasa katika taifa letu. Ujio wa vyama vingi mnamo 1992, haukuondoa umuhimu wa misingi hii bali ulipanua matumizi ya demokrasia iliyojengwa katika uhuru wa mawazo. Taifa ni mkusanyiko wa taasisi na watu mbalimbali, wenye lengo moja lakini kwa njia mbalimbali. Kutokana na wingi huu, taifa letu daima ni juu ya vyama, taasisi na makundi.

Taifa huongozwa na katiba iliyo kiini cha sheria zote. Taifa haliongozwi na ilani za vyama. Serikali haiongozwi na ilani za vyama. Serikali huongozwa na katiba, sheria, kanuni na mapokeo mema (misingi na tunu za taifa). Serikali husimamiwa na bunge huru lililo sauti ya wananchi. Wananchi ndilo chimbuko la madaraka ya bunge. Bunge halisimamiwi na ilani, chama chochote wala mtu awaye yote. Kwa umoja wetu na kwa nyakati zetu, hivi sasa tunashuhudia matukio yaliyo kinyume na tunu na misingi iliyolilea taifa letu. Baadhi ya matukio hayo ni:

I. Hofu iliyojengwa katika matukio halisi yakiwamo utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.

II. Kupungua na hatimaye kutoweka kwa uhuru wa kujieleza, kukusanyika, na kupata habari. Kwa mwenendo huu, kuna hofu kuwa hata uhuru wa kuabudu uko mashakani.

III. Kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi. Hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.

IV. Kukosekana kwa mazingira ya haki na uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi zote zimeghubikwa na ubabe, vurugu, hila, na vitisho.

V. Utekelezaji wa mipango ya maendeleo wenye mwelekeo wa kiitikadi. Hatua hii imeimarisha ubaguzi wa kiitikadi katika taifa letu na kukuza migawanyiko.

VI. Kushamiri kwa chuki mioyoni mwa watu ambalo ni chimbuko la visasi, kukata tamaa, na ushiriki mdogo wa wananchi katika chaguzi na maisha ya siasa.

VII. Udhalilishaji wa kauli njema isemayo "Maendeleohayanachama". Udhalilishaji huu unafanyika kwa njia ya kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo zinazotokana na watu wanaobadili vyama ili kuleta maendeleo. Tunajiuliza, kama maendeleo hayana chama, kwa nini mtu anajiuzuru chama fulani, eti kwenda kuleta maendeleo katika chama kingine? Mchezo huu unagharimu fedha nyingi na maisha ya watu wanaokufa, kujeruhiwa na uharibifu wa mali.

Mambo haya ni tishio linalohatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

3. MasualaMtambuka
Kanisa ni alama ya uwepo wa utume wa kuleta na kutunza matumaini katika jamii. Ukimya wa Kanisa katika masuala yanayoigusa jamii ni ukwepaji wa wajibu wake. Lakini pia sauti ya Kanisa isiyomilikiwa na mtu isipokuwa Mungu tu, ni chachu ya amani na matumaini. Kwa dhamiri safi inayotokana na utambuzi wa "Wakatiwa Mungu"(Kairos) katika taifa letu, tunawiwa kutambua masuala mtambuka yanayogusa maisha ya watu kipekee na kwa njia nyingi na kuyatolea ushauri ufuatao:

I. Kuhitimisha mabadiliko ya mara kwa mara katika mfumo wa elimu nchini ili kuondoa mwanya wa kila mtendaji mkuu wa wizara kuja na sera yake. Elimu ni kitovu cha ustawi wa taifa, kisiwe kinachokonolewa chokonolewa kila wakati. Sekta zote nchini hujenga mafanikio yake katika mafanikio ya mfumo thabiti wa elimu.

