Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Queen Darlen Amkana Alikiba Kweupe

0
0
Mwanadada Queen Darlen ameamua kufunguka na kusema kuwa hana ukaribu wowote na Alikiba zaidi ya kwamba walikuwa wakifanya kazi pamoja na hiyo yote ilikuwa ni kwa sababu walikuwa chini ya uongozi unaofanana.

Queen Darleen amesema huwa anapoulizwa na media kuhusu Alikiba hapendi kumzungumzia kwa madai kuna watu watatafsiri tofauti.

Wasanii hao ambao mwanzoni watu walidhani ni ndugu walishafanya wimbo pamoja na Queen Darleen amesema ni kwasababu kipindi hicho yeye na Alikiba wote walikuwa chini ya label moja. Queen Darleen amesema Hana ukaribu wowote na Alikiba tangu zamani ilikuwa ni kazi tu

Pia akizungumza na GPL Queen Darleen amesema wakati anaanza muziki takribani miaka 15 iliyopita hakupata usumbufu wa rushwa ya ngono toka kwa wanaume walio kwenye tasnia Kama baadhi ya wasanii wa kike kwasababu yeye alishikwa mkono na Dully Skyse kwa hiyo akizinguliwa tu kwa mambo ya kijinga alikuwa akimwambia Dully .

Emmanuel Mbasha Akanusha Tetesi za Kutoka Kimapenzi na Agness Mmassy

0
0
Msanii wa nyimbo za injili Emmanuel Mbasha amefunguka na kuamua kuweka wazi mahusiano yake na mwanamitindo maarufu nchini agnes mmasy na kusema kuwa watu wamekuwa wakizusha kuhusu yeye kutoka kimapenzi na mwanadada huyo lakini taarifa hizo sio za kweli.

Katika Ukurasa wake wa instagram , Mbasha aliandika “Nakanusha yote ni uongo, sia mahusiano na huyu dada kabisa na wanaoendelea kuzusha  na kueneza huu uongo basi na mungu wangu atawalipa.sio kweli.”

Kumekuwa na tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano kati ya mwimbaji huyo na mwanadada huyo ambaye ni mwanamitindo ambaye amekuwa akipiga picha za uchi mara nyingi na kuziweka katika mitandao ya kijamii

Hata hivyo kwa rekodi ya hivi karibuni, Emmanuel Mbasha alikiri kutokuwa na mwanamke tangu alipoachana na mke wake Florah na kusema kuwa kwa sasa  amejikita zaidi katika swala la uokovu na kwamba kuwa na mahusiano kabla ya ndoa ni kuzini na asingependa kufanya kitu hicho.

Naibu Spika Tulia Ackson afunguka Mazito kuhusu Mange Kimambi....Msikilize Hapa

0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefunguka na kusema kuwa yeye hana uhakika kama mwanadada mwanaharakati wa mitandaoni Mange Kimambi kama ni binadamu wa kawaida kama yeye.

Tulia Ackson amesema hayo alipohojiwa na moja ya chombo cha habari na kusema kuwa kwa sasa hawezi kusema kama mwanadada huyo anakosea au laa kwa kuwa hana uhakika kama yupo kama yeye na kusema labda akipata fursa ya kuonana naye na kuona kweli yupo kama yeye ndiye anaweza kuwa na la kusema.

"Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua chakuzungumza naye lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata fursa ya kumshauri nikionana naye.

"Siwezi kusema anakosea kama nilivyosema sijajua yeye ni mtu wa namna gani kwa hiyo huenda hakosei labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti hivyo kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea" alisema Tulia Ackson 

==>Msikilize Hapo

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Casto: Tunda Kutembea na Diamond Sio Tatizo, Nipo Tayari Kumuoa....Tazama Picha Hapa Wakila Bata

0
0
Mtangazaji wa Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na Tunda Sebastian na kudai kuwa yupo tayari kumuoa na hajali kama ameshawahi kuchukuliwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Siku za hivi karibuni uhusiano wa Tunda na Casto umetengeneza sana headlines Kwenye social media hasa kwa sababu Tunda alikuwa na urafiki na Muna ambaye ni mzazi mwenzake na Casto  kwaiyo yeye kutembea na mwanaume wa rafiki yake ni kama unafki.

Mwezi uliopita ilisemekana kuwa Tunda ni mjamzito na Baba alitajwa kuwa ni Diamond lakini Casto amesema habari hizo sio za kweli kwani Tunda ana Kitambi  kwa sababu anapenda kula ingawa anafanya mazoezi.

