Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

PICHA: Uzinduzi wa Albamu ya Diamond Watikisa Kenya

$
0
0
Msanii  wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezindua rasmi albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’ jijini Nairobi na kufanya bonge la shoo akiwa na timu nzima ya WCB.

Mbali na WCB, wasanii wengine waliopada jukwaani na kutikisa katika shoo hiyo, ni msanii wa Marekani, Omario.

Albamu mpya ya Diamond imesheheni ngoma 20 kali zikiwemo alizowahi kuzitoa kipindi cha nyuma na nyingine mpya.

Bilioni 10 za Rais Magufuli kuanza kujenga ofisi za idara ya uhamiaji Dodoma

$
0
0
Waziri wa mambo ya ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma mjini, mkoani humo ambapo ndipo patajengwa Ofisi za makao makuu ya Idara ya uhamiaji.

Tayari Rais Magufuli, ameshatoa kwa idara hiyo Sh. bilioni 10 na kwamba ujenzi wa ofisi hizo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza wakati alipotembelea ofisi hizo leo, Dk Mwigulu amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuwapa fedha hizo ambzo ni Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji.

Amesema tayari kwasasa eneo kubwa lenye mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa idara hiyo.

“Eneo limeshapatika kubwa la kutosha la kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo muheshimiwa Rais amesemea wakati anatuhaidi kutupa fedha hizi sasa tumepata eneo la kutosha ambalo lipo karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa,zimamoto na ofisi zingine za serikali ambapo itasaidia kama mtu akifika uhamiaji anaweza kupata zingine ambazo zipo karibu,” Aliongeza waziri mwigulu.

Waziri mwigulu ametoa rai kwa idara ya uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma kwani kama wangefata kupata fedha katika bajeti ya wizara ingechukua mda mrefu kupatikana fedha hizo hivyo kufanya kazi kwao vizuri kunamfanya hata yeye kuwa waziri wa mamboya ndani mzuri.

Naye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amemshukuru muheshimiwa Rais Magufuli kwa kuwapa fedha hizo kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote.

“Sisi kama idara tunajukumu la kufuata taratibu zote kwa haraka iwezekanavyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liweze kukamilika kwasababu kama fedha zipo,”alisema Dkt. Anna.​

Wastara Amchana Mange Kimambi....."Ana Cheti Cha Mirembe"

$
0
0
Msanii wa maigiizo nchini Wastara Juma amefunguka na kuongelea yaliyokuwa yanajiri alipokuwa hospitali na kusema kuwa kipindi yupo katika matibabu yake nchini india , mwanaharakati Mange kimambi aliwapigia simu madaktari na kuwadanganya kuwa ni dada wa Wastara na kutaka kujua  details zake.

Wastara alisema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha kikaangooni live  kinachorushwa na EATV,  Ambae alizusha uongo mwingi kuhusu matibabu ya msanii huyo baada ya kuonekana kwa cannula ambae ilisemekana kuwa imegeuzwa kwa mujibu wa Mange ingawa Wastara mwenyewe alikataa swala hilo.

"Mange kimambi aliwahoji madaktari nikiwa india,mimi nikashaanga kuona madaktari wanakuja wananiuliza mimi ni nani Tanzania, nikawajibu mimi ni msanii ....wakaniuliza  kama ninamfahamu huyu mtu anaitwa Mange Kimambi anasema kuwa ni dada   yangu, na pa ni mwamndishi wa habari anakuulizia, nikawajibu sina dada mwenye cheti cha milembe."

Wastara anasema kuwa kama mange kimambi angekuwa na akili basi alitakiwa kuangalia ile cannula vizuri kabla ya kuanza kuweka maneno katika mitandao kuhusu kudanganya

Okoa Ndoa Yako Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Tiba Asilia Itokanayo Na Mizizi Na Magamba Ya Miti Shamba:

$
0
0
Kwa utafiti mkubwa uliobainika wanaume asilimia 70 wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo 

NA ndio chazo kikubwa kinachosababisha ndoa au mahusiano mengi kuvunjika .Mwanaume anatakiwa awe na uume mrefu kuazia nchi 5,6,7,au 8 vinginevyo mwanaume huyo atakuwa na upungufu  wa vichocheo hivi HORMONES ZA GETROGEN

Tumia dawa YA MWIMALA huboresha uume wako saizi upendayo

SHAFTI POWER ni dawa ya nguvu za kiume hutibu matatizo matatu kwa pamoja;
1 kushindwa kurudia tendo na mwili kuchoka 
2 kuwahi kufika kileleni 
3 kulegea kwa misuli na uume, kusinyaa 

