Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yatenga Shilingi Bilioni 5 Kwa Ajili Ya Kununua Mashine Nyingine Ya Kupima Vipimo Vya TB

$
0
0
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini jana jijini Dar es salaam.

“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka  vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.

Waziri Ummy alisema kuwa takribani  watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.

Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za  ,Kairuki, Agakhan,  Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.

Watuhumiwa Wawili Wa Ujambazi Wauawa Wakijibizana Risasi Na Polisi

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limesema watu wawili wanaotuhumiwa ni majambazi wameuawa wakati wakijibizana kwa risasi na Polisi.

Pia limesema limekamata silaha mbili AK 47 zenye namba UB38341997 na risasi 17 ndani ya magazine na AK47 1967TY4577 na risasi 24 ndani ya magazine pamoja na pembe za ndovu vipande 9 katika pori la Makerema wilayani Kasulu.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Maltin Otieno leo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari na kusema ilipofika majira ya saa 5:00 usiku  wa Machi 19, 2018 kwenye pori la Makere katika Kijiji cha makere wilayani Kasulu watu wawili ambao ni Norbert Andrew na Bukuru Stiven ambaye ni mkimbizi kambi ya Nyarugu waliuawa kwa kushambuliwa na majambazi wenzao wakati wakienda kuwaonesha Polisi silaha ambazo walikuwa wamezificha porini.

Amesema watu hao walikamatwa katika tukio moja la kuvunja kibanda na kuiba na mmoja wa majambazi hao waliangusha simu eneo la tukio iliyowezesha polisi kumkamata.
 
"Baada ya kuhojiwa na polisi waliwataja wenzao na kufanikiwa kuwakamata wanne.Katika mahojiano walikiri kuhusika na matukio ya mauaji  na uvamizi katika nyumba za watu wilayani hapo.

"Hata hivyo baada ya mahojiano hayo mtuhumiwa aliwaongoza Polisi mpaka kambi ya Nyarugusu na kufanikisha kukamatwa mtuhumiwa mwingine na baada ya kupekuliwa alikutwa na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya uhalifu,"amesema.

Amesema baada ya kukutwa na silaha hizo alieleza kuna silaha nyingine tano amezificha porini,hivyo polisi waliondoka na watuhumiwa hao na walipofika maeneo ambayo wameficha silaha ndipo risasi zilianza kupigwa na majambazi wenzao.

Aidha Kamanda Otieno amewaomba wakimbizi wote wenye silaha katika kambi za wakimbizi kuzisalimisha polisi kabla ya Machi mwishoni na baada ya hapo watanzaa msako kupitia kamati ya ulinzi na usalama na mkoa huo.

Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma

$
0
0
Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.
 
Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
 Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika

BREAKING: Rais Magufuli Katengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)

$
0
0
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni na kuivunja bodi hiyo. Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.

Shilole:Mume Wangu Hakasiriki Akiniona Nakata Viuno Hadharani

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka na kukiri haoni ubaya wa yeye kukata mauno stejini maana yupo kazini.

Suala limekuwa ishu baada ya video yake akiwa anatumbuiza stejini huku anakata  mauno kihasara hasara stejini kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Ndipo watu kuanza kuhoji inakuwaje mke wa mtu anafanya mambo yake hadharani lakini Shilole amewazima watu hao na kusisitiza kuwa Mume wake anajua anachofanya hivyo haoni kama kuna tatizo.

Shilole amefunguka alipohojiwa na Global Publishers kuhusu hilo na kuweka wazi kuwa anawashangaa watu wanaozungumza kuhusu hilo wakati wanajua wazi kuwa ile ndio kazi yake na mume wake Uchebe analitambua hilo hivyo hana neno juu ya hilo.

"Mume wangu Uchebe (Ashraf) anajua nikiwa kazini, chochote naweza kufanya jukwaani, haoni shida maana ananipenda na kazi yangu hivyo wanaosema ninawasihi waache kwani pale nilikuwa kazini kwa hiyo lazima niwapagawishe mashabiki wangu”.