Casto amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Lemutuz Tv ambapo amekiri kuwa anampenda Tunda na yuko tayari kumuoa:

"Kuhusu Tunda kuwa na Diamond mimi hainisumbui wala hainihusu as long as tangu nimeenda kuwa naye I think kama mwezi na zaidi sasa tupo wenyewe na tunapendana na umri unaenda na maisha yanabadilika hivyo sidhani kama nina kosa kuweka wazi kuwa Nampenda Tunda na nina mpango wa kumuoa”.

Casto pia ameweka wazi kuwa hakuna bifu lolote kati ya Tunda na Muna maana yeye na Muna waliachana muda mrefu uliopita na hivi sasa wanalea tu mtoto wao pamoja kwahiyo hakuna sababu ya Muna kuwa na wivu baada ya kumuona yeye na Tunda wako pamoja.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 23

TIRA yazifutia leseni kampuni nne za udalali na ushauri

0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) imefuta leseni za kampuni za udalali na ushauri wa Bima kutokana na kukiuka taratibu za uendeshaji wa biashara za bima.

Akizungumza na wanahabari jana  jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Bima wa TIRA, Dkt. Baghayo Saqware amesema kampuni hizo zimekuwa zikichafua taswira ya biashara ya bima pamoja na kutishia soko la bima nchini.

“Makampuni haya yameshindwa kuwasilisha tozo za bima kwa makampuni ya bima, hivyo kuwanyima wateja wa bima haki ya kunufaika na fidia ambazo zingetolewa na makampuni endapo fedha hizi zingewasilishwa,” amesema.

Dkt. Saqware amezitaja kampuni hizo ikiwemo Kampuni ya Udalali wa Bima ya Hans, Kampuni ya Endeavour, Leegend of East Africa na Kampuni ya Swift.

Amesema TIRA inaendelea kushirikiana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili kuzichukulia hatua za kisheria baadhi ya kampuni zisizowasilisha ada za bima kwa kampuni za bima husika baada ya kupokea kutoka kwa wateja pamoja na kukwepa ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na mamlaka hiyo.

Amezitaja kampuni hizo kuwa ni, Kampuni ya Udalali wa Bima ya Pacific na Kampuni ya Core.

Mwalimu Akamatwa na Polisi kwa kumkashfu Rais Magufuli

0
0
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu serikali na kumkashfu Rais Magufuli  kuwa ni Dikteta na anaminya demokrasia.

Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiwe

Meya Aagiza Halmashauri Ziajiri Watu wa Kuzika Wafu Waliokosa Ndugu Dar

0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote jijini hapa kuajiri watumishi ambao watakuwa wanafanya kazi ya kuzika miili ya watu ambao watabainika kuwa hawana ndugu.

Meya Mwita ametoa kauli hiyo jijini hapa, Machi 21, 2018 kwenye kikao cha robo ya pili ya Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaeleza madiwani hao kuwa jukumu la kuzika marehemu wasiokuwa ndugu ni la jiji, kwakushirikiana na halmashauri hivyo wanapaswa kuwajibika katika hilo.

Amefafanua kuwa hadi sasa jiji limeshanunua gari pamoja na mahitaji mengine ya kuhifadhia miili hiyo pindi inatokea na kwamba changamoto iliyopo ni watu ambao watashirikiana kutekeleza jukumu hilo.

“ Mtakuabliana na mimi kwamba tulishakubaliana kwamba jambo hili lifanyike kwenye halmashauri zetu, lakini hadi sasa Kinondoni pekee ndio wametimiza agizo hili, sasa ninaagiza tena halmashauri nyingine za jiji hili kuajiri watu hao” amesema Meya Mwita.

Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini hapo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza makubaliano hayo.

“Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzikwa na jiji, natulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda,” amesema.

Amefafanua kuwa watu wasiokuwa na ndugu wanapokufa, wanapokaa hospitalini zaidi ya siku 20,jiji linalazimika kuwazika hivyo wapo ambao wanazikwa kwenye halmashauri mbalimbali.

Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu wake katika kuzika marehu hao kila halmashauri linajukumu la kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.

Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ya kuzika miili ya watu ambao wamefariki na hawana ndugu.

“Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka,” amesema Meya Mwita.

Malawi Kuanza Kuleta wangojwa Wao Muhimbili Badala ya Kuwapeleka India

0
0
Katibu Mkuu  Wizara ya Afya ya Malawi Dkt. Charles Mwansambo  ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ili kupata uzoefu wa namna Taasisi hiyo inavyotoa huduma za kibobezi (super specialist).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo jana Jijini Dar es Salaam Dkt. Mwansambo alisema ametembelea MOI ili kuona uwezekano wa kuwaleta wagonjwa wa Malawi kupata huduma za Kibingwa za Mifupa, Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu badala yakuwapeleka India.