Tunatibu presha, fangasi, busha bila kupasua, vidonda vya tumbo, kisukar,i kutopata choo, magonjwa ya moyo, kupooza viungo, ngiri,

Tunapatika mbagara karibu na amana benki kwa wateja wa mwanza na mikoa jirani yupo wakala wetu au wasiliana nami DR MFAUME SIMU NO 0789234653. HUDUMA IZI UTAZIPATA POPOTE ULIPO

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

POLISI: Asiyejua kufa akachungulie kaburi

$
0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Nsatu Marijan amesema hali ya usalama nchini imezidi kuimarika kwani hakuna tishio lolote la kiuhalifu linaloweza kutokea kwasababu Jeshi la Polisi limejipanga ipasavyo na halishindwi na chochote.

Kamishna Marijan ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa salamu za kumuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro katika uzinduzi wa vituo vidogo vya polisi vinavyo hamishika 'mobile Police Station' ambapo vitaanza kutumika katika mkoa wa kipolisi Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

"Jeshi liko imara, matukio ya uhalifu nchini yamepungua sana, hakuta tishio lolote ambalo lipo nje ya uwezo wa Jeshi la Polisi kushindwa kulikabiri. Sisi kama Jeshi la Polisi tutaendelea kuhakikishia nchi hii inaendelea kuwa salama ili wawekezaji na wananchi waweze kufanya shughuli zao bila ya taflani yeyote", amesema Kamishna Marijan.

Pamoja na hayo, Kamishna Marijan ameendelea kwa kusema "kama mtu ana wasiwasi na Jeshi letu basi ajaribu kufanya lolote maana wanasema asiyejua kufa basi akachungulie kaburi. Sisi tupo imara tutaendelea kuwa imara".

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema vituo hivyo vilivyo zinduliwa leo vitatumika kwa kadri ya maelekezo ya maeneo yenye uhalifu utakapotokea eneo fulani na endapo utapungua basi watavihamishwa na kwenda eneo jingine lenye uhalifu.

BREAKING: Afande Sele ajiunga rasmi CCM.....Rais Magufuli Ampokea

$
0
0
Msanii mkongwe nchini Afande sele ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) leo mbele ya Rais Dkt. Magufuli kwa lengo ka kuunga mkono jitihada zake anazozifanya katika kupigania na kukiomba chama kimpokee kama kijana wao

Afande Sele ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatumbuiza muziki kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro walioweza kuhudhuria shughuli za uzinduzi wa kiwanda cha Sigara mkoani humo na Rais Magufuli.

"Nataka nimuhakikishie Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwamba mimi ni mtu wakufikiri, mbishi na mgumu sana katika kukubali jambo fulani lakini niseme kwa uwazi kabisa tangu ulipochukua madaraka ya kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM umeweza kuinyosha nchi na kukisafisha chama chako na kimeweza kurudi katika uimara wake kama alivyokuwa anataka muasisi wetu wa taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere lakini leo kimekuwa hivyo", amesema Afande Sele.

Pamoja na hayo, Afande sele ameendelea kwa kusema "naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi naomba nikuhakikishie kwamba leo hii kutoka kwa dhati ya moyo wangu nimeamua nisimame upande mmoja na wewe ili nisiachwe katika maendeleo. 

"Ninaamini kabisa Mhe. Rais sasa hivi Tanzania kama gari basi dereva ametulia na gari linakwenda na mimi kama abiria niachwe ninywe soda yangu kwa amani kwasababu naamini kabisa chombo chetu kinaenda sehemu salama na sipendi kesho historia ije kunihukumu kwa watu wale ambao hawakuchangia walichonacho katika kufikisha mahali kinapoenda.

"Nawaomba viongozi ngazi ya mkoa wa CCM mnipokee kijana wenu nije kuongeza nguvu", amesisitiza Afande sele.

Waziri Mwijage Aweka Jiwe La Msingi La Ujenzi Wa Majengo Ya Viwanda....Mavunde Awataka Wajasiriamali Dodoma Kuchangamkia Mikopo Kutoka Sido

$
0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh Charles Mwijage(MB) ameweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Majengo kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo katika eneo la Kizota-Manispaa ya Dodoma ambapo jumla ya viwanda vidogo 45 vinatazamiwa kuanzishwa kupitia utaratibu wa Clusters “Kongani” na pia kutoa mafunzo kwa Wajasiriamali mbalimbali.