II. Uwezeshaji wa vijana kupata mikopo ya elimu ya juu uwe shirikishi na usiokuwa na "ubaguzi" kati ya wanafunzi wa vyuo binafsi na wale wa serikali; sayansi na sanaa; wazazi maskini na wenye nafasi; waliosoma shule binafsi na wale wa shule za serikali, n.k. Kwa kuwa huu ni mkopo, jitihada ziwekwe zaidi katika urejeshaji wa mkopo huo kwa kuzingatia kuwa huu ni mkopo kwa mtoto siyo kwa mzazi.

III. Vyombo vya usimamizi wa sheria na utoaji haki vionekane vinatenda haki sawa kwa watu wote na makundi yote bila kuacha ishara za fadhila au kukomoana.

IV. Wajibu wa serikali kikatiba katika kulinda uhai wa raia wake, uonekane unatekelezwa bila kuacha mwanya wa kuituhumu serikali. Ukiachwa mwanya katika ulinzi wa uhai wa raia, waweza kutumiwa na mamluki kujichukulia sheria mkononi kwa niaba ya serikali. Damu isiyo na hatia

ina madhara kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo. Mpaka sasa tumeshuhudia umwagaji wa damu unaotusuta sisi sote na mamlaka zote. Mungu anatusuta watanzania kama alivyomsuta Kaini: "Sautiyadamuyanduguyakoinanililiakutokakatikaardhi" (Mwanzo 4:10).

V. Uhai wa mtu una thamani isiyopimika. Ni wajibu usiokwepeka kuulinda na kuutunza uhai kwa vitendo halisi. Endapo uhai umepotea katika mazingira yoyote, uchunguzi huru na wa haki ufanyike na taarifa zitolewe kwa wakati muafaka ili kujenga jamii yenye imani kwa serikali na vyombo vyake. Matukio ya mauaji ya askari wetu, mauaji ya raia, majaribio ya kuwaua wanasiasa, utekaji, na uteswaji visipochunguzwa na kutolewa taarifa, ni shina la hofu na uchungu katika jamii. Jamii iliyojaa hofu na uchungu, haiwezi kuwa na maendeleo wala kuwa na roho ya uzalendo.

VI. Ili kulipatia taifa letu ufumbuzi wa mambo yote tuliyotaja na kushauri kwa wakati huu na ujao; tunaisihi serikali ya awamu ya tano, kurejea mchakato wa upatikanaji wa KATIBA MPYA ya wananchi, iliyopendekezwa na wananchi kupitia Tume ya Warioba. Watanzania wengi wanaona na kuamini kuwa KATIBA MPYA ina majibu ya kukidhi mahitaji ya taifa letu kwa sasa na baadaye. KATIBA MPYA ni zao la utashi wa Watanzania kupitia tume ya Warioba iliyokuwa na uwakilishi mpana wa taifa letu.

VII. Aidha, tunawashauri raia wema, kwa njia za kidemokrasia kupitia majukwaa ya kikatiba yaliyo katika maeneo yao, kudai upatikanaji wa KATIBA MPYA. Itapendeza ikiwa KATIBA MPYA itapatikana kabla ya uchaguzi mkuu ujao. Mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano yatadumu iwapo kuna KATIBA MPYA inayolinda mazuri. Kiongozi mzalendo si mbadala wa KATIBA MPYA. Tanzania yenye amani na maendeleo ni tunda la itikadi zote, dini zote, makabila yote na makundi yote chini ya KATIBA MPYA.

C. HITIMISHO
Kufufuka kwa Yesu Kristo ni kiini cha Matengenezo ya Kanisa. Kwamba, katikati ya jamii iliyokata tamaa na kutawaliwa na hofu, Kristo alifufuka na kuleta matumaini mapya. Kwamba, katikati ya wasiwasi wa Kanisa kupoteza nguvu ya utume wake, Roho Mtakatifu aliongoza Matengenezo ya Kanisa. Kwa hiyo Matengenezo ni endelevu katika jamii ya watu na taasisi zao. Muasisi wa Matengenezo Dr. Martin Luther yungali analiwajibisha Kanisa kuzingatia utume wake unaoleta matumaini mapya kila siku. Waliobatizwa wote ni wamisionari tunaotumwa na Bwana wetu Yesu Kristo (Yohana 20:21). Imetupasa kuwa nuru na chumvi ya jamii na kuwa mawakala wa uhuru, umoja na amani.