” Nimefurahi kuona kuwa tuna huduma nzuri za kibingwa kwa jirani zetu wa Tanzania, hili ni jambo jema na litatupunguzia gharama za kuwapeleka wagonjwa India badala yake tunawaleta hapa MOI” alisema Dkt.Mwansambo.

Aidha, Dkt. Mwansambo alipata fursa ya kutembelea vyumba vya upasuaji vya MOI, vyumba vya wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU), wodi za watoto na wodi maalum za kisasa za kulipia.

Kutokana na mafanikio ya miundo mbinu ya kisasa yaliyopo MOI Dkt. Mwansambo ameonyesha dhamira ya dhati ya kuleta madaktari wanafunzi hapa  ili wapate ujuzi wa zaidi.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI  Mhandisi .Reginald Kimambo alimueleza Dkt. Mwansambo kwamba huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo zimebobea katika  Mifupa, Ajali, Upasuaji wa ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu pamoja na kutua mafunzo kwa madaktari bingwa wa COSESCA.

Ziara hii imekuja baada ya mkutano wa 65 wa Mawaziri wa  Afya wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Kati na Kusini uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi

0
0
Viongozi wanne wa Chadema wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk  vicenti Mashinji.

Viongozi hao ambao  wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.

 Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe.

Awali Mbowe  ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.

Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya  kumuunganisha  Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.

Ebitoke Akanusha Kumroga Ben Pol

0
0
Msanii wa filamu na mchekeshaji hapa bongo Ebitoke, ameweka wazi juu ya kufufuka kwa penzi lake na Ben Pol ambaye hapo awali alidai hapokei hata simu zake, na hivi karibuni kuanza kuwa pamoja tena.

Ebitoke amesema kwamba kitendo cha yeye kuonekana na Ben Pol kwenye kazi zake za comedy ni kwamba alishamuahidi kuwa atamsaidia kwenye kazi zake, na si ndumba kama baadhi ya watu wanavyodai, kutokana kwamba penzi lao lilishakufa.

“Sijamroga Ben Pol, hata hivyo kipindi cha kati kati ambacho mahusiano yetu hayakuwa sawa, sio kwamba hayakuwa sawa ni kwamba alinituliza nisiongee sana kwenye mitandao baada ya ile kusema hapokei simu zangu na kuwa niweze ku-manage mahusiano, tulikaa kama mwezi mzima tulikuwa hatuongelei chochote, lakini aliniahidi kuwa atanisaidia kazi ndo hivyo tunasaidiana”, amesema Ebitoke.

Wawili hao bado kuna sintofahamu kama ni kweli wapenzi, kwani mara nyingi Ben Pol amekuwa sio mtu wa kufurahia suala la mahusiano yake na Ebitoke kuwa wazi.

Makonda Awaita Ofisini Kwake Wanawake Waliotelekezwa Na Waume Zao

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  amewataka wanawake wote waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto wafike ofisini  Jumatatu ya  Aprili 9 kwa lengo la  kupatiwa msaada wa kisheria.

Taarifa ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

"Huduma hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali yako itasimama na wewe hadi upate haki yako," amesema Makonda.

Lady Jay Dee asema kulia sasa basi....Atambulisha Wimbo Mpya wa ANAWEZA

0
0
Msanii  wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura, maarufu "Lady Jay Dee" ameendelea kuonyesha ukongwe wake katika sanaa hiyo baada ya jana kutambulisha kibao chake kipya kiitwacho Anaweza.

Lady Jay Dee au Komando ameutambulisha wimbo huo sambamba na kutoa video ili kuwavuta karibu mashabiki wake ambao wanafahamu kiwango chake.

Lady Jay Dee, alisema kuwa kibao hicho kitengenezwa na mtayarishaji Spicy Judoka wa Nigeria huku video ikisimamiwa na Justin Compus Lutona wa Afrika ya Kusini na lengo la kuchanganya wataalamu hao ni kuhakikisha kazi yake inakuwa na hadhi ya kimataifa.

Alisema kuwa baada ya kukamilisha kazi hiyo, anajiandaa kufanya onyesho la muziki na tayari ameanza maandalizi kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wake.