Diamond aeleza bifu yake na Ali Kiba ilivyosukwa ‘kumuua Kimuziki’

$
0
0
Diamond Platinumz amedai kuwa uhasama kati yake na Ali Kiba ulipikwa na chombo kimoja cha habari kwa lengo la kumuondoa kwenye ramani ya muziki.

Bosi huyo wa WCB amefunguka katika mahojiano na Lil Ommy wa Times FM, ambapo amedai kuwa uhasama huo ulikuwa miongoni mwa mbinu za muda mrefu zilizoshindwa za kutaka kumuua kimuziki.

Amesema kuwa baada ya kugundua mbinu hiyo, alikutana na Ali Kiba jijini Nairobi na akazungumza naye kuhusu hilo na wakakubaliana hakuna tofauti kati yao.

Diamond ambaye anapromoti albam yake mpya ya ‘A Boy From Tandale’ alisema kuwa tofauti kati yake na Ali Kiba haiko kiuhalisia kwani inatengenezwa na watu wasiomtakia mema na kukuzwa na mashabiki. 

Aliongeza kuwa njama na jitihada za kutaka kumuangusha kimuziki zilianza miaka minne iliyopita lakini haziwezi kufanikiwa. Alisisitiza kuwa hakuna anayeweza kumuua kimuziki akiwa hai, “labda unitoe uhai, lakini kuniua kimuziki haiwezekani.”

Lil Ommy alitaka kujua kama nyimbo za Ali Kiba zitachezwa kwenye vituo vya Wasafi Radio na Wasafi  TV.

“Bro nisikudanganye, pale atachezwa kila msanii na yeyote mwenye talent (kipaji). Hadi sasa pale watu wanabishana kuhusu slogan (kauli mbiu), kuna wanaosema ‘Welcome Home’ na ‘Hii ni Yetu Sote’. Kwa hiyo hii ni ya wasanii na haipo kwasababu ya matabaka,” alijibu.

Chibu alisema kuwa ushikirikiano wa wasanii ndio utakaoendelea kuukuza muziki wa Bongo Fleva na sio uhasama na ushindani usiokuwa na lengo zuri.

Mikoa Yatekeleza Agizo la Waziri.....Viwanda 1,300 vyajengwa Ndani ya miezi mitatu

$
0
0
Utekelezaji  wa agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa uliotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, umefikia asilimia 49.4, viwanda 1,285 vikijengwa kati ya 2,600.

Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya Tamisemi na mikoa mjini hapa jana, Jafo alisema viwanda hivyo vimejengwa ndani ya miezi mitatu tangu kutolewa kwa agizo hilo.

Alisema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa na kila mkoa unatakiwa kuhakikisha unajenga viwanda 100 kufikia Desemba 31, mwaka huu.

“Viwanda hivi vilivyojengwa vina mchanganyiko mbalimbali vikiwamo viwanda vikubwa, vya kati na vidogo, mna mikakati mikubwa ambayo itawezesha kuwa na mchanganyiko wa viwanda vikubwa na vidogo,” alisema Jafo.

Alibainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa, ajenda ya Rais John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda inatekelezwa na kuwataka waendelee kuitekeleza.

Awali wakuu wa mikoa walitoa taarifa zao za ujenzi wa viwanda hivyo kufuatia agizo alilolitoa huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akibainisha kuwa katika mkoa wake tangu kutolewa kwa agizo hilo, viwanda 88 vimeshajengwa.

Hata hivyo, Makonda alisema kumekuwa na changamoto ya umeme na maji na kuiomba serikali kuliangalia suala hilo ili kuendelea kuvutia wawekezaji zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema katika mkoa huo wamejenga viwanda 22 ambavyo ni vikubwa na vya kati na vingine vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.

