Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Irene Uwoya: Nimemzidi Dogo Janja Kila Kitu Labda Yeye Kanizidi Dhambi tu

$
0
0
Msanii wa bongo movie  Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.

Irene Uwoya ameyasema hayo jana alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena  cha Clouds Radio  alipokwenda yeye na mumewe huyo.

Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu  hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.

"Ni kweli nimemzidi  umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata.
 
"Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo“

Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio hela bali ni mapenzi ya dhati.

"Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa."

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 45 na 46 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                             
ILIPOISHIA 

“Mariamuuuuuuuuuuu”
Niliisikia sauti ya Mama Marim iliyo zidi kunichanganya na kujikuta nikikaa chini sakafuni huku machozi yakinilenga lenga. Nikanyanyuka taratibu na kumtazama Mariam, jinsi alivyo lala hajabadilisha hata mkao, mapigo yake ya moyo yamesimama kabisa jambo lililo zidi kunichanganya maradufu na saa yangu ya ukutani inaonyesha ni saa mbili kasoro usiku na muda si mrefu Babyanka atakuja kunipitia kwa ajili ya kwenda Marekani kuifanya kazi ya muheshimiwa riaisi.

ENDELEA
Mlango wa chumbani kwangu ukagongwa na kuyafanya maoigo yangu ya moyo kuzidi kwenda kasi kwa maana ninatambu atakuwa ni mama Mariam. Nnikashuka kitandani kwa haraka, nikafungua friji nikatoa chupa yenye maji ya baridi na kumwagia maji hayo Mariam usoni. Cha kumshukuru Mungu, akakurupuka huku akiwa anagema sana.
Nikawahi kumziba mdomo ili asiweze kupika kelele zitakazo sikika nje kwa maana mama yake amesha fika.
“Dany”
“Shiii”
“Mariammuuuu”
Tuliisikia sauti ya Mama Mariam akiita akiwa uwani na ttayari alisha ondoka mlangoni mwangu. Wasiwasi ukaanza kumjaa Mariam, akaanza kushuka kitandani huku akiwa anahema, akajaribu kupiga hatua mbili mbele ila nikagundua kwamba mwendo wake umebadilika na ana chechemea.
“Mungu wangu, Dany mama si atajua kwamba nimeutoa usichana wangu”

“Jikaze utembee vizuri, hatokustukia”
Nilizungumza huku nikimkalisha kwenye sofa taratibu. Tukatazama usoni, hapakuwa na aliye muongelesha mwenzake, hata sauti ya mama Mariam inayo ita ikawa haiendelei tena.
“Ngoja nitoke nikamzuge mama yako, hakikisha unafanya unatoka humu ndani asije kukustukia”
“Sawa”
Nikachukua taulo langu na kujifunga kiunoni mwangu,  nikachukua sabuni yangu na kutoka chumbani kwangu, kwenye kordo sikumkuta mtu wa iana yoyote. Nikaelekea kwenye mlango wa mbele ambapo nilihisi naweza kumkuta mama Marim, kwa bahati nzuri nikakutana naye mlangoni akiwa anaingia. Nikamshika mkono na kutoka naye nje.
“Vipi mbona unamwagikwa na jasho?”
“Nilikuwa ninafanya mazoezi, nikaoge kwa maana kuna sehemu nahitaji kuelekea”
“Unaeleka wapi tena honey”
“Ninakwenda nje ya nchi kikazi, kwahiyo sinto kuwepo Tanzania kwa siku kadhaa”
“Jamani Dany, hata kiu yangu hujaimaliza na wewe unataka kuondoka?”
“Imetokea kwa dharula tu, ndio maana nilipo isikia sauti yako nikatafuta ili niweze kukueleza juu ya hili mpenzi wangu”
“Na safari hiyo unaondoka saa ngapi?”