Taifa letu lilipata uhuru mwaka 1961 bila kumwaga damu. Roho ile ile ya majadiliano na maridhiano iliyokuwamo ndani ya waasisi wa taifa letu, inatakiwa kila wakati. Uhuru ulioletwa kwa majadiliano, utunzwe na kulindwa bila ulazima wa kumwaga damu ya watanzania. Uhuru na Umoja ndizo ngao zetu zilizolitunza taifa kwa zaidi ya miaka 50.

Sisi tulio maaskofu kwa neema ya Mungu, tunaleta wito kwenu wenye imani katika dini mbalimbali, kuliombea taifa letu. Kuwaombea wote wenye madaraka ili wajaliwe hekima, busara na upendo kwa taifa na watu wake. Kupitia jumuia ndogo ndogo na sharika zote, waombee viongozi wetu ili Mungu awajalie na kuwatunuku kiu ya kutenda haki, kusikiliza kuliko kusema, kuelekeza kuliko kuamrisha, kuunganisha kuliko kutawanya, kupenda watu kuliko kutamani kupendwa na watu, kutamani kutumika kuliko kutumikiwa (Marko 10:45), kuheshimu kuliko kuheshimiwa.

Ujumbe wa Pasaka unatuhimiza kuthamini uhai. Bwana wetu Yesu Kristo alikubali kufa ili kuhifadhi uhai wetu. Kwa kufa kwake na kufufuka, amekomesha kifo na mawakala wake. Tunaitwa kuthamini uhai na kutoruhusu tena watu kuteswa na kuuawa. Kwa hekima yote na unyenyekevu, tunasihi tena, kwamba ikubalike kuwa hitaji la watanzania walio wengi kwa sasa ni KATIBA MPYA. Katiba Mpya ipatikane ili kukuza na kuimarisha mfumo wa utawala utakaolinda uhai wa watu, raslimali za nchi, tunu za taifa, uhuru wa mihimili ya dola, na uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.

TunawatakiaPasakanjemayamwaka2018,naMunguawabarikininyote. 

Serikali yakanusha kufungia mitandao ya kijamii

$
0
0
Kumekuwa na uvumi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii kutoka kitengo cha Rais, Ikulu idara ya Mawasiliano ikidai kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imearifu wananchi wake kufungia mitandao ya kijamii nchini endapo itatumika vibaya.

Kufuatia habari hiyo ambayo hata hivyo inaonesha ni ya mwaka 2017,  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa mapema leo hii ameikanusha barua hiyo na kudai kuwa haijachapishwa na idara yake.

Msigwa amewasihi Watanzania kuipuuza habari hiyo kwani ni uvumi ambao hauna ukweli wowote, kwani Serikali haijatoa wala kuzungumzia swala hilo.

Diva: Natongozwa zaidi ya Mara 2000 kwa Meseji, Nalazimika Kubadili Laini hata Mara 7 kwa Mwezi

$
0
0
Mtangazaji maarufu wa kituo cha Clouds FM, Diva The Bawse amedai kuwa baada ya kumwagana na aliyekuwa Boyfriend wake Heri Muziki amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa wanaume hadi inakuwa kero.

Akifunguka kwenye mahojiano yake na Bongo5, Diva amesema kupitia simu yake ya mkononi amekuwa akipata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume wengi wakimtongoza, kitu ambacho kila mwezi kinamfanya abadilishe laini zake mara saba.

Maisha ya kuwa single ni mazuri ingawaje nimekuwa nikipata usumbufu mkubwa kwenye simu yangu yaani napata meseji zaidi ya 2,000 na zote kutoka kwa wanaume, kitu ambacho kinanipa wakati mgumu kwani wananifanya nibadili laini mara saba kwa mwezi,“amesema Diva.