“Changamoto iliyopo ni nishati ya umeme na kwa mkoa wetu tunahitaji tuwe na megawati 800,” alisema Ndikilo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, alisema zimetengwa hekari 307,595 kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na hadi sasa tangu kutolewa kwa agizo la Jafo, vimejengwa viwanda 45 vipya ambavyo vimetoa ajira mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, alisema mkoa wake unaendelea kutekeleza mkakati wake wa bidhaa moja kwa wilaya moja na kwamba tangu agizo hilo, viwanda 18 vipya vimejengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema viwanda vipya vilivyojengwa mkoani kwake ndani ya agizo hilo ni 124 huku Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack, akisema kwake amejenga viwanda 126.

Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli

$
0
0
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (Tuico), kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi), yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa Tuico taifa, Paulo Sangeze, alisema, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.

Akizungumza katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu, iliyowashirikisha viongozi wa matawi mbalimbali ya  Tuico mwishoni mwa wiki, iliyofanyika jijini hapa, Mwenyekiti wa Tuico taifa, Sangeze, alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.

Alisema baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari wamepanga maadhimisho hayo kwa mwaka huu, yatafanyika mkoani Arusha katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Katibu wa Tuico, Boniface Nkakatisi, alisema maandalizi hayo yanaenda na mialiko ya wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini, wanachama  wa Tuico, mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.

Haji Manara Aingilia Kati Sakata la Diamond na Naibu Waziri

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kumkingia kifua msanii Diamond na wenzake ambao wamekuwa wakitetea haki zo kwa Naibu waziri ambae ameibuka na sera ya kuwafungia wasanii kwa madai kuwa wanaimba nyimbo zisozokuwa na maadili katika jamii.

Hivi karibun Diamond aliongea katika media moja na kusema kuwa hata kama atatakiwa kulala jela kwa sababu ya muziki basi atafanya ilimradi kutetea haki ya muziki kwa sababu watu wanaofungia muziki huo hawajui historia ya muziki wala msanii wanaemfungia.

Haji Manara amesema  kuwa pamoja na kwamba wasanii wanaweza kuwa wamefanya kosa lakini wanapaswa kuangaliwa kwa jicho la pili na kwa upande wa Diamond ni msanii mkubwa mbaye amekuwa akiiwakilisha nchi katika mambo mbalimbali.
 
"Ngoja na mimi nispitwe na hili..inawezekana kuwa kama binadamu anaweza kuwa amekosea , lakini inabidi tutambua kuhusu muziki wa kisasa na soko lake linataka nini..by the way diamond na wenzie tunawatumia sana katika maswala ya kijamii  na hata kampeni zetu za kisiasa,na huyu ni brand kubwa ,,,walau tufanye staha kidogo na tujitaidi tupende vya kwetu.

NB.mimi napenda muziki mzuri sina cha timu wala cha baba yake na timu….hawakawii wabongo. @diamondplatinumz"

RC Makonda atoa taarifa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria

$
0
0
TAARIFA YA MKUU WA MKOA DAR ES SALAAM KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA KWA AFISA UBALOZI WA SYRIA.
Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.

Nawaomba sana wananchi wa Dar es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.

Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.

Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.

Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam

Basata wasema Diamond Amefanya Makosa Makubwa kumjibu Waziri Shonza

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza amesema mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond amefanya makosa kumjibu Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akifananisha kitendo hicho na kuitukana Serikali.

Diamond Platnumz na naibu waziri huyo waliingia katika vita ya maneno baada ya Serikali kufungia nyimbo 15 mwezi uliopita, zikiwemo mbili za mwanamuziki huyo.

Mngereza amesema Diamond anapaswa kuelewa kwamba maneno machafu anayoyatoa dhidi ya waziri huyo  ni sawa na kuitusi serikali jambo ambalo hata ukienda katika sheria za kimtandao anaweza kujikuta anaingia matatizoni.