“Saa mbili hii ndio naondoka, hapa nimemaliza kufanya mazoezi na ninahitaji kueleka bafuni, nijiandae niondoke”
Mama Mariam akatazama kila sehemu ya eneo hili la nje tulipo kisha akanikumbatia na kuanza kuniyonya mdomo wangu. Tukalifanya tendo hilo kwa dakika kadhaa kisha tukaachiana.
“Nakuomb nikaoge”
“Sawa honey, ila Marim umemuona?”
“Nilimuona pale nilipo rudi na nikamuomba ufunguo, baada ya hapo sikufahamu ni sehemu gani aliyo elekea”
“Yaani huyu mtoto sijui atakuwa amekwenda wapi, ngoja nikamtazame hapo mbele kwa mama Jenifa”
“Sawa”
Mama Mariam akanipiga busu la mdomo kisha akatoka getini, alipo funga geti kwa haraka nikaingia ndani moja kwa moja nikaeleka chumbani kwangu, nikaufungua mlango na kuingia ndani. Sikumkuta Mariam, nikashusha pumzi na kuelekea chumbani kwake, nikamkuta akiwa amesimama katikati ya chumba huku amefunga kanga kifuani.
“Mama yako amekwenda kwa mama Jenifa, sasa fanya ukaoge kisha urudi ulale sawa?”
“Sawa”

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Tatu ( 33 )

$
0
0
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Gafla tukastukia akiichomoa bastola yake na kutonyooshe sisi na Rahma na kwastory nilizo wahi kuzisikia mtaani kweni ni kwamba huyu mzee anatabia ya kutembea na wasichana wadogo japo sikuwahi kumshuhudia na kwa story nyingine nilizo zipata mtaani ni kwamba alimuua mke wake kwa kumpiga rasasi baada ya kufumaniwa akiwa na binti mdogo

ENDELEA
Mlio wa bastola ya mzee Ngoda ukanifanya nifumbe macho huku nikisikilizia ni wapi risasi yake ilipo tu,Swali nililo nalo kichwani kwangu ni kwamba ni wapi risasi ilipo tua kwa maana mwilini mwangu sikusikia maumivu ya aina yoyote na kama imempiga Rahma wangu mbona sijasikia sauti yoyote ya yeye kutoa maumivu.Kwa haraka ni kafumbu macho na kumtazama Rahma na kumkuta akitetemeka kwa woga
“Angalieni nyuma yenu”
Tukageuka na kukuta nyoka mkubwa akining’inia kwenye tawi la mti huku kichwa cheke kikiwa kimetawanywa na risasi aliyo pigwa na Mzee Ngoda

“Mwanajeshi anatakiwa kuwa na hisia za kitu chochote cha Atari kitakacho kuwa karibu yake ila nakushangaa Eddy wewe nyoka yupo nyuma yako wala hustuki kwa kitu cha ina yoyote”
Kutokana na mstuko wala sikujua nimjibu kitu gani mzee ngoda,Rahma akanishika mkono na kunikumbatia huku akiendelea kutetemeka.Mzee Ngoda akapanda kwenye gari na kutuomba na sisi tupande,taratibu nikamshika Rahma mkono na tukapanda kwenye gari na safari ikaendelea ambayo tayari nilisha anza kuitilia mashaka na sikujua ni wapi tunapoelekea.Tukafika kwenye moja ya jumba kubwa lililo jegwa vizuri na Mzee Ngoda akasimamisha gari nje ya jumba hili na akatuomba tushuke kwenye gari

“Karibuni sana wanangu hapa ni nyumbani kwangu”
Mzee Ngoda alizungumza huku akitoa funguo nyingi na kufungua geti la chuma lililopo kwenye jumba hili,kisha akafungua na mlango mwengine na tukaingia ndani japo kuna giza kuba.Akawasha swichi na taa za ndani zikawaka
“Hapa ni kwangu huwa nikiwa na mawazo sana huwa ninakuja huku kupumzika kama wiki kisha ninarudi tena mjini”
“Unakuja kupumzika peke yako?”
“Ndio ninakuja peke yangu na niwatu wengi hawaijui hii nyumba yangu kwa maana ipo porini sana”
“Ni kubwaa”

“Yaa ina eneo kubwa kwa huko nyuma kuna bustani za maua ya kutosha sema sasa hivi ni usiku sana….Hii nyumba niliinunua kwa rafiki yangu alikuwa ni mwanajeshi wa kijerumani kipindi cha miaka ya semanini”
“Ahaa sawa”
Mzee Ngoda akatuonyesha chumba cha kulala ambacho ni kikubwa sana na kina vitu vichache vya dhamani pamoja na kitanda kikubwa cha duara ambacho tangu nizaliwe sikuwahi kulala,nikakichunguza chumba kizima  na kuridhika na mazingira yaliyopo humu ndani.Nikavua nguo zangu na kupanda kitandani na Rahma akafanya kama nilivyo fanya mimi na ikawa ni siku nyingine ya furaha katika mahusiano yetu baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha.Baada ya kupeana haki ianyo stahili kila mmoja akapitiwa na usingizi mzito