Mbali na usumbufu huo, Diva amesema kuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram pia amekuwa akikumbana na usumbufu kama huo DM.

Kwa sasa mrembo huyo amesema kuwa ameshapata mwanaume ambaye ndiye anaamini kuwa atakuwa baba watoto wake siku za usoni ingawaje amekataa kumuweka wazi kwa sasa.

Kwa upande mwingine Diva ametangaza kuachia albamu yake mwaka huu ya ‘ALA ZA ROHO’ ambayo itakuwa na mastaa kibao kutoka nje ya nchi.

Mwigulu Nchemba Ataka VIBOKO Vitumike Shuleni Ili Kuwajengea Maadili Wanafunzi

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya ndani, Dk  Mwigulu Nchemba amewataka walimu kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi kwa kuwafundisha maadili mema na inapobidi matumizi ya fimbo yatumike.

Akizungumza katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari  Lulumba Wilaya ya Iramba mkoani Singida, jana, Dk Nchemba alisema walimu wanatumia fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi ili kutengeneza hatma ya nchi.

“Kuna wakati walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi lakini ninyi hamuoni hii na kulalamika tu, kinachofanyika ni kwa manufaa yetu…niwaombe kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni hivyo ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk Mwigulu.

Alisisitiza kuwa ni lazima kuendelea kulinda hadhi za walimu kwa kuwapatia miundombinu bora ya ofisi na vyumba vya madarasa.

Alisema majengo ya taasisi yanapaswa kuwa bora zaidi na sio kutumia ramani za awali pekee kwani zinapaswa kuboreshwa kulingana na maendeleo yaliyopo.

“Naunga mkono ujenzi huu wa mabweni ya wanafunzi, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu hivyo nachangia mifuko 200 ya saruji nawaahidi pia kutoa Sh milioni sita,” alieleza.

Mkuu wa Wilaya Iramba, Emmanuel Luhaula alisema shule higo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kutokana na umahiri wa walimu kwani watoto hao wanajua kujieleza kama vile wanasoma chuo kikuu.

Alisema wananchi wa Iramba wanatakiwa kujivunia  kuwa na shule zao pamoja na walimu hao ili kuboresha elimu wilayani humo.
 
“Unafanya jitihada ili kuhakikisha kila sekondari kunajengwa mabweni ili kuondoa kero za wanafunzi.Sisi wa Iramba tushindwe wenyewe kukutumia. Nimekuwa Mbunge lakini anayoyafanya mbunge huyu Mimi sikuyafanya,” alisema Luhaula.

Naye, Mkuu wa shule hiyo, Jeremiah Kitiku alisema licha ya kufanya vizuri kitaaluma, wanakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa baadhi ya majengo, upungufu vitabu vya masomo ya kiada 274.
 
“Mahitaji ya vitabu vya kiada no 2,802 vilivyopo 2,328 upungufu ni 274. Pia tunachangamoto ya kutokuwa na uzio kwa usalama wa wanafunzi, walimu na mali za shule,” alisema Kitiku
 
Hata hivyo, alisema malengo ya shule hiyo ni ukarabati wa vyumba tisa vya madarasa na  ofisi za nane za walimu ambazo zitagharimu Sh Milioni 169.4.
 
Katika harambee hiyo, saruji iliyokusanywa ni mifuko 209, ahadi  ya fedha ni 8,486,000, ahadi ya mifuko ya saruji 572, Gypsum 50 na  nondo tani moja jumla ya ahadi na fedha taslimu ni 19,494,300

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE; 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO 0754372325/ 0689013109/ 0620806813 

HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Kutana na Mtaalamu wa Kusafisha Nyota, Mvuto wa Biashara na Mapenzi

$
0
0
Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH issa simba said Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
 
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Issa simba said Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
 
Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi zaidi 

+255 622588038au 0679119679 au +255 764318107
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images