Mngereza amesema wamesikitishwa na kauli ya Diamond na kusisitiza kwamba ni vyema akafuata taratibu katika kulalamikia suala hilo ikiwemo kuandika barua kama alivyomuelekeza Waziri Shonza.

Ameongeza kuwa si lazima msanii aandikiwe barua pale anapokosa kama ambavyo Diamond ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter, kwamba Shonza angemwandikia barua kabla ya kumfungia.

Amebainisha kuwa si kila mwanamuziki anayefanya makosa huwa anaandikiwa barua.

Katika malalamiko yake, Diamond amesema naibu waziri huyo amekuwa akikurupuka kufungia nyimbo na pia kutowaandikia barua rasmi ndio maana ameamua kuyazungumza kwenye redio na mitandao ya kijamii.

Jana Waziri Shonza alisema hawezi kujibizana na Diamond kwa sababu alichofanya si maamuzi yake binafsi na kwamba kama anaona ameonewa apeleke malalamiko yake kwa maandishi.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE; 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO 0754372325/ 0689013109/ 0620806813 

HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi? Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Tupo Mbagala

Jinsi Ya Kuandaa Na Kutayarisha Lishe Maalumu Ya Kuongeza Na Kunenepesha Mwili

$
0
0
Kama umekonda  na  kudhoofika  mwili  kutokana  na  sababu  mbalimbali  kama  vile kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kupatwa  na  msongo  mawazo, basi  fuata  maelekezo  yafuatayo  ili  upate  kujua  namna  ya  kuandaa  na  kutayarishe  lishe  maalumu  ya  asili  itakayo  kusaidia kunenepa  na  kurejesha  afya  ya  mwili  wako  katika  hali  yake  ya  kawaida.

MAHITAJI:
1.    Dawa  Lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili

2.   Asali  ya  tende

3.   Ufuta

4.     Ukwaju

5.    Kitunguu  swaumu

6.   Giligiliani

7.    Juisi  ya  Komamanga na  Asali

MATAYARISHO  NA  MATUMIZI
Matumizi  ya  lishe  hii, yame  gawanyika  katika  awamu  kuu  mbili. Awamu  ya  kwanza, itachukua  siku thelathini  na  awamu  ya  pili  itachukua  siku  thelathini pia.

Katika  awamu  ya  kwanza , mgonjwa  atatumia  DAWA  LISHE  YA  KUNENEPESHA  MWILI, ASALI  YA  TENDE  NA  UFUTA  na  awamu  ya  pili, mgonjwa  atatumia   UKWAJU, KITUNGUU  SWAUMU, GILIGILIANI  na  JUISI  YA  KOMAMANGA  & ASALI  kwa  kufuata  utaratibu  utakao  elezwa  hapo  chini.

AWAMU   YA   KWANZA
SIKU   THELATHINI  ZA  KWANZA

Mahitaji

1.   Dawa  lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili

2.   Ufuta

3.   Asali  ya  Tende  (   Dates  Syrup )

MATAYARISHO  , MAELEKEZO  NA  MATUMIZI
1.   Dawa –Lishe  ya  Kunenepesha  Mwili

Chukua  vijiko   vitatu vikubwa  vyenye  dawa  yako, kisha  changanya  na  maji  nusu  lita halafu chemsha  hadi  itokote, Ikiisha  tokota, ipua  acha  ipoe  kidogo kisha  tumia  kunywa  pamoja  na  machicha  yake.  Utafanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda wa  siku  thelathini.

2.   Ufuta : Matayarisho : Chukua  vijiko  vikubwa  vinane  vyenye  ufuta, kisha  changanya  na  lita  moja  na  nusu  ya  maji. Kama  hauna  tatizo  na  sukari, unaweza  kuongeza  na  sukari  kiasi ili  kuipa  ladha.  Ikisha  tokota, ipua iache  ipoe  kiasi  kisha  tumia  kula  ufuta wote  pamoja  na  supu  yake  ama  juisi  yake. Utafanya  hivyo mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.