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Wizara Saba Kukutana Kutatua Changamoto Za Mazingira Ya Biashara Na Uwekezaji Mpakani Mwa Tanzania Na Zambia

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WIZARA SABA KUKUTANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA
--------------------------------

Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini, imeamua kuzikutanisha wizara saba zinazohusika moja kwa moja na changamoto zinazopunguza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji katika mkoa wa Songwe na maeneo yaliyopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora amesema mara baada ya kuhitimisha  ziara yake  tarehe 17 Machi, 2018, atakutana na makatibu wakuu wa wizara zinazopaswa kutoa suluhisho la changamoto hizo.

“Nitakutana na makatibu wakuu wenzangu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa  na Serikali za mitaa (TAMISEMI) na naamini maazimio tutakayotoa katika kikao hicho yatakuwa suluhisho la kuondoa changamoto zinazojitokeza hapa mpakani mwa Tanzania na Zambia” , amesema Kamuzora.

Akibainisha changamoto za mazingira ya Biashara na uwekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema, changamoto kubwa mpakani hapo ni usalama kwa wafanyabiashara na biashara zao, ambapo kwa mazingira ya mpaka huo imekuwa vigumu kuuimarisha.

“Mpaka wetu umejengwa kila mahali , hivyo uhalifu unakuwa mgumu kuuzuia Kuna watu wanakunywa pombe Zambia ambazo tumezizuia hapa nchini kuuzwa, na kurudi wamelewa Tunduma, suala la biashara haramu ya ubadilishaji wa fedha inayofanywa mtaani  kinyume na sheria na taratibu za nchi ni changamoto , lakini wafanyabiashara wanakwepa kodi kutokana na kuwa kunabaadhi ya watanzania sehemu ya nyumba zao  zipo Zambia nyingine ipo Tanzania hivyo ushuru wa forodha haukusanywi kwa madai wanapeleka bidhaa hizo kwa watanzania kwani hawapitishi bidhaa hizokwenye lango husika” alisema Galawa

Galawa amebainisha mipango ambayo Mkoa umejipanga katika kuhakikisha wanakabili changamoto hizo, kuwa ni kuliweka Daftari la wakaazi katika mfumo wa kielektroniki ambalo litajumuisha wakaazi wote wa Tunduma kuanzia umri wa mwezi mmoja na litakuwa linahuishwa kila wakati, Upimaji wa mji waTunduma nao unaendelea na kila mmiliki  wa ardhi atapewa hati, pia litajengwa soko kubwa mpakani hapo ili kufanya menejimenti ya biashara mpakani.

Aidha, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu alikutana na wadau wa sekta binafsi, pamoja na wateja katika Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma, ambao walishauri sekta zinazohusika na Mazingira ya Biashara na Uwekezaji mpakani hapo kwa upande wa Tanzania  na Zambia zikutane ili  kuharakisha kutatua changamoto zinazopunguza ufanisi wa biashara mpakani hapo.

Lengo la Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini ni Kupunguza gharama za Kufanya biashara nchini kwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji, mpango huo unaotekelezwa na Idara, Wizara na Wakala wa Serikali  kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Mwigulu Nchemba Awachana Wanafunzi Na Harakati Zao Za Siasa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza  taswira mbaya za serikali  badala yake kuwa na mitazamo chanya.

Aliyasema hayo jana katika kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.

Alisema wanafunzi hawatakiwi kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani yenyewe haina muda wa kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.

“Nilishawahi kufanya harakati nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu yamekuja kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” alisema Dk Mwigulu.

Alisisitiza kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya serikali bila  kuangalia masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.

“Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa kuwa kimya Bali kuwa na mitazamo chanya naukiona mwanazuoni anabisha jambo jema ujue kuna kasoro,” alisema

Makonda awaagiza wananchi kutupa taka kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wananchi wa mkoa huo ambao maeneo yao yamekaa na takataka muda mrefu bila kuzolewa kwenda kuzitupa nyumbani kwa wenyeviti wa Serikali za Mitaa.

Ameyasema hayo leo Machi 17, kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wa kuendeleza utalii wa jiji hilo.

Makonda amesema haiwezekani tunakuja na mpango wa utalii lakini jiji bado linaonekana chafu na kutaka kila kiongozi kuwajibika katika kulisimamia hilo.

“Nawaambieni wananchi kuanzia leo kama mna uhakika mmelipa tozo ya kuzolea taka na taka hizo hazijazolewa kwa muda mrefu, zipelekeni nyumbani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa yenu halafu yeye atajua wapi pa kuzipeleka,” amesema Makonda.

Amesema katika mpango huo anategemea kuona mambo manne yakifanyika ikiwamo suala zima la usafi, utalii, stendi za mabasi za kisasa na masoko ya kisasa ambayo yatawawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao mahali pazuri.

Kwa upande wake Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, ameupongeza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuja na mpango huo na kuahidi kwamba ofisi yake itatoa ushirikano kuona jambo hilo linafanikiwa.

Tanzania kukumbwa na Kimbunga, TMA yaeleza

$
0
0

Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imekanusha kutokea kwa hali ya Kimbunga "ELIAKIMU" katika maeneo yanayozunguka nchi na kudai Kimbunga hicho kipo kwenye visiwa vya Madagascar.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa hivi punde na kurasa rasmi za mamlaka hiyo Machi 17, 2018 na kusema ni ukweli Kimbunga kinachojulikana "ELIAKIMU" kipo eneo la Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madagascar na kinaelekea Kusini mwa kisiwa hicho.

Aidha, Mamlaka ya hali ya hewa imesema imefuatilia mwenendo wa Kimbunga hicho tangu kilipojitokeza mapema mnamo Machi 15, 2018 majira ya saa 11 asubuhi na kutoa utabiri wa hali ya hewa nchini kwa kuzingatia mifumo yote ya hali ya hewa inayojitokeza.

Kwa upande mwingine, mamlaka hiyo imesema itajitahidi kutoa taarifa  na tahadhari za utabiri kadri inapobidi kufanya hivyo.

Makonda apiga marufuku Wasanii Kukamatwa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amepiga marufuku kukamatwa wasanii pindi wanapokuwa wanapiga picha au kuigiza katika maeneo ya bandari yanayoonesha taswira ya Jiji inavyoonekana kiujumla kwa madai kitendo hicho wanalitalitangaza kitalii.

Makonda ametoa kauli hiyo leo (Machi 17, 2018) wakati wa ghafla ya uzinduzi wa kazi za kutangaza utalii katika Jiji la Dar es Salaam na kusema amepata malalamiko mengi kuhusiana na wasanii wanaokamatwa na wakiwa wapo katika shughuli za kuutangaza kiutalii mkoa wake.

"Kwenye mkoa huu wa Dar es Salaam nimepewa taarifa kwamba kuna wasanii wakitaka kupiga picha katika baadhi ya kule kwenye meli 'bandarini' kwa kutaka kuonesha tu sura ya Dar es Salam inavyoonekana wakati wakitokea upande wa pili kule wa Kigamboni kuna watu wanajitokeza na kuwakamata wakati wanataka kuutangaza mkoa wao na vitu vizuri vilivyopo ndani yake", amesema Makonda.

Aidha, Makonda amesema wasanii hao hao wakienda kuigiza katika maeneo machafu huwa hakuna mtu anayejitokeza kuwakamata au hata kuwazuia jambo ambalo lina mkera kwa upande wake.

"Sasa kuanzia leo hakuna kuwakamata wasanii wanapofanya matukio yao ya kurekodi ndani ya mkoa wa Dar es Salaam wanakibali kutoka kwangu. Sehemu ambazo utahitaji kupata kibali ni Ikulu, Mahakamani na Jeshi la Polisi lakini hayo maeneo mengine yote unaruhusiwa kurekodi na huko wakitaka kibali njoo ofisini kwangu mimi nitakusaidia upate kufanya kazi yako", amesisitiza Makonda.