Waziri Mwijage amewataka wanaDodoma kujifunza masuala ya Ujasiriamali kupitia SIDO na kuanzisha Viwanda vidogo kwa sababu Wizara yake imedhamiria kuwainua Wajasiriamali wadogo kuanzisha viwanda vingi vidogo katika kuchochea uchumi wa Viwanda.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amemshukuru Waziri Mwijage kwa kusimamia upatikanaji wa eneo hilo la ekari 11 ambalo SUMA JKT watajenga **Industrial sheds **za kuweka Viwanda vidogo 45 na hivyo kuinua uchumi wa wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Viwanda.

Mavunde pia amewataka Wajasiriamali wa Jimbo la Dodoma Mjini kuchangamkia fursa za mikopo kupitia mfuko wa uwezeshwaji wajasiriamali(NEDF) uliopo chini ya *SIDO* ili wapate mitaji ya kuanzisha na kuendeleza viwanda.

Naye Lt Col. Mahenge kutoka **SUMA JKT **ameahidi kuifanya kazi hiyo ya ujenzi kwa muda uliokubaliwa na kwa kiwango cha hali ya juu ili majengo hayo yatumike kirahisi kwa kazi iliyokusudiwa.

Masauni Ajitosa Sakata la Maandamano Nchi Nzima

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amejitosa sakata maandamano linalosambaa katika mitandao ya kijamii, kwa kuwaonya wanaotishia kuandamana kwa kusema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama viko imara.

Masauni ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Machi 15, jijini Dar es Salaam wakati akipokea vituo sita vya polisi vinavyohamishika vilivyotolewa na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

“Kuna watu wako ndani ya nchi na wengine nje ya nchi wanaotaka kukwamisha ajenda ya maendeleo watupeleke kwenye ajenda zisizo za msingi.

“Utasikia mwingine anasingizia polisi kuwa katekwa kumbe kajiteka mwenyewe, mwingine anataka watu waandamane, yaani watu waache kutumia fursa zilizopo kwa mfano jana Rais kazindua reli ya umeme ambayo mimi nilikuwa naiona Ulaya leo inajengwa Tanzania, waache  kutumia fursa za viwanda vinavyoibuka kwa wingi kama uyoga eti wakaandamane.

“Ninachoweza kuwahahikikishia ni kwamba vyombo vyetu viko imara,” amesema Masauni.

Dawa Ya Asili ya Kuondoa Chunusi, Harufu Mbaya na Nguvu za Kiume

$
0
0
"NI DR. CHIEF MALUNDE PEKEE ANAETIBU NGUVU ZA KIUME NA KUMTULIZA UMPENDAE KWA KUTUMIA DAWA ZA ASILI"
-baada ya kujichimbia katika nchi za kiarabu kwa zaidi ya miaka (10)sasa amewasili nchini na dawa za tiba asilia.
 
1/NGOLO 3 POWER-ni dawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, ina ubora wa hali ya juu wa kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wasiojiweza kufanya tendo la ndoa, inaimarisha misuli iliyolegea na kusinyaa, inarutubisha mbegu za kiume na kukufanya uchelewe kufika kileleni kwa dk.15-25 kuwa na hamu na tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila kuchoka, inarefusha uume inchi 5-8 na kunenepesha hadi cm 4 kwa wenye maumbile madogo, dawa hii imeboreshwa na hutibu matatizo haya kwa muda mfupi tu.
 
2/MAGOYE MVUTO- dawa hii ina uwezo mkubwa sana kumvuta na kumtuliza aliekuacha awe mpenzi, mme/mke itamfanya akutafute mwenyewe ndani ya masaa 3tu na kukutimizia mahitaji yako kwa haraka na kumfunga asiwe na mtu mwingine.
 
3/SUPER LUBEJA- ni dawa ya kushepu umbo no.8 mguu wa bia, kuongeza hips, na makalio kwa muda wa siku 5tu unapata saizi uipendayo, kuondoa makovu, chunusi, harufu mbaya ya mwili michirizi, kupunguza tumbo na maziwa kwa siku 6tu.
 
4/NG'WESHI MIX- ni dawa ya biashara ya kupata wateja wengi, kusafisha nyota, kurudishwa kazini na kupandishwa cheo, kurudisha mali iliyoibiwa au kudhurumiwa.
 
PIA TUNATIBU MAGONJWA SUGU KAMA: vidonda vya tumbo, ngiri, chango na uzazi kwa kina mama: (dawa zote hazina madhara kwa mtumiaji) HUDUMA HIZI UTAZIPATA POPOTE ULIPO: TUNAPATIKANA DSM BUGURUNI SHELI AU PIGA SIM NO_ 0763-181099.