(N.B:   KAMA  UNA  NAFASI,  BADALA  YA  KUTUMIA  VIJIKO  VINANE  TU VYA  UFUTA  KWENYE LITA  MOJA  NA  NUSU  YA  MAJI, WEWE  TUMIA  ROBO KILO  YA  UFUTA  KWENYE  LITA  TATU  YA  MAJI, CHEMSHA  HADI  ITOKOTE,  IACHE  IPOE, KISHA  TUMIA  KULA . FANYA  HIVYO  MARA  MBILI  KWA  SIKU  ASUBUHI NA  JIONI  KWA  MUDA  WA SIKU  THELATHINI )

2.   ASALI  YA  TENDE
3.   Tumia  kula  vijiko vikubwa  vinne  vya  tende  mara  mbili  kwa siku  asubuhi  na  usiku   kwa  muda  wa  siku  thelathini. Yaani  asubuhi  kula  vijiko  vikubwa vinne  na  usiku  kula  vijiko  vikubwa vinne  vya  asali  ya  tende.

( HABARI  NJEMA  KWA  WATEJA  WETU  NI  KWAMBA, ASALI  YA  TENDE  SASA  INAPATIKANA  MOJA  KWA  MOJA  DUKANI   KWETU . UTAPATIWA  DAWA  LISHE  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE  UTAKAYO  ITUMIA  KWA  MUDA  WA  SIKU  THELATHINI  KWA  UTARATIBU  WA  MAELEKEZO  HAYO  HAPO  JUU )
AWAMU   YA  PILI
Awamu  ya  pili  ya  lishe  hii, itaanza  baada  ya  kukamilika  kwa  siku  thelathini  za  kutumia  dawa  lishe, ufuta  pamoja  na  asali  ya  tende. Kama  ilivyo  kuwa  kwa  awamu  ya  kwanza, awamu  ya  pili  pia  itachukua  muda  wa  siku  thelathini

MAHITAJI, MATAYARISHO   NA  MATUMIZI

1.  UKWAJU
Matayarisho na  Maandalizi
Chukua ukwaju  kiasi  cha  robo kilo , weka  kwenye  maji  kiasi  cha  lita  moja, ongeza pilipili  manga kiasi cha  kijiko kimoja kidogo  ( tea spoon ) halafu ongeza sukari  vijiko  vitatu vikubwa, ongeza karafuu  ya unga  kijiko kimoja kidogo, pamoja  na hiriki vijiko  vikubwa  viwili.

Ukisha  fanya  hivyo, chemsha  hadi  mchanganyiko  wako  utokote. Ukisha  tokota, ipua  na  kuchuja  kisha  weka  kwenye  chombo  kisafi.

MATUMIZI :
Tumia  kunywa  mchanganyiko  huu kila  siku  asubuhi  baada  ya  kunywa  chai. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

2.   JUISI   YA  KOMAMANGA  NA  ASALI
Matayarisho  na  Matumizi

Tayarisha  juisi  ya  komamanga  kiasi  cha  nusu  lita, changanya  na asali ya  kawaida  vijiko vikubwa    vinane, kisha  ongeza  chumvi kijiko kidogo( tea spoon)

Koroga  mchanganyiko  wako  halafu  tumia  kunywa. Utafanya  hivyo  mara  moja   kwa  siku kwa  muda  wa  siku thelathini.

Matunda  ya  makomamanga  yanapatikana  masokoni, ingawa  mara  nyingi  hupatikana  kwa  uchache. Kama  utabahatika  kupata matunda  mengi, basi  unashauriwa  kuyachukua  kwa  wingi  na  kuyahifadhi, sehemu  salama ili usipate  usumbufu  wakati  wa  kutumia  tiba  yako.