Pamoja na hayo, Makonda ameendelea kwa kusema "leo hii Ikulu ya Marekani 'White House' inajulikana kutokana na muvi zao wengine hatujawahi kutembelea baadhi ya nchini lakini ukiangalia 'movie' unaambiwa ndio sehemu fulani unakubali kumbe hata wakati mwingine unadanganywa".

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema inapaswa ifike wakati wasanii waliopo nchini Tanzania hasa katika jiji lake wawe wanarekodi kazi za kwa uhuru bila ya kupatiwa shida ya aina yeyote ile.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya March 18

Polepole Amtaka Zitto Kabwe Atafute Kazi Nyingine ya Kufanya

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefunguka na kusema Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mwaka 2020 atafute kazi nyingine ya kufanya kwa sababu jimbo hili litarudi kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Polepole amesema hayo Machi 17, 2018 wakati akifanya ukaguzi wa mradi wa kusambaza maji mkoa wa Kigoma ambapo amesema kuwa wanataka kuhakikisha kuwa mkoa huo unapata maji safi kabla ya mwaka 2020.

"Mkandarasi ameniahidi mpaka mwezi wa tano maji yataanza kutolewa kwa karibia asilimia mia moja katika mji wote wa Kigoma Ujiji na maeneo ya pembezoni na mimi nimezungumza na viongozi wenzangu wa CCM wafike hapa mwezi mmoja kutoka leo kujiridhisha juu ya maendeleo ya kukamilisha mradi huu na kupeleka maji katika mji wetu wa Kigoma , sisi tunafanya hivi sababu tunao mkataba na wananchi na tunataka kuukamilishe mapema kabisa kabla ya 2020 ili ifikapo 2020 basi mbunge wa hapa atafaute kazi nyingine" alisisitiza Polepole

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole yupo mkoani Kigoma katika ziara ya Kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mwaka 2015 - 2020

Naibu Waziri Mavunde Kalazwa Morogoro

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro akisumbuliwa na homa kali.

Mavunde amesema alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia Jumapili baada ya kujisikia vibaya na saivi anaendelea kupatiwa matibabu

Mwanamke anyongwa hadi kufa na watu wasiojulikana

$
0
0
Watu wasiojulikana wamemnyonga hadi kufa Salome Paschal (30) mkazi wa Kijiji cha Zunzuli katika Kitongoji cha Kituli, Kata ya Salawe wilayani Shinyanga na kisha kuutupa mwili wake kwenye kichaka.

Akizungumza leo Jumapili Machi 18, 2018 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, polisi wanaendelea kufanya uchunguzi kwa aliyehusika na mauaji ya hayo.

Akisimulia tukio hilo, mume wa Salome aitwaye Isaya Mshomari amesema mkewe ameuawa Machi 17, 2018 saa nane mchana kwa maelezo kuwa alimuaga kuwa anakwenda sokoni kununua mahitaji ya nyumbani kisha aje awapikie wafanyakazi waliokuwa shambani.

Zitto Kabwe Alishitaki Jeshi La Polisi Mahakamani

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo, Kabwe Ruyagwa Zitto amefunguka na kusema kuwa chama chake tayari kimefungua kesi ya Kikatiba katika mahakama Kuu Dar es Salaam kulishtaki jeshi la polisi.

Zitto Kabwe amesema hayo leo Machi 13, 2018 wakati akitoa tathmini ya ziara alizofanya kutembelea Madiwani katika kata mbalimbali nchini zinazoongozwa na ACT Wazalendo ambapo amedai katika ziara hiyo wamebaini mambo mengi ikiwa pamoja na hali ya maisha kuwa ngumu sana, migogoro ya ardhi, kukosekana kwa huduma ya Maji safi na salama, ukosefu wa huduma bora za afya, tatizo la Miundombinu ya Usafirishaji.

Kiongozi huyo aliendelea kuweka wazi mambo mbalimbali ambayo wamefanikiwa kuyaona katika ziara hizo kuwa ni pamoja na  ukosefu wa pembejeo za Kilimo, ukosefu wa masoko ya mazao ya wavuvi, wakulima na wafugaji, kushuka kwa bei ya mazao yao, kupanda kwa gharama za maisha ya watu, kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi, upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, vyoo pamoja na walimu, na kuzorota kwa hali ya usalama wa wananchi pamoja na mali zao, hali mbaya ya ajira kwa vijana pamoja na uminywaji mkubwa wa demokrasia na uhuru wa watu kukusanyika na kujieleza.

"Tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli, ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza. Tunaamini Mahakama itatenda haki kwenye suala hili" alisema kiongozi huyo

Aidha Zitto Kabwe ametoa ushauri kwa serikali kuhusu suala la Demokrasia nchini na kusema kuwa mazungumzo ya kitaifa ndiyo yanaweza kuwa na jibu kuhusu masuala haya na kuleta utatuzi juu ya jambo hili.

"Demokrasia na Ustawi wa Taifa tunaendelea kusisitiza rai yetu kuhusu umuhimu wa kuitisha Mkutano wa Kitaifa wa maridhiano ya kisiasa kama jukwaa la kuzijadili changamoto za uendeshaji wa siasa nchini. Jambo hilo litaondoa uadui unaoendelea kukua sasa kati ya serikali na wananchi, viongozi wa dini, mashiriki yasiyo ya Kiserikali, taasisi za wanafunzi, pamoja na vyama vya Upinzani. Tunaamini mazungumzo ya Kitaifa ndio jambo sahihi la utatuzi wa suala hili" alisisitiza Zitto Kabwe

Lipumba Ampiga Kijembe Maalim Seif

$
0
0
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema chama hicho kilimdekeza kwa kiasi kikubwa Katibu mkuu wake, Seif Sharif Hamad.

Profesa Lipumba amesema hali hiyo imesababisha CUF kushindwa kupata viongozi watakaoingia katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na kutokuwepo kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar aliyepo upande wa Maalim Seif, Nassor Ahmed Mazrui amesema chama hicho hakimdekezi katibu huyo, bali kinaringia kura anazopata kila anapowania urais wa Zanzibar.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumapili Machi 18, 2018 wakati akifungua kikao cha kwanza cha kawaida cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF kinachofanyika makao makuu ya chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam.

“CUF tumemdekeza kwa muda mrefu na zile nyimbo tulizokuwa tukiimba ya kuwa akipata Seif tumepata sote zilikuwa zimemuingia kichwani kwelikweli na yeye alitafsiri kuwa akikosa Seif tumekosa sote,” amesema.

“Matokea yake tumekosa kuwa na uwakilishi katika Baraza la Uwakilishi jambo ambalo limetuathiri kisiasa hasa Zanzibar. Hili kosa kubwa tuliowakosea Wazanzibari”

Katika ufafanuzi wake, Mazrui amesema Maalim Seif anabebwa na kura za urais wa Zanzibar na wananchi wameonyesha wazi kumpenda na kumkubali.

 “Maalim Seif anatamba na kura na watu wanampenda. Kura ni demokrasia ndicho anachoringia katibu mkuu wangu, mbona yeye (Profesa Lipumba) akigombea anapata kura chache na kila kukicha zinashuka hajioni?” amehoji Mazrui.

“Mimi ni mfanyabiashara nikiona mambo hayaendi sawa katika shughuli zangu nafanya mabadiliko ili kuimarisha . Kwa hiyo CUF tunamthamini sana Maalim Seif na kila kukicha anatuongezea majimbo.”

Amesema ziara yake ya Pemba imesaidia kuimarisha chama hicho na hivi sasa wananachi na viongozi wa CUF wanaijua vyema Katiba ya chama tofauti na hapo awali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 19

Harmorapa Amtolea Povu Uchebe na Kudai Ameolewa na Shilole

$
0
0
Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena  na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.

Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:

"Uchebe mtoto wa kiume umeacha Kupiga  spana umekimbilia Kuolewa. Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu  vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.

Mkapa sasa ataka mdahalo kujadili kushuka kwa elimu

$
0
0
MKUU wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema elimu ya Tanzania ina mushkeli, hivyo unatakiwa kuitishwa mdahalo, kubaini chanzo cha tatizo na changamoto zinazokwamisha kupanda kwa elimu nchini na kuzitafutia ufumbuzi wa kuiboresha.