Aliwataja wasanii wengine ambao wanamuunga mkono kuwa ni Rutta Bushoke, Nikki Mbishi na Judoka anayeimba muziki wa Hip Hop na kueleza kuwa nyota wengine atawatangaza hapo baadaye.

“'Nimemiss' jukwaa, nimemiss watu wangu, nimemiss ile kazi ya kusimama masaa kadhaa na kuwasiliana na watu wanaounga mkono muziki wangu kwa miaka nenda, rudi.

Nimeamua sasa kuwa nitafanya haya matamasha mara kwa mara ili mwisho wa siku muziki wangu uendelee kuishi miongoni mwa mashabiki wangu kwa sababu tukisema ukweli ndio kitu ninachokipenda, muziki”, alisema Lady Jay Dee ambaye ana albamu saba.

Sakata la Korosho ya Tanzania Kukutwa na KOKOTO Vietnam Kusomba Wengi.....Waziri Tizeba Atoa Maagizo Mazito kwa IGP

0
0
Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba, ameagiza kuwasilishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) orodha ya watu wote waliohusika katika sakata la korosho za Tanzania zilizokutwa na kokoto nchini Vietnam ili wakamatwe na kuhojiwa.

Hata hivyo, amesema taarifa zinasema jambo hilo si la kwanza kufanyika nchini. Dk. Tizeba alitoa agizo jana baada ya kuwasilishwa taarifa ya uchunguzi korosho hizo iliyotolewa na kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Dk. Tizeba alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mathew Mtigumwe, kuwasilisha orodha hiyo kwa IGP ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

“Waende sasa wakahojiwe rasmi na vyombo vya dola, naomba hili lifanyike leo (jana) ili wahojiwe kwamba wewe fulani ulikuwa mahali fulani wajibu wako ulikuwa huu hukufanya hivyo, na kama wakibainika wana kesi ya kujibu sheria ichukue mkondo wake,” aliagiza Tizeba.

Alisema katika ripoti hiyo kuna majina ya watu waliohusika katika kusimamia shughuli yote ya usafirishaji wa korosho kuanzia iliponunuliwa, makampuni ya usafirishaji, waliofanya ubadilishaji kwenye shirika la meli nchini (Nassaco).

“Majina yao yamo na Ofisa wa Serikali wa Mamlaka ya Mapato (TRA) aliyetakiwa aweke ‘seal’ kwenye hizo kontena kwa wakati baada ya kuwekwa kwenye magunia ili kujiridhisha kwamba alichokishuhudia kinawekwa kwenye kasha hakitabadilishwa na kuweka lakiri ya serikali kwamba humo ndani kuna mzigo uko ndani ya udhibiti wa forodha, huyu naye anafahamika kwa jina,” alisema.

Alisema kwanini baada ya kufungwa makontena hayo yalibaki kwa siku tano hadi sita yawezekana hakukuwa na meli ya kusafirisha, lakini yale ya kusafiri yanakwenda yanapata nafasi kampuni ya kimataifa ya kuhudumia Shehena za makontena Bandarini (TICTS) ambapo makontena ambayo yamefika huwa yanatoka kupisha yanayosafirishwa.

“Tutajua huyu naye ni nani ambaye pia yumo humu ambaye alitakiwa kuyatoa Nassaco kuyapeleka Ticts na TPA (Mamlaka ya Bandari), tutataka tujue hayo mambo nyie haikuwa kazi yenu kuchukua hatua, kazi yenu ilikuwa ni kukusanya taarifa,” alisema Tizeba.

Alisema ubalozi wa Vietnam ulifikisha serikalini malalamiko rasmi kuhusu mawe yaliyopatikana kwenye viroba vya korosho nchini humo.

“Mimi binafsi niliongea naye na akanionyesha kwa namna mbalimbali jinsi wafanyabiashara wa Vietnam walivyokuwa wamepokea korosho zilizochanganyika na vitu mbalimbali ikiwamo mawe,” alisema Tizeba.

Alieleza kuwa taarifa ya Balozi ilionyesha korosho imenunuliwa mkoani Lindi, lakini akitazama mawe yaliyokuwamo sio ya Nachingwea au Liwale kunakopatikana mwambao wa pwani.

Alibainisha pia jambo jingine ambalo limeendelea kujitokeza ni kuwapo kwa mchanga kwenye magunia ya korosho na siku nne zilizopita imegundulika kontena moja lilikuwa limechanganywa na mawe katika Bandari ya Dar es Salaam.

Dk. Tizeba alisema mtu amenunua tani 20 za Korosho zinaondolewa tani 3 au 1.5 badala yake yanaingizwa mawe au mchanga na michikichi.