Mbali  na  kutumika  katika lishe  ya  kuongeza  na  kunenepesha  mwili, tunda  la  komamanga, linasaidia  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa. Kwa  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa, kula  walau  tunda  moja  la  komamanga  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo. Utapata  matokeo  mazuri . ( HII  ITAWASAIDIA  ZAIDI  WALE  AMBAO  TATIZO  LAO  LA  KUTOKWA  NA  HARUFU  MBAYA  YA  KINYWA  LIMEANZIA  KINYWANI  NA  SIO  TUMBONI

ALTERNATIVE (MBADALA )  WA JUISI  YA  KOMAMANGA  ILIYO  UNGWA  NA  ASALI.

Kama  utashindwa  kupata makoma manga, basi  utafanya  kama  ifuatavyo :

KITUNGUU  SWAUMU
Chukua punje  nne  za  vitunguu  swaumu, zitwange kisha  tia  kwenye  maji nusu lita halafu ongeza  juisi  ya  ndimu  moja  au  limao  moja kisha  chemsha hadi mchanganyiko  wako  uchemke.

Matumizi :  Tumia  hivyo kila  siku  usiku baada  ya  kula  chakula cha  usiku. Utafanya  hivyo  kwa  muda  wa  siku  thelathini mfululizo.

AU
Vile vile , mbadala  mwingine wa  kutumia  juisi  ya komamanga  iliyo  changanywa  na  asali, unaweza  kutumia  JUISI  YA  GILIGILIANI  kwa  kufuata  utaratibu  ufuatao :

JUISI   YA   GILIGILIANI
MATAYARISHO   NA   MATUMIZI YA  JUISI  YA  GILI GILIANI

Chukua giligiliani  fresh, kisha zi -blend ( ZISAGE ) ili  kupata  juice  yake  kiasi  cha  robo  lita.

 Ndani  ya  juisi  yako  ya  giligiliani, kamuliamo ndimu fresh moja, halafu  ongeza  chumvi  kiasi robo  kijiko  kidogo ( tea spoon), koroga  kisha  tumia  kunywa.  Utakunywa  usiku  baada  ya  kula  chakula  cha  usiku. Utafanya  hivyo mara   moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo.

PIA : Jenga  utaratibu  wa  kuwa  unakula    giligiliani kwa wingi. Hakikisha  katika  kila  mlo  wako, inakuwepo  mboga  ya  giligiliani  pembeni.

VITU   VINGINE VYA   KUZINGATIA..
Pamoja na kutumia  lishe  hii  ya  asili  kwa  kufuata  utaratibu  huo  hapo  juu, unashauriwa  kuzingatia  matumizi  ya  vyakula  vifuatavyo:

TANGAWIZI
Jenga  tabia  ya  kuwa  una tumia  tangawizi, kila  mara  upatapo  nafasi.  Utaratibu  wa  jinsi  ya  kutayarisha  tangawizi ni  kama  ifuatavyo :

Chukua kipande  kimoja  cha  tangawizi, kisha  kitwange  halafu ongeza  vikombe  viwili vya  maji  vyenye  ujazo  wa  milimita  mia  mbili  na  hamsini ( 250 mills). Chemsha pamoja  kisha ongeza  maziwa  kiasi cha  robo lita  na  sukari ili kupata  ladha.  Fanya  hivi  kila  mara  uapatapo  nafasi. Ukiweza kufanya  hivyo walau  mara  mbili  kwa  siku, itakuwa  vizuri  zaidi.

  AU  chukua  kipande  kimoja  cha  tangawizi, kitwange kisha  chemsha pamoja  na  chumvi nusu  kijiko  kidogo  kwenye  maji kiasi  cha  nusu   lita  halafu tumia  kunywa  kikombe  kimoja  nusu  saa  kabla  ya  kula  chakula chako  cha  asubuhi, mchana  na usiku.

HIRIKI
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakunywa  mara  kwa  mara  chai  iliyo  changanywa  na  hiriki.