Mkapa ambaye alikuwa Rais wa Awamu ya Nne, alitoa kauli hiyo katika sherehe ya kumuaga Makamu wa Mkuu wa UDOM aliyemaliza muda wake, Profesa Idrisa Kikula na kumkaribisha Profesa Egid Mubofu chuoni hapo. 

Katika kuikwamua elimu nchini, Mkapa alimwagiza Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Mubofu kuitisha mdahalo chuoni hapo, ambao hautahusisha wanataaluma wa Udom peke yao, bali na wadau wa elimu kutoka katika taasisi, jumuiya au jamii nyingine, kujadili mstakabali wa elimu nchini ambao hauendi vizuri.

Kabla ya kuitisha mdahalo huo, Mkapa alimwagiza Profesa Mubofu, kufanya hadidu za rejea kwa kusoma hotuba aliyotoa wakati akizungumza na Baraza la Chuo hicho mwaka jana, ambapo aliagiza kuwepo na juhudi za makusudi kuhakikisha mkakati unawekwa kuboresha elimu nchini. 

“Mdahalo huo wa wadau wa elimu utaweza kubainisha ni wapi elimu nchini imekwama, sababu zinazochangia na changamoto zinazochangia na wapi twende au tuirekebishe, kwani amekuwa akisikia kwamba nchi hii kielimu ni ya chini kuliko Kenya na Uganda, ila hana uhakika kuhusu hilo,” alisema.

Mkapa alisema anasoma sana magazeti, wakati mwingine hadi anamkera mkewe, lakini kupitia maoni ya watu mbalimbali zikiwemo barua za wasomaji wanalalamika kwamba elimu imeshuka, ina mushkeli, na yeye kama raia ana wajibu wa kutoa maoni yake kuhusu mustakabali wa elimu nchini. 

“Tatizo sijui ni nini, ni lugha, ratiba ya masomo, ushirikiano au ni ushirikishwaji wa waliiohitimu, wanafunzi, wakufunzi, wazazi au tatizo ni nini, mdahalo unaweza kutoa jawabu la wapi hatujaenda vizuri tujirekebishe ili tusonge mbele kielimu,” alisema.

Alitoa mfano wa matokeo ya Kidato cha Nne, mwaka jana yaliyotangazwa mwaka huu, ambapo katika shule 10 zilizofanya vizuri, shule za serikali ni mbili na zilizobaki nane ni za watu binafsi au kanisa. 

“Kwa nini si za serikali ambayo ndiyo inayosimamia elimu nchini?” Alihoji. Aliwapongeza Profesa Kikula na wenzake, Profesa Shaban Mlacha na Profesa Ludovick Kinabo, kwa kukifikisha chuo hicho kilipo kutoka kuwa pori lenye jengo moja la Chimwaga hadi kuwa mji wa majengo na kitaaluma.

Aliiomba serikali iwape tuzo kwa kazi hiyo kubwa. Akizungumza baada ya kuvua joho la uongozi chuoni hapo, alioushika tangu Februari mwaka 2007, Profesa Kikula alisema Udom ilikuwa pori na sasa ni chuo kikubwa na cha pili kwa ubora Tanzania. 

Alisema kuwa aliahidi kwa Mkapa wakati huo kwamba iwe mvua au jua, lazima chuo kisimame na ndivyo ilivyo. Wakati akimtambulisha Profesa Mubofu aliyemteua kushika nafasi ya Makamu wake, Mkapa alisema Makamu huyo mpya ni Mwalimu, Mhadhiri, Kiongozi na Mbobevu katika taaluma.

Alimtaka asiwe na shaka kusimamia chuo, kwani ataweza, lakini akaiomba serikali kumpa msaada wa fedha kuendeleza ujenzi wa majengo chuoni hapo. 

Akizungumza baada ya kuvikwa joho la Makamu Mkuu wa Chuo na kukabidhiwa zana za kazi, Profesa Mubofu aliahidi kuendeleza kazi iliyoanzwa na mtangulizi wake Profesa Kikula, akaahidi kwenda kwa viwango kwani amekwenda chuoni hapo akitoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Alisema alikubali jukumu la kusimamia chuo hicho na kwamba atatumia taaluma, akili na maarifa yake yote kusimamia taaluma, utafiti na ushauri na hasa kuondoa changamoto zilizopo katika chuo hicho chenye wahadhiri na wanafunzi na watumishi 27,000 na kuhakikisha kinasonga mbele. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Gaudentia Kabaka alimkaribisha Makamu Mkuu wa Chuo hicho, na kumhakikishia ushirikiano katika kuinua taaluma, kuongeza utafiti na ushauri katika kuhakikisha chuo hicho chenye umri wa miaka 10, kinazidi kubwa bora zaidi.