Alisema atampatia ripoti hiyo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ili aweze kuona mambo yanayohusu wizara anayosimamia na kama kuna uwezekano wa kuboresha ufanyike.

“Pia taasisi zingine za serikali zinazohusika na masuala haya ambapo kuna maghala yanayosimamiwa na Wizara ya viwanda na biashara nitampa hii ripoti Charles Mwijage,” alisema.

Alisema kwa upande wa serikali wanaendelea na jitihada kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na kwamba leo au kesho watakutana na wabunge kutoka Vietnam.

“Tutakutana nao tuzungumze hili suala la korosho tuliweke vizuri, tumekutana na Balozi ambaye kasema wabunge hao wapo nchini na wangependa na wao kusikia.Tulikuwa tunasubiri ripoti yenu ilituwape picha kamili" Alisema

Kilichomo ndani ya Ripoti
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, yenye wajumbe tisa Khasim Mbofu, alisema makontena yaliyokutwa na kokoto hizo ni kutoka Tanzania na pia limekutwa kontena bandarini lenye mchanga badala ya korosho likisafirishwa kupelekwa nchini humo.

Alisema kamati ilipata uhakika kuwa makontena hayo yalitokea Newala mkoani Mtwara na viashiria vikubwa vinaonyesha zilitoka Tanzania.

“Uthibitisho ni namba ya kontena ambazo zilikutwa kule zipo katika kumbukumbu ya bandari ya Dar es Salaam na bandari ya Nassaco, pia walibaini si jambo geni kutokea nchini na kwamba vyama vya ushirika vya msingi vya Pangateni, Mnyawi na Nguvumoja na Mkiu navyo vimeshawahi kukutwa na tatizo hilo,” alisema.

Alieleza wakiwa bandarini walipata habari kuwa kuna kontena ambalo lilidhaniwa kuwa lina korosho zinazopelekwa Vietnam limebainika kuwa lina maboksi ya mchanga.

“Tumeenda kuona kontena lilosadikika kuwa liliwekwa korosho zilizobanguliwa kwenda nchini Vietnam badala yake yamejaa mchanga na hili lilibainika katika scanner,” alisema.

Alisema walibaini baada ya korosho zilizokutwa na kokoto kuhamishwa kutoka katika malori na kwenda katika makontena ilichukua siku nne kufunga lakiri.

“Eneo jingine la viashiria vya mchezo huu ni kwamba ulichezwa nchini kwa kuwa kontena hizi ilichukua siku 10 kutolewa bandari kavu ya Nassaco kwenda TICTS,” alisema.

Kadhalika, alisema wamebaini kuna mianya kati ya ghala kuu na bandarini na hakuna ulinzi wa kudhibiti.

“Tumetembelea mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi, maghala na viwanda vya kubangua korosho na kufanya mahojiano na watu mbalimbali ukiwamo ubalozi wa Vietnam,” alisema.

Mapendekezo
Makamu huyo alisema vyombo vya uchunguzi vifanye uchunguzi wa kina kuhusu bandari ya Nassaco ambako ndiko korosho hizo zilitolewa katika malori na kuwekwa katika makontena kubaini uhalisia wake.

Pamoja na hayo, alishauri Serikali ifunge scanner yenye nguvu itakayoweza kubaini kilichomo ndani ya magunia ikiwa ndani ya kontena na pia walibaini kuwepo kwa uhaba wa vitendea kazi katika bandari kavu ya Nassaco kutokana na kuwapo kwa malori mawili badala 12.

Alisema kamati ilishauri kupitiwa upya kwa sheria ya korosho na kanuni zake zipewe upya ili ziendane na biashara ya zao hilo na pia kufungwa kwa mizani katika bandari kavu ya Nassaco.

“Pia bandari ya Mtwara iboreshwe ili kuwa na uwezo wa kusafirisha korosho inayozalishwa katika mikoa ya kusini, na Serikali ihakikishe Mkoa wa Pwani unaingia katika mfumo wa stakabadhi ghalani kwa sababu katika hizo korosho zilizokutwa Vietnam kuna gunia 10 pia mbazo zilikutwa na chikichiki,” alisema.

Aliongeza: “Yaani michikichiki inalimwa Kigoma sasa inakuwaje unakuta katika korosho?” alihoji.


Bara la Afrika Kuwanyika Mara Mbili

0
0
Wanajiolojia wameeleza kwamba Tanzania na baadhi ya nchi nyingine za Afrika, zitameguka na kuwa visiwa.