Huna Sababu ya Kuaibika Tena.....Jipatie Dawa Asili ya Tatizo la Nguvu za Kiume

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMU ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744 594 994

Kamati ya Maadili TFF yamfungia Michael Wambura kujihusisha na soka maisha

$
0
0
Sekretariati ya Shirikisho la soka Tanzania TFF ilimfikisha Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kwenye kamati ya maadili akikabiliwa na tuhuma tatu ikiwemo kupokea fedha za malipo TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.

Jana mchana afisa habari wa TFF Clifford Mario Ndimbo aliwaambia waandishi wa habari kwamba Wambura amefanya makosa hayo huku akijua anashusha hadhi ya shirikisho hilo ikiwa ni kinyume na katiba ya TFF.

Ndimbo alisema  Wambura alikuwa na uhuru wa kufika mwenyewe mbele ya kamati na kutoa utetezi wake kwa njia mdomo, kutuma kwa maandishi au kupeleka mashahidi au kutuma mwakilishi ambaye ataambatana na barua ya uwakilishi. Wambura alituma mwakilishi ambaye ni Wakili Emanuel Muga kwa ajili ya kumtetea.

Alisema kamati hiyo iliyokaa jana ikiongozwa na Mwenyekiti wake Hamidu Ally Mbwezereni, wamemkuta na makosa matatu yatakayomfanya Wambura asijihusishe na masuala ya soka.

Kosa la kwanza amevunja kifungu no 73 kwa kupokea malipo yasiyo halali ya TFF, ambapo faini yake ni milioni 10, kutojihusisha na soka miaka mitano au maisha.

Kosa la pili kugushi malipo kwa jina la TFF enzi hizo (FAT), ambapo amezuiliwa kujihusisha na soka kwa miaka 5.

Kosa la tatu linalomkabili ni kushusha hadhi ya TFF, kosa ambalo adhabu yake iliyotolewa ni kutojihusisha na soka maisha.

Wakili wake, Emmanuel Muga amesema hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake kwa sababu kamati ilikuwa na dhamira yake ya kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo (jana Machi 14, 2018).

“Ni kweli sikupewa nafasi ya kumtetea kwa sababu kamati ilikuja ikiwa na dhamira yake kutaka kulimaliza suala hilo siku hiyohiyo. Kwa hiyo nilivyowasilisha masuala ya kisheria ambayo ni ya kikanuni, kamati ilikataa ikasema sisi tunaamua tunavyoona”-Emanuel Muga, Wakili wa Wambura.

Urusi Yaionya Uingereza Kutolitisha Taifa Hilo

$
0
0
SERIKALI ya Urusi imeionya Uingereza kuacha kulitisha taifa lenye nguvu ya nyuklia.

Badala yake imemtaka Waziri Mkuu wa Uingereza, awasilishe sampuli ya sumu ya Novichok iliyotumika kumshambulia jasusi wa zamani wa Urusi.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa Urusi mjini London, ni kupitia sampuli hiyo ndiyo itaweza kuifanya Urusi ifikirie kutoa maelezo inayotaka Uingereza kuhusu sumu hiyo.

Kutokana na msimamo huo wa Serikali ya Rais Vladimir Putin, saa 24 zilizotolewa na Uingereza kuitaka Urusi kutoa maelezo kuhusu kuhusishwa kwake na shambulizi la sumu dhidi ya Sergei Skripal na binti yake Yulia zimemalizika pasipo kueleza chochote.

Uhusiano kati ya Uingereza na Urusi umezorota kwa haraka katika kipindi cha siku 10 tangu jasusi huyo na binti yake kushambuliwa kwa sumu mjini Salisbury, kusini magharibi mwa Uingereza.

Juzi Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, alisema kuna uwezekano mkubwa Urusi inahusika kwa njia moja au nyingine kwa sababu imeshindwa kudhibiti sumu hiyo.

Lakini Urusi kupitia ubalozi wake mjini London, ilisisitiza haitatekeleza wito huo hadi pale itakapopokea sampuli ya kemikali hiyo, huku pia ikitoa mwito kufanyika uchunguzi wa pamoja kuhusu hilo.

Ubalozi huo umeongeza Urusi haihusiki na shambulizi hilo kwa namna yoyote na kuonya Uingereza inapaswa kutambua watajibu vikali adhabu yoyote itakayotolewa.

Umesema hizo ni njama za kuivuruga Urusi inayoandaa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia.

May alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya Urusi iwapo itashindwa kutoa maelezo ya kina kuhusu tuhuma hizo kufikia usiku wa kuamkia jana.

Hatua zinazofikiriwa ni pamoja na kuzuia mali za viongozi wa Urusi na maofisa wengine wa nchi hiyo.

Pia kuzuia Urusi kuwekeza katika masoko ya kifedha ya Uingereza na kuwafukuza wanadiplomasia wa nchi hiyo.

May alitarajia kuainisha hatua hizo mbele ya Bunge jana baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Taifa.

Rais Magufuli Aagiza wafanyabiashara wadogo wa Stendi Morogoro Wasibughudhiwe.....

$
0
0
Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina  moja la Avintishi, leo amejitoa kimasomaso na kumueleza Rais John Magufuli kuhusu kero wanayopata wafanyabiashara ndogondogo ikiwamo kunyang’anywa bidhaa zao.

 Mama huyo alimwambia Rais Magufuli leo, Machi 15 katika uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Philip Morris, Morogoro.

“Wanatunyang’anya bidhaa zetu, na sisi hatuna mtu wa kutusaidia, wanapochukua, wanatutoza fedha na wanachukua bidhaa. Na umri huu hatuwawezi vijana wadogo,” alisema mama huyo.

Baada ya kueleza hayo, Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, John Mugarula kujibu kero zilizoibuliwa na mama huyo.
 
Mkurugenzi huyo, alisema wanawaondoa wafanyabiashara hao kwa sababu wametengewa maeneo maalumu na aliibua pia  suala la kipindupindu kuwa ni sababu ya kuwaondoa wafanyabiashara hao.

 Baada ya hapo Rais, alimuhoji mama huyo, ni kiasi gani alitozwa na askari mgambo wa manispaa, mama huyo akaeleza kuwa alitozwa Sh200, 000.

Rais alihoji tena, iwapo mama huyo anamkumbuka askari mgambo aliyemtoza kiasi hicho?

“Kwa sababu ya kitete na woga, siwezi kumkumbuka,” amejibu mama huyo.

Baada ya kusema hayo, Rais alimpa mama huyo fedha na kumtaka mkurugenzi kumpa kiasi kingine cha fedha mama huyo.

Kadhalika, Rais aliagiza kuanzia leo, wafanyabiashara hao wasibughudhiwe kwa sababu ni watoto wa maskini.

 Wageni wengine waliokuwapo katika uzinduzi huo, akiwamo Mbunge wa Viti Maalumu, (CCM) Getrude Rwakatare, waliinuka na kumchangia fedha mama huyo.

Tundu Lissu awekewa chuma mguuni

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekewa chuma katika mguu wake wa kulia ili kuimarisha mfupa wa paja.

Rais huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jana Machi 14, 2018 alifanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia kama alivyoshauriwa na madaktari wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji.

Lissu amesema operesheni hiyo iliyochukua saa mbili ilifanywa na timu ya madaktari bingwa chini ya uongozi wa Profesa Willem-Jan Mertsemakers.

“Operesheni ilienda vizuri na kwa sasa naendelea na dawa na mapumziko hospitalini kwa muda wa angalau wiki tatu zinazokuja,” amesema Lissu.

 “Wameniwekea chuma cha kuimarisha mfupa wote wa paja la kulia. Pia wamechukua vipimo ili kuangalia kama hakuna tatizo la bacteria kabla hawajafunga kabisa sehemu ya kwenye goti ambayo haijaunga hadi sasa.”

Mke wa Lissu, Alicia amesema anamshukuru Mungu kwamba upasuaji huo umekwenda vyema.

TANGA RAHA- Sehemu ya Thelathini na Moja ( 31 )

$
0
0
AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Wakaanza kupigana na ikamlazimu mwenye kipande cha bangi mdomoni kukitema pembeni huku kikiendelea kuwaka na kikaangukia kwenye mafuta ya pretroli yanayotoka kwenye tanki lililo pasuka la gari aina ya Scani ambayo yamesambakaa barabarani na ndani ya dakika mlipuko mkubwa ukatokea na kusababisha idadi kubwa ya watu wanao gombania viroba vya unga na vindoo vya mafuta kurushwa mbali na wengine kupoteza maisha

ENDELEA
Moshi mwangi na harufu kali ya moshi wa mafuta aina ya Petrol ikatawala katika eneo zima la eneo rulilopo huku vilio vikianza kutwala kwa wale walio wapoteza ndugu zao kwenye ajali ya moto.Ikanilazimu kumsogeza madam Zena pembeni zaidi ili kuepuka kuunguo kwa moto unaosambaa kwenye hili eneo kwa kupitia upepo mkali.Gari za Polisi mbili zikafika katika eneo la tukio na sikujua ni nani aliye wataarifu na baada ya muda gari za zima moto na gai ya wagonjwa ikafika katika sehemu ya tukio na kuanza kupakiza baadhi ya wagojwa mahututi ikiwemo madam Zena na wakawahishwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga iitwayo Bombo.