MACHUNGWA
Jenga utaratibu  wa  kuwa  unakula  machungwa kwa  wingi,  kwa  kadri utakavyo  weza. Unashauriwa  kuwa  unachanganya na  chumvi  kidogo  pamoja  na  pilipili  manga.

KWA  MAHITAJI  YAKO  YA  DAWA-LISHE  YA  KUNENEPESHA  & KUONGEZA  MWILI  PAMOJA  NA  ASALI  YA  TENDE.

Kwa  mahitaji  yako  ya  DAWA-LISHE ya  kuongeza & kunenepesha  mwili, pamoja  na  asali  ya  tende, fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI   UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA  0766 53 83 84.

Kwa wateja  wetu  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  dukani  kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  walipo ( HOME & OFFICE  DELIVERY  )

Kwa wateja  waliopo  nje  ya  mkoa   wa  Dar  Es  Salaam,  watatumiwa  dawa  kwa  kutumia  mabasi  mbalimbali.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.

Kwa  wateja  waliopo  ughaibuni, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

Na kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu :


Lemutuz Amkingia Kifua Diamond....Amtuhumu Naibu Waziri Kushirikiana na Watu Kumshusha Diamond

$
0
0
Wakati BASATA wakimtuhumu Diamond kulewa na umaarufu na kufanya abishae na Naibu waziri ambaye anawakilisha Serikali, bado huko katika mitandao ya kijamii watu wamezidi kuonyesha hisia zao juu ya jambo hilo kwa kudai kuwa Naibu waziri anatafuta kiki kwa lengo la Kumshusha Diamond.

Mwanahabari  na Blogger, Le Mutuz ameibuka na kudai kwa Naibu Waziri amekuwa akitumiwa na watu wenye chuki kubwa na muziki wa Diamond ili kuua muziki wake na sio vinginevyo.

Le Mutuz anasema kuwa  huu ulikuwa ni wakati wa serikali kuona mchango wa Diamond hasa baada ya kuchaguliwa kwenda kufanya show ya ufumbuzi wa kombe la Dunia.                                                                                                    

Lemutuz ambaye amesema kuwa pamoja na kwamba Mh Juliana Shonza ni mwana CCM mwenzake lakini anaona kabis katika hili la kuwafungia na kubishana na Diamond katika mitandao ya kijamii hawezi kunyamaza kimya.

Hata hivyo Lemutuz amemhusisha Julana Shonza na moja ya kiongozi wa kituo fulani cha radio “MUNGU MTU” ambacho hajakitaja na kusema kuwa wamekuwa wakishirikiana ili kumtua Diamond katika nafasi kubwa ya mafanikio ya kimuziki aliyonayo.

Hatimaye Abdul Nondo amefikishwa Mahakamani....Ni Baada ya Kusafirishwa Usiku na Kurudishwa Iringa

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2018 kupelekwa mkoani Iringa.

Taarifa zilizotolewa na wakili wake, Jebra Kambole leo Jumatano Machi 21, 2018 zinaeleza kuwa sasa Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.

Nondo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 na siku inayofuata akaonekana mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa ambako alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kurejeshwa Dar es Salaam.

Tangu akamatwe Nondo hajawahi kuzungumza na wakili wake wala mtu yeyote wa karibu yake jambo ambalo limekuwa likipingwa na watetezi wa haki za binadamu.

Jana, Jebra alisema kuwa wamefungua kesi kwa ajili ya kuiomba mahakama mambo matatu, kwanza kumpa dhamana Nondo, pili kutoa amri ya kuwapa mawakili haki ya kuonana na Nondo na kingine ni kuitaka mahakama itamke mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ameshikiliwa  kinyume cha sheria.

Nondo asomewa mashtaka mawili, anyimwa dhamana

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imezuia dhamana ya Mwenyekiti wa Mtandao Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kwa sababu za usalama wake ikieleza kuwa bado maisha yake yapo hatarini.