Hata hivyo, wamesema mchakato huo utachukua mamilioni ya miaka.

Wamesema kuibuka kwa ufa mkubwa katika eneo la Bonde la Ufa, Kusini Magharibi mwa Afrika kutasababisha nchi za Kenya, Tanzania, Djbouti na Msumbiji kumeguka.

Pamoja na hayo, mjiolojia mwandamizi wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Gabriel Ndogoni alisema  kuwa kumeguka huko kutasababisha baadhi ya nchi za Afrika ambako Bonde la Ufa linapita kuzungukwa na bahari.

“Zitakuwa kama ilivyo kwa visiwa vya Madagascar au Zanzibar,” alisema.

Ndogoni alisema kwa waliosoma Jiografia, mchakato huo ni kama ule wa kugawanywa kwa mabara saba, “Zile nguvu za kupasuka kwa miamba hadi yakawepo mabara saba duniani bado zinaendelea. Mkondo huu wa Bonde la Ufa, ulianzia Kaskazini mwa Afrika katika nchi za Djibouti, Kenya mpaka Kusini mwa Tanzania.”

Alisema mkondo wa kwanza upo Ethiopia na kwa upande wa Kenya kuna miwili ambayo mmoja ndio uliopita hadi katika baadhi ya maeneo ya Tanzania kama Manyara, Singida, Iringa na Mbeya.

Alisema kasi ya maeneo hayo kujitenga ni milimita 0.1 Kusini mwa Afrika na milimita 6.5 Kaskazini mwa Afrika na kwamba Tanzania ipo katikati ya maeneo hayo.

“Kumeguka huku kwa bara la Afrika kunaleta wasiwasi kwa sababu kunatokea katika makazi ya watu,” alisema.

Dk James Hammond wa Idara ya Sayansi na Uhandisi kutoka Chuo cha Imperial cha London alinukuliwa na jarida la mtandaoni la Mail & Guardian akisema, “Katika miaka milioni kadhaa ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara mbili, na kuunda bahari mpya hapo katikati. Ukitumia jiografia ya sasa, bara hilo jipya litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania.”

Baadhi ya wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji.

Hivi karibuni, maofisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kenya (KeNHA) wakishirikiana na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya kisasa, walifika katika bonde hilo kuziba baadhi ya nyufa.

Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba hali hiyo ilitokana na shughuli ya kijiolojia chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa vipande vikubwa vya ardhi.

Siku chache baadaye, ufa huo uliendelea kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo lililosababisha magari yenye kubeba mizigo mizito kushindwa kupita. Pia ufa huo ulianza kuathiri nyumba za wakazi.

“Mkandarasi na wahandisi wako hapo kwa sasa na watabaki ili kufuatilia yanayojiri kutokana na shughuli za kivolkano ambazo zilisababisha ufa huo,” naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa Kenya, Charles Njogu alisema baada ya ukarabati huo mara ya kwanza.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE; 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO 0754372325/ 0689013109/ 0620806813 

HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Nafasi Ya Uchawi Kwenye Kamali

0
0
NAFASI   YA   UCHAWI   KWENYE   KAMALI
NA.  DOKTA  MUNGWA  KABILI…0744  000  473.

=============================================================
Watu mbalimbali  wamekuwa  wakitaka  kujua  maoni  yangu  kuhusu  nafasi  ya  uchawi  kwenye  kamali  na  michezo  ya  bahati  nasibu.  Yafuatayo  ndio  maoni yangu.

Toka  enzi  na  enzi  watu  wamekuwa  wakitumia  uchawi  ili kupata ushindi katika   kamali  na  katika  hilo  zimekuwa  zikitumika  kila  aina  ya  ndumba za kichawi   kuanzia  wale  walio  tumia  mashimo  ya  Nyegere, mafuta  ya  usiku, Pete za  bahati, Ngekewa,  Ndagu, sungura  weupe  nakadhalika nakadhalika.

Uchawi  una  nafasi  kubwa  sana  katika  kamali.  Maisha  ya  wacheza  kamali  mahali  popote  duniani  hutawaliwa  na  uchawi.

Uchawi  huanza  kutawala  maisha  ya  mcheza  kamali  kuanzia  siku  anapo  anza  rasmi  kucheza  kamali  mpaka  siku  atakayo  ingia  kaburini.

Uchawi  huwatawala  wacheza  kamali   wakiwa  duniani  n ahata   baada  ya  kuondoka duniani.