 Msongamano wa magari mengi yaliyo simama kutokana na ajali ikazidi kuongezeka na kusababisha msongamano mkubwa wa magari mengi yanayotoka mkoani na yanayokwenda mkoani.Maiti za wanakijiji walio ungua katika mlipuko zikaanza kukusanywa eneo moja na nikajikuta nikitafuta sehemu nikisimama kutokana na kushindwa kuiangalia miili ya watu wengine kwa maana imeharibika kiasi kwamba inatisha.Hadi inafika saa tatu usiku magari yakaanza kuruhusiwa kuendelea na safari baada ya magari yaliyo pata ajali kusogezwa barabarani.

Nikarudi kijijini na kukuta nyumba nyingi zikiwa zimetawaliwa na vilio kiasi kwamba hata raha ya viroba vya unga na vindoo vya mafuta ya kupikia ikawa imetoweka miongoni mwa wanakijiji wengi,Kutokana sikuwa mwenyeji kwenye kijiji hichi mojo kwa moja nikafikizia kwa bibi aliye nihudumia kipindi nikiwa nimeokotwa porini,akanipatia chakula nikala na kwenda kuoga kasha nikarudi ndani na kumkuta akichanganya changanya dawa zake kama kawaida

“Unajisikiaje sasa mjukuu wangu?”
“Kdogo afadhali bibi yangu”
“Mshukuru Mungu kwa yale yote yaliyo tokea na ameweza kukuokoa hadi ukafikia kuwa na hali kama hiyo”
“Ni kweli bibi na vipi mbona hauendi kwenye misiba?”
“Mbona hiyo sio misiba mjukuu wangu”
“Sio misiba kivipi bibi?”
“Mjukuu wangu kwenye ulimwengu huu kuna mambo mengi sana ambayo wanadamu huwa tunayapitia na kuyafanya,Yakiwemo mazuri na mabaya”
“Ni kweli bibi ila sijakuelewa ni kwanini umesema kuwa sio misiba?”
“Watu hao hawajafa kilicho tokea kwenye hiyo ajali ni kiini macho tu ila watu wanao sadikika kufa kwenye hiyo ajali wote wapo hai”
Nikajihisi kama mwili ukiwa umesizi kidogo huku nikifikiria cha kumuuliza bibi kwa maana ninacho kisikia hapa ni kama vile nipo ndotoni vile na ikanilazimu kuamini ninacho ambiwa hapa ni kweli na wala sio ndoto

“Kwa nini bibi?”
“Kwa malezo zaidi nitakufwata usiku nikakuonyesha hao watu sehemu walipo”
“Usiku kivipi?”
Bibi akanyanyuka na kuingia ndani kwake na kuniacha na alama ya kuuliza huku mapigo ya moyo yakiaanza kunienda mbio hata hamu ya kulala ikaanza kunitoweka.Nikatoka nje kwa kunyata na nikafanikiwa na kukuta bado wenye misiba wakiendelea kupiga makalee ya kuomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.Nikaanza kutembea kuelekea barabarani na kukuta  na watu wengine wakiendelea kusafisha safisha barabara huku gari aina ya Rosa iliyo pata ajali ilinyanyuliwa na gari maalumu lenye winchi na kuwekwa barabarani
“Kaka hili gai lenu munalipeleka wapi?”
Nilimuuliza mmoja wa wafanyakazi walio kuwa wakijishuhulisha na jinsi ya kuinyanyua gari hii ya abiria
“Tanga mjini”
“Samahani kaka sijui ninaweza kupata japo kanafasi ka kujishikiza na hadi huku munapo elekea?”
“Kwani wewe unakwenda wapi?”
“Mimi ninakwenda Tanga mjini?”
“Sasa huku ilikuwaje ukaja?”