Akizungumza leo Jumatano Machi 21, 2018 Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, John Mpitanjia amesema anaomba muda wa kusoma vifungu vya sheria mpaka Machi 26, 2018 ili kujihakikishia kama mtuhumiwa hatakuwa hatarini iwapo atapatiwa dhamana.

Akisoma mashkata yanayomkabili Nondo, Wakili wa Serikali, Abeid Mwandalamo amesema anatuhumiwa kwa makosa mawili.

Amesema kosa la kwanza ni  kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa eneo la Ubungo Dar es Salaam na kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.

Katika shtaka la pili, wakili huyo amesema Nondo ametoa  taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na kupelekwa kiwanda cha Pareto Mafinga. Hata hivyo, Nondo alikana mashtaka hayo.

Mwanadalamo amesema ushahidi bado haujakamilika hivyo wanaomba siku chache, kwa kipindi watakachokuwa wanafanya upelelezi mtuhumiwa asipewe dhamana.

Amedai kuwa kwa sababu bado wanafanya upelelezi kwa rafiki wake wa karibu, kama atapewa dhamana anaweza kuingilia na kuharibu upelelezi huo.

Wakili wa utetezi, Chance Luwoga amesema mashtaka aliyosomewa Nondo yanaruhusu kupewa dhamana.

Polisi Dodoma imewakamata watu wawili kwa kusambaza taarifa za maandamano ya April 26 2018.

$
0
0
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limewakamata na kuwashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kwenye mitandao ya kijamii yanayotarajiwa kufanyika April 26 mwaka huu.

Kamanda wa polisi wa mkoa Dodoma Gilles Muroto amesema watu hao wamekua wakisambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii kuhamasisha watu kuandamana huku wakijua ni kosa kisheria.

Aidha Kamanda Mruto ametoa wito kwa watu kutofuata mkumbo kuhamasisha watu kufanya maandamano kwani ni kosa kisheria na kuwa yeyote ambaye atakamatwa atashughulikiwa kisheria.

"Watu hawa wamekuwa wakihamasisha wananchi kufanya maandamano, tulishasema Serikali haijalibiwi leo tunaanza kutoa mifano kwao. Wale wote wanaoijaribu Serikali tutahakikisha tunawachukulia hatua za hali ya juu sana”

Mbali na hilo Kamanda Mruto amesema kuwa upelelezi ukikamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kuhusu kuhamasisha watu kufanya maandamano kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamepangwa kufanyika April 26, 2018 nchi nzima na yakiratibiwa na mwanadada Mange Kimambi kupitia mitandao ya kijamii.

Necta yafanya mabadiliko mtihani darasa la saba

$
0
0
Wanafunzi wa darasa la saba ambao watafanya mtihani mwaka huu watakutana na mabadiliko ya mfumo wa utungaji  wa mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi .

Mabadiliko hayo yamefanywa na Baraza la Mitihani la Taifa  (Necta) jana na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde.

Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi amesema mabadiliko hayo aliyatangaza Dk Msonde katika mkutano mkuu wa tano wa maofisa elimu mkoa na wilaya unaofanyika Dodoma.

Nchimbi amesema katika muundo huo mpya kila somo litakuwa na maswali 45, kati ya hayo, maswali 40 yatakuwa ya kuchagua jibu sahihi na matano yasiyo ya kuchagua (yatakuwa ya kujieleza/kuonyesha njia na jibu nk).

Amesema maswali 40 kila swali litakuwa na alama moja na maswali matano kila swali litakuwa na alama mbili huku majibu ya maswali 40 yatajibiwa kwenye OMR FORM na maswali matano yatajibiwa kwenye karatasi maalum itakayoandaliwa.

Kutokana na muundo huo mpya, Necta imetoa wito kwa walimu wakuu kuanza kuwapima wanafunzi kwa kutumia mabadiliko hayo ili kuwajengea uzoefu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images