Ninasema  hivyo  kwa  sababu, moja  kati  ya  ndumba  zenye  nguvu  sana  katika  kamali  ni  zile  zinazo  tokana  ama  kutayarishwa  kwa  kutumia  makaburi  ya  wacheza  kamali  mashuhuri.  Wacheza  kamali  ninao  wazungumzia  hapa  ni  wale  ambao  waliyatoa   na  kuyatumia  maisha  yao yote  kwenye  mchezo  wa  kamali.

Kwa  mtu  ambae  alitajirika  kupitia  Kamari, kaburi  lake  huwa  lulu  yenye  thamani  kubwa  sana  katika  uchawi  wa  kamali . Watu hutumia  kaburi hilo  kutengeneza  ndumba  kwa  ajili  ya  kupata  mali  na  utajiri  kwa  njia  ya  kamali. Ndumba  hizo  huwasaidia  kushinda  kwenye  kamali.

Kwa  watu wengi  wanapo sikia  kuhusu  uchawi  wa  makaburini, akili  zao  moja  kwa  moja  huwa  zinaenda  kwenye  uchawi  wa  kuzika  nyota  za  watu, kuzika  kesi, kuzika  ndoa, mahusiano, biashara  za  watu , kuwatia  watu  nuksi, mabalaa  na  mikosi  nakadhalika.

Wasicho  kifahamu  ni  kwamba, makaburi  yanaweza  kutumika  kutengeneza  ndumba nzuri kutegemeana  na  nani  amelala  kwenye  kaburi  hilo.

Kwa  mfano  kwa  wale  walio fiwa  na  mama  zao  wazazi  na  wanataka  kutengeneza  ndumba  za  mapenzi, basi wanaweza  kutengeneza  uchawi  mkubwa  sana  wa  mapenzi  kwa  kutumia  mchanga  ulio  chotwa  kitaalamu kwenye  sehemu  ya  moyo  wa  kaburi  la  mama  ake  huyo. 

Sio hivyo tu, yapo  makaburi  ambayo  mchanga  wake  hutumika  kutengeneza  ndumba  ambazo  ni  tofauti  sana  na  dhana  iliyo jengeka  miongoni  mwa  watu  wengi  kuhusu  makaburi.

Kwa  mfano  kaburi  alilala  mtu  aliye  agwa  mara  mbili, kaburi  alilolala mtoto  wa  mwaka  mmoja na uchawi  katika  mapenzi, kaburi  alilo  zikwa  mtu ambae  msiba  wake  ulikaa  sehemu  mbili  tofauti ndani  ya  mji  mmoja , kaburi  alimo lala  marehemu  ambae  maiti  yake  iligombewa mahala pa  kuzikwa  nakadhalika.

Sasa  basi  mchanga  kutoka  kwenye  kaburi  alilo zikwa  mtu  aliye  tajirika  kupitia  kamali   hutumika  kutengeneza  uchawi  wa  kuwatajirisha  watu  kwa  njia  ya  kamali.

Kinyume  chake, kaburi  alimo zikwa mtu  ambae  alifilisika  kupitia  kamali,  mchanga  wake  hutumika  kutengeneza  uchawi  wa  kuwafilisi  watu, kuwatia  umasikini na  ufukara  pamoja  na  kuwafanya  watu  wenye  mali  nyingi  kufilisika  kwa   kuwekeza  pesa  zao  kwenye  biashara  zenye  risk kubwa.

Kwa  hiyo  kamali  ni  mchezo  unao  husisha  uchawi  na  ushirikina  kwa  kiwango kikubwa  sana.  Hii  ni kwa  sababu  kamali  ni  mchezo  wenye  pesa  nyingi  sana. Katika  ulimwengu  wa  kitabibu, kamali  haichukuliwi  tu kama  mchezo wenye  kuhusisha  bahati   ya  mtu, isipokuwa    huchukuliwa  kama  shughuli au  biashara  nyingine  yoyote  ile  yenye  kuleta  fedha  na  mali  nyingi  kama  vile biashara  ya  uchimbaji wa  madini nakadhalika.

Kwa  sababu  hiyo  basi  wacheza  kamali  wakubwa  wakubwa  wanapo  enda  kwa  waganga  kwa  ajili  ya  kupata  ndumba  za  kuwawezesha  kupata  mafanikio   kupitia  kamali  huwa  huwa  wanafanyiwa   ndumba  za  kuleta  mali  na  utajiri, kama  ambavyo  anaweza  kufanyiwa  mtu  ambae  anaingia  kwenye  biashara  ya  madini nakadhalika.