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 43 na 44 )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  

Mama Mariam akajinyanyua taratibu kutoka kwenye mapaja yangu na kukaa pembeni huku akiendelea kuhema sana. Akamshuka jogoo wangu kwa mkono wake wa kushoto na kuanza kuminya minya ili kuwamalizia waarabu weupe watoke.  Akanyanyuka na kulifwata taulo lililopo kitandani, akiwa karibu ya kitanda nikamuona akiinama chini kama anaokota kitu akanyanyuka na kunigeukia sura yake nikaiona ikiwa imebadilika, moja kwa moja nikayapeleka macho yangu kwenye mkono wake, nikaona akiwa ameshika chupi ya bikini.
“Dany hii si chupi ya Asma, imefwata nini humu chumbani mwako”
Mama Mariam aliniuliza kwa saui ya hasira hata sura yake ya mapenzi mazito aliyo kuwa ananionyesha dakika chache zilizo pita ikapotea kabisa.
  
ENDELEA  
Nikabaki nikiwa nimemkodolea macho pasipo kuzungumza kitu chochote. Mama Marima akanifwata kwenye sofa nililo kaa huku akiendelea kuwa katika hali ya hasira.

“Hii chupi ya Asma humu ndani kwako imefwata nini?”
“Kwani hizo chupi zina majina?”
Ilinibidi kumuuliza mama Mariam kwa ukali, hadi akapunguza hasira yake, taratibu akakaa pembeni yangu.
“Umekazania kusema chupi chupi, huyo Asma ni lini nimeonana naye, lini ameingia ndani kwangu. Nimerudi nasikia amepotea narudi leo unaniambia maswal ya chupi wewe vipi, unahisi mimi ni mtu wa kumtomb** kila mwanamke humu ndani ya nyumba yako. Tuheshimieane bwana, kukupa nafasi ya kuwa na mimi sio kutaka kutawala kila kitu kwenye maisha yangu, utambue kwamba nina mpenzi wangu na anahaki ya kuja hapa muda wowote na si Asma au wewe”
Nilizungumza kwa ukali hadi mama Fatuma akatulia kimya, hakuwa na chakuzungumza zaidi ya kutetemeaka kwa woga, kwa manaa tangu aweze kunifahamu leo ndio ameweza kuisikia sauti yangu ya hasira na hata sura yangu imebadilika.

“Naomba unisamehe Dany mpenzi wangu ila…”
“Ila nini, unaleta wivu wakitoto wakati wewe ni mtu mzima hata mimni ndogogo kwako. Hembu nisikilize vizuri, ninaweza hata haya mapenzi nikayaua kuanzia leo na huto weza kunifanya kitu cha ina yoyote sawa”
Kuzungumza hivyo kukamchanganya zaidi mama Maria, aliye jikuta akipiga magoti chini kwa haraka na kuikusanya mikono yake mbele na kuniomba msamaha huku machozi yakimwagika. Nikamtazama kwa hasira iliyo changanyikana na uongo mtupu kwa maana kitu anacho kizungumza ni kweli hii chupi ya Asma, ila kutokana sihitaji ukweli kuweza kujulikana na huo Asma mwenyewe amekuwa ni adui kwangu, ilinibidi kuigiza ukali kumfanya mama Mariamu kuniamini na kuto nihisi vibaya.
“Dany ukifanya hivyo utanniua mpenzi wangu, samahani sana kama nimekuudhi, maisha yangu kwa sasa yanakutegemea wewe kwa kunipa furaha please baba angu nisamehe”

Nikaka kimya na kijifanya simuangalii kabisa usoni mwake, huku moyoni nikijisemea kimoyo moyo kwamba aliti angejua huyo Asma amemzidi viwango kwenye swala la kitandani wala asinge jisumbua kuniomba msamaha.
“Dany tazama jinsi ninavyo kutunzia penzi lako. Ni watu wanaume wengi wanapenda kunitongoza na wana maisha yao mazuri ila nina kataa kutokana na penzi lako”
“So unaniambia hivyo ukimaanisha kwamba wewe ni mzuri sana au?”
“Hapana Dany, nazungumza hivyo ili uweze kutambua thamani ya penzi lako kwangu, sina mwanaume mwengine ambaye anaweza kulihiili penzi langu zaidi yako, ndio maana nina wivu na wewe”
“Ila utambue kwamba nina mpenzi wangu”
Hapo mama Mariamu akaka kimya huku akitafakari cha kuzungumza, taratibu akanitazama huku akijifuta machozi.
“Dany nakubali hata kuwa mwanamke wa pili kwako, natambua umri ndio unafanya mapenzi yetu yawe hivi, umri ndio unafanya mimi kuwa mwanamke wa pili kwako”
“Unaweza kuwa wa kwanza, ila hujafanya kitu cha kunifanya nikuweke wa kwanza”

Taarifa ya Sido kwa kamati ya Bunge yakataliwa

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imesusia kupokea taarifa ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), huku ikitoa onyo kwa wateule wa Rais John Magufuli kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kwa kasi inayohitajika.

Agizo hilo limetolewa leo Machi 15, 2018 mkoani Singida ambapo kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Suleiman Sadiq walipofika kutembelea viwanda kadhaa mkoani humo na mwenyeji wao alitakiwa kuwa ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Akizungumzia leo, Sadiq amesema kamati ya Bunge inapotembelea anapaswa kuwapo waziri, naibu waziri au katibu mkuu, lakini “tumemkuta naibu katibu mkuu na maofisa wengine wa wizara na wale wa Sido, ambao hawakuwa wamejindaa na tumeikataa taarifa yao.”

Amesema Mwijage alipaswa kuwapo wameelezwa amekwenda Morogoro kuhudhuria ufunguzi wa kiwanda cha Sigara eneo la Kingolwira.

“Kwa sasa tupo tu tunatembea tembea hapa Singida, lakini tuseme hawa watendaji wa Rais Magufuli wanapaswa kujitambua na kutekeleza wajibu wao. Kama wameshindwa kutoa ushirikiano kwetu hata kwa kumtuma naibu waziri (Stella Manyanya) au katibu mkuu, hii Tanzania ya viwanda kweli itakuja kama hakuna ushirikiano,” alihoji Sadiq.

Sadiq ambaye ni mbunge wa Mvomero amesema, “tumsaidie Rais Magufuli na sisi katika taarifa yetu tutajua kipi cha kufanya tutakaporudi Dodoma, kwa hiyo sisi kama wabunge hatujapenda kilichotokea leo.”

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 16

Jengo La Abiria Kiwanja Cha Ndege Dodoma Kuboreshwa

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, ametoa miezi miwili kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuhakikisha linakamilisha uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika kiwanja cha ndege cha Dodoma ili kuwezesha jengo hilo kuhudumia abiria wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Ametoa agizo hilo, mkoani Dodoma katika hafla ya utiaji saini mkataba wa uboreshaji wa jengo baina na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) na NHC na kusema  kuwa kukamilika kwake kutawezesha abiria zaidi ya 100 kuhudumiwa kwa wakati mmoja ambapo kwa sasa jengo linahudumia abiria 35.

“Mkataba tunaoshuhudia ukisainiwa leo unaitaka NHC kukamilisha mradi huu ndani ya miezi mitatu lakini niagize mradi huu ukamilike ndani ya miezi miwili kwa sababu fedha zipo na cheti mlichonacho cha daraja la kwanza kinaonyesha namna mnavyoweza kufanya kazi hii kwa haraka’ alisema Mhandisi Nditiye.

Aidha Naibu Waziri Mhandisi Nditiye ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), pamoja na maboresho hayo kuhakikisha inafanya maboresho kwa kujenga maduka ya kubadilishia fedha na bidhaa ili abiria watakaotumia kiwanja hicho hiyo waweze kupata huduma mbalimbali wakati wanaposubiria kupanda ndege.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Dodoma kwa sasa ndio Makao Makuu ya Serikali hivyo miradi yote inayotekelezwa chini ya Wizara lazima izingatie viwango na thamani ya fedha ili kuendana na hadhi ya mji.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Mheshimiwa Antony Mavunde ameipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo na kumuomba Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, kuwafikiria wananchi waliopisha upanuzi wa kiwanja hicho kwa kuwalipa fidia mapema.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamuhanga amesema Serikali inaendelea na mipango ya kuboresha viwanja vya ndege mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga.

Ameongeza kuwa Serikali imepanga kujenga Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa katika eneo Msalato ambapo kwa sasa wataaalam wanapitia usanifu wa kiwanja hicho na wakati wowote zabuni itatangazwa ambapo kiwanja hicho kitaweza kuhudumia ndege kubwa za kisasa kwani kinatarajiwa kuwa barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa Kilomita 4.5 mpaka 5.

Awali akitoa taarifa yake kabla ya utiaji saini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), Richard Mayongela, amesema kuwa Fedha zinazotumika kukarabati jengo hilo ni fedha za ndani za mamlaka hivyo jengo hilo litakamilika kwa wakati na viwango.

Uboreshaji wa jengo la abiria lililopo katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma utagharimu takribani kiasi cha shilingi milioni 600 na utahusisha mifumo ya kisasa ya Tehama, mifumo na maji taka , mifumo ya matangazi ya ratiba za ndege pamoja na mgahawa.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images