TRA Yasamehe....Yaagiza Maduka, Biashara Zilizofungwa Zifunguliwe

$
0
0
Mamlaka  ya Mapato Tanzania (TRA), imeagiza biashara zote, yakiwamo maduka ilizofunga katika mikoa ya kusini Lindi na Mtwara, zifunguliwe na kuendelea kuhudumia jamii na Serikali iweze kupata kodi yake.

Aliyetangaza kusitishwa kwa uamuzi huo ni Kamishna wa kodi ya mapato za ndani, Elijah Mwandumbya, kwenye kikao cha pamoja kati yake na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi.

Mwandumbya alitoa agizo hilo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wadau hao kwamba baadhi ya wafanyabiashara wakiwamo wa vifaa vya ujenzi, soda na vyakula katika mikoa hiyo, wamelazimika kuzifunga kwa madai kukadiliwa kodi kubwa tafauti na kile wanachokipata.

Kamishna huyo alisema uamuzi wa kufunga biashara sio jambo la busara, kwani licha ya kuwaathiri wafanyabiashara wenyewe, pia athari huigusa Serikali, kutokana na sehemu kubwa ya mapato yake kutokana na kodi zinazolipwa na wafanyabiashara.

“Sisi TRA ni wakala tu wa kukusanya maduhuri ya Serikali, leo mnapofunga mnategemea inapata wapi fedha za kutekeleza masuala ya maendeleo kwa jamii, ”alisema Mwandumbya.

Alisema Serikali inapokusanya kodi inaiwezesha kutekeleza kwa majukumu yake, ukiwamo ujenzi wa vituo vya kutolea huduma kwa jamii, ununuzi wa dawa na vifaa tiba, miundombinu ya mawasiliano ya barabara, umeme na nyinginezo.

Aliwataka wafanyabiashara kuhakikisha wanaweka vizuri mahesabu yao, ili kuepuka usumbufu wa kukadiliwa kiwango kikubwa cha kodi tafauti na kile wanachokipata.

Baadhi ya wafanyabiashara, Obodea Swai, Said Namachokole, Ally Pepe, Selemani Ahamadi na Ally Bushiri walisema hivi sasa wafanyabiashara wengi wamelazimika kufunga shughuli zao kutokana na kiwango kikubwa cha kodi wanayokadiliwa.

Pia walimueleza Kamishna huyo kuwa hawakatai kulipa kodi kama sheria inavyowataka, lakini wanashindwa kutokana na mzunguko mdogo wa kifedha unaochangiwa na kukosekana kwa viwanda katika Mkoa wa Lindi.

“Tambueni watu mnaowaleta kuhudumu huku mnawapeleka mkoa masikini, hivyo msiwapangie viwango vikubwa vya ukusanyaji kodi,” alisema Namachokole.

Hatua hiyo ya TRA imechukuliwa siku chache baada ya Rais John Magufuli kutoa maelekezo ya kuangaliwa upya kodi wanazotozwa wafanyabiashara, kutokana na malalamiko mengi ya kukadiliwa kodi kubwa.

Akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa awamu ya pili ya reli ya kisasa kutoka Dodoma hadi Morogoro, Jumatato iliyopita, Rais alimwagiza Waziri wa Fedha na Mipango na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wanaondoa kero za kodi ili kutoa hamasa kwa wananchi kulipa kodi kwa manufaa ya taifa.

Alisema ni vyema TRA ikaangalia kodi inazotoza kwa kuwa inawezekana zingine ni kubwa mno kuliko miradi ambayo wananchi wanatekeleza au kuwekeza.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, badala ya kuwa motisha kwa walipakodi, inakuwa kero kwa walipakodi, hivyo badala ya kulipa kodi wanabuni mbinu za kuwepa kodi wakati wangeelimishwa vizuri, wangeweza kulipa kodi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images