Hapa  nawazungumzia  wacheza  kamali  wanao cheza  mamilioni  ya  mapesa  kwenye  makasino  makubwa  na  ambao  kamali  ndio  chanzo  chao  kikuu  cha  mapato.

Kamali  ni  mchezo  wenye  ushindani  mkubwa  sana   ambao ndani  yake  unawahusisha  watu  wengi na  ambao  wengi  wao wanatumia  uchawi  kushindana.

Katika ulimwengu  wa  kitabibu  mcheza  kamali  huchukuliwa  kama  mtu  anae fanya  biashara  nyingine  yoyote  yenye  pesa nyingi  kama  vile  biashara  ya  uchimbaji  na  uuzaji  wa  madini  nakadhalika.

Na  hii ndio  sababu  kuu   wacheza  kamali  wanapo  enda  kwa waganga  kwa  ajili  ya  kupewa dawa za  kuwasaidia   kupata  mafanikio  katika  kamali  hupewa  ndumba  za mali  na  utajiri.

Mfano  pete  maalumu wanazo vaa  wacheza  kamali  ambao  watu  wengi  huziita  pete  za  bahati, si pete  za  bahati  kama  watu wengi  wanavyo  fikiri  isipokuwa  ni  pete    maalumu  za  majini  wa  mali na  utajiri.  Watu  wanao vaa  pete  hizo  wanakuwa  wameunganisha  nyota  zao  na  majini  hao  wa  mali  na  utajiri  ambao  huwasaidia  kuvuta  na  kupata mali  kwa  njia ya  mchezo  wa  kamali.

Hata  wale  wanao  chanjiwa ndumba maalumu  kwa ajili  ya  kamali, wengi  huchanjiwa  ngekewa  au  dawa  maalumu za  kuvuta  mali na  utajiri  ambao  huupata  kwa  njia  ya  kamali.

Mchezo  wa  kamali  ni  mchezo ambao  una  miiko  mingi  ambayo  wacheza  kamali  wengi  huifuata  na  kuiishi.

Ni mchezo  wenye pesa  nyingi  sana  ambao  unaweza  kubadilisha  maisha  ya  mtu usiku na  mchana. Na  kama  wasemavyo  wahenga, palipo na  riziki  hapakosi  fitina.

Hata wewe  unaetafuta  riziki nautajiri  kwa  njia  ya  kamali  unaweza  kufanyiwa  fitina  pia  na  wachawi.

Wachawi  wanajua  kuwa  kwenye  kamali  kuna  mamilioni ya  pesa na wanaweza  kukutupia  nuksi  itakayo  kufanya  usifanikiwe  kushinda  kamali  kwa  sababu  kwa  wao  wachawi  kamali  ni  shughuli  ama  biashara  nyingine  yoyote  ile.

Hata  hivyo, kamali  pia  ni mchezo  unao  weza  kumtia  mtu  umasikini  na  ufukara  ndani  ya  muda mfupi  sana.

Kwa Makala mbalimbali  kuhusu  ulimwengu  usio onekena, tembelea:

                www.mungwaherbalist.blogspot.com

Lulu Diva: "Msinifananishe na Shilole"

0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya muziki wa mduara Lulu Diva ‘Diva Divana’ ameibuka na kusema hataki kufananishwa na msanii mwenzake Shilole.

Lulu Diva amewataka mashabiki ambao wanafananisha rekodi zake na na miondoko ya nyimbo za Shilole waache kumpambanisha naye kwani hataki beef naye.

Lulu Diva amefunguka hayo Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, ambapo amedai anamheshimu Shilole kama dada yake hivyo hatopenda kuwa na beef naye:

"Hapana Jamani hakuna mtu ambaye anapotezwa kila mmoja anaimba mziki wake na mimi Shilole namheshimu kama dada na anafanya mziki wake wa kwake peke yake yaani hata ukiangalia mziki anaofanya na mziki wangu ni vitu viwili tofauti ni watu tu wanatengeneza vitu ili waweze kutuchonganisha”.

Lulu Diva aliendelea kumwagia Sifa Shilole huku akisisitiza hataki bifu naye:

"No mimi namheshimu sana as a sister she is a legend,ameanza mziki kabla yangu, anajua vitu vingi kwenye gemu kabla yangu.... kwaiyo wasitengeneze hiyo kitu mpaka mimi nikawa kuna kitu nataka kujua kuhusu mziki nikashindwa kumfuata kwa sababu ya maneno, kwaiyo naomba hivyo vitu visiwepo mimi nafanya mziki wangu mimi kama mimi